CCM: Maalim Seif ni msingi wa Maendeleo ya sasa Zanzibar

Maneno hayo yamesemwa jioni ya leo tarehe 28/02/2021 na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Ndugu Abdallah Mabodi, alipofika na ujumbe wa Sekretarieti ya Chama hicho kwa upande wa Zanzibar, kutoa mkono wa pole kwa Uongozi wa Chama cha ACT Wazalendo katika Ofisi kuu za Chama cha ACT zilizopo Vuga Wilaya ya …

Dk Mwinyi asema Serikali inathamini mchango wa vyuo vikuu nchini

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema serikali ya mapinduzi Zanzibar inathamini mchango wa vyuo vikuu Nchini katika kuwafinyanga wataalamu wa fani mbali mbali wanaowezesha kuchangia maendeleo ya Taifa. Rais Dk. Hussein Mwinyi ameleza hayo katika hotuba iliosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais …

Mradi wa viungo kuwanufaisha wakulima kiuchumi

Mradi wa viungo (Spices) Zanzibar unaotarajiwa kuwanufaisha wakulima zaidi ya 21,000 umeelezwa kuwa umekuja wakati sahihi na utasaidia kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa ahadi za Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Hassan Mwinyi katika kuwaletea maendeleo wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba. Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu mkuu Wizara ya Biashara Zanzibar Dkt …

Jamii yashauriwa kupinga vitendo vya udhalilishaji

Jamii nchini imeshauriwa kuwa na msimamo wa pamoja katika kupinga vitendo vya udhalilishaji vilivyoshamiri ndani ya visiwa vya Zanzibar ili kupunguza machungu kwa waathika wa vitendo hivyo wakiwemo wanawake na watoto. Makamu wa Pili wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alitoa ushauri huo mara baada ya kukamilika kwa ibada ya sala ya Ijumaa …