CCM Zanzibar imeshindwa, tena si kidogo

Hapana chembe ya shaka kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 CCM ilishindwa. Tena si kushindwa kidogo imeshindwa kiasi ambacho hakuna wasiwasi wowote kwamba Chama cha Upinzani CUF ndio washindi wa dhahir. Kwa kulinganisha takwimu zilotolewa katika vituo ambazo CUF ilifanya bidii ya ajabu kuzikusanya ambapo taarifa hizo zina matokeo ya vyama vyote, na CUF kuchukua …