Michezo

Bonanza la mpira wa magongo (Hockey) Zanzibar

Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa magongo (HOCKEY) Zanzibar Ramadhan Pandu Makame ameiomba Serekali pamoja na wadau wa Michezo kusaidia upatikanaji wa vifaa vya mchezo huo ili waweze kuuendeleza na kushiriki katika mashindano ya ndani na nje ya nchi…Ramadhan ameyasema hayo katika Bonanza la Mchezo huo lililoandaliwa na chama hicho kwa lengo la kujindaa na mashindano ya Mapinduzi Cup yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es laam Januari 09 mwakani. Amesema Vifaa vya mchezo wa Mpira wa Magongo ni ghali sana kiasi cha wao kushindwa kumudu kuvinunua na hivyo kulazimika kuomba msaada ili wasaidiwe kupatikana kwake. Ameongeza kuwa Zanzibar kuna vipaji lukuki vya mchezo huo lakini kinachokosekana ni vifaa na ushajihishwaji wa vijana kujiunga na mchezo huo. Ramadhan amedai kuwa kama kutakuwa na ushirikiano wa kutosha na kuwezeshwa kikamilifu chama hicho anaamini kuwa Zanzibar inaweza kuwa na timu zinazoweza kufanya vizuri katika mashindani ya kitaifa na kimataifa. Endelea kusoma habari hii

Japan yaahidi Ujenzi wa Uwanja wa Michezo Pemba

Jumla ya Shilingi milioni 200 za kitanzania zinatarajiwa kutolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya kugharimia Uwanja wa michezo mbalimbali utakaojengwa Kisiwani Pemba. Balozi wa Japan nchini Tanzania Takumi Shimojo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk ofisini kwake leo Kikwajuni mjini Zanzíbar. Amesema Serikali ya Japani inakusudia kujenga uwanja wa Michezo kisiwani Pemba mara tu nchi hiyo itakapoidhinisha kuanza kwa kazi hiyo hapo mwakani. Amefahamisha kuwa Uwanja huo utakaojumuisha michezo ya Judo, Karatee,Mpira wa Kikapu, mpira wa mezani na michezo mingine utajengwa ikiwa ni njia ya kuimarisha mahusiano mema kati ya Japan na Zanzíbar. Endelea kusoma habari hii

Munir Zakaria afutiwa cheo chake na ZFA

CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimemuengua Munir Zakaria kuwa Ofisa Habari na msemaji wake, pamoja na kumteua Suleiman Mahmoud Jabir, kuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Abdallah Juma Mohammed kuwa Mwanasheria wa chama hicho. Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano wa kamati tendaji ya chama hicho uliofanyika juzi kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean View, chini ya Mwenyekiti Amani Ibrahim Makungu ambaye ni Rais wa ZFA Taifa. Katibu Mkuu wa ZFA Taifa Kassim Haji Salum, ameliambia gazeti hili kuwa, kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, msemaji wa mambo mbalimbali yanayokihusu ni Rais kwa kushauriana na Katibu Mkuu. “Kwa mujibu wa katiba yetu, Rais ana nafasi nne za kufanya uteuzi wa watu wa kumsaidia kazi, lakini pia ndani ya katiba hiyo, hakuna nafasi ya Ofisa Habari, na kazi ya kukisemea ni ya Rais kwa kushirikiana na Katibu Mkuu”, alifafanua. Endelea kusoma habari hii

Epukeni udanganyifu katika michezo- Maalim

Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar imesema itafanya kila liwezekanalo ili kuiwezesha ligi ya vijana Zanzibar iweze kusonga mbele. Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Said Ali Mbarouk alitoa ahadi hiyo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, wakati kamati ya ligi hiyo Central Taifa ilipokutana na Maalim Seif ofisini kwake Migombani. Aliahidi kuwa Wizara ya habari itatafuta fedha kwa njia yoyote ili kuhakikisha kuwa fainali za ligi hiyo inayotarajiwa kufikia kilele chake July mwaka huu kwa timu za Juvinail, Junior na Central zinafanikiwa. Alisema ligi hiyo ni muhimu katika kuibua vipaji vya vijana ambavyo vitasaidia kuinua soka la Zanzibar. Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewataka viongozi wa ligi hiyo kuwa na dhamira ya kweli katika kuendeleza ligi hiyo, sambamba na kuepukana na vitendo vyovyote vya udanganyifu katika kuibua vipaji vya wanasoka vijana. Sisi serikali tuko very serious na mimi binafsi niko interested kuona hadhi ya michezo inarejea Zanzibar, kwa hiyo na nyinyi viongozi muwe serious kwa hili”, alisistiza Maalim Seif. Endelea kusoma habari hii

Wasanii msiige na kupotosha – Maalim Seif

Mabadiliko ya Kiulimwengu ambayo yaligusa kila pembe ya kimaisha kuanzia miaka ya 1980s, yalileta Mapinduzi makubwa katika nyanja hii ya mawasiliano na sanaa kwa ujumla. Tumeshuhudia faida zake, lakini pia na madhara makubwa. Kati ya madhara makubwa kubwa zaidi ni kuporomoa kwa mila na tamaduni za nchi kama hizi zetu. Maendeleo hayo yalituathiri zaidi nchi masikini kwa sababu tumekuwa ni wapokeaji tu wa mambo tunayotayarishiwa na mataifa yenye nguvu. Watu wetu hasa vijana wamekuwa wakikumbatia tamaduni na mila za kigeni na hasa za nchi za Kimagharibi. Mabadiliko hayo ambayo yamepewa jina la Utandawazi yamesabisha utaratibu wa mawasilinao kuwa tafauti na ule wa zamani. Vituo vya Senema tulivyotangulia kuvitaja hapo awali ni kwa nadra sana sasa kuviona. Kwa mfano Zanzibar vituo hivyo vingi hivi sasa vimegeuzwa ‘Super Markets’ ofisi na zimekuwa sehemu za biashara, lakini hazioneshi tena filamu. Filamu zilizokuwa zikioneshwa kwenye televisheni hivi sasa zinauzwa mikononi kama njugu kupitia CD na DVDs, huku kukiwa na urahisi mkubwa kwa mtu kuangalia picha anazotaka, hata kupitia simu yake ya mkononi au kompyuta. Endelea kusoma taarifa hii 

Serikali yadhamiria kurejesha hadhi ya michezo Zanzibar

Mashindano ya soka katika Jimbo la Magogoni yajulikanayo kwa jina la “Jihadi Cup”, yalifikia kilele chake jana kwa kuzikutanisha timu za Sayari na Taifa Jipya za jimbo hilo ambapo timu ya Sayari iliibuka kidedea. Mtanange huo uliopigwa katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali, vyama vya siasa na chama cha soka Zanzibar ZFA akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad pamojan na Mwakilishi wa Jimbo hilo ambaye kabla ya uteuzi wa hivi karibuni uliompeleka Waziri wa Mifugo na Uvuvi, alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo.Timu ya Sayari iliibuka mshindi wa kombe hilo la Jihadi na kukabidhiwa pamoja na mambo mengine Kombe na shilingi laki nne taslim, baada ya kumshinda mpinzani wake timu ya Taifa Jipya kwa mikwaju ya penalty. Dakika 90 za mchezo zilimalizika kwa timu hizo kuwa na nguvu sawa ya kufungana na (mabao 2-2) na ndipo sheria ya kupiana mikwaju ilipochukua nafasi yake ambapo Sayari ilishinda mikwaju yote 5 dhidi ya Taifa Jipya iliyopoteza mkwaju mmoja na mwisho kuugomea ikijua kuwa tayari imeshashindwa. Endelea kusoma habari hii

Hizbu Ut Tahrir walaani udhamini wa pombe Zanzibar

Pia, udhamini huu umeleta idhilali na fedheha kubwa itakayowagaeuza vijana wa umma mtukufu wa kiislamu kuwa vibarua kwa gharama duni (thamanu bakhiys) kuitangaza kampuni ya ulevi ili izidi kuendeleza maovu mengi katika jamii ya Kiislamu na wanaadamu kwa jumla. Yametendeka haya ilhali unajuulikana wazi uharamu wa ulevi Kiislamu, ikiwemo kuutengeza, kuuza, kuusafirisha, kuutangaza nk. Na zaidi ya yote Uislamu umeweka bayana kwamba ulevi ndio mama wa maovu yote, na ni kazi ya Shetani. Adui mkubwa anayeshika bendera ya kupotosha Waislamu na wanadamu kwa ujumla.Endelea kusoma habari hii 

 

Kampuni ya bia yadhamini ligi kuu Zanzibar

BAADA ya kilio cha muda mrefu, hatimaye Ligi Kuu ya Soka Zanzibar imepata mdhamini na sasa itajulikana kama, ‘Zanzibar Grand Malt Premier League’. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa udhamini huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Saidi Ali Mbarouk, alizitaka klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Zanzibar, kusimamia na kuweka mbele suala la nidhamu, sambamba na kuepuka malumbano na migogoro isiyo na tija katika soka. Mbarouk alisema kampuni ya kinywaji baridi kisicho na kilevi cha Grand Malt, imedhamini Ligi Kuu ya Zanzibar , kwa mkataba wa miaka mitatu, kwa gharama ya sh milioni 140, ukijikita katika suala la utoaji huduma katika usafiri, malazi, chakula na zawadi kwa klabu zitakazoshiriki ligi hiyo. Katika hafla hiyo iliyowashirikisha viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), na wale wa klabu za soka, Waziri Mbarouk, alisema nidhamu ni nyenzo muhimu katika uendelezaji wa soka, kwa kuzingatia kuwa hakuna mdhamini atakayefurahia kudhamini ligi ambayo daima inakabiliwa na migogoro. “Njia pekee ya kuwatia moyo wadhamini hawa, pamoja na wengine wenye azma ya kuidhamini ligi hii ni kudumisha nidhamu na kuepuka migogoro,” alisema. Endelea kusoma habari hii

Maximo ashauri jinsi ya kupata wachezaji bora wa timu ya taifa

Vilabu vya soka nchini vimeshauriwa kuwa na timu nzuri kuanzia ngazi ya watoto wenye umri wa miaka nane, vijana na kuendelea ili kupata timu bora ya Taifa. Wito huo umetolewa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Star Marcio Maximo wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Sao Paul. Maximo alisema kuwa timu nyingi ambazo ni bora na zinafanya vizuri katika mchezo wa soka zimekuwa zikiwaandaa watoto wenye vipaji vya mchezo huo wangali wadogo ili waweze kuwa wachezaji wazuri hapo baadaye.Kocha Maximo pia alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Mrisho kikwete, ambapo alimnshukuru sana Rais kwa ushirikiano wa hali ya juu aliompa wakati alipokuwa akiifundisha Taifa Stars miaka takriban mitatu iliyopita. Kwa upande wake Rais Kikwete alimpongeza Kocha Maximo kwa juhudi zake za kuendeleza soka la Tanzania, akimwambia uwepo kwake Tanzania kuliasidia sana kuiweka nchi katika ramani ya mchezo huo. Endelea kusoma habari hii

Steven Kanumba afriki dunia

Wakati wazanzibari wakijitayarisha kusoma khitima ya aliyekuwa Muasisi wa Taifa lao la Zanzibar, wameamka na kupata taarifa kwamba Msanii Maarufu katika tasnia ya filamu nchini Steven Kanumba amefariki dunia jana usiku kufutia shambulio la kusukumwa ingawa taarifa kamili za kifo hicho bado hazijafafanuliwa kwa kina na vyombo vinavyohusika lakini kwa taarifa za awali zinasema kwamba alisukumwa akiwa nyumbani kwake baada ya kutokea kutofahamiana kati yake na mpenzi wake Lulu binti mwenye umari wa miaka 18. Endelea kusoma habari hii

Timu ya Habari yapokewa na Naibu Waziri

Timu za Wizara ya Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo, Habari Sports na  Habari Queen, ambazo zilishinda michuano ya Kombe la NSSF jijini Dar es Salaam zimewasili leo Zanzibar na kupata mapokezi ya aina yake ambayo yaliongozwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Bi Hindi Hamad Khamis. Mara baada ya kuwasili bandarini Zanzibar vikosi hivyo vililakiwa kwa ngoma aina ya Boso ambapo wachezaji wa timu hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa Wizara hiyo walishiriki kusakata burudani hiyo ya ushindi. Katika mchezo wa fainali kwa upande wa soka timu ya Habari Spots ilifanikiwa kuwatandika wenyeji wa michuano hiyo timu ya NSSF kwa jumla ya mabao 4-0 katika uwanja wa Sigara-Chang’ombe ambapo kwa upande wa netiboli Habari Queen waliwagonga kinadada wa TBC kwa magoli 30-10. Endelea kusoma habari hii

Wachezaji wamshambulia muamuzi

WACHEZAJI wa timu ya Kikwajuni jana walimshambulia mwamuzi wa Kimataifa, Waziri Sheha Waziri kwa kipigo kwa madai ya kutoridhika na maamuzi ya mwamuzi huyo. Tukio la wachezaji hao kumshambulia mwamuzi huyo lilifanyika mara baada ya mwamuzi huyo kupuliza kipenga cha kumalizika kwa mchezo huo uliochezwa kati yao na timu Zimamoto.Mchezo huo ambao ulichezwa kwenye dimba la Mao Dze Tung mjini hapa ulimalizika kwa timu ya Kikwajuni kufungwa bao 1-0. Mbali na sababu hiyo pia wachezaji hao walidai kuwa wamelazimika kuchukuwa hatua hiyo baada ya mwamuzi huyo kuwatolea lugha ya matusi wakiwa kiwanjani.Ni mwamuzi gani yule anafikia hatua ya kututukana kiwanjani halafu tuseme mpira utakuwa kwa hali hii hauwezi kukuwa”, alisikika Omar Mohammed Kuzu akisema wakati mchezo huo ukiwa unaendelea. Hata hivyo baadhi ya wadau waliohudhuria mchezo huo walikizungumzia kitendo hicho kwa hisia tofauti huku wengine wakisema kuwa kitendo hicho hakiendani na maadili ya mchezo huo.Endelea kusoma habari hii

Zanzibar, Rwanda patamu leo

TIMU ya taifa ya soka ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ leo itashuka dimbani kupambana na Rwanda ‘Amavubi’ kwenye mchezo wa robo fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Endelea kusoma habari hii

AMINI AUNDA KUNDI LA MUZIKI

MTOTO wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amin Salmin ‘Mourinho’, amenzisha kundi jipya la muziki wa Taarab linalojulikana kwa jina la T Moto Morden Taarab ‘Real Madrid’ linaloundwa na wasanii mahiri waliopata kutamba katika makundi ya Jahazi Morden Taarab, Five Star na mengineyo.Akizungumza na Sufianimafoto, Amin alisema kuwa ameamua kuleta mabadiliko na ushindani katika muziki wa taarab kutokana na muziki huo kutokuwa na makundi yenye ushindani wa kisanii zaidi ya majungu na kufanya baadhi ya makundi yakivunjika kwa kushindwa kutoa upinzani na kubuni vitu vipya vinavyoweza kusaidia kulibakiza kundi katika jukwaa la muziki huo.Endelea kusoma habari hii

GRAND MALT WATO VIFAA VA MICHEZO

TIMU ya soka ya Baraza la Wawakilishi Zanzibarimefanikiwa kupata mdhamini katika bonanza linalotarajiwa kufanyika Septemba 8 mwaka huu huko Mkoani Arusha.Watunga sheria hao wa Zanzibarwamepata udhamini huo kutoka kwa watengenezaji wa kinywaji baridi cha Grand Malt ambapo kampuni hiyo ilikabidhi vifanaa mbali mbali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi.Endelea kusoma habari hii

 

KIWANJA CHA MPIRA MWELEO

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hatua ya wananchi wa kijiji cha Bweleo kujenga uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu, inakwenda sambamba na sera ya Serikali ya kulitangaza Taifa kupitia michezo.Endelea kusoma habari hii

MICHEZO HUJENGA AFYA

MICHEZO hujenga afya pamoja na uhusiano na mashirikiano mema katika jamii hivyo hatua ya kutembeleana kimechezo kati ya wanamichezo wa Afisi ya Rais Ikulu Dar-es-Salaam na wanamichezo wa Ikulu ya Zanzibarkutazidi kujenga uhusiano kimichezo na kikazi.Endelea kusoma habari hii

 

MASHINDANO YA NGUMI KUTAFUTA MSHINDI

25 02 2011

MASHINDANO ya Taifa ya ngumi za ridhaa kutafuta mabingwa wa Taifa, yamepangwa Febuari 27 hadi Machi 5 mwaka huu, katika uwanja wa ndani wa Taifa, Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa nane mchana.Timu mbalimbali kutoka mikoani, zimewasili juzi ambapo jana, mabondia hao walipimwa uzito uzito na afya katika uwanja huo kuanzia saa 2:00 asuhubi pamoja na kuendesha kozi fupi kwa makocha.Endelea kusoma habari hii

PBZ YASAIDIA BONANZA LA WAANDISHI ZANZIBAR

23 02 2011

BENKI ya watu wa Zanzibar imeahidi kuendelea kutoa misaada kwa huduma za kijamii ikiwa ni hatua ya kuthamini mchango wa wananchi katika kuimarisha huduma za Benki hiyo.Mkurugenzi wa Benki hiyo, Juma Amour, alieleza hayo jana wakati akitoa maelezo katika hafla ndogo ya kuchangia Michezo ya Bonanza linaloandaliwa na Shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

KAMPUNI ZA SIMU ZAGOMA KUDHAMINI MARIDHIANO CUP

4 02 2011

BAADHI ya makampuni ya simu za mikononi yaliopo nchini tamekataa kudhamini michuano ya kombe la maridhiano yaliopangwa kufanyika leo Zanzibar yakiwa na lengo la kuimaridha umoja na mshikamano uliopo nchini baada ya kuafikiwa kwa maridhiano ya kisiasa ya mwaka juzi hapa nchini. Kombe hilo ni hatua moja ya kutilia nguvu umoja na mshikamano kwa wananchi wote Zanzibar ambapo vijana wameandaa mashindano ya mpira wa miguu kwa lengo la kuhamasisha maridhiano yalofikiwa mwishoni mwa mwaka juzi ambayo yamepewa jina la Kombo la Maridhiano.Endelea kusoma habari hii

MZANZIBARI ASHINDA UREMBO AUSTRALIA

31 01 2011

MZANZIBARI aliyeshinda tuzo ya Miss Africa Australia Zaituni Mohammed Hunt. ameahidi kufanya kazi na taasisi mbali mbali zenye kufanya kaziya kijamii hapa Zanzibar ilikukuza vipaji na fusa kwa vijana nawanawake.Hunt (20) aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habarikatika mkutano hapo jana na kuongeza kuwa anaelewa mchango mkubwa unaotarajiwa kutoka kwa Wazanzibari wanaoishi nje.Endelea kusoma habari hii

 

TUMEJIZATITI KUCHUKUA KOMBE-SIMBA

29 12 2010

TIMU ya Soka ya Simba imesema kwamba itashusha kikosi kamili cha timu hiyo katika mashindano ya kombe la Mapinduzi yatakayofanyika Januari 12 mwaka huu.Meneja mkuu wa klabu hiyo, Innocent Njovu alisema timu yake itawashirikisha wachezaji wazoefu na sio kama inavyofikiriwa na wapenzi wa soka kwamba italeta wachezaji wachanga kwa ajili ya mpambano huo unaotarajiwa kupata mashabiki wengi.Endelea kusoma habari hii

UCHAGUZI WA ZFA KUFANYIKA KESHO PEMBA

28 12 2010

UCHAGUZI Mkuu wa Chama Cha Soka Zanzibar unatarajiwa kufanyika kesho kisiwani Pemba. Uchaguzi huo ambao unashirikisha wagombea wa nafasi ya Urais na Makamo wake utasimamiwa na kamati ya Uchaguzi ya ZFA chini ya Mwenyekiti wake Ali Suleiman Shihata.Katika uchaguzi huo kuna wagombea tisa ambao wanne kati yao wanagombea nafasi ya Urais na watano wanagombea nafasi ya Makamo wa Rais, wawili kutoka Kisiwani Pemba na watatu Unguja.Endelea kusoma habari hii

MWANDISHI WA CHANNEL TEN KUWANIA URAIS ZFA

20 12 2010

MWANDISHI wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten Munir Zakaria amechukuwa fomu kugombea nafasi katika kinyanganyiro cha urais wa Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA).Munir alichukuwa fomu hiyo leo asubuhi na alikabidhiwa na afisa mwandamizi wa Baraza la Michezo la Taifa, Mustafa Omar huko Mwanakwerekwe nje kidogo ya mji wa Unguja na kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali.Endelea kusoma taarifa hii

 

KOCHA WA MZUNGU AHAMIA AZAM FC

14 12 2010

CHAMA Cha Soka Zanzibar (ZFA), kimethibitisha kocha wa timu ya Taifa


Zanzibar Heroes Stewart John Hall ameamuwa kuondoka na kujiunga na timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa chama hicho, Ali Fereji Tamim amesema ni kweli kocha huyo amefunguwa mazungumzo na Azam FC ya kuanza kukinoa kikosi cha timu hiyo.Endelea kusoma habari hii

LIGI KUU VIJANA WAKOSA WAFADHILI

13 12 2010

LIGI Kuu ya Vijana ya mpira wa mikono Zanzibar inatarajiwa kuanza Disemba 18 mwaka huu huku ikiwa na ukata wa kifedha kutokana na kukosa wafadhili wa kuiunga mkono lihi hiyo.Ligi hiyo imeandaliwa na Chama Cha Mpira wa Mikono Zanzibar (ZAHA), itafanyika huko Kitogani wilaya ya kusini Unguja.Endelea kusoma habari hii

UCHAGUZI WA ZFA DISEMBA MWAKA HUU

13 12 2010

MCHAKATO wa uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi mbali mbali za uongozi unaendelea katika kadhaa ya Unguja na Pemba huku uchaguzi mkuu ukitarajiwa kufanyika Disemba 31 mwaka huu Kisiwani Pemba.Kwa mujibu wa msemaji wa Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA) Maulid Hamad Maulid alisema hadi sasa mchakato huo unaendelea vyema katika ngazi za wilaya zote.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR HEROUS WAPEWA MATUMAINI

25 11 2010

BAADHI ya wapenzi wa soka nchini wametoa ahadi za kutoa kitita cha fedha na zawadi mbali mbali kwa timu ya Taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’ iwapo itakapofikia nafasi nzuri katika mashindano ya Chalenji yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni nchini.Ahadi hizo zimetolewa juzi katika uwanja wa Amaan katika pambano la kirafiki kati ya timu ya Zanzibar Heroes na Dar All Stars ambapo Zanzibar Heroes ilifunga Dar All Stars goli 1-0.Endelea kusoma habari hizi

ZANZIBAR HEROES YAPATA MDHAMINI

24 11 2010

TIMU ya Taifa ya Visiwani Zanzibar, Zanzibar Heroes ambayo inatarajiwa kushiriki katika michuano ya Chalenji hivi karibuni imepata mdhamini ambae ataidhamini timu hiyo katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 27.Zanzibar Heroes ambayo imedhaminiwa na hoteli ya Zanzibar Ocean View kwa shilingi milioni tisa,ambapo Meneja wa hoteli hiyo Hashim Salum Hashim alisema kuwa katika mashindano hayo kila mechi itakabidhiwa fedha taslim kwa aajili ya mashindano hayo.Endelea kusoma habari hii

WACHEZAJI WATAKIWA KUWA NA NIDHAMU

24 11 2010

WACHEZAJI wa timu ya Taifa ya Zanzibar wametakiwa kuwa na wawasiliano mazuri baina yao na viongozi wa timu ili iweze kufanikiwa katika mashindano ya Chalenji yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni nchini Tanzania.Ushauri huo umetolewa na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo, Abdillah Jihad Hassan,wakati alipokuwa akiiaga timu hiyo na kuikabidhi bendera huko katika Ofisi za Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) iliyopo Bwawani Mjini Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

 

DCMA WAENDA MAYOTTE KUFUNDISHA MUZEKA

15 10 2010

WALIMU wanne kutoka Chuo cha Muziki cha Nchi za Jahazi (DCMA) cha Zanzibar, wameondoka nchini tarehe 7 Oktoba 2010 kwa safari ya kuelekea kisiwani Mayotte kwa ajili ya kuendesha warsha ya muzeka wa Taarab asilia.Warsha hiyo ambayo imeandaliwa na kufadhiliwa na Idara ya Utamaduni ya Mayotte itafanyika kuanzia tarehe 7 hadi 25 Oktoba, 2010. Walimu watayoendesha warsha hiyo kwa niaba ya Chuo cha DCMA ni Mohammed Issa ‘Matona’, Rajab Suleiman, Mohammed Othman na Kesi Juma.Endelea kusoma habari hii

WANAFUNZI ULIZENI MASWALI-SHAABAN

15 10 2010

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Said Shaaban amewataka wamakocha wanaopatiwa mafunzo kutooneana haya na aibu ya kuuliza wakati wanapopoatiwa mafunzo, iwapo ataona kuna kitu hajakifahamu.Hayo ameyaeleza jana katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar wakati akifungua mafunzo ya siku tano yanayoendeshwa na kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ Stewart John Hall.Endelea kusoma habari hii

WACHEZAJI WAPYA WASAJILIWA

8 10 2010

TIMU ya Soka ya Polisi Bridge inayoshiriki ligi daraja la Kwanza Taifa, imesema kwamba katika msimu wa usajili mwaka huu, wamepanga kusajili wachezaji wachanga na wenye vipaji ili kuhimili vyema mikiki mikiki ya ligi hiyo.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Katibu Mwenezi wa timu hiyo Hashim Mlenge alisema kwamba mpaka sasa wamepanga kusajili wachezaji watano katika nafasi za ushambulizi na mlinda mlango.Endelea kusoma habari hii

TFF WATAKIWA KUNYAMAZA NA ZFA

7 09 2010

CHAMA Cha Soka Zanzibar (ZFA) kimemji juu Florian Kaijage aache mara moja kukisema chama hicho kwa mtazamo yake kwani kwa kufanya hivyo kutaharibu mahusiano yaliyopo kati ya vyama hivyo.Kauli ya ZFA imekuja kufuatia hivi karibuni kwa msemaje wa TFF Kaijega kupitia vyombo vya habari alikaririwa akitaka ZFA iwache kuitaja TFF katika sakata la kumchezesha mchezaji Said Mussa katika michuano ya Chalenj (U20) yaliyomalizika Eritrea hivi karibuni.Endelea kusoma habari hii

KIINGEREZA MUHIMU KWENYE MAFUNZO-ZFA

31 08 2010

CHAMA Cha Soka Zanzibar (ZFA) kimesema ufahamu wa lugha ya kingereza ni sifa muhimu kwa makosha watakaopata mafunzo kutoka kwa kocha muingereza Stewart John Hall.Kocha huyo kutoka Uingereza amefunga mkataba wa miaka mitano na chama cha soka Zanzibar ZFA kufundisha makocha wazalendo na pia kufundisha timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes).Endelea kusoma habari hii

MSHAMBULIAJI ZNZ AENDA MISRI

31 08 2010

MSHAMBULIA mahiri wa timu ya Taifa ya Vijana Zanzibar chini ya miaka 20 ‘Karume Boys’, Ali Badru anatarajia kuondoka nchini kwenda Misri kuripoti katika timu yake mpya.Kwa mujibu wa Taarifa toka kwa Katibu Mwenezi wa chama cha soka Zanzibar Maulid Hamad Maulid, katika safari hiyo itakayofanyika Septemba mbili mchezaji huyo ataandamana na Kocha mkuu wa Karume Boys Abdel fattah Abbas.Endelea kusoma habari hii

MAULID ASHINDWA KUGOMBEA UBUNGE

15 08 2010

Maulid Hamad Maulid

KATIBU Mwenezi wa Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) Maulid Hamad Maulid amesema tuhuma zinazomkabili za kupandikizwa kumshambulia mwizi kwa panga ndizo zilizomfanya ashindwe kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Jang’ombe kama alivyopanga awali.Maulid alitoa ufafanuzi huo alipohojiwa Mjini hapa kufuatia kuvuma habari za Katibu huyo na kutangaza kuwa anagekuwa miongoni mwa wagombea ambao wangeingia katika mchakato huo kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM).Endelea kusoma habari hii

ZFA KUVIADHIBU VILABU VYA SOKA

15 08 2010

Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA) kimesema hakitovumilia kuviadhibu vilabu vinavyoleta vurugu na kupiga waamuzi viwanjani ikiwa pamoja na kufungia wachezaji na viongozi ili kuvifanya viwanja vya michezo kuwa ni sehemu ya burudani.Kauli ya ZFA imekuja baada ya tukio la wiki iliyopita timu ya New Boko kudaiwa kumpiga mwamuzi hadi kuzirai katika mchezo wa kupanda daraja la kwanza.Katibu Mwenezi wa ZFA, Maulid Hamad Maulid amethibitisha kupokea taarifa za waamuzi na Kamisaa wa mchezo ambapo Kamati Tendaji itakaa wakati wowote kuanzia sasa ili kulijadili tukio hilo.Endelea kusoma habari hii

KERO ZA MUUNGANO ZAIBUKIA MICHEZONI

12 08 2010

KERO za Muungano zimeibukia katika sekta ya michezo bada ya chama cha Netiboli Zanzibar (CHANEZA) kullamika kuwa timu ya netiboti ya taifa haina sura ya muungano kutokana na wachezaji walioteuliwa kuwa wanatoka upande mmoja wa muungano.Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa chama hicho Rahima Bakari amesema timu ya taifa ya netiboli iliyoweka kambi katika shule ya Filbert Bayi haina wachezaji kutoka Zanzibar.Alisema wachezaji wote 34 waliopo katika kambi hiyo wameteuliwa bila ya kufuata taratibu kutokana na chaneza imetengwa katika utaratibu mzima wa kuwapata wachezaji hao.Endelea kusoma habari hii

KARUME BOYS YAELEKEA ERITREA

12 08 2010

TIMU ya soka ya Zanzibar chini ya mika 20 (U 20) Karume Boys imeondoka Zanzibar jana kuelekea Eritrea katika michuano ya Chalenji huku matumaini ya kushindwa yakiwa makubwa.Hali hiyo imetokana na maandalizi iliyopata kwa kipindi cha miezi miwili ikiwa ni pamoja na kuwekwa kambini nchini Misri ambapo pia ilicheza mechi kadhaa za kirafiki.Kati ya mechi hizo karume Boys ilishinda mechi 3 ikatoka sare mechi mbili na kupoteza mchezo mmoja ikiwa chini ya kocha raia wa Misri Abdelfatah Abbass.Endelea kusoma habari hii

KOCHA MZUNGU KUANZA KAZI SEPTEMBA

12 08 2010

KOCHA mpya wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Muingereza Stewart John Hall amepanga kuanza kutoa mafunzo kwa makocha wa Zanzibar kuanzia Septemba 3 mwaka huuKocha huyo amefunga mkataba wa kuinoa Heroes wa miaka mitano chini ya ufadhili wa kampuni za FCL ya Dar e salaam na GSB ya Marekani ikiwa ni pamoja na mafunzo ya makocha.Akizungumza na mwananchi kisiwani hapa katibu mwenezi wa ZFA Hamad Maulid Hamad alisema mafunzo hayo yatawahusisha makocha wa timu za ligi kuu na daraja la kwanza.Endelea kusoma habari hii

MAMA KARUME AIPA YANGA UBANI

15 04 2010

HOFU ya mpambano wa jadi imezidi kutanda baada ya timu ya soka ya Yanga kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya kufuata ubani kwa Mama Fatma Karume. Baada ya kuwasili jana asubuhi, walikwenda nyumbani kwa Mama Fatma Karume na walikuwa na mazungumzo mafupi kabla ya kurejea Dar es Salaam. Wakati Yanga wakivamia visiwani humo, tayari mahasimu wa Simba wapo huko kwa wiki mbili sasa wakijiandaa na mechi hiyo ya kihistoria. Simba inaendelea na mazoezi kwenye Viwanja vya Fuoni.Endelea kusoma habari hii.

TFF SIO WAUNGWANA- ZFA

16 03 2010

CHAMA Cha Soka Zanzibar (ZFA) kimesema hatua ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kuandaa timu ya taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20, kwa vijana wa Tanzania bara pekee si ungwana hasa katika wakati huu.Imeelezwa kwamba kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu na kanuni za makubaliano baina ya pande mbili hizo za vyama vya soka kati ya ZFA na TFF zinazochukuliwa kufuatia mzozo uliotokezea mwaka uliopita.Katibu Mwenezi wa Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA) Maulid Hamad Maulid amesema kuwa kitendo cha Shirikisho hilo wao wamekichukulia ni kama sehemu ya kuitenga Zanzibar na watu wake.Amesema kutokana na timu iliyoundwa ilikuwa inahitajika kuwa na wazanzibari waingizwe katika timu hiyo hata kama ni wawili lakini sio kukosekana kabisa.“Nashangaa timu imeundwa na tayari imeshaanza mazoezi hivi juzi, lakini sioni hata mzanzibari mmoja ndani ya kikosi hicho, na ilikuwa ni lazima awepo japo wachezaji wawili au hata mmoja lakini sio kuwa hakuna hata mmoja kutoka Zanzibar” alisema Maulid.Endelea kusoma habari hii

MAFUNZO KWENDA KENYA

10 03 2010

TIMU ya Soka ya Netiboli ya Mafunzo ya Wanawake imethibitisha kushiriki katika mashindano ya Kombe la Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika April 24 mwaka huu nchini Kenya. Akingumza na gazeti hili Katibu wa Michezo wa Mafunzo Makame Haji Fadau kuwa tayari timu yake imeshatuma uthibitisho wa maneno kwa chama cha Mchezo huo Zanzibar (CHANEZA), ambapo baadae itafuata barua rasmi ya kuthibitisha kwao. “Tumeshatuma barua ya maneno na hivi sasa tunajitayarisha kwa ajili ya kutuma barua ya maandishi kwa chama hicho”, alieleza katibu huyo. Hata hivyo alisema kwamba katika mashindano hayo wana imani kwamba timu yake itafanya vizuri zaidi, na kurejea na ubingwa na kuwataka wapenzi na wanachama wa timu yao kutokuwa na wasiwasi juu ya mashindano hayo. “Naamini kuwa vijana wangu wataweza kurudi nchini humu wakiwa na ushindi katika mashindano hayo kutomana na viwango vya kuonekana kuwa ni vizuri na kuwa tayari kwa ajili ya kimashindano” alisema Fadau.Hata hivyo Fadau alisema kuwa hivi sasa timu yake tayari imeshaanza mazoezi kujiandaa na mashindano hayo, ambayo amesema kwamba yatakuwa na ushindani mkali katika kunyang’anyia kikombe hicho.Endelea kusoma habari hii

RIADHA ZANZIBAR KWENDA KENYA

3 02 2010

TIMU ya Taifa ya Zanzibar ya Riadha inatarajia kwenda nchini Nairobi kwa ajili ya kushiriki mashindano ya mbio za nyika ya Afrika Mashariki na Kati.
Mashindano hayo ambayo yamepangwa kufanyika Febuari 27 mwaka huu, yameandaliwa na Shirikisho la mchezo huo Afrika Mashariki na Kati (EAAR).
Akizungumza na Mwananchi Katibu Mkuu wa chama cha riadha Zanzibar, Khamis Gulam alisema kuwa timu hiyo ya taifa inatarajiwa kuondoka nchini Febuari 24 mwaka huu ikiwa inaundwa na wachezaji 10 wakiwemo wanawake na wanaume, pamoja na viongozi watatu akiwemo na mwalimu mmoja.Gulam alisema kuwa tayari maandalizi kuhusu mashindano hayo yameshaanza lakini hakuwa tayari kuwataja wachezaji ambao watakwenda kushiriki mashindano hayo, kwa kile alichodai ni mapema mno kutoa orodha ya majina yao.Alisema kwamba kwa sasa ni mapema mno kuwataja wacheza hao, ila kwa sasa wamekusanya wachezaji 20 na wako katika hatua ya mwisho na wanaendelea na mchakato wa kutafuta wachezaji hao 10.Endelea kusoma habari hii

TUMEMUONESHA MAXIMO-SHAMHUNA

17 12 2009

WAZIRI wa Habari Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Zanzibar (SMZ) Ali Juma Shamuhuna, amesema kuwa pamoja na watanzania bara kuiita timu ya taifa ya Zanzibar Heroes ni wala urojo, lakini sasa wameitambua kuwa ni tishio kubwa katika medani za soka kutokana na kipigo walichowapa nchini Kenya .Alisema kuwa hali hiyo wameitambua mara baada ya vijana wa Zanzibar Heroes kuigandamiza timu ya Tanzani bara goli 1-0 katika kuwania ushindi wa nafasi ya tatu katika michuano ya Chalenj yaliomalizika hivi karibuni nchini Kenya.Shamuhuna ambaye pia ni Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar aliyasema hayo jana wakati akiipokea timu hiyoyenye wachezaji 19, pamoja na viongozi 9, mara baada ya kuwasili katika Bandari ya Malindi Unguja ikitokea Kenya kupitia jijini Dar-essalam wakati wa majira ya saa 6:45 za mchana.Alisema mkuwa ushindi uliopatinakana kwa timu hiyo umeweza kutoa funzo kubwa kwa Tanzani bara pamoja na kocha wao Marcio Maximo ambaye aliitambua kuwa Zanzibar ina kiwango kikubwa cha soka mara baada ya kupata kipigo cha mbwa.“Marcio Maximo ameweza kuitambua kuwa Zanzibar ina wachezaji bora na wa hali ya juu kimchezo kutokana na kipigo alichikipata kutoka kwa vijana wa Zanzibae Heroes
katika mashindano ya Chalenj katika hatua ya kuwani nafasi ya tatu katika mashindano hayo” alisema Shamuhuna.Endelea kusoma habari hii

SMZ YAAHIDI KITITA KWA ZANZIBAR HEROES

8 12 2009

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeahidi kutoa zaidi ya shilingi millioni 17 kuwazawadia wachezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’kabla ya timu hiyo kurejea nchini.Pia serikali imesema imefurahishwa na kipingo walichokionesha wachezaji wa timu ya Zanzibar Heroes kwa timu ya Zambia katika mashindano chalenji yanayoendelea nchini Kenya katika kinyanganyiro cha kutinga nusu fainaliza mashindano ya Chalenji.Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni naMichezo Zanzibar, Dkt. Omari Dadi Shajaak, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Migombani Mjini Unguja jana.Alisema fedha hizo ambazo zitatolewa kwa kila mchezaji atajinyakulia kitita cha dola 500, za kimarekani, huku kila kiongozi atazawadiwa dola 700, kama ni kifuta jasho cha kutinga nusu fainali.Alisema kuwa hatua iliyofikia timu ya Zanzibar Heroes kutinga nusu fainalini miongoni mwa ishara ya timu hiyo kuwa makini katika mafunzo waliyoyapata kutoka kwa Makocha wao katika kuhakikisha timu hiyo inafikia malengo yaliokusudiwa pamoja na kuitangaza Zanzibar katika medani za soka.“Ni dhahiri kuwa mafunzo waliyopata wachezaji wetu kutoka Makocha waona kuyafuata vilivyo ni njia moja wapo iliyowafanya kufanikiwa katika kutinga nusu fainal na tunatumai itafikia katika hatua za fainal na kurejea nchini na uhindi kabisa” alisema Shajak.Endelea kusoma habari hii

SIMBA YAAKHIRISHA KUJA ZENJ

7 12 2009

TIMU ya wekundu wa Msimbazi Simba, kutoka jijini Dar-es Salam ambao walitarajiwa kuwasili hapa kucheza mechi za kirafiki na timu za Zanzibar Ocean View na Polisi wamesema wameamua kusitisha ziara hiyo kutokana na kukabiliwa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Timu kutoka Uganda.Mwenyekiti wa Simba Fun Club Zanzibar, Mohammed Kajole, alisema kwamba amepokea taarifa kutoka kwa uongozi wa Simba jijini Dar-es-Salaam, kuwataarifu juu ya kuahirishwa kwa ziara hiyo.Kajole, alisema kwamba timu hiyo imepanga kucheza mechi hiyo ya kimataifa Disemba 9 mwaka huu siku ya Uhuru wa Tanzania Bara, na baada ya hapo ndipo watakapokuja hapa kucheza na timu hizo ili kujiandaa na kombe la Tusker.Mwenyekiti huyo wa Simba Fun Club, hapa Zanzibar, alisema ingawa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo walikuwa na hamu kubwa ya kuiona timu yao lakini wasivunjike moyo kwani mpango wa kuja bado upo pale ingawa itakuwa kwa siku chache tofauti na hapo mwanzo ambapo wangekaa kwa wiki mbili.Aidha alisema taratibu zote zilizopangwa awali ikiwemo utoaji wa kadi za wanachama wa Simba Fun Club, Zanzibar, itabaki pale pale na kwamba wale wanachama ambao bado hawajapata kadi mpya wajiandae kwa hilo.Endelea kusoma habari hii

MAXIMO ACHANGANYIKIWA CHALENJI

30 11 2009

KOCHA Marcio Maximo anajua atakuwa kwenye wakati ngumu zaidi kuliko kipindi chochote alichokaa Tanzania endapo kikosi chake cha Kilimanjaro Stars kitapoteza mchezo wa leo dhidi ya ndugu zao wa Zanzibar Heroes katika mechi ya kufa au kupona ya michuano ya Chalenji. Mbrazil alishudia Kilimanjaro Stars wakipokea kipigo cha mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya mabingwa watetezi, Uganda, The Cranes. Katika mchezo huo, Zanzibar ikishinda itakuwa imejihakikishia nafasi ya kuvuka hatua ya makundi huku Kili Stars ikibakiza saa chache za kuendelea kuishi mjini hapa ikishindwa kuvuka hatua hiyo ya awali ya michuano ya mwaka huu. Hii ni mara ya pili kwa timu hizo kukutana katika mchezo wa kuamua hatma yao, katika michuano hiyo iliyofanyika mwezi Januari mwaka huu nchini Uganda, Tanzania ilikwenda kwenye mchezo dhidi ya Zanzibar wakihitaji kushinda ili kufufua matumaini yao ya kusoga mbele kama ilivyo sasa. Katika mchezo huo uliochezwa mjini Kampala kwenye Uwanja wa Nakivubo, Kilimanjaro Stars ili shinda kwa mabao 2-1 shukrani kwa Danny Mrwanda na Athumani Idd, huku lile la kufutia machozi la Zanzibar likifungwa na Nadir Haroub ‘Canavaro’. Hali hiyo imemfanya kocha Maximo kusema kuwa hakuna shaka kwamba itakuwa ni kazi ngumu kwao hasa ikizingatiwa ukweli kuwa wachezaji wa timu hizo mbili wanajuana udhaifu, ubora.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAE HEROUS JUU CHALENJI

30 11 2009

TANZANIA imetupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya Chalenji mjini Mumais jana kwa matokeo ya furaha na uzuni kutoka kwa timu zake za Zanzibar Herous kuisambarati Burundi 4-0, huku Kilimanjaro Star wakilala kwa mabao 2-0 kutoka kwa mabingwa watetezi Uganda. Bao la mapema lilofungwa kwa kichwa mshambuliaji Owen Kasule akiunganisha krosi ya Godfrey Walusimbi dakika ya 2 ya mchezo lilitosha kuichanganya Kilimanjaro Stars walionekana kupwaye zaidi kwenye nafasi ya kiungo kabla ya Mike Serumaga kufunga bao la pili dakika 88. Viungo Tony Maweje na Senyonjo wa Craines alitawala sehemu ya kati na kuwachanganya kabisa Shabani Nditi, Juma Nyoso na kuwafanya wasionekana kabisa.Beki Nyoso alitolewa nje kwa kadi mbili za njano baada ya kumchezea vibaya Senyonjo huku awali akiwa ameunawa mpira makusudi hivyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Vita kuu katika mchezo huo ilikuwa ni kwenye winga ambao upande wa kushoto Juma Jabu alikuwa na kibarua cha kumzuia Danny Wagaluka, huku Shadrack Nsajigwa wakionyeshana na Steven Bengo wote ni wachezaji ya Yanga. Kili Stars iliuanza mchezo huo kwa kujilinda zaidi jambo lilokosesha amani kocha Marcio Maximo ambaye alikuwa akipiga makelele ya kuwawata wachezaji wake wasogee mbele.Endelea kusoma habari hii

MWENDESHA PUNDA ANYAKUA SHILINGI MILIONI 1

26 11 2009

KIJANA machachari wa kuendesha Punda anayetambulika kwa jina la Kiatu Ame amefanikiwa kukitia mikononi kitita cha shilingi 1,000,000 baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya mbio za Punda yaliyofanyika mjini Zanzibar. Kijana huyo ambae alikimbia kwa muda wa dakika 35:06 kumalisha mbio hizo za kilomita sita kutoka kiwanja cha Kibandamaiti hadi uwanja wa Maosetong. Nafsi ya pili ikikwenda kwa Makame Khamis, aliyetumia muda wa dakika 36:00 na kufaniiwa kujinyakulia kibunda cha shilingi 700,000. Mashindano hayo yaliyoteka mashabiki wengi, alishuhudiwa alishuhudiwa kijana Mwinyi Said akifutika shilingi 500,000 baada Punda wake kukamata nafasi ya tatu, huku akiwa nyuma ya kijana kiatu ambaye ni mshindi. Nafasi ya mshindi wa nne wa michuano hiyo, ilichukuliwa na Abdulla Khamis ambaye alijizolea shilingi 200,000. Washindi hao walikabidhiwa hundi za fedha hizo na mgeni rasmi Meya wa Manispaa ya Zanzibar Mahboub Juma. Meya huyo, aliwataka washiriki wa mashindano hayo kuwatunza zaidi wanyama wao, ili wawe na afya njema kwa ajili ya kushindanisha kwenye mashindano mbali mbali yatakayowashirikisha wanayama wao.Endelea kusoma habari hii

ZFA WASI WASI MTUPU UCHUKUAJI FOMU

26 11 2009

CHAMA Cha Soka Zanzibar (ZFA )Wilaya ya Kati, kimepata wasiwasi kutokana na kusuasua kwa zoezi la uchukuaji fomu za usajili kwa timu zilizoko wilayani humo. Katibu wa ZFA wa wilaya hiyo Mwandazi Zubeir Said, amesema chama chake kinashangazwa na mwamko mdogo walionao viongozi wa klabu za madaraja mbalimbali ambazo zinatarajiwa kushiriki ligi za wilaya hiyo mwakani. Said bado idadi ya timu zilizofika kuchukua fomu ni ndogo kulinganisha na wingi wa timu hizo, jambo linaloishangaza ZFA wilayani humo.Endelea kusoma habari hii

JUVENTUS YAINGIA NUSU FAINALI ZNZ

26 11 2009

TIMU ya Juventus ya Meli nne, imetinga fainali ya michuano ya Jimbo la Mwanakwerekwe baada ya kuiadhiri New Embassy ya Kwerekwe kwa mabao 5-3 kwa njia ya matuta. Miamba hiyo ilialazimika kusaka mshindi kwa penelti baada ya kuzitafuna dakika 90 wakiwa sare ya bao 1-1, huku kila timu ikinuwia kufa na kupona ili mkuweza kuutia mikononi ushindi wa pambano hilo . Pambano hilo la ‘Shamsi, Sereweji Cup’, lililopigwa katika kiwanja cha Magirisi, lilikuwa kali huku kila timu ikionesha dhamira ya kuvuka kizingiti hicho. Juventus iliyokuwa na baadhi ya nyota wa ligi kuu akiwemo Sabri Ramadhan ‘China‘ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao mnamo dakika ya 30 lililofungwa na Mohamed Makarani ambalo lilidumu hadi mapumziko. Wanaume hao walikianza kipindi cha pili kwa nguvu huku timu ya Embassy ikionekana kutawala mchezo huo kwa nia ya kutaka kusawazisha bao hilo ili kuondoa aibu kwa wapenzi wao.Endelea kusoma habari hii

KONDE YAPONGEZWA

26 11 2009

TIMU ya Jimbo la Konde, imemwagiwa pongezi kwa kuweza kutwaa ufalme wa mashindano ya soka kwa timu za majimbo kwa hapa Zanzibar mwaka huu yaliomalizika hivi karibuni. Pongezi hizo zimetolewa na uongozi wa timu ya jimbo la Fuoni ambayo ndiyo iliyokuwa ikiushikilia ubingwa wa mashindano hayo kwa kuubeba kwenye mashindano ya mwaka jana yaliyoshirikisha timu za Unguja pekee. Katibu wa timu ya Fuoni, Haji Issa Kidali, alisema ingawa timu yake imeutema ubingwa huo, timu ya Konde inastahili pongezi kwa kuonesha ujasiri kwenye mashindano hayo na kufanikiwa kuvaa taji hilo. Kidali alisema haikuwapitikia katika mawazo yao kwamba Konde ingeweza kufikia hatua ya kutwaa ubingwa, lakini inaonesha dhahiri jinsi vijana hao walivyokuwa wamepania tangu mwanzo wa ngarambe hizo. “Ingawa ubingwa huo umetoka mikononi mwetu, huo ndio mchezo, hatuna budi kuivulia kofia timu ya Konde kwa mafanikio hayo”, alisema Kidali. Mdau huyo alisifu hatua ya Konde kufungua ukurasa mpya katika medani ya soka kwa kuhimili vishindo vya michuano hiyo mbele ya timu nyengine kubwa, ambazo zinatajika kisoka hapa nchini.Endelea kusoma habari hii

WAPYA WAGOMEA MAZOEZI MIEMBENI

23 11 2009

WACHEZAJI wa timu ya soka ya Miembeni waliosajiliwa kutoka nje yaZanzibar, wameripotiwa kugomea mazoezi kwa kile kilichoelezwa kutokujua hatima na muelekeo sahihi katika usajili wao katika msimu ujao wa ligi kuu ya Soka visiwani Zanzibar.Habari za uhakika kutoka ndani ya timu hiyo, zimefahamisha kuwa, wakati wachezaji wengine wakifanya mazoezi, wageni hao walibaki kando wakifanya kikao na viongozi wa timu hiyo.Mmoja wa wachezaji wa kikosi hicho aliyekataa kutajwa jina lake gazetini, alisema wakati wakijiandaa kufanya mazoezi, wachezaji waliosajiliwa kutoka hapa nchini, walijikuta wakiwa peke yao huku wageni hao wakiangalia tu.“Kwa kweli sikufahamu kilichokuwa kikiendelea, lakini nilisikia wanataka kugoma kwa sababu wamekuwa wakihangaishwa juu ya hatma ya usajili wao”, alisema mchezaji huyo na kuongeza kuwa ukweli halisi wanaujua wenyewe.Hata hivyo, Meneja wa timu hiyo Abubakar Bakili, alikanusha kuwepo kwa mgomo huo akisema hakuna hata mchezaji mmoja aliyekuwa hajalipwa kwa ajili ya kusajiliwa, na wale wasiosajiliwa waelewe kiwango chao hakiridhishi.“Sikiliza, ukiona mchezaji hakusajiliwa katika timu hana kiwango, tumewaangalia viwango vyao na kuchukua wanaofaa, hao wadaodai kuachwa hawatufai watafute timu ziko nyingi”, alisema Bakili.Endelea kusoma habari hii

MUDA WA KUCHUKUA FOMU WAONGEZWA

23 11 2009

KAMATI ya Central Wilaya ya Mjini imeongeza muda wa uchukuaji wa fomu za usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuwa ambapo sasa utafikia kikomo chake mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba mwaka huu. Akizungumza na Mwanaspoti Katibu wa Kamati hiyo Kijo Nadir Nyoni alisema kuwa wameamuwa kuongeza muda wa uchukuaji fomu hizo baada ya klabu nyingi kutojitokeza kuchukuwa fomu hizo hadi hivi sasa.Alisema kuwa kati ya klabu 105 vilivyochini ya kamati hiyo mpaka sasa ni vilabu 65 ndivyo vilivyochukuwa fomu hizo kutoka madaraja tofauti, hali ambayo inaonesha ni asilimia ndogo ya vilabu shiriki viofika chamani na kuchukua fomu hizo.“Tumeona bora tuongeze muda kwani mpaka sasa tunavilabu 65 ndivyo vuilivyochukuwa fomu hizo wakati ukiangalia tunavilabu zaidi ya 100″, alisema katibu huyo.Hata hivyo alisema wakati muda huo utakapomalizika hawataongeza muda mwengine na klabu ambacho, hakitochukuwa fomu kitakuwa tayari kimejiondoa kwenye mashindano ya ligi inayoandaliwa na kamati hiyo.“Pindipo hadi mwisho wa mwezi huu kama kutakuna na baadhi ta timu bado hazijajitokeza na kuchukua fomu za usajili, basi chama kitasitisha zoezi hili na timu ambayo haijakamilisha utaratibu huo zitakuwa imejiondoa katika mashindano hayo msimu ujao” alisema Katibu huyo.Endelea kusoma habari hii

UWEZO NDOGO NI CHANZO CHA KUFANYA VIBAYA

23 11 2009

CHAMA Cha Mpira wa Mikono Zanzibar (ZAHA), kimesema sababu ya kufanya vibaya kwa timu za Zanzibar katika mashindano ya nchi za Afrika Mashariki na Kati, ni kuwa na uzoefu mdogo kwa timu hizo katika ushiriki wa mashindano hayo.Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Chama hicho Mussa Abdurabi, wakati akizungumza na Mwanaspoti, juu sababu iliyochangia timu za Zanzibar, kuharibu katika mchezo huo na kupelekea kuchukua nafasi za mwisho katika mashindano hayo yalimazizika hivi karibuni.Alisema hali hiyo kwa kiasi kikubwa inatokana na timu hizo kukosa ushiriki kwa kipindi kirefu katika mashindano hayo, hali ambayo inachangiwa na ukosefu wa kifedha kwa Chama cha Mikono Zanzibar (ZAHA) za kuanzisha mashindano ya kila mara kwa timu hizo.“Tunaweza kusema kuwa hali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa fedha kufanyia mashindano hapa nchini na wakati mwengine pia huwa tunakosa udhamini wa kwa timu zetu za ushiriki mashindano hayo wakati yanapofanyika katika nchi nyengine” alisema Katibu huyo.Hata hiyo katibu huyo alisema kuwa hali hizo kwa kiasi kikubwa zimechangia kuzifanya timu za Zanzibar kukosa kushiriki kikamilifu, kitendo ambacho kinaonesha wazi kuwa ndio sababu za kutokuwa na uzoefu wa kukutosha katika mashinmdano hayo na kukamata nafasi za mwisho.Endelea kusoma habari hii

SHAMHUNA AOTA ZNZ KUTAMBULIWA NA FIFA

23 11 2009

WAZIRI wa Habari,Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna, amesema ujio wa Kombe la Dunia Visiwani humu, inawezekana ikawa ni njia moja wapo ya kufunguka milango ya Zanzibar kwa kutambulika katika Shirikishho la Soka Duniani (FIFA).Alisema kuwa milango hiyo itakapofunguka basi ni matumaini yake kuwa Zanzibar, itaweza kulitwaa Kombe hilo wakati wa ushiriki wao katika mashindano ya soka ya dunia mwaka wowote.Shamuhuna aliyasema hayo jana mara baada ya kuwasili kwa Kombe la Dunia katika bustani mpya ya Forodhani Mjini Unguja, ambapo hapo palitengwa kuwa ni kifikio cha Kombe hilo hadi saa kumi na mbili za jioni ya jana kabla ya kombe hilo kurandishwa katika mitaa mbali mbali ya Zanzibar likielekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kurejea jijini Dar-es Salaam.Alifahamisha kuwa matuamini hayo yatakuwa makubwa sana pale Shirikisho la Soka Duniani litakapoipatia uanachama wa kudumu Zanzibar katika Shirikisho hilo.Hata hivyo Shamuhuna alisema kuwa ujio huo umeweza kujenga historia mpya Zanzibar kutokana na hii ni mara ya kwanza kifika kombe hilo visiwani humu na kushuhudiwa wa viongozi, wanamichezo pamoja na mbali mbali kwa macho yao.Alifahamisha kuwa ujio hu utaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuinua hamasa za wanamichezo kwa kuongewza bidii wakati wakiwa michezoni na hatimae kuinua vipaji vyao kwa haraka.Endelea kusoma habari hii

TUMIENI MASHINDANO HAYA VIZURI-SHAMHUNA

20 11 2009

WAZIRI wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna amewataka wanamichezo nchini kuyatumia mashindano ya Mapinduzi CUP kuwa ni njia moja wapo ya kuwaletea maendeleo ya kukuza vipaji vyao vya soka.Shamuhuna aliyasema hayo jana wakati wa makabidhiano ya hundi ya fedha ya shilingi millioni 25 za udhamini kutoka Kampuni ya Simu za Mkononi Voda Com kwa ajili ya mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi lake mwezi ujao visiwani Zanzibar.Makabidhiano ambayo yalifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliopo Kilimani Mjini Unguja, Shamuhuna alisema kuwa itakuwa si jambo la busara kwa wachezaji kupata udhamini huo kisha wao wakashindwa kuutumia kwa kukuza vipaji vyao.Sambamba na wito huo kwa wachezaji Shamuhuna aliipongeza Kampuni ya Voda Com kwa jitihada zake za kusaidia katika fani za michezo hapa nchini hatua ambayo inaonesha dhamira yeke na lengo la kukuza na kuviendeleza vipaji vya vijana hasa wale wenye kuinukia katika michezo.Alizidi kusema kuwa jitihada za kampuni hiyo zinaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa wanamichezo kupata fursa ya kuchezea soka katika vilabu vya nje ya nchi, ambalo ni soka la kulipwa.Endelea kusoma habari hii

WEKEZENI KATIKA MICHEZO-KARUME

19 11 2009

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume amesema kuwa mafanikio yaliopatikana katika michezo hapa Zanzibar yanatokana na mashirikiano ya pamoja na kusisitiza kuwa ipo haja ya kuekeza zaidi katika miundombinu ya michezo.Rais Karume aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipokuwa na mazungumzo na wanamichezo wa Zanzibar walioshiriki michezo mbali mbali na kuibuka washindi katika mashinado ya ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kuwakabidhi zawadi alizowaandalia.Katika maelezo yake, Rais Karume alieleza kuwa ni jambo la faraja kwa vijana kuendeleza utamaduni wa michezo hapa Zanzibar kwani kuna historia refu ya michezo hatua ambayo imejenga uhusiano, maelewano, ushirikiano mzuri. Hivyo alitoa wito kwa vijana kufuata kanuni, taratibu na nidhamu katika michezo ili wapate mafanikio zaidi.Rais Karume alisema kuwa michezo ni kiungo kikubwa cha kujenga umoja na mshikamano katika jamii hivyo juhudi zilizochukuliwa na vijana hao za kuendeleza michezo mbali mbali na hatimae kushinda na kupata medali za aina zote ni za kujivunia.Aidha, Rais Karume alisema kuwa mafanikio katika sekta za maendeleo ikiwemo michezo hapa Zanzibar yameweza kupatikana kutokana na kushirikiana kwa pamoja katika kutatua changamoto mbali mbali zilizokuwepo.Endelea kusoma habari hii

MSHINDANO YA AFRIKA MASHARIKI YAPATA MSIBA

19 11 2009

KATIBU Msaidizi wa Shirikisho la mpira wa Mikono Tanzania (TAHA) Keptein Sudi Omari, amefariki dunia juzi akiwa visiwani Zanzibar katika usimamizi wa mashindano ya mchezo huo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati yanayoendelea kutimua vumbi.Kifo cha Ketpein Sudi kilitokea juzi majira ya saa tatu za usiku akiwa katika Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja, ambapo hadi sasa bado hakuna kauli yoyote inayothibitisha kutendeka kwa ubaya juu ya kifo chake.Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Mikono Tanzania (TAHA), Nicolas Mihayo, alisema kuwa kifo cha keptein Sudi, ni kifo ambacho kilitokea ghafla bila ya hata kuugua na homa ya muda mrefu au kuugua na kiiungo chake kimoja.Nicolas alifahamisha kuwa awali jioni ya juzi Keptein Sudi walikuwa naye pamoja katika usimamizi wa mashindano hayo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja, hadi saa kumi na moja za jioni, ambapo hapo waliondoka pamoa na Keptein Sudi na kuelekea katika Hoteli ya Bwawani ambayo ilikuwa ni mafikio katika kipindi chote cha mashindano.Endelea kusoma habari hii

JKU WALAZWA CHINI NA MAGEREZA BARA

19 11 2009

TIMU ya Magereza Wanaume kutoka Tanzania Bara inayoshiriki michuano ya Mpira wa Mikono (Hand ball) kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, imezidi kuwa na matumaini na mashindano hayo baada ya jana kuwalaza maafande wa JKU, kutoka Zanzibar kwa magoli 38-26.Katika mchezo huo ambao ulikuwa na shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu ya JKU, ambao walifika kiwanjani hapo kwa kuishuhudia timu yao inavyofanya manyanga katika mashindano hayo.Hata hivyo vijana wa Magereza hawakushtuka na kidedea hicho wanachomwagiwa vijana wa Zanzibar, ila wao walizidisha bidii katika mchezo na kufanikiwa kuiumbua timu ya JKU bila ya huruma.Pamoja na mchezo huo lakini pia kulikuwa na mchezo kati ya JKT na Cersals kutoka nchini Kenya timu ambazo ni za Wanawake, lakini mchezo huo ulimilikiwa vyema na maanti wa Kenya kwa kuwapachika JKT, jumla ya magoli 26-12.Nayo timu ya Difence kutoka Ethiopia waliwazawadia vijana wa Nyuki ya Zanzibar magoli 23-23, mchezo ambao ulikwenda sambamba na mchezo wa Cersals kutoka Kenya ya Wanaume kwa kuwaifunga timu ya Ruwey kutoka Congo DRC, kwa magoli 33-31.Hata hivyo vijana wa kiume wa Black Mamba kutoka Kenya waliwaliwararua maafande wa JKU, wa Zanzibar kwa magoli 24-20, huku wanadada wa Magereza wakiwatundika vibaya mabanati wenzao wa Krikos wa Ethiopi magoli 26-16.Endelea kusoma habari hii

ZANTEL YAJITOA UDHAMINI ZNZ

19 11 2009

KAMPUNI ya Simu za Mkononi Zantel, imetangaza kujitoa katika udhamini wa ligi kuu ya Soka Zanzibar msimu ujao wa ligi kuu inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani 2010.Katika taarifa fupi ya Kampuni hiyo iliyotumwa kwa Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA) uamuzi huo umefikiwa baada ya tathmini ya kina ya uongozi wa Zantel juu ya udhamini wake huo. Kampuni hiyo iliyokuwa ikidhamini ligi kuu kwa misimu miwili iliyopita, imesema haina tena dhamira ya kuendelea na udhamini huo kwa ligi ya mwaka ujao.Haikuelezwa kwa undani sababu za msingi za kujitoa huko zaidi ya uongozi huo kuiambia ZFA kwamba iko huru kutafuta mdhamini mwengine kubeba mashndanio hayo mwakani.Katibu Mkuu wa ZFA Mzee Zam Ali alisema chama chake kimeshtushwa na uamuzi huo, akisema umekuja ghafla huku kukiwa kumebakia muda mchache kabla kuanza kwa ligi ya mwakani.Hata hivyo, alisema ZFA inajipanga kutafuta mdhamini mwengine na kwamba imeanza mazungumzo na baadhi ya kampuni ingawa hakuwa tayari kuzitaja akisema bado ni mapema.Endelea kusoma habari hii

KOMBE LA HIJJA SALEH KUANZA MWEZI HUU

19 11 2009

MASHINDANO ya Mpira wa Kikapu kumsaka Bingwa wa Zanzibar yajulikanayo kwa jina la ‘Karume CUP’ yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba katika kiwanja cha Gymkhana Mjini Unguja.Taarifa za Kamati ya michuano hiyo, zimemtaja Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Haroun Ali Suleiman, kuwa ndiye atakaeyafungua mashindano hayo ambapo yeye atakuwa ndie mgeni rasmi.Mwenyekiti wa mashindano hayo, Abdallah Hassan aliwatoa wasi wasi mashabiki wa mchezo huo, akisema baada ya kimya kirefu cha kukosa burudani sasa michuano hiyo imeiva na kuwataka kujitokeza kwa wingi kiwanjani kuzishangilia timu zao.Aidha alisema Mke wa Rais Mama Shadya Karume, ataendelea kuyafadhili mashindano hayo kama alivyofanya katika miaka minne ya awali.Hassan alisema jumla ya timu 20 zikiwemo 14 za wanaume na sita za wanawake, zimethibitisha kushiriki kinyang’anyiro hicho kinachosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo huo unaovuta hisia za watu wengi.Endelea kusoma habari hii

VIJANA WA ETHIOPIA WATAMBA AFRIKA MASHARIKI

18 11 2009

MASHINDANO ya mpira wa mikono (Hand ball) kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati yamezidi kupamba moto, ambapo vijana wa kiume kutoka nchini Ethiopia wanaonekana kutamba zaidi katika ngarambe hizo za aina yake.Ethiopia imezidi kuonesha kiwango cha hali ya juu baada ya kuwagandamiza vijana wa Miti Ulaya kutoka Kisiwani Pemba kwa magoli 35-4 mchezo ambao uliwafanya watu wa visiwani kutoamini kipigo hicho kwa ndugu zao hao.Katika mchezo mwengine timu ya Magereza Wanaume kutoka Tanzania Bara iliweza kuchezeshwa mchaka mchaka na timu ya Black Mamba kutoka nchini Kenya kwa kupachikwa magoli 35-32 bila ya huruma.Hata hivyo katika pambano jengine timu ya JKU, Wanaume kutoka Zanzibar imeanza kuona mwezi kwa kuwatundika vijana wa Rwanda kwa magoli 27-25, mchezo ambao umeanza kutoa sura ya matumaini kwa mashabiki na wapenzi wa visiwani Zanzibar.Kwa upande wa timu za Wanawake timu ya Ngome kutoka Tanzania Bara imeweza kufanikiwa kuwacharaza vijana wa timu ya Krikos kutoka Ethiopia kwa magoli 27-12, mchezo ambao ulimilikiwa zaidi na timu ya Ngome.Endelea kusoma habari hii

TIMU ZA ZANZIBAR ZACHAPWA VIBAYA

17 11 2009

MICHUANO ya mpira wa mikono (Hand ball) kwa nchi ya Afrika Mashariki na Kati, imezidi kupamba moto huku timu za Zanzibar zikiyajutia mashindano hayo moyoni mwao kwa kukubali kuwa mwenyeji kutokana na kipigo kikali wanachokipata kutoka kwa wageni wao.Katika ngarambe hizo vijana wa Zanzibar wamezidi kucharazwa vikali ambapo timu ya wanadada ya maafande wa wenye dhamana ya fedha Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar walipata sulubu ya kuangushiwa magoli 22 -8, kutoka kwa timu ya Krikos kutoka nchini Ethiopia.Wakati wana dada hao wakichapwa bila ya huruma ndugu zao wa Nyuki Wanaume wakipata adhabu isiyo na muombolezaji ya magoli 35-20 kutoka kwa timu ya Cerel inayotokea nchini Kenya.Wakati vijana wa Zanzibar wakipata kipigo hicho timu ya Ngome ikilala vibaya kwa kupata kipigo cha magoli 35 kwa 20 kutoka kwa ndugu zao wa Magereza zote zikiwa zinatokea Tanzania bara.Endelea kusoma habari hii

AFRIKA MASHARIKI KUTIMUA VUMBI

17 11 2009

BURUDANI za mashindano ya mpira wa mikono kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati zimeanza kutimua vumbi visiwani Zanzibar, ambapo jumla ya timu 42, kutoka nchini 14, kutoka nchi hizo zinashiriki ngarambe hizo.Mashindano hayo ambayo yameanza kufungua pazia lake vibaya kwa upande wa timu ya KMKM kutoka Zanzibar katika fungua dimba iliweza kupata kichapo mwanana cha magoli 30-13, kutoka kwa maafande wa Magereza wa Kiwira ya Tanzania Bara.Katika ufunguzi huo timu ya KMKM, ilikuwa imezidiwa wakati wote wa mchezo, huku vijana wa kiwira wakionesha uwezo mkubwa wa kutwaa ushindi wa mchezo huo, kutokana na kikosi chao kuwa cha kuvutia na kujaa kila aina ya fani kwa wachezaji wake.Hata hivyo, licha ya timu ya KMKM, kuwa na uwezo mdogo dhidi ya vijana wa Kiwira, lakini hawakutakaa kukubali matokeo yao kuwa mabaya zaidi, bali walizidisha ulinzi ili kuweza kuepukana na kipigo kikubwa.Hadi mwisho wa mchezo huo Kiwira imetoka nje ikiwa na ubabe wa kuikandamiza timu ya KMKM kwa jumla ya magoli 30-13, na kuifanya kutoamini kipigo hicho ambacho hawakukitegemea kwa siku hiyo.Endelea kusoma habari hii

MPIRA YA MIKONO NOVEMBA MWAKA HUU

10 11 2009

MASHINDANO ya mpira wa mkono (Hand ball), kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake rasmi November 15, mwaka huu visiwani Zanzibar.Mashindano hayo ambayo yatashirikisha timu za wanawake na wanaume ambapo timu za wanawake zitakuja nne na timu za wanaume ambapo congo pekee italeta timu za wanawake.Kitimtim hicho ambacho hadi sasa kinaonesha nia nzuri ya kufanyika Zanzibar ambapo nchi pekee itakayoshiriki kutoka nje ya Tanzania ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amabyo itakayotoa idadi kubwa ya timu inatarajiwa kushiriki kikamilifu kwa kuja na timu nne kutoka kwao.Kenya ikidhamiria kuingiza vikosi vyake vinne visiwani humu, ambapo jirani zao wa Uganda wao wakisema watatoa timu tatu tu za vijana ili kuja kushiriki.Hata hivyo kwa nchi ya Burundi wao wamesema mwaka huu hawatokuwa na timu nyingi zitakazowakilishi mashindano hayo ila watayawakilisha mashindano hayo kwa timu moja tu.Nao wana Ruwanda wameahidi kutoa timu tatu tu, ambazo zitashiriki katika mashindano hayo, huku Congo Brazaville, ikija nchini na timu moja.Endelea kusoma habari hii

RAIS KUZINDUA TIMU ZA VIKOSI ZNZ

7 11 2009

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid karume1Karume leo (Jumapili) anatarajiwa kuzindua mashindano ya soka kwa timu za vikosi vya ulinzi na usalama yanayofanyika katika viwanja vya Ziwani Mjini Unguja.Mashindano hayo ambayo ndio mara ya kwanza kufanyika visiwani humu kwa vikosi hivyo yamepewa jina la ‘Ujirani mwema’ kwa lengo la kudumisha umoja na ushirikiano baina ya walinzi hao.Akizungumza na gazeti hili Katibu wa kamati ya mashindano hayo Nassor Salum (Jazira), kuhusiana na mandalizi ya ngarambe hizo, alisema kuwa tayari wameshakamilisha mipangilio yote hadi hivi sasa kinachosubiriwa ni dakika za kuanza kwa ngrambe hizo tu.Nassor alisema kuwa katika matayarisho hayo tayari wameshafanikiwa kupata zawadi za washindi wa mashindano hayo, ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shiling 500,000, huku wa pili akiondoka na shilingi 300,000 na mshindi wa tatu ataangukia shilingi 200,000.Hata hivyo katibu huyo alisema kuwa mbali na zawadi hizo lakini pia kutakuwa na medani kwa washindi hao ambazo tayari zimeshakabidhiwa kwa kamati ya mashindanmo hayo kutoka kwa wadhamini wake.Endelea kusoma habari hii.

ZFA NA MIKAKATI YA KUPAA KIHABARI

6 11 2009

CHAMA Cha Soka Zanzibar (ZFA), kimetangaza siku moja maalum ya kila mwezi kuwa viongozi wa chama hicho watakutana na waandishi wa habari ili kuweza kuzungumza nao juu ya mustakabali wa soka unavyoenelea hapa nchini.Mpango huo umeelezwa kuwa utafanyika kila ifikapo tarehe 15 ya kila mwezi ambayo itakuwa ni siku maalum kwa waandishi kufika katika chama hicho kwa lengo la kupata ufafanuzi zaidi juu ya kila jambo lililotokezea ndani ya chama hicho.Tangazo hilo limetolewa mbele ya waandishi wa habari na Makamo wa Rais wa chama hicho Haji Ameir, huko afisini kwake Bwawani Mjini Unguja ambapo aliwataka waandishi wa habari kuweza kuuliza maswali mbali mbali juu ya chama hicho na michezo nchini.Alisema wameamua kutanga hivyo ili kulifanya soka la Zanzibar, kutambulika zaidi kwa wadau na wapenzi kupitia vyombo vya habari kwani vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika jamii na bila ya shaka kupitia mchakato huo soka nchini itaimarika na kutaweza kupatikana tija ndnai yake.“Wadau wengi wamekua wakilalamika juu upataji wa habari za ukuaji wa soka hapa nchini kutoka ndani ya chama chetu hivyo hatua hii tunaamini kuwa itasaidia kwa kiasi kikubwa wapenzi kusikia taarifa mbali mbali na mambo ambayo yanendelea katika chama chetu” alisema.Hata hivyo alifahamisha kuwa sasa ni kipindi kirefu soka la hapa nchini limekuwa likisuasua, jambo ambalo linachangia ukosefu wa maendeleo hadi leo na hivyo kuahidi suala hilo kushughulikiwa.Endelea kusoma habari hii

ZAHA YALILIA UKATA WA FEDHA

6 11 2009

UONGOZI wa Chama Cha Mpira wa Mikono Zanzibar (ZAHA) umesema matatizo yanayokikabili chama hicho ya kukosa msukumo wa kifedha katika mchezo huo kwa kiasi kikubwa unachangia kutokuwepo kwa timu nyingi nchini.Katibu wa Chama hicho, Mussa Abdurabbi, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa hivi karibuni, juu ya vitendo vinavyochangia kuwepo kwa vilabu vichache nchini.Alisema kuwepo kwa hali inasababisha kuwepo kwa vijana wengi ambao wanataka kujiunga na mchezo huo kukata tamaa nao kutokana na ukosefu wa udhamini wa vifaa vya kucheza mchezo huo.“Wapo vijana wengi wanataka kujiunga na mchezo wetu lakini kutokana na ufinyu wa wafadhili wa kuwapatia vifaa ndio sababu kuu inayowafanya vijana hao kutokuwa na hamu na mchezo huu””alisema.Hata hivyo alifahamisha kuwa hali hiyo mara nyingi pia huwa ni sababu moja wapo ya vijana kutojitokeza kwa wingi na kuanza kuunda timu zao ili kuweza kushiriki vyema katika mchezo huo.“Wanamichezo wengi wanataka kuunda timu za mchezo huo lakini wanashindwa kutokana na wimbi kubwa la wadhamini limeelemea katika mchezo wa soka tu, na sio katika michezo mengine na hili ndio tatizo “alisema katibu huyo.Endelea kusoma habari hii.

OCEAN VIEW YAPATA MWALIMU WA SWEDEN

6 11 2009

KLAB ya Soka ya Zanzibar Ocean View inayoratajiwa kushiriki ligi kuu mwakani imemtambulisha rasmi kocha mpya kutoka nchini Sweeden, atakayekinoa kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.Kocha huyo anayetambulika kwa jina la Henrik Lindberg, awali alikuwa nchini Tanzania na kampuni ya Civil Siciety Project, inayojishughulisha na uinuaji wa vipaji kwa vijana katika soka.Katika kipindi alichokaa nchini Tanzania kisichopungua mwaka mmoja kocha huyo alifanikiwa kuinua vipaji vya vijana katika mchazo wa mpira wa miguu katika mikoa mbali mbali ikiwamo Tanga na Kisiwani Pemba.Kabla ya hapo kocha huyo alikuwa nchini Sweden pamoja na Norway kwa zaidi ya miaka kumi kwa kazi kama hiyo kwa vijana wan chi hizo ambapo amekuwa akiwafundisha vijana katika kuendeleza mchezo huo.Mapema akimtambulisha kocha huyo katibu wa timu hiyo, Hashim Salum, alisema kuwa wameamua kumchagua kocha huyo kukifunza kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao“Tumeamua kumuwinda kocha huyo kwa kutambua kuwa anaweza kuifikisha timu yetu katika medani ya kutambulika kimchezo na si vyenginevyo tunajua uwezo wake ni mkubwa katika michezo:”alisema.Endelea kusoma habari hii

WADAU SAIDIENI TIMU ZENU ZISHINDE-ZFA

3 11 2009

CHAMA Cha Soka Zanzibar (ZFA) kimesema wakati umefika kwa wadau kuzisaidia timu za taifa ili kuziwezesha kushiriki vyema katika mashindano mbali mbali nchini.Chama hicho kilisema wadau hao wasisubiri timu hizo kutwaa ubingwa tu na ndio hapo waanze kizishangalia na kuaza kuzisifi timu na viongozi kwa uhodari wao hadi kufanikisha ubingwa huo bali wafanye juhudi zaidi katika kukabiliana na ushindi huo.Kauli hiyo imetolewa na Makamo wa Rais wa Chama hicho, Alhaj Haji Ameir, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Bwawani Mkoa wa Mjini Unguja.Alisema wadau wa michezo wengi wao inaonesha dhahiri kuwa hawana uzalendo na timu zao wala nchi yao kutokana na timu hizo huiwakilisha nchi na sio watu maalum lakini wengi wao wanaonekana kushangilia watu bianfsi badala ya timu.Makamo huyo alisema kuwa mara nyingi wadu wa soka hapa nchini wamekuwa wagumu katika kuunga mkono harakati za kuzisaidia timu za taifa, ila wadau hao hujivunia sifa pindi timu hizo zikifanya vizuri.Endelea kusoma habari hii

MPIRA WA WAVU HADI MASHULENI

2 11 2009

CHAMA Cha Mchezo wa Mpira wa Wavu Zanzibar kimesema kimo katika mikakati maalum ya maandalizi ya kuufikisha mashuleni mchezo huo ili kuweza kuibua vipaji bora.Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Chama hicho, Amani Muhammed wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko Ziwani Mjini Unguja kufuatia mikakati malum ya chama hicho.Alisema kuwa wameamua kuingia mashuleni ili kuweza kuufanya mchezo huo kutambulika kama ilivyo michezo mengine, ikitamba kwa umaarufu mkubwa ambapo mchezo maarufu kwa sasa ni mpira wa miguu.“Michezo mingi imekuwa ikitamba kwa umaarufu kutokana na michezo hiyo kupata bahati kubwa ya washiriki, hivyo nasi tukaona ipo haja sasa kuingia ndani ya shule ili kupata vipaji vitakavyotufanyab kutambulika” alisema.Katibu huyo alizidi kufahamisha kuwa ni matumaini yao makubwa kuwa mashuleni wataweza kuibua vipaji kama walivyokusudia, kutokana na wanafunzi hupatikna kwa muda mwingi tofauti na watu wa mitaani.“Wachezaji wengi wa mitani huwa tunawakosa kutoknn a hali zai z kimaisha, hivyo tunaamini wazi kuwa tukiingia mashuleni tutaweza kufanikiwa kuwanao wanafunzi kwa muda mwingi michezo “alisema katibu huyo.Endelea kusoma habari hii

FIFA YAITHIBITISHIA ZNZ KOMBE LA DUNIA

29 10 2009

SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limeithibitishia Zanzibar kuwa ni (0)miongoni mwa miji ambayo itayopata bahati ya kutembelewa na ziara ya kombe la dunia kwa mwaka 2009 inayodhaminiwa na Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola.Kauli ya shirikisho imetolewa na Meneja masoko wa kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola Afrika Mashariki na kati tawi la Tanzani Ritta Tsehai, wakati akizungumza na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Hotel ya Zanzibar Ocian View ilioko kilimani Mjini Unguja ambapo alisema uamuzi wa shirikisho hilo umekuja kufuatia kuonekana kwa amani, nidhamu na kiwango kizuri cha soka kwa wananchi wa visiwa hizi.Ritta alisema kuwa uamuzi wa shirkisho la soka duniani wa kulifikisha kombe la dunia visiwani humu ulikuwa ni mgumu sana , kutokana na shirikisho hilo tayari lilikuwa limeshatoa ratiba nzima ya ziara ya kombe hilo tangu mwaka jana.Hivyo kutokana na jitihada za Coca Cola, pamoja na historia nzuri ya watu wa Zanzibar, ya kuliomba shirkisho hilo kuifanya ziara hiyo hadi Zanzibar, shirkisho hilo liliweza kukubali kwa urahisi.“Coca cola ikiwa ni mdhamini wa mashindano ya Taifa ya vijana ya Copa Coca Cola, mwanzoni mwa mwaka huu ilifurahishwa kuona timu ya Mji Unguja ikitawazwa kuwa bingwa wa michuano hiyo, nao wakaona ni vyema kuipigia kelele ziara ya kombe la dunia ifike hadi Zanzibar” alisema.Endelea kusoma habari hii

TUTATUMIA KAMBI YETU VYEMA-SIMBA

28 10 2009

gTIMU ya soka ya Simba ya jijini Dar-es Salam, ambayo ipo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kujipiga msasa katika kuendelea na ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, imesema itaitumia vyema kambi hiyo kwa kuhakikisha kiti cha uongozi wa ligi hiyo unabakia katika mikono yao milele. Akizungumza na gazeti hili Meneja wa timu hiyo Innocent Njovu, alisema kuwa ni matumaini yao makubwa kuwa kambi yao hiyo wataotumia katika misingi mema kama ilivyo dhana kuu uongozi. “Ni matarajio yetu makubwa kuwa kambi yetu hii ya Zanzibar tutaitumia vizuri katika kipindi chote na hatimae kwa ajili ya matumaini ya kukimata kiti cha uongozi wa kitimtim cha ligi kuu ya Tanzania bara”alisema Njovu. Njovu alizidi kufahamisha kuwa wanafaraja kubwa kwa timu yao hiyo kufunga kambi kwa mara nyengine katika visiwa vya Zanzibar, kutokana na mazingira ya visiwa hivi kuwa ni mazuri. “Tumeona ni bora kufunga kambi kule kule Chuo Cha Chukwani Zanzibar, kutokana na mazingira yake kuwa ni mazuri na ya kuvutia, lakini pia mazoezi yetu yatakuwa muda wa jioni na asubuhi”alisema. Hata hivyo wachezaji wawili wa kikosi hicho akiwamo Nurdin Bakari pamoja na Haruna Moshi, wanatarajiwa kuwasili jioni ya juzi wakitokea jijini Dar-es Salam ambao wataungana na wenzao 26, katika kambi ya mazoezi.Endelea kusoma habari hii

WAFUNDISHENI VIZURI WACHEZAJI-NAHODHA

28 10 2009

WAZIRI Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha, amesema itakuwa nia aibu kubwa kwa makocha kuwapa mafunzo vijana Boniface%20Ambanitangu wadogo, lakini wakichaguliwa kwenda timu za Taifa vijana hao kupewa mafunzo mapya ya kuanza kupiga mpira vizuri. Waziri Shamsi aliyasema hayo juzi wakati akifungua Mashindano ya Majimbo yaliofanyika huko katika dima la uwanja wa la Mao Dzedong, Mjini Unguja, Alisema kuwa si jambo la kufurahisha hata kidogo kwa makocha kufanya kazi kubwa kwa vijana wao wadogo kisha vijana hao wakatolewa kaosa yasio na maana katika kulisakata kabumbu. “Itakuwa ni aibu kubwa kwa wachezaji wafunzwe kwa kipindi kikubwa kisha wakichaguliwa katika timu za Taifa wapewe mafunzo hayo hayo baada ya kupewa mafunzo mengine ya mbinu mpya ya soka” alisema Nahodha. Hivyo alifahamisha kuwa ipo haja kubwa kwa makocha kuitumia nafasi hiyo ya mashindano ya majimbo kwa kuwangarisha vijana wao ili kuweza kuwa mfano mwema pindi vijana hao wakichaguiliwa katika timu za taifa. Sambamba na hilo Nahodha, alisema kuwa ni jambo la kushangaza sana kwa baadhi ya Klabu ambazo zinashiriki ligi kuu, katika usajili wake kukimbilia wachezaji kutoka nchi za Nje hali ya kuwa ndani ya visiwa hivi wapo wenye sifa nzuri sana na wa kuvutia mashabiki.Endelea kusoma habari hii

MAFUNZO KUTANGAZA KIKOSI CHAKE

28 10 2009

maximongassaMABINGWA wa soka visiwani Zanzibar timu ya Mafunzo tayari imetangaza kikosi chake kipya kwa ajili ya ligi kuu msimu ujao pamoja na mashindano mengine mbali mbali wanakayokabiliana nayo. Kikosi hicho ambacho kitawajumuisha jumla ya wachezaji 32, ambao wanatarajiwa kuwa ni tisho kubwa katika usajili wao kutokana na kikosi hicho hivi sasa kuwa tishio visiwani humu . Katibu wa timu hiyo Makame Fadau, alisema kuwa ni matarajio yao makubwa kuwa kikosi hicho cha wachezaji 6, wepya pamojan na 26 wale waani katika msimu huu kitarudisha tena heshma ya timu hiyo. “Kikosi ambacho tumekifanyia usajili katika kujiandaa na ligi msimu ujao pamoja na mashindano mengine tunatarajia kuwa cha aina yake kwa kurejesha heshma kubwa katika timu yetu” alisema Fadau. Hata hivyo Fadau alikitaja kikosi hicho kuwa ni pamoja na mchezaji mpya ambae ni mlinda mlango Ramadhan Ali “Chachala” aliyeachwa na klabu ya KMKM.Wachezaji wengine ni ni Majid Shaaban ( New Boko)Wahid Chinga(JKU) Ali Bajaka (Jamhuri) Hussein Rashid (Miembeni) na Ali Abdallah (KVZ).Endelea kusoma habari hii

 

KUWENI NA UMOJA – NAIBU WAZIRI

28 10 2009

NAIBU Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo amewataka viongozi wa mchezo wa Wavu (Voliball) bwana kifupiZanzibar kushirikiana kwa pamoja hadi kuhakikisha mchezo huo unatambulika kama ilivyo michezo mengine. Naibu Mahmoud aliyasema hayo jana wakati akifungua Bonanza maalum kwa Mchezo huo kanda ya Mjini Unguja, lililofanyika huko uwanja wa Mwembe Kisonge. Alisema wakati umefika kwa viongozi wa mchezo huo kuacha tafauti zao ambaya katika mchezo huo na badala yake kushikamana katika kuinua vipaji vya wanamichezo hapa Zanzibar. “Ni vyema kwa wenye tofauti katika mchezo huu sasa wakaziwachilia mbali ili kuweza kuwa pamaoja na kuhakikisha kuwa wanatoa wanamichezo bora wenye kutambulika ndani na nje” alisema. Hata hivyo alifahamisha kuwa sasa ni muda mrefu sana tangu mchezo huo hapa Zanzibar kuchezwa, lakini bado matunda ya mchezo huo hayajaonekana kwa wapenzi na mashabiki wake.Endelea kusoma habari hii

KOMBE LA HIJA SALEH KUANZA TENA

28 10 2009

kombKITIMTIM cha michuano ya soka ya kombe la Hijja Saleh, inatarajiwa kuendelea katika mzunguuko wa pili Oktober 26 Visiwani Zanzibar, baada ya timu kuwa mapumzikoni kwa kumalizika mzunguuko kwa kwanza. Mzunguuko huo wa pili utarajiwa kuzikutanisha jumla ya timu nne, ikiwamo Leeds ambayo itakwaruzana na vijana wa timu ya Kishoka huko katika dimba la uwanja wa Misuka. Huko vijana wenye kula embe bila ya kuzijua hesabu yake kutoka Bungi watatia hamkani na vijana wa timu ya Kivumbi, pambano ambalo litachezwa katika dimba la uwanja wa Bungi Wilaya ya kati Unguja. Mashindano ya kumuenzi Muasisi wake Hija Sale na kupewa jina lake yanazishirikisha jumla ya timu sita ambazo ni mabingwa kutoka Wilaya zote za Unguja tu, Pamoja na mashindano hayo ambayo mwaka jana yalifanyika kwa kushirikisha kombaini za wilaya kumi za Zanzibar,mwaka huu yameamuliwa kushirikisha klabu bingwa za wilaya sita za Unguja pekee. Huko kisiwani Pemba mashindano hayo bado yana kitandawili cha kufanyika vyeama kwa kukosa mdhamini wa kuyapa tafu kuanzia mwanzo hado mwisho, ingawa wao wenyewe wanamichezo wa huko kuamua kucheza mashindano hayo. Hata hivyo Katibu wa Central Taifa Hussein Ali Ahmada, alisema kuwa licha ya kuwa michuano hiyo itachezwa katika vituo viwili tofauti.Endelea kusoma habari hii

VILABU WATAKIWA KUWA WASTAARABU

28 10 2009

mayVILABU vya Soka nchini hususan vinavyoshiriki ligi kuu Zanzibar, daraja la Kwanza Taifa na Taifa, vimetakiwa kujaribu kuwa na ustaarabu wakati wanapohitahi kuchukuwa wachezaji kutoka ngazi za chini. Vilabu hivyo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa zaidi na vilabu vinavyolea vijana kutokana na tabia ya kuchukuwa wachezaji huku wakishindwa kuwajali walezi hao.Akizungumza na gazeti hili Katibu wa timu ya Syria inayoshiriki ligi ya daraja la Central, Mohammed Suleiman Nyanga, alisema kuwa viongozi wa vilabu hivyo wanapaswa kuwa na ustaarabu pamoja na uadilifu wakati wanapotaka kusajili mchezaji kutoka madaraja yao , ili kuona na wao wanajaliwa katika kulea watoto hao. Alifahamisha kuwa vilabu vinavyoshiriki madaraja ya Central, Juvinile na Junior wanakuwa na kazi kubwa ya kulea vijana mpaka kufikia hatua ya kuwapata wao, hivyo vitendo vua kuwachukuwa wachezaji bila ya uadilifu unawavunja moyo kwa vile hupoteza nguvu zao nyingi katika kulea vijana hao. “Wao waelewe kuwa sisi ndio tuliofanya kazi kubwa mpaka wakawaona wao, sasa wakati wanataka kuchukuwa wachezaji hawapaswi kuchukuwa kinyemela, na kushindwa kukumbuka nguvu zao walizopoteza”, alisema.Endelea kusoma habari hii

MAVETERANI WATAKA KUUNGOA UONGOZI WA ZFA

28 10 2009

ZumnaUMOJA wa wachezaji wa soka wa zamani wa Zanzibar wanaotambulika kwa jina la (Maveterani) wamesema ipo haja kwa uongozi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kuondoshwa kwa nguvu zote kutokana na utendaji wao kuwa si wakuridhisha.Walisema tangu kukaa katika nyazisha zao hizo bado mabadiliko katika mchezo huo visiwani humu hajabadilika hata kwa asilimia 55, ila kikubwa zaidi ni kuuporosha tu mchezo huo.Mmoja wa Maveterani hao ambaye hakutaka kutajwa jina lake aliyasema hayo juzi, wakati akizungumza na gazeti hili juu ya hali ya soka hapa Zanzibar linavyopelekwa katika dimbwi la maji machafu.Alisema kuwa tayari wao kwa pamoja wameshakaa kikao ambacho kimeweza kujadili mambo mbali mbali yatakayowafanya kuondoa uongozi uliopo kwa maslahi ya maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.Alizidi kufahamisha kuwa miongozi mwa mambo ambao walijadili ni kupanga mkakati wa kuwafahamisha wanamichezo wote wa Zanzibar juu ya nia yao njema ya kutaka kuuondoa uongozi ulioko.Ili waweze kutafuta uongozi wenye sifa ya kuongoza nafasi hizo, kwa kuhakikisha kiwango cha soka visiwani humu kinaendelea na kupatikan vipaji.Endelea kusoma habari hii

KOMBE LA DUNIA LINAKUJA ZNZ

28 10 2009

spikaSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imewataka wananchi na wapenzi wa michezo hapa nchini kuacha dhana ya kutofika kwa ziara ya kombe la dunia visiwani Zanzibar kama baadhi ya vyombo vya habari vinavyonadi.Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamuhuna, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocian View Mjini Unguja.Alisema kwamba wananchiw anatakiwa kuwa na matumaini mazuri ya kuliona kwa macho yao na kulipokea kwa shangwe kombe hilo ifikapo November 21, mwaka huu.Kauli hiyo imetolewa na Shamuhuna alisema kuwa tayari baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikitangaza vibaya juu ya ujio wa ziara ya kombe la duania, kwa kusema kuwa inawezekana kwa asilimia kubwa lisifikie Zanzibar, hivyo hakuna haja kwa wananchi na wapenzi wa michezo wa visiwa hivi kuwa na matumaini ya kuliona kwa macho yao.Shamuhuna alisema kuwa hiyo si kauli njema kwa vyombo hivyo kwa kuwapa matumaini mabaya wananchi hao juu ya ujio wa kombe hilo.Waziri Shamuhuna aliwahakikishia wananchi kuwa ziara ya kombe la dunia itafanyika bila ya wasi wasi visiwani kama inavyotarajiwa ambapo kombe hilo litachukua muda wa masaa manne katika kisiwa cha Unguja.Endelea kusoma habari hii

  

TUMEMALIZA MALUMBANO-SMZ

22 10 2009

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kwamba malumbano shayaliyokuwepo kati ya vyama vya soka vya ZFA pamoja na TFF yamekwisha baada ya kupatiwa ufumbuzi na viongozi wa ngazi za juu nchini.Naibu Waziri wa Habari, Utangazaji na Michezo Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo aliwaambi wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wakati akijibu swali aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa hali ya maelewano na matatizo ya vyama vya soka nchini ZFA pamoja na TFF yamefikia wapi hadi sasa.Kombo alisema malumbano kati ya vyama vya soka nchini pamoja na taasisi nyengine yamepatiwa ufumbuzi na kwa sasa kinachofanyika ni utekelezaji wa walioafikiana katika vikao vya pamoja kati ya pande mbili hizo.“Vikao vya viongozi wa ngazi za juu vimefanyika katika hatua mbali mbali…Mawaziri wetu wawili wa pande mbili walikaa pamoja Mheshimiwa George Mkuchika mheshimiwa Ali Shamuhuna walikutana na kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo…sasa kinachofuatia ni utekelezaji tu” alisema Kombo.Alisema kwa upande wa masuala ya nje, Zanzibar inatumia mwamvuli wa Tanzania hivyo pande mbili hizo zimetakiwa kuainisha maeneo mbali mbali ya ushirikiano kama vile misaada, mafunzo, ushirikiano wa timu katika michuano ya kimataifa ikiwemo FIFA.Endelea kusoma habari hii

SKWASH KWENDA NAIROBI

17 10 2009

michezoMWANADADA wa Kizanzibari, anayetambulika kwa jina la Fatma Saleh, anatarajiwa kushiriki katika mashindano ya mchezo wa Skwash yatakayofanyika Nairobi nchini Kenya kuanzia Novemba 16 hadi 22, mwaka huu. Mwanadada huyo itakuwa ni mara yake ya pili kushiriki mashindano hayo nchini humo, ambapo mara ya kwanza alishiriki mwaka uliopita na kufanikiwa kutwaa ubingwa kwa nafasi za wanawake, Akithibitisha ushiriki wa mwanadada huyo Katibu wa Chama cha Skwash Zanzibar, Haji Vuai Uzia, alisema kuwa tayari wameshakamilisha hatua zote za ushiriki kwa mwanadada huyo na hivi sasa kilichobakia ni kusubiri muda wa mashindano kuanza. “Hatuna wasi wasi juu ya ushiriki wa Fatma kilichobakia kwake ni kujinoa kwa ajili ya kusuburi hayo mashindano tu na hakuna kitu chengine” alisema Uzia. Hata hivyo Uzia alisema kuwa mualiko huo kwa Mwanadada huyo umekuja kufuatia mwaka uliopita mwanadada huyo kuondoka nchini humo na ubingwa, Hivyo mara hii atalazimika kwenda kuutetea ubingwa wake kama ilivyo kawaida ya michezo mbali mbali ya hapa nchini na nje ya nchi. “Mualiko wa Fatma unatokana na ubingwa alioupata mwaka uliopita huko nchini Kenya, hivyo na mwaka huu atalazimika kwenda ili kuutetea ubingwa wake” alisema Uzia.Endelea kusoma habari hii

 

ZNZ HAIJATHIBITISHA USHIRIKI

17 10 2009

WAKATI baadhi ya timu kutoka nje zikiwa zimethibitisha kushiriki simbajktmashindano ya mpira wa mikono Afrika Mashariki na Kati, bado timu za Zanzibar hazijaweza kufanya hivyo kwa uhakika. Katibu Mkuu wa Chama cha mchezo huo Zanzibar Mussa Abdurabbi, ameliambia aiyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa, wakati nchi za kigeni zimethibitisha kwa barua, timu za hapa visiwani zimesema kwa maneno tu kwamba zitashiriki lakini hadi sasa hazijaandika barua yoyote. Alisema kauli za mdomo hazipokelewi na chama chake kuwa ni uthibisho rasmi na wala hazikubaliki katika kanuni za kuendesha mashindano hivyo iapo timu hizo zitataka kushiriki zitalazimika kuthibitisha kwa maandishi kama walivyofanya nchi nyengine ambazo zimethibitisha ushiriki wao. Mbali na kutegemea timu nyingi zitoke Zanzibar, alisema ni KMKM pekee ndiyo iliyoonesha nia ya kushiriki tafauti na timu nyengine ambazo zitatakiwa kuthibitisha kama zimechukua uamuzi wa kushiriki mashindano hayo. Aidha alisema licha ya ugumu wa mashindano hayo, lakini baadhi ya timu za shule nazo zimejitokeza kutaka zishirikishwe katika kinyang’anyiro hicho.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR HEROES KUONESHA UBABE

17 10 2009

Zuma aponaTIMU ya soka ya Taifa ‘Zanzibar Heroes’ juzi iliweza kuonesha makali yake kwa kuichapa timu ya vijana wa Karume Boys bao 1-0, katika mpambano maalum visiwani humu. Katika pambano hilo ambalo lililofanyika katika dimba la uwaja wa Maotuse tung Mjini Unguja, timu ya Zanzibar Heroes iliweza kuwamilikiwa vyema vijana wa Karume Boys katika dakika zote za mchezo ambao ulikuwa na mvuto wa aina yake. Mchezo huo ulianza vyema huku mashabiki wa timu hizo wakionekana kuwa na furaha kubwa katika nyuso zao huku uwanja ukijaa mashabiki wakiwa na hamu ya kuona hali ya ngarambe hizo zenye kuvutia kwa mashabiki wa soka. Mchezo huo uliendelea vyema katika kipindi cha kwanza kwa timu ya Zanzibar Heroes kuweza kufanikiwa kuziona nyavu za ndugu zao wa Karume Boys, kupitia mchezaji wao Sadik Habib katikka dakika ya 34. Bao ambalo liliwafanya vijana wa Karume Boys kutoamini macho yao kwa vijana hao kwa kuwaona ni wadogo kwa maungo huku wakiwa sawa na wao lakini ndani ya miguu yao mmejaa kila aina ya madaha ya mchezo.Endelea kusoma habari hii

WACHEZAJI WAKIMBIA MAZOEZI

WACHEZAJI wa timu ya Soka ya Miembeni kuhudhuria katika mazoezi mimibado ni kitendawili, kufuatia wachezaji hao kutoonekana kwenye mazoezi hayo kama ilivyo kawaida ya wanandinga wa timu hiyo. Mazoezi hayo ambayo yalianza Septemba 28 mwaka huu, katika viwanja vya Mnazimmoja, yalionekana kutawaliwa na wageni zaidi kuliko wenyeji wa timu hiyo. Katika ufatiliaji wa mazoezi hayo unaofanywa na gazeti hili, juzi pia uliwakuta wachezaji wageni wakiweza kufanya mazoezi huku akiongezeka mchezaji mmoja aliyekuwa akiichezea timu ya JKU Juma Khalifa ambae anatarajiwa kusajiliwa na uongozi wa timu hiyo. Ufatiliaji wetu katika viwanja vya mazoezi ya timu hiyo, ulibaini kuwa bado achezaji hao hawajapatia tarifa sahihi juu ya uanzaji wa mazoezi hayo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Meneja wa timu hiyo Abuubakar Bakil Haji, alisema kuwa ni kweli hawajapatia taarifa hadi wanaanza mazoezi hayo, lakini alidai kuwa sio sababu ya kuwa wanashindwa kuhudhuria kwa vile tayari wameshatoa taarifa kupitia vyombo vya habari mbali mbali juu ya kuanza kwa mazoezi hayo. Endelea kusoma habari hii

VIONGOZI WA TIMU LAWAMANI

Inzamam-ul-Haq afungiwa michezo minneBAADHI ya viongozi wa timu za majimbo wilaya ya kati unguja wamekuwa wakiwatupia lawama viongozi wakuu ndani ya majimbo hayo kwa kuzipa kisogo timu hizo. Hayo yamebainika kufuatia malalamiko kadhaa kutoka kwa viongozi walioachiwa kuzishughulikia timu hizo katika mashindano hayo ya majimbo yaliomalizika hivi karibuni ndani ya wilaya hiyo. Kauli hizo za lawama zimekuwa zikitupiwa zaidi katika timu za majimbo ya Koani na Uzini ambayo yameonekana kuwa mayatima na hatimae kushindwa kufanya vizuri katika ligi hiyo ulkilinganisha na timu ya jimbo la Chwaka. Viongozi hao wa jimbo la Koani walisikika wakisema kuwa viongozi hao wa jimbo lao hawafahamu ushiriki wa timu hiyo hadi wapate barua kutoka katika ofisi za wilaya jambo ambalo linawashanagaza viongozi hao. Walifahamisha kuwa suala la kuwaandikia barua ili kuwajuulisha kushiriki kwao katika mashindano hayo yanayochezwa nchi nzima itakuwa ni vigumu kwao kwani wakitaka hivyo basi wafike katika ofisi za wilaya wao wenyewe ili kujua kitu gani kinaendelea.Endelea kusoma habari hii

MAANDALIZI YA MAPINDUZI

Eto'o na RijkaardMAANDALIZI ya mashindano ya kombe la Mapinduzi ambayo hufanyika kabla ya Januari kumi na mbili yamo katika hatua nzuri na ya kuridhisha imeelezwa. Hayo yamebainishwa na Katibu wa Chama cha soka Wilaya ya Mjini Unguja, Nassor Salum Ali, wakati akizungumza na gazeti hili huko visiwani Zanzibar. Katibu huyo alisema kuwa tayari mipango yote imeshakamilika na kilichobaki sasa ni kutaraji hivi karibuni kumtangaza mdamini maalum wa mashindano hayo. Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kuzishirikisha timu nane ambazo zitagawiwa katika makundi mawili, ambapo kundi moja litacheza katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, na jengine katika uwanja wa Mao Dze Tong hapa Zanzibar . “Ninaweza kusema kuwa mashindano yetu yameshakamilika kutokana na hivi sasa tunasubiri muda uliopangwa wa kumtangaza mdhamini maluma wa mashindano hayo kwa mwaka huu” alisema. Hata hivyo katibu huyo alsema kuwa alisema kuwa bado hawajapanga timu zitakazoshiriki kwenye mashindano hayo lakini wanakusudia kuwaingiza mabingwa wa Zanzibar timu ya Mafunzo na Jamhuri kutoka Wete Pemba.Endelea kusoma habari hii

CHWAKA YAIFUNGA KOANI 2-0

TIMU ya jimbo la Chwaka inayoshiriki michuano ya ligi ya majimbo ndani ya wilaya ya kati imefanikiwa kuutwaa ubingwa wa ligi hiyo baada ya Kanu asema mie na watotokuifunga timu ya jimbo la Koani mabao 2-0.Mchezo huo wa fainali ambao ulichezwa katika dimba la Hanyegwa mchana ulikuwa mkali kiasi huku kila timu ikitaka kutwaa taji hilo ili kujiwekea heshima. Timu hizo zilianza mchezo kwa kasi ikiwa kila timu ikionesha ustadi wa kutandaza kabumbu na hatimae kupelekeana mashambulizi kwa zamu. Chwaka ikicheza kwa kujiamini zaidi wakiwa chini ya Kocha wake mkuu Mohamed Hilal (Tedy)iliweza kuwamudu zaidi wapinzani wake na hatimae kufanikiwa kuandika bao la kuongoza lilofungwa na mchezaji wake Mussa Magarawa mnamo dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza. Kuingia bao hilo timu ya Koani ilikuja juu na kupeleka mashambulizi langoni kwa timu ya Chwaka kwa nia ya kutaka kusawazisha bao hilo bali wasahambuliaji wake walionekana hawakuwa makini. Hatimae mnamo dakika ya 40 wakaweza kujipatia bao la pili lilifungwa kwa njia ya mkwaju wa penanti na mchezaji Mohammed Mbonde ,kufuatia mlinzi wa timu ya Koani kumfanyia madhambi mchezaji Matteo Antony.Endelea kusoma habari hii

MIEMBENI YAPATA MATUMAINI

Gattusso amwaga wino hadi 2011KLABU ya Soka ya Miembeni imepata matumaini mapya ya kuimarika katika medani la soka duniani, baada ya mmiliki klabu ya Soka ya Chelsea ya Uingereza Roman Abrohamvic, kuahidi timu hiyo kuipa msaada. Ambao utaweza kuwasaidia katika kushiriki mashindano mbali mbali ya ligi kuu ya Zanzibar pamoja na mengine yatakayotokezea. Ahadi nono ya Bosi huyo ameitoa mbele ya viongozi wa timu hiyo wakati akiwa ziarani nchini humu hivi karibuni,Akisimulia kuhusu hadi hiyo huko Rahaleo Mjini Unguja, Meneja wa klabu hiyo Abubakar Wakili , alisema kuwa Bosi huyo tayari ameshafanya mazungumza ya awali na uongozi wa timu hiyo juu ya dhamira yake ya kukisaidia kikosi cha Miembeni. “Tayari mazunguzo ya awali baina ya uongozi wa Miembenia na Bosi huyo wa Chelsea tayari yameshafanyika ya kutaka kukisaidia kikosi chetu” alisema. Endelea kusoma habari hii.

KIKUNDI CHAZINDULIWA  

KIKUNDI Cha Uhamasishaji juu ya masuala ya ukimwi Unic Theatre Arts’ kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao.Kikundi hicho ambacho Celebrations_Pembakinaundwa na wanachama zaidi ya 30 kitakuwa kinatowa elimu ya ukimwi kwa njia ya jukwaa, mijini na vijijini.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Meneja wa Vipindi wa kikundi hicho Khalid Abdallah, alisema kuwa wameanzisha kikundi hicho ili kutoa elimu ukimwi katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar , juu ya kujikinga na janga hilo.Alisema kuwa katika kufanikisha hilo tayari vijana wanaounda kundi hilo wameshapatiwa elimu ya kutosha juu ya kujikinga pamoja na kuishi kindoa na mtu ambae tayari ameambukizika bila ya kupata madhara yoyote mtu huyo.“Vijana wetu wako sawa kwani miongoni mwa mambo muhimu ambayo tumewafunza ni mtu kuishi na muathirika wa ukimwi kindoa bila ya kupata madhara yoyote mtu huyo”alisema.Endelea kusoma habari hii.

UMOJA NA USHIRIKIANO NI NGANO  

UMOJA na ushirikiano watakaoupata kutoka kwa wanachama wao ndio njia pekee itakayowawezesha timu hiyo kutokufa kama inavyodaiwa.Kauli hiyo imetolewa na katibu wa timu ya Miembeni Othman Dadi, wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kuhusiana na uvumi uliovuma kwa baadhi ya wadau wa soka hapa nchini.Timu hiyo ambayo baada ya kukimbiwa kwake mengi yalizuka hasa ikidaiwa kuwa ndio mwisho wa kuonesha maendeleo yake kisoka kama zilivyokufa timu nyengine.Dadi alisema kuwa iwapo wanachama wataonesha ukakamavu na upenzi wa timu yao wanauhakika kuwa timu yao itasonga mbele na sio kurudi nyuma kama wanavyodai wadau hao.“Sioni sababu ya kufa kwa timu yetu kwani sisi wenyewe tumejipanga upya na tunahakika kama tutakuwa na nguvu za pamoja kati yetu na wanachama basi itasonga mbele”, alisema katibu huyo.Katibu huyo ambae alionekana kukerwa na kauli hiyo alieleza kuwa timu yao itaweza kusimama kwa uwezo wa mungu na itaonesha makeke yake kuliko awali.Endelea kusoma habari hii

MIEMBENI KUTUMIA 80 MILLIONI

KLABU ya soka ya Miembeni inatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni 80, kwa ajili ya matayarisho mbali mbali ya timu hiyo kwa ajili ya kukiandaa DSC03450kikosi chake na ngarambe za ligi kuu mwakani pamoja na mashindano ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), yanayotarajiwa kuanza Januari mwakani. Kiasi hicho cha fedha kinarajiwa kutoka kwa wanachama wazalendo wapatao 200, pamoja na michango ya viongozi waliokuwepo sasa ndani ya timu hiyo ambao ndio wanaokiongoza kikosi hicho.Akizungumza na maandishi wa habari huko Rahaleo Mjini Unguja, Katibu wa timu hiyo Othman Dadi alisema kuwa miongoni mwa matumizi yatakayotumika mara baada ya fesdha hizo kukusanywa ni pamoja na usajili wa wachezaji, Kocha, vifaa vya ofisi pamoja na mambo mengine yanayoikabili timu.“Kwa kweli hivi sasa ndio tunaanza kuiandaa timu hivyo fedha nyingi zitatumika ili kuiwezesha kuifufua timu yetu, tunatarajia hapo baadae tutaongeza zaidi fedha hizo”alisema.Endelea kusoma habari hii

MIEMBENI KUSAIDIWA

ROONEYMMILIKI wa klabau ya Soka ya Chelsea ya Uengereza Roman Abrohamvic, ameahidi kuipa msaada timu ya Soka ya Miembeni ya Zanzibar katika mashindano mbali mbali inayotarajiwa kushiriki. Ahadi nono ya Bosi huyo ameitoa mbele ya viongozi wa timu hiyo wakati akiwa ziarani nchini humu hivi karibuni,akisimulia kuhusu hadi hiyo huko Rahaleo Mjini Unguja, Meneja wa klabu hiyo Abubakar Wakili , alisema kuwa Bosi huyo tayari ameshafanya mazungumza ya awali na uongozi wa timu hiyo juu ya dhamira yake ya kukisaidia kikosi cha Miembeni. “Tayari mazunguzo ya awali baina ya uongozi wa Miembenia na Bosi huyo wa Chelsea tayari yameshafanyika ya kutaka kukisaidia kikosi chetu” alisema Wakili alifahamisha kuwa mazungumzo hayo ya awali kwa uongozi wa Miembeni na Bosi Abrohamvic, yalimefanyika huko Mkoani Arusha Tanzania Bara, lakini bosi huyo hakuweza kumaanisha ni msaada gain atakaoutoa kwa klabu hiyo. Mazungumzo ambayo yalianza kuzaa matunda mazuri ya mafanikio kwa uongozi juu ya kuwa na uhakika wa kupatiwa ufadhili pamoja na ushirikiano baina ya timu ya Miembenia na Chelsea.Endelea kusoma habari hii

 

UJAUZITO WAKWAMISHA SOKA

1

KUFA kwa timu za soka za wanawake katika Wilaya ya Kati, kumeelezewa kunatokana na wachezaji kukumbwa na mitihani mbalimbali ya kidunia ikiwemo kupata ujauzito wa wasichana hao.Katibu wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Wilaya ya Kati Mwandazi Zubeir Said, alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa, wilaya yake ilikuwa miongoni mwa maeneo ya kwanza kuanzisha timu hizo na wachezaji walikuwa na ari ya mchzo huo aali.Alisema jitihada hizo zimeishia njiani kutokana na sababu mbali mbali na kusababisha timu hizo kufa jambo ambalo linasikitisha kuona wanawake wa wilaya hiyo wamekuwa wakishindw ana sehemu nyengine visiwani hapa.Akizitaja timu hizo ni pamoja na Bungi Sisters na Koani Sisters, ambazo kuna tetesi kwamba zimekufa kutokana na wachezaji wake wengi kutojishughulisha tena na mambo ya michezo ingawa alisema ofisi yake haina uhakika juu ya hilo.Said alifahamisha kuwa timu mbili hizo ziliweza kuiletea sifa wilaya ya kati kwa kuwa timu hizo ni miongoni mwa zilizocheza ligi ya Zanzibar na kuonesha uwezo mkubwa kisoka.Endelea kusoma habari hizi.

ORLANDO YAJIPANGIA USHINDI

TIMU ya New Orlando ya Ubago inayocheza ligi daraja la tatu Wilaya ya DSC03331Kati, imesema inajiandaa kikamilifu kuhakikisha inapanda ngazi katika msimu ujao.Miongoni mwa mikakati ya timu hiyo inayokusudia kufanya katika msimu ujao ni kushiriki michuano ya kuwania ng’ombe ili kupima uwezo wa wachezaji wake na kasoro za kikosi hicho.Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza baada ya kumalizika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kushirikisha timu mbali mbali za Shehia ya Koani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Mlezi wa timu hiyo New Orlando, Suleiman Said Bangaya, amewambia waandishi wa habari kwamba timu yake inakusudia kutumia michuano hiyo kwa lengo la kubaini kasoro ili kuweza kusuka kikosi imara kitakachoweza kuhimili vishindo vya ligi hiyo.“Tumedhamiria kupanda daraja kwa kila hali, na tukifanikiwa njia ya kwenda hadi daraja la kwanza kanda itakuwa nyeupe kwetu na tutakapomaliza mfumo wa Ramdhani inshaallah tutafanya mazoezi na matayarisho makubwa ili tupande daraja aktika msimu ujao”, alisema Bangaya.Alisema michuano hiyo itasaidia kujua wapi panahitaji marekebisho, na mazoezi ya nguvu yatafanyika kabla kikosi hicho kuingia mawindoni kusaka wachezaji wenye sifa kwa ajili ya ligi ijayo.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR QUEEN‘S KUPAA UJERUMANI

Zimamoto by Masoud Khamis DSC05613TIMU ya Taifa ya Soka la Wanawake ‘The Zanzibar Queens’ imeondoka nchini na kuelekea nchini Ujerumani kushiriki mashindano maalum ya kimataifa kwa wanawake. Ziara hiyo ni mualiko kutoka kwa klabu ya FFC Turbine Potsdam, ikiwa ni matunda ya filamu iliyorekodiwa Visiwani Zanzibar mwaka 2004 inayoonesha maendeleo ya mchezo huo kwa timu za wanawake.Mratibu wa shughuli hiyo ni Kiongozi wa Shirika la Kijerumani (RAA) Bi Birgit Mitawi Mjerumani anayeishi visiwani Zanzibar kwa miaka kadhaa . Jumla ya wachezaji 13 na viongozi wawili watakuwemo kwenye msafara huo amabpo wanatarajiwa kuondoka na shirika la ndege la Qatar majira ya saa 7:00 mchana katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasra Juma Mohammed, aliwataja wanasoka hao kuwa ni Zubeda Abbas Abdallah, Flora Raphael Kayanda, Mwasiti Juma Suleiman, Feruzi Ally Amir, Nasriya Hashir Abdallah, Pulkeria Ignas Charaji na Siajabu Hassan Ali. Wengine watakaokuwemo katika msafara huo ni Sabah Hashim Yussuf, Warda Khalid Abdallah, Ibtisam Salum Yussuf, Msimu Suluhu Hassan, Mwajuma Zubeir Nassib na Khatima Mwalim Khamis (Nahodha).Endelea kusoma habari hii

VYUO VYA MAFUNZO WATIMIZA AHADI

WAKATI uongozi wa Vyuo vya Mafunzo ukitimiza ahadi ya kuwatunukia vyeo baadhi ya wachezaji ikiwa zawadi kwa kutwaa ubingwa wa soka mwaka huu wengine 13 wameanza kupiga kwata kwa ajili ya ajira. Idara hiyo iliwaahidi vyeo pamoja na ajira kwa wale waliokuwa si waajiriwa wake, wachezaji wa timu hiyo iwapo wangebeba ubingwa wa soka katika ligi kuu iliyomalizika Julai mwaka huu. Katibu wa Idara ya Michezo katika kikosi hicho Makame Fadau, aliwataja nyota wanaoanza mafunzo kwa ajili ya kuajiriwa rasmi, kuwa ni Mwadini Ali, Sadik Habib, Zahor Salmin, Maulid Ngaga, Haji Ramadhan, Haji Kombo, Hamid Ali, Ramadhan Kassim, Waziri Salum, Hassan Ahmada na Said Mussa. Aidha alisema waliokwaa vyeo vya ukoplo ni Haji Abdi, Haji Hassan, Murtala Kibamba, Abdallah Bakari, Bakari Ayoub, Mohammed Golo, Hassan Ali, Hassan Kiboje, Salum Mpangani, Suleiman Kassim, Abdulrahman Krishna na Mbarouk Zahran. Mwanandinga Masoud Hamad ndiye pekee aliyevishwa cheo cha usajenti kutokana na umahiri wake mkubwa aliouonesha wakati wote wa ligi kuu ya Zanzibar ilipoikuwa ikitimua vumbi visiwani hapa.Endelea kusoma habari hii

KITENDAWILI CHA UCHAGUZI CHANEZA

CHAMA Cha Netiboli Zanzibar (CHANEZA) bado kina kitendawili kikubwa katika hatua ya kufanya uchaguzi wake kutokana na kutojitokeza wagombea wa nafasi mbili muhimu ambazo ni muhimili mkubwa wa chama hicho. Hali hiyo imekifanya chama hicho kushindwa kufanya uchaguzi huo kama kilivyoagizwa na Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BMTZ) miezi kadhaa iliyopita ya kukitaka chama hicho kikamilishe mambo yote yanayohusu uchaguzi na wagombea. Hata hivyo kukwama kwa uchaguzi huo kumesababishwa na kutokuwepo wagombea wa nafasi za Mwenyekiti na Katibu wala watu wanaotajwa kutaka kuwania viti hivyo, jambo ambalo bado ni kitandawili kwa wadau na wapenda mchezo huo visiwani humu. Kaimu Katibu Mkuu wa CHANEZA Rahima Bakari, ameliambia gazeti hili kuwa, bado chama chake hakijajua lini waitishe uchaguzi bila kwanza kupatikana kwa wagombea wa nafasi hizo. “Mpaka sasa hatujui lini tuitishe mkutano wa uchaguzi kutokana na matatizo yaliomo ndani ya chama chetu ya kukosekana kwa wagombea wa nafasi hizo, ambazo ndio tegemeo la chama chetu” alisema.Endelea kusoma habari hii

MAFUNZO KUVUKA MAJI

KATIKA kuhakikisha inajiandaa vyema kukabiliana na vishindo vya michuano ya klabu bingwa Afrika na ile ya Kagame, timu ya soka ya Mafunzo inatarajia kuvuka maji na kwenda nchi jirani kwa ajili ya mazoezi. Mafunzo ilifanikiwa kupata uwakilishi huo baada ya kuivua ubingwa Miembeni kwenye ligi kuu iliyomalizika Julai mwaka huu. Katibu wa Idara ya Michezo wa Vyuo vya Mafunzo Makame Fadau, amesema bado uongozi wake haujajua ni nchi gani watakwenda, lakini tayari umeanza maandalizi ya ziara hizo. Alisema kwa vile wanafahamu ugumu wa mashindano yanayowakabili, wameona ni vyema timu hiyo ikapata mechi za kujipima nguvu dhidi ya timu za nje zenye uzoefu wa michuano hiyo ya Afrika. “Mashindano ya Afrika ni magumu, tumejifunza kutoka kwa wenzetu waliowakilisha nchi kabla, ni lazima tujenge kikosi imara kuhakikisha tunafika mbali”, alisema. Fadau alieleza kutokana na umuhimu wa maandalizi mazuri na ya kutosha, timu hiyo inajipanga kuanza mazoezi mapema mara baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.Endelea kusoma habari hii

TAIFA YA VIJANA YAWA YA KUDUMU

CHAMA Cha Soka Zanzibar (ZFA) kimesema hakitoivunja tena timu ya taifa ya vijana ‘U-17’ Karume Boys kama ilivyokusudiwa na badala yake kikosi hicho kitaimarishwa zaidi. Akizungumza na waandishi wa Habari, Rais wa chama hicho Ali Fereji Tamimu, huko Afisni kwake Bwawani Hotel Mjini Unguja.Wakati akimtambulisha kocha mpya wa timu ya taifa Abdelfatah El Masqsood kutoka nchini Misri ambaye amechukua nafasi ya kocha Badr El Din Haddad, aliyemaliza muda wake. Rais Fereji alisema kuwa nia ya chama hicho ya kuitawanya timu hiyo hivi sasa imeshaondolewa na hakutegemewi kufikiriwa tena kuisambaratisha timu hiyo. “Hivi sasa hatuna nia tena ya kuivunja timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, na badala yake tutaiimarisha ili kuwa tishio kubwa” alisema. Tamim alifahamisha kuwa hatua hiyo imekuwa kufuatia timu hiyo kurundi nchi Sudan hivi karibuni katika mashindano ya Chalenji na kuonesha kiwango kizuri.Endelea kusoma habari hii

MATENGENEZO YA UWANJA WA AMANI YARIDHISHA

MATENGENEZO ya uwanja wa mpira wa Amani Mjini Unguja, yanaendelea katika hatua nzuri na huku matumaini yakiwa kukamilika katika kiwango kizuri. Akizungumza na mwanandishi wa habari Mratibu wa Ujenzi wa Uwanja huo, Juma Ali David alisema kuwa matengenezo hayo yanakwenda katika hali ya kurithisha na iliyo nzuri kabisa. “Matengenezo ya uwanja wa Amani hadi hivi sasa yanakwenda vizuri sana na tunategemea kwenda hadi mwisho katika hali yenye matumaini ya ubora zaidi na bila ya shaka uwanja utakuwa mzuri utakapokamilika”alisema. David alisema kuwa katika matengenezo hayo hivi sasa wapo katika matengenezo ya taa, vyoo pamoja na majukwaa ambayo hayo yanatarajiwa kukamilika baada ya kipindi kifupi kijacho. Hata hivyo alisema kuwa pamoja na matengernezo hayo lakini pia kuhusu suala la maji uwanjani hapo kunatarajiwa kuwa na kisima pekee cha uwanja huo.Endelea kusoma habari hii

WASANII WAPINGA UNYANYASAJI DHIDI YA ALBINO

KIKUNDI Cha Sanaa ya Maigizo kijulikanalo kwa jina la ‘Sauti ya Samba_Mapangala_by_Eirik_Folkedal_DSC_9824_HRSimba’ (Moyo wa Simba), kinatarajia kuonesha Filamu maalum inayohusu unyanyasaji na ukatili wanaofanyiwa walemavu wa ngozi nchini (Albino) mapema mwezi ujao.Akizungumza na waandishi wa habari huko afisini kwake, Jangombe Mjini Unguja, Katibu wa kundi hilo, Abdallah Ramadhan Feruzi, alisema kuwa matayarisho kwa kiasi kukubwa ya filamu hiyo tayari yameshakamilika kilichobaki sasa ni kusububiri muda uliopangwa na uongozi ili kuweza kuikamilisha rekodi pamoja na kuirusha hewani tu.“Matayarisho ya Filamu yetu hadi sasa tayari yana sura nzuri na ya kuridhisha kilichobaki ni kusubiri kauli ya mwisho ya uongozi ili kuweza kuitawanya katika Mikoa mbali mbali ya Tanzania “alisema Feruzi.Hata hivyo alifahamisha kuwa katika uingizaji wa Filamu hiyo pamoja na wao kuchukuwa sehemu kubwa ya kuingiza wakiwa si wagonjwa wa nguzi yaani Albino, lakini pia itawashirikisha baadhi ya Maalbino wakiwamo watoto na watu wazima ili nao waweze kutoa michango yao kwa jamii juu ya vitendo viovu wanavyofanyiwa.Endelea kusoma habari hii

MASHABIKI WASHUHUDIA MPAMBANO

P1040314MASHABIKI wa soka waliofika uwanja wa Mao Dzedong kushuhudia mpambano kati ya timu ya Taifa ‘Zanzibar Heroes’ na Azam FC, walikumbwa na fadhaa kubwa baada ya kuona jezi za Heroes zikiwa zimehifadhiwa ndani ya kipolo.Kama hilo halitoshi, aidha jezi hizo zilikuwa zikitia harufu mbaya kudhihirishga kuwa hazikwua zimefuliwa kwa siku kadhaa.timu hiyo ilipocheza na timu ya Azam FC ambayo ilikuwepo Zanzibar kwa ziara ya siku nne ya kujiandaa na ligi kuu ya Tanzania Bara.Mashabiki hao ambao walionekana kushangazwa sana na kitendo hicho walisikaika wakisema kuwa kweli timu hiyo haina matunzo kwani licha ya kuwa jezi hizo zimehifadhiwa ndani ya kipolo hicho pia zinaonekana kutofuliwa kutokana na kutoa harufu mithili ya mdudu aliyekufa na kuoza.Wakati ikijitokeza hali hiyo baadhi ya mashabiki waliokuwepo hapo walisikika wakisema kuwa utaratibu huo sio mzuri na unatia aibu kwa vile timu hiyo ni ya Taifa, hivyo kufuatia hivyo inatoa sura mbaya kwa taifa.“Ni aibu kwa timu ya Taifa kuwekwa katika mazingira haya, kwani hata vilabu vina afadhali kwa vile huingia uwanjani wakiwa katika hali ya unadhisdhifu alisema shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hassan Haji Hamza.Endelea kusoma habari hii

MIEMBENI YATHIBITISHA USHIRIKI

TIMU ya soka ya Miembeni imethibitisha rasmi ushiriki wake kwa chama cha soka Zanzibar (ZFA) wa mashindano ya shirikisho Baran Afrika yatakayofanyika mwakani.Klabu hiyo imeweka bayana hiyo baada ya kuikamata nafasi ya pili ya ligi ya Zanzibar na kufanikiwa kupata nafasi ya ushiki huo, ambapo nafasi ya kwanza ya ligi hiyo ilikamatwa na timu ya Mafunzo.Kwa mujibu wa habari kutoka kwa katibu wa chama cha soka Zanziba (ZFA) Mzee Zam Ali, zinasema kuwa timu hiyo tayari imeshatuma barua yake chamani hapo ya ushiriki wa mashindano hayo iliyo rasmi.“Miembeni tayari imeshatuma barua yake ya ushiriki chamani hap iliyo rasmi kilichobaki sasa ni matayarisho yao tu” alisema.Katibu huyo alifahamisha kuwa katika barua ya timu hiyo iliyotumwa Agost 15, mwka huu imesema kuwa timu hiyo iko tayari kushiriki kombe hilo.Endelea kusoma habari hii

VILABU KUWANIA URAIS ZFA

IKIWA siku zinazidi kumalizika za kukiwania kiti cha Uraisi wa Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA), umoja wa Vilabu Zanzibar umeibuka na kusema kuwa una nia ya kutoa mgombea wa kuania kiti hicho katika uchaguzi utakaofanyika mwakani.Hayo yameelezwa na Katibu wa Umoja huo Issa Ameir Issa, wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni.Alisema kuwa tayari wameshakubaliana na viongozi wenzake ili kulipitisha jina la mrithi huyo ambae atawania nafasi hiyo, ambae hakuwa tayari kulitaja.Alisema kuwa mpaka sasa bado hawajawa tayari kumtaja mrithi huyo, kwa kile alichodai kuwa ni mapema mno kumuweka hadharani.“Jina tunalo lakini bado kuliweka hadharani kwa vile ni mapema mno, ila tu muda utakapokaribia basi tutamtangaza”, alisema Katibu huyo.Endelea kusoma habari hii

WADAU WAMKATAA KATIBU WAO

WADAU wa mchezo wa kikapu (Basketball) Zanzibar wamemjia juu Katibu wa chama hicho, Abdurahman Muhammed Hassan kwa madai kwamba hafai kuendelea na uongozi wa ngazi hiyo kwamba hawamtambui.Wadau hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao waliyasema hayo hivi karibuni wakati wakizungmza na gazeti hili Mjini Unguja, kufuatia katibu huyo kuandaa mashindano maalum kwa timu za mchezo huo.Walisema kuwa kiongozi huyo hafai kuongoza wala kuendesha mashindano ya aina yoyote kutokana na hivi sasa hawezi kutambulika kama ni kiongozi.“Si kitendo kizuri kwa katibu huyo kuyafanya madaraka kama ni yake hali ya kuwa na uhakika wa kuwa hivi sasa haipaswi kufanya wala kuendelea kufanya mashindano ya aina yoyote” walisema.Hata hivyo walizidi kufahamisha kuwa ndani ya katiba ya chama hicho ya mwaka 1990, kuna kifungu kinachofahamisha kuwa kiongozi yoyote ana muda wake maalum wa kushika nyazifa, hivyo na muda wa kiongozi huyo tayari umekwisha kamilika.Endelea kusoma habari hii.Endelea kusoma habari hii

UDHAMINI WAKOSESHA SKWASH ZNZ KUTOTAMBULIWA

michezoKUKOSEKANA kwa udhamini kumeelezewa kuwa ndio sababu inayoufanya mchezo wa skwashi kutotambulika hapa Zanzibar kama ilivyo michezo mingine.Katibu wa Chama cha Skwashi Zanzibar Haji Uzia Vuai, amesema wadau wengi wa michezo hapa nchini wameelekeza zaidi nguvu zao kudhamini michezo mingine hasa mpira wa miguu na kuipa kisogo michezo midogo.Akizungumza na gazeti hili huko afisini kwake Ziwani, Katibu huyo alisisitiza haja ya kupatikana nguvu ya kifedha ili kuimarisha mchezo huo na kuwapatia mashabiki burudani mbadala badala ya kujikita zaidi katika soka pekee.Alifahamisha kuwa chama chake kipo tayari kushirikiana na wadau wowote watakaojitokeza kudhamini mchezo huo kwa lengo la kuutangaza ili utambulike kitaifa na kimataifa.“Sisi kama chama tuko tayari kuutangaza mchezo huo kila pembe hapa nchini na kwengineko lakini hili linategemea zaidi nguvu ya udhamini, tunaomba wadau waungane nasi katika azma hiyo”, alisema.Endelea kusoma habari hii

MAKAMPUNI YASHAURIWA

jechaWAFANYABIASHARA na wenye makampuni mbali mbali visiwani Zanzibar wameshauriwa kushiriki katika kusaidia na kufadhili mambo mbali mbali hususan ya kuutangaza utamaduni wa Zanzibar. Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo,Mahmoud Thabit Kombo wakati alipokutana na uongozi wa Chuo cha Muziki wa Nchi za Jahazi (DCMA) pamoja na wafanyabiashara mbali mbali wakati wa ufunguzi wa onesho la urithi hapo chuoni kwao DCMA.Kombo alisema ni vyema wafanyabiasha ra kusaidia katika maswala ya utamaduni ambayo ndio yanayosaidia kuitangaza nchi yetu kupitia wageni mbali mbali wanaovitembelea visiwa vya Zanzibar.Alisema kufadhili katika fani hiyo ya sanaa za asili sio kuitangaza fani hiyo pekee bali pia kutangaza kazi ambazo zinafanywa na kampuni hizo.“Tunashukuru visiwa vyetu vina wafanyabiashara mbali mbali na kampuni nyingi sana, kwa hiyo tuna kushaurini muje mudhamini huu utamaduni wetu ambao ndio unaoelezea historia yetu sisi Wazanzibari,”alisema.Hivyo Waziri Kombo aliwapongeza wafadhili mbali mbali ambao wanaokisaidia na kukifadhili chuo cha Muziki Zanzibar ambacho ndio kinachofunza na kurithisha utamaduni wa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii.

MASHABIKI WASHUHUDIA MPAMBANO

MASHABIKI wa soka waliofika uwanja wa Mao Dzedong kushuhudia mpambano kati ya timu ya Taifa ‘Zanzibar Heroes’ na Azam FC, walikumbwa na fadhaa kubwa baada ya kuona jezi za Heroes zikiwa zimehifadhiwa ndani ya kipolo.Kama hilo halitoshi, aidha jezi hizo zilikuwa zikitia harufu mbaya kudhihirishga kuwa hazikwua zimefuliwa kwa siku kadhaa.timu hiyo ilipocheza na timu ya Azam FC ambayo ilikuwepo Zanzibar kwa ziara ya siku nne ya kujiandaa na ligi kuu ya Tanzania Bara.Mashabiki hao ambao walionekana kushangazwa sana na kitendo hicho walisikaika wakisema kuwa kweli timu hiyo haina matunzo kwani licha ya kuwa jezi hizo zimehifadhiwa ndani ya kipolo hicho pia zinaonekana kutofuliwa kutokana na kutoa harufu mithili ya mdudu aliyekufa na kuoza.Wakati ikijitokeza hali hiyo baadhi ya mashabiki waliokuwepo hapo walisikika wakisema kuwa utaratibu huo sio mzuri na unatia aibu kwa vile timu hiyo ni ya Taifa, hivyo kufuatia hivyo inatoa sura mbaya kwa taifa.“Ni aibu kwa timu ya Taifa kuwekwa katika mazingira haya, kwani hata vilabu vina afadhali kwa vile huingia uwanjani wakiwa katika hali ya unadhisdhifu alisema shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hassan Haji Hamza.Endelea kusoma habari hii

MIEMBENI YATHIBITISHA USHIRIKI

TIMU ya soka ya Miembeni imethibitisha rasmi ushiriki wake kwa chama cha soka Zanzibar (ZFA) wa mashindano ya shirikisho Barani Afrika yatakayofanyika mwakani.Klabu hiyo imeweka bayana hiyo baada ya kuikamata nafasi ya pili ya ligi ya Zanzibar na kufanikiwa kupata nafasi ya ushiki huo, ambapo nafasi ya kwanza ya ligi hiyo ilikamatwa na timu ya Mafunzo.Kwa mujibu wa habari kutoka kwa katibu wa chama cha soka Zanziba (ZFA) Mzee Zam Ali, zinasema kuwa timu hiyo tayari imeshatuma barua yake chamani hapo ya ushiriki wa mashindano hayo iliyo rasmi.“Miembeni tayari imeshatuma barua yake ya ushirki chamani hap iliyo rasmi kilichobaki sasa ni matayarisho yao tu” alisema.Katibu huyo alifahamisha kuwa katika barua ya timu hiyo iliyotumwa Agost 15, mwka huu imesema kuwa timu hiyo iko tayari kushiriki kombe hilo.Endelea kusoma habari hii.

CENTRAL YAJIPANGA UPYA

MABINGWA wa Central timu ya Leads United imesema kuwa imejipanga imara katika msimu wa ligi ujao, ili kuweza kutetea vyema ubingwa wao.Akizungumza na gazeti hili Rais wa timu hiyo Khatib Juma, alimwambia mwaandishi wa habari hizi, kuwa katika kuhakikisha hilo wanatatarajia kutafuta wachezaji wenye viwango bora ambao watahimili vishindo vya ligi hiyo.Alifahamisha kuwa tayri tumeshaanza mazungumzo na wachezaji kutoka timu mbali mbali na wameweza kuonesha matumaini ya kuwasajili na kama watawapata wachezaji hao basi nia ya kuutetea ubingwa wao itakuwa imetimia.“Tumeshaanza mazungumzo na wachezaji mbali mbali, na wameonesha nia nzuri tu ya kutukubalia na tukiwatia mikononi basi timu yetu itaweza kutetea ubingwa wetu”, alisema rais huyo.Endelea kusoma habari hii.

BAZA YATANGAZA TAREHE YA MWISHO

P1030907CHAMA Cha Mchezo wa Kikapu Zanzibar (BAZA) kimetangaza rasmi tarehe ya mwisho kwa timu zote kurejesha fomu za ushiriki katika mashindano ya Karume Cup yanayotarajiwa kufanyika kabla ya sherehe za Januari mwakani.Akizungumza na gazeti hili karibuni katibu wa chama hicho Abdul-rahman Muhammed Hassan huko Maisara Mjini Unguja, alisema kuwa tarehe ya mwisho ya urejeshaji wa fomu hizo ni Agost 27,mwaka huu.“Timu zote tunazitaka kurejesha fomu hizo Agost 27, baada ya siku hiyo fomu hatutozipokea tena” alisema Katibu huyo.Hata hivyo Kataibu huyo alifahamisha kuwa pindi timu itayoshindwa kurejresha fomu kwa muda ulipangwa na chama hicho basi hatua kali zidi yao itachukuliwa kwa mujibu wa sheria za chama hicho.“Hatutoiwachia timu yoyote ile iyakayo kwenda kinyume na taratibu za chama chetu katika hatua hii ya urejeshaji wa fomu”alisema.Endelea kusoma habari hii.

NYERERE BOYS KUSAJILI WACHEZAJI NYOTA

UONGOZI wa timu ya Nyerere Boys umesema kuwa katika kuimarisha timu yao ina mpango wa kusajili nyota saba katika msimu wa usajili ujao.Akizungumza na gazeti hili Rais wa timu hiyo Musa Mzirai alisema kuwa miongoni mwa wachezaji waliopanga kuwasajili ni wale waliong’ara katika timu ya Mkoa wa Mjini Magharibi pamoja na hata kuchukuwa baadhi ya wachezaji waliochezea ligi kuu mwaka jana pamoja na kuwarejesha wachezaji wao wa zamani.“Msimu huu tunataka kurejesha ubingwa wetu na tumeona ili tuweze kufanikiwa basi tujipange vyema katika usajili, na tukifanikiwa hapo tutaweza kufikia”, alisema Mzirai.Aidha alisema kuwa wakati wanampango wa kusajili nyota hizo saba pia uongozi huo umetangaza kuwaacha wachezaji watano kutokana na sababu mbali mbali.Miongoni mwa wachezaji hao ni Soudi Mwinyi Ali, Shaibu na Mohammed Hassan ambao wameachwa kwa sababu ya utovu wa nidhamu huku Ussi Khamis na Ali Juma Ame viwango vyao kushuka pamoja na kutojituma ipasavyo katika mechi.Endelea kusoma habari hii.

 

MADADA WASHINDA WAKO JUU

BENDERAMADADA wa timu ya Mwembeladu wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Wavu (Volball) kanda ya Unguja, baada ya kuwalaza mabanati wenzao wa Starnet kwa seti 3-0.Pambano hilo la mwisho kwa maanti hao ambalo lilikuwa la vuta nikuvute kwa maati wote hao kuukodolea macho ubingwa huo, lilifanyika katika dimba la uwanja wa Mafunzo Mjini Ungja na kuhudhuriwa na shangwe la mashabiki , huku wakionekana kuwa na hamu kubwa kushuhudia fainal hiyo.Katika fainal hiyo timu ya Mwembeladu iliweza kuumiliki mchezo huo kuanzia mwanzo hadi mwisho na kufanikiwa kuondoka kiwanjani hapo na ubingwa.Lakini kwa upande wa pambano la mwisho kwa wanaume lililofanyika mapema timu ya Mafunzo iliweza kuwachara vijana wa Chui kwa seti 3-0, na kufanikiwa kuuny’akua ubingwa wa ligi hiyo.Mara baada ya kumaliza mapambano hayo mabingwa wa ligi hiyo waliweza kukabidhiwa vikombe, na mlezi wa mchezo huo Bi Moza Thabit, huku timu ya Starnet Wanawake wakikabidhiwa kikombe cha nidhamu.Endelea kusoma habari hii

MIKAKATI YA DCMA YAIMARIKA

KATIKA mikakati ya kuendeleza mafunzo ya utamaduni, Chuo cha Muziki wa Nchi za Jahazi (DCMA) kimeongeza taaluma kwa wanafunzi wa chuo taarabhicho ambapo sasa kitawafundisha jinsi ya kutengeneza ala za muziki.Hatua hiyo inafuatia mafanikio ya mpango wa chuo hicho katika kutoa elimu ya muziki pamoja na uimbaji wa nyimbo za taarab pamoja na ngoma za asili.Afisa Uhusiano wa chuo hicho Lionnie Schollmayer, amesema uamuzi huo umetokana na kutokuwepo mafundi wa kutengeneza ala pale zinapoharibika.Amesema kuwa mafunzo hayo yameanza Julai 30, mwaka huu chini ya mkufunzi Sameer Totah kutoka Palestina ambapo wanafunzi hao, wameonesha ufahamu mkubwa katika kuyafuatilia.Lionnie alisema kuwa hadi hivi sasa wanafunzi hao wameanza kutengeneza ala mbali mbali ambazo zinatumika katika upigaji wa taarab asilia.Endelea kusoma habari hii.

AZAM FC YACHAPWA NA ZANZIBAR HEROES

maximongassaTIMU ya Soka ya Azam FC kutoka jijini Dar es Salam iliopo visiwani humu kwa ajili mazoezi yake ya mwisho imeangwa rasmi na vijana wa timu ya ‘Zanzibar Heroes’ kwa kuchapwa bao 1-0 bila ya huruma. Katika pambano hilo ambalo lililofanyika katika dimba la uwajua wa Mautsetung Mjini Unguja, timu ya Azam iliweza kumilikiwa vyema na vijana wa Zanzibar katika dakika zote za mchezo. Mchezo huo ulianza vyema huku mashabiki wa timu hizo wakioneka kuwa na furaha kubwa katika nyuso zao huku uwanja ukijaa mashabiki wakiwa na hamu ya kuona hali ya ngarambe hizo za mwisho kwa timu ya Azam. Mara tu ya mchezo huo kuanza vijana wa Zanzibar waliweza kuutia mpira miguuni mwao na kufanikiwa kuliona lango la Azam FC na kuanza kuzitikisha nyavu zao, kupitia mchezaji wake Hassan Seif ‘Banda’ mnamo dakika ya pili ya mchezo huo. Bao hilo ambalo liliwafanya Azam kutoamini macho yao kwa vijana hao kwa kuwaona ni wadogo kwa maungo lakini ndani ya miguu yao mmejaa kila aina ya madaha ya mchezo.Endelea kusoma habari hii

ZFA YATUPILIA MBALI RUFAA YA NEW TOWN

CHAMA Cha Soka Zanzibar (ZFA) kimeitupia mbali rufaa iliyokatwa na timu ya New Town ya kutoa malalamiko juu ya timu ya Kichakanyuki kwa kumchezesha mchezaji Yussuf Khamis ikidai kuwa mchezaji huyo si halali. Mwanandinga huyo alicheza katika mechi ya ligi ya mabingwa kanda ya Unguja baina ya timu hizo kwenye kiwanja cha Kiembesamaki ambapo miamba hiyo ilishindwa kufungana. Kwa mujibu wa barua ya ZFA Taifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Mzee Zam Ali, kikao cha Kamati Tendaji kilichofanyika Augosti 4, mwaka huu kusikiliza lalamiko hilo, ilibainika kuwa mchezaji huyo alihamshwa kihalali akitokeatimu ya Kama Stars mwaka 2007. Aidha imeelezwa kuwa, Kama Stars iliridhia uhamisho huo pamoja na ZFA Wilaya ya Magaharibi, na tangu wakati huo mwanandinga huyo amekuwa akiicheza timu ya Kichakanyuki na kwamba hajahamishwa na timu nyengine yoyote. Hata hivyo, ZFA iligundua kuwepo kwa mchezaji mwengine katika klabu ya Kama Stars mwenye jina la Yussuf Khamis ambae hahusiani na huyo aliyehamishwa kwenda Kichakanyuki ya Jambiani Mkoa wa Kaskazini Unguja.Endelea kusoma habari hii

MAFUNZO WAWACHARAZA CHUI 3-0

TIMU ya Mafunzo Wanawake inayoshiriki ligi ya kanda Unguja kwa mchezo wa Wavu imewaumbua vijana wa Chui kwa kuwacharaza seti 3-0 Pambano hilo ambalo lilipigwa katika dimba la uwanja wa Mafunzo, na kuhudhuriwa na mashabiki wengi wa mchezo huo ambao kila mmoja alikuwa na hamu ya kuona timu yake inaondoka kiwanjani hapo na ushindi. Mchezo huo ulianza vyema kwa wanadada wa Mafunzo kuanza mashambulizi ya kasi katika upande wa mabanati wa Chui huku wakiwa na tia ya kutoka uwanjani hadi ushindi. Mashambulizi hayo yalianza kuzaa matunda kwa Mabanati wa Mafunzo kuanza kujipatia seti ya kwanza bila ya tabu yoyote huku wakicheza kwa ari kubwa. Kipigo ambacho kiliwafanya akina dada wa timu ya Chui nao kuanza kuongeza ari ya mchezo na ushindani mkubwa ili nao waweze kurejesha kipigo hicho na hatimae kuwaongeza seti zilizosalia.Ngarambe hizo ziliendelea kwa kwa Mabanati wa Mafunzo kujipatia seti ya pili na kuwafanya mashabiki wa timu ya Chui kukata tamaa ya ushindi wa mechi hiyo. Hata hivyo seti hiyo iliwafanya akina dada wa timu ya Chui kuanza kupagawa kwa kipigo hicho na kuwapa nafasi nzuri mabanati wa Mafunzo kwa kuwamalizia Seti ya tatu bila ya majibu yoyote.Endelea kusoma habari hii.

KUWENI WAADILIFU-SEREWEJI

WAAMUZI nchini wametakiwa kuwa waadilifu wakati wanapokuwa wanachezesha michuano mbali mbali ili kuhakikisha kiwango cha mchezo wa mpira wa miguu kinapanda.Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Mwanakwerekwe Haji Juma Sereweji alipokuwa akizindua michuano ya ligi ya Majimbo ndani ya Wilaya ya Magharibi huko katika uwanja wa Kiembesamaki.Alisema waamuzi hao wanatakiwa kuwa waadilifu zaidi ili kuweza kuinua kiwango hicho cha soka nchini kwa kuwa baadhi ya waamuzi wamekuwa wakishindwa kufanya uadilifu katika uchezeshaji.Mbunge huyo alisema waamuzi wamekuwa ni wahimili wakuu katika soka hivyo hawana budi kutumia ujuzi huo walionao kwa kuzifanya haki pale inapohitajika kufanyika na badala yake kuachana na tabia ya udanganyifu na kuelemea upande mmoja kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha vurugu viwanjani humo.Aidha alisema kuwa michezo ni furaha na hatimae hujenga udugu miongoni mwao hivyo aliwataka wachezaji hao kuitumia fursa hiyo waliyoipata katika kujiendeleza zaidi kisoka ili kufikia katika hatua bora na kuhatimae kupatikana timu bora ya wilaya na hadi taifa.Endelea kusoma habari hii

TUNAVUNJA KAMBI YETU- SIMBA

P1040325TIMU ya Wekundu wa Msimbazi leo inatarajia kuvunja kambi yake rasmi ya muda wa wiki tatu iliyokuja kujipasha misuli visiwani hapa na kujiandaa kuondoka na kuelekea Jijini Dare-es Salaam kwa ajili sherehe pamoja na kushiriki ligi kuu ya Tanzania Bara. Akizungumza na gazeti hili Meneja wa timu hiyo Innocent Njovu, huko Chukwani nje kidogo ya Mjini wa Zanzibar, alisema kuwa kikosi chake kimelazimika kuondoka visiwani humu baada ya kukamilisha wiki tatu zilizopangwa awali na uongozi wa timu hiyo.Menje huyo alisema kwamba kwa upande wa wachezaji wake wanaonesha kuwa wapo tayari kwa ajili ya kinyanganyiro cha ligi kuu pamoja na yale ya shirikisho la soka Barani Afrika. “Sina wasi wasi na kikosi changu, hivi sasa kipo katika hali nzuri ya kiushindani na pia nipo tayari kukikabili kikosi chengine chochote ambacho tutakachopangiwa katika mashindano ya ligi kuu”alisema Njovu kwa kujiamini. Hata hivyo alifahamisha kuwa ni matarajio yake makubwa kuwa kambi walioifunda visiwani humu itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa sana katika kuitangaza timu hiyo katika medani ya soka nchini na nje ya nchi. Alisema katika kipindi chote walichokaa visiwani humu wameweza kujifunza mbinu mbali mbali za michezo pamoja na kuwaweka katika hali ya ukakamavu wachezaji wake wote waliokuwa chini ya kocha Mzambia Patrik Phiri ambaye ni kocha mashuhuri kwa kunowa timu. Endelea kusoma habari hii

EDI BUSHIRI ACHUKULIWA MORO UNITED

TIMU ya Soka ya Taifa ya Zanzibar chini ya miaka 20′ Karume Boys pamoja na ile ya Jeshi la kujenga Uchumi (JKU) zote zimo tabuni baada ya mlinda mlango wao nambari moja Muhammed Abdallah ‘ Edi Bushiri’ kuchukuliwa na timu ya Moro United inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara. Kabla ya kuondoka visiwani humu mchezaji huyo hivi karibuni alizungumza na gazeti hili na kusema kuwa safari yake imemfanya afarajike kwa kuona kuwa matumaini yake ya kucheza soka nje ya Zanzibar yametimilia. Bushiri alisema kuwa kupata nafasi hiyo ya kuchezea katika timu hiyo ameona kwamba kiwango chake katika mchezo wa soka kinaendelea kupanda hatua kwa hatua. “Nimefarijika kupata nafasi hii kuchezea nje ya Zanzibar na nafikiria kuwa nafasi hii itanisaidia kupandisha kiwango changu cha siku hadi siku,”alisema Bushiri alieleza kwamba amesaini mkataba na timu yake hiyo kwa mwaka mmoja wa kushirikiana na Moro United katika kinyang’anyiro cha ligi kuu ya Vodacom. “Nashukuru Soka ni sehemu ya maisha yangu najua nikiwa na timu yangu mpya maendeleo mengi nitayapata.”aliongezea.Endelea kusoma habari hii.

TUNAANGALIA USHINDI TU-SIMBA

KLABU ya Timu ya Soka ya Simba imesema hivi sasa haiangalii mechi yake na timu ya Yanga, bali wanachoangalia ni ubingwa tu, katika Ligi Kuu ya kochaTanzania Bara.Alizungumza na Mwandishi wa habari hizi Meneja wa timu hiyo, Innocent Njovu, huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, alisema kuwa wakati uliobakia sasa sio wa kuiangalia timu ya Yanga kama wataiweza kumudu kimchezo watakapocheza pamoja.Meneja huyo alisema kuwa nafasi ya hivi sasa ni kukiandaa kikosi chake na ngarambe nzima ya ligi kuu, ambayo mara hii inatarajiwa kuwa ya aina yake kwa timu zote kujinoa vema.“Huu si muda wa kuiangalia timu ya Yanga kama tutamudu nayo au laa, ingawa ni mabingwa watetezi, lakini haitupaswi kufanya hivyo tu” alisema Njovu.Meneja huyo aliongeza kwamba “Lakini pia katika ligi kuu hiyo hatutocheza na timu ya Yanga tu, bali kuna chungu ya timu ambazo nazo zina uwezo mkubwa wa mchezo na tunatarajiwa kucheza nazo pia” alisema Njovu.Hata hivyo Njovu alisema kuwa kinachoendelea sasa katika kikosi chake ni kuangalia zaidi ratiba ya ligi hiyo ili kuweza kuisoma timu iliyopo mwanzo kucheza nayo katika utaratibu wao ratiba hiyo.Endelea kusoma habari hii

UGOMVI WA VIONGOZI WAUTUATHIRI

TIMU ya Soka ya Simba imesema malumbano kati ya Mwenyekiti wa klabu hiyo Hassan Dalali pamoja na makamu wake Omar Gumbo, bado hayajaathiri kambi ya mazoezi visiwani Zanzibar.Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni Meneja wa timu hiyo Innocent Njovu, huko Chukwani nje kidogo ya Mjini wa Zanzibar wakati timu hiyo ikipata dozi la mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuwaandaa na ligi kuu Tanzania bara.Njovu alisema kuwa pamoja na malumbano yasio na msingi kwa viongozi hao lakini kwa upande wa kambi yao bado yajajaleta athari ya aina yoyote mimiile.Alifahamisha kuwa malumbano ya viongozi hao kwa upande wake haweza kuyasimulia hata kidogo, kutokana na wenye kazi ya kusimulia kadhia hiyo ni viongozi maalum wa timu hiyo.“Siwezi kusimulia kuhusu hali ya malumbano kwa viongozi wetu hao kutokana na wenye kazi hiyo sio mimi” alisema.Hivyo alifahamisha kuwa kambi ya timu hiyo iliyopo Zanzibar kwa uda wa wiki tatu inaendelea vizuri na wala hawategemei kuyumba, bali wanategemea kuongeza ari kubwa ya mchezo.Endelea kusoma habari hii

HATUJABAHATISHA-WACHEZAJI

simbaWACHEZAJI watatu wa kigeni wa timu ya Simba, Emmanuel Okwi, Joseph Owino pamoja na Hilary Echesa, wamesema kujiunga na timu hiyo sio kitendo cha kubahatisha wala kutapatapa bali walisema kuwa kutokana na hadhi kubwa iliyonayo timu hiyo katika ukanda wa Mashariki wa Bara la Afrika ndio sababu kuu iliyowafanya kujiunga nayo.Wachezaji hao waliyasema hayo wakati wakizungumza na gazeti hili huko Chukwani nje kidogo ya Mjini Zanzibar ambapo ndipo ilipo kambi ya timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na ligi kuu ya Tanzania Bara.Vinara hao walizidi kufahamisha kuwa hadi hivi sasa hawana wasi wasi juu ya kujiunga na Simba katika kilisakata kabumbu na wataendelea na mazoezi kwa lengo la kufanikisha mazoezi hayo.Wachezaji hao waliahidi kufanya vyema katika kitimtim cha ligi kuu ya Tanzania bara pamoja na ile ya Shirikisho barani Afrika hapo mwakani.Kwa upande wa mazoezi kwa timu hiyo kuingia machimboni visiwani humu walisema kuwa uongozi wa timu hiyo umefanya maandalizi ya kisayansi na kwamba hawajapata kuyaona katika timu zao wanazotoka.Endelea kusoma habari hii.

MASHABIKI WATAKA MECHI YA SIMBA ZNZ

MASHABIKI wa mchezo wa mpira wa miguu visiwani Zanzibar wamesikitishwa na hatua ya timu ya Simba iliopo visiwani hapa kuondoka bila kuonesha mchezo mmoja katika viwanja vya Zanzibar.Hatua hiyo bebanatobanaimekuja baada ya viongozi wa timu hiyo kutaka kuondosha timu bila ya kucheza mchezo mmoja jamo ambalo mashabiki hao wamesema hawatokuwa radhi kwa timu yao kufanya mazoezi wiki tatu wakiwa visiwani na kuondoka bila ya kuwaona wakicheza mechi hata moja.Malalamiko hayo yamekuja kufuatia taarifa za awali kuwa timu hiyo itamaliza ziara yake ya mazoezi bila ya hata kucheza mechi moja katika viwanja vya Zanzibar.Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini hapa mashabiki hao wamesema pamoja na kupata faraja kwa timu yao kufanya usajili wa kutisha na kuamua kua Zanzibar kwa mazoezi maana yote itatoweka iwapo timu yao itaondoka bila ya kucheza mechi na kuwaridhisha wapenzi wa soko visiwani hapa.Endelea kusoma habari hii.

JANGOMBE UNAKABILIWA NA UKATA

WAKATI michuano ya majimbo wilaya ya mjini ikipamba moto timu ya jimbo la Jang’ombe ipo katika hali mbaya kutokana na kukabiliwa na ukata na nusura isishiriki michuano hiyo.Uchunguzi umebaini timu hiyo ilifanikiwa kufanya usajili katika dakika za majeruhi kwa ukosefu wa fedha hali iliyopelekea kushindwa hata kufanya mazoezi hivi sasa. Habari kutoka mmoja kati ya viongozi wa timu hiyo aliyekataa jina lake kutajwa amesema hata mechi ya kwanza ilipocheza na jimbo la Mpendae timu hiyo haikuwahi kufanya mazoezi hata siku moja.“Tumekuwa kama yatima asiyekuwa na wazazi maana tulikuwa tayari tunafikiria kujitoa katika mashindano kwa kukosa uwezo na hatujui huko mbele itakuwaje” alisema shabiki huyo.Endelea kusoma habari hii.


HATUMPI ADHABU MHUNZI-CUF

CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimesema licha ya Mwakilishi wake Abass Juma Muhunzi kukaidi amri ya uongozi wa chama hicho kutokwenda Dodoma kushiriki katika michezo na timu ya bunge chama hicho Abass Juma Mhunzi (CUF)Chambanihakitomuadhibu kamwe.Hayo yalisemwa na Mnadhimu wa baraza la wawakilishi kambi ya upinzani Haji Faki Shaali wakati alipoulizwa kuhusu hatua zipi za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya Mwakilishi huyo kwa kukaidi amri ya chama.‘Hatuna mpango wa kumpa adhabu yoyote ile ingawa ni kweli alikaidi amri ya chama…sisi tuliamuwa kutokwenda Dodoma kushiriki katika michezo na timu ya Wabunge na Wawakilishi lakini yeye alipinga uamuzi huo hivyo ni uamuzi wake kushiriki hakutaka kutusikiliza sisi hatuna lolote la kumfanya katika uamuzi wake”alisema Shaali.Shaali alisema huo ni uamuzi wake na alichofanya ni sawa sawa na chama hakitokaa kumjadili na kumpa adhabu kwa kuwa kila mmoja ana maamuzi yake licha ya kuwa anapaswa kusikiliza maamuzi ya chama lakini kama hataki kusikiliza hilo ni juu yake.Wiki iliyopita timu ya baraza la wawakilishi ilifanya ziara kwenda Dodoma kushiriki michezo mbali mbali na timu ya wabunge katika ziara ya kudumisha uhusiano na mashirikiano mazuri ya kudumisha muungano kati ya tanznaia bara na Zanzibar. Endelea kusoma habari hii.

UGANDA MABINGWA NETIBOLI

mshindiMABANATI wa Timu ya Uganda walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika katika mashindano ya kimataifa ya vijana waliochini ya umri wa miaka 21, baada ya kuwalaza wenyeji wao kwa mabao 60-26, katika pambano la fainali lililochezwa Kiwanja cha Jimkanah Mjini Unguja Mkoa wa Mjini Magharibi. Fainali hiyo ambayo ilichezwa majira ya saa 10:30 jioni katika sherehe hizo za mchezo huo zilihudhuriwa na wananchi mbali mbali waliongozwa na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Shadya Karume, ambae ndie aliyekabidhi zawadi kwa washindi hao walioshinda katika mashindano hayo. Mabanatio wa Uganda walionekana kuwabana mno wapinzani wao katika mashindano hayo iliweza kuidhibiti kikamilifu ngome yao na kuzidhia mashambulizi langoni kwa wapinzani wao, ambapo kota ya kwanza ilimalizika wakiongoza kwa kuwa na mabao 13-9, huku wakienda mapumziko wakipata mabao 26 na Tanzania 14. Tanzania ambayo ilizidiwa kwa kila idara ilijitahidi kucheza kwa uangalifu ili kukimbia kuingiziwa mabao mwengi lakini wafungaji wao Siamini Ramadhan na Fatma Yasoda, ambao walishindwa kuingizia mabao mengi timu yao, kutokana na kuwekewa ukuta mgumu katika lango la wapinzani wao. Endelea kusoma habari hii.

RUDISHENI HESHIMA YA MICHEZO ZNZ

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kurudisha mfumo wa ligi kuu ya Muungano ili kuleta DSC01756ushindani wa soka nchini.Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa Jimbo la Gando (CUF) Said Ali Mbarouk wakati akichangia makadirio mapato na matumizi ya bajeti ya wizara ya habari, utamaduni na michezo kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika baraza la wawakilishi mjini hapa.“Katika kuimarisha na kuleta ushinsani wa soka ipo haja ya kurudisha ligi kuu ya muungano ambayo ilikuwa na msisimko wa hali ya juu na ushindani katika mchezo wa mpira wa miguu.”alisema Mbarouk.Alisema ligi kuu ilileta usdhindani mkubwa katika mchezo wa mpira wa miguu,na kusaidia kuleta ushindani wa soka kati ya timu za Zanzibar pamoja na zile kutoka Tanzania Bara.Mbarouk ambaye alikuwa mmoja ya wachezaji mpira waliowahi kuzichezea timu mbali mbali kisiwani Pemba alisema soka kwa sasa imepoteza hadhi yake pamoja na vilabu kuporomoka.Alisema katika miaka ya 1985-95 vilabu ya Miembeni,Small Simba pamoja na Malindi vilikuwa na hadhi kubwa pamoja na kupata umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kwa uwezo mkubwa wa wachezaji wake kurandaza kandanda.Endelea kusoma habari hii.

SMZ YAKERWA NA MALUMBANO YA ZFA NA TFF

bwana kifupiSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesikitishwa na malumbano yanayoendelea ambayo hana lengo la kujenga na kusongeza mbele soka nchini kati ya viongozi wa taasisi mbili za michezo.Malumbano hayo ni kati ya Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambayo yameelezwa kutokuwa na faida yoyote kwa wananchi wa Tanzania zaidi ya kudumaza michezo.Waziri wa Habari, Utamaduni Michezo, Ali Juma Shamuhuna wakati akiwasilisha makadirio mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika baraza la wawakilishi mjini hapa.Shamuhuna alisema katika kulipatia ufumbuzi tatizo hilo tayari serikali zote mbili kupitia FIFA nambari ya wageni lazima iwe ndogomawaziri wake wanakusudia kukutana wakati wowote kuanzia sasa.“Mimi na mwenzangu Mkuchika pamoja na Joel Bendera tunakusudia kukutana na kulipatia ufumbuzi tatizo hilo kwa lengo la kuona suala la michezo linaimarika kwa sababu hivi sasa kuna matatizo kwa kuwa malumbano hayeshi kila kukicha” alisema Shamuhuna.Endelea kusoma habari hii

MASHINDANO YA KIKANDA KUANZA JULAI

shamhunaKAMATI ya michuanao ya majimbo kwa upande wa Ungauja, imesema imo katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za mashindamo hayo ambayo yanasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka visiwani hapa.Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa mashindano hayo, Issa Ahmada ofisini kwake Rahaleo Mjini Unguja, alisaema hivi sasa mashindano hayo wamo katika hatua za ukamilishaji wa taratibu za michuano hiyo ambayao yanatarajiwa kuanza Julai 15, mwaka huu.Aliseama kuwa miongoni mwa hatua hizo ambazo hivi sasa zimeanza kufuatiliwa ni kukutana na Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna, ambaye tayari wameshakutana naye na kutoa baraka zake juu ya mashindano hayo.Mweyekiti huyo alifahamisha kuwa Waziri Shamuhuna alitoa baraka hizo kwa kutoa nasaha zake kubwa kwa viongozi wa mashindano hayo ambapo alitaka waandaaji wa mashindano hayo wahakikishe mashindano hayo yanakwenda kwa salama na amani, pamoja na kuhakikisha utaratibu wa wachezaji uwe na mpangilio mzuri na kuepukana na matatizo yanayoweza kutokea katika viwanja vya michezo.Endelea kusoma habari hii.

ZIFF KUANZA LEO ZNZ

WAZIRI Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar (SMZ) Shamsi Vuai Nahodha leo (Jumamosi) anatarajiwa kufungua Tamasha la Kimatafia la Nchi za Jahazi (ZIFF) litakalorindima hadi Julai 4, mwaka huu Ngome Kongwe audience_best_by_Anthony_Turner_DSC_0104Mkoa wa Mjini Magharibi. Akizungumza na wandishi wa habari Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Profesa Martin Muhando katika viwanja vya Ngome Kongwe mjini Unguja, alisema wameamua kumualika kiongozi kuwafungulia tamasha hilo ili kuweza kupata baraka za Serikali. Alifahamisha kuwa wanaamini kuwa watakapopata baraka hizo ni matarajio yao ya kuwa tamasha hilo kuwa la aina yake ambapo aliwataka wananchi kushiriki kwa wingi aktika tamasha hilo. Endelea kusoma habari hii.

NETI BOLI VITUKO VITUPU

MICHUANO ya klabu bingwa ya netiboli Zanzibar yamezidi kuingia katika sura mpya kwa mashabiki na wachezaji kuchagawa kwa kupandisha NETIBOLImashetaji kiwanjani hapo.Hamkani hiyo ya kuchagawa kwa mashabiki na wachezaji hao ilitokea katika mchezo kati ya timu ya wanadada wa Amani ya Mabanati wenzao wa Tukoimara uliofanyika katika uwanja wa Gymkhana Mkoa wa Mjini Unguja. Burudani hiyo ilianza katika robo ya tatu ya mchezo huo, wakati Tukoimara ikiwa na magoli 22 huku Aman wakiwa na 17, ambapo shabiki wa timu hiyo alianza kupandisha shetani aitwae Ruhani na kudai kuwa timu yake imeekewa vizizi katika uwanja huo hali iliyosababisha yeye kupandisha mashetani. Endelea kusoma habari hii.

ZE COMEDY YATINGA ZNZ

KUNDI la maagizo ya vichekesho la Ze Comedy, kutoka jijini Dar-es-Salam linatarajiwa kushiriki katika Tamasha la Kimataifa la Nchi za Jahazi (ZIFF) litakaloanza kurindima jumamosi ijayo katika Visiwani Zanzibar. Kwa mujibu wa habari kutoka kwa Mratibu wa Muziki wa tamasha hilo la ZIFF, Hassan Mussa, zinasema kuwa kundi hilo tayari limeshatoa kauli ya kukubali ushiriki huo katika tamasha hilo. “Kilichobaki hivi sasa ni kusubiri siku tu ya kuwasili visiwani hapa ili kuweza kutoa burudani kwa wapenzi mbali mbali”alisema Hassan. Aidha alifahamisha kuwa lengo la kulialika kundi hilo ni kuupamba ukumbi wa Tamasha hilo ili kila atakayefika aweze kuondoka na furaha kulupitia kundi hilo. Endelea kusoma habari hii.

LIGI KUU YAZIDI KUPAMBA MOTO ZNZ

Kikosi kipya cha MoroccoMICHUANO ya ligi ya mabingwa visiwani hapa imezidi kupamba moto kwa kila timu kuonesha kiwango chake kwa mchezo cha kuwa na matumaini ya kutwaa ubingwa huo. Katika mapambano yaliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana Mjini Unguja timu nne za Wanadada ziliweza kuumana vikali huku kila timu ukicheza kwa vidosho vya hali ya juu. Wanadada hao waliweza kuanza pambano hilo kwa timu mbili baina ya maafande wa JKU, wakiumana na maanti wenzao wa Sogea huku wenzao wakisubiri wamalize ili nao kuingia kiwanjani hapo. Mchezo huo ulikuwa ni mnono kwa maanti wa JKU kwa kuwalaza wenzao hao kwa magoli 79-15. Endelea kusoma habari hii.

FC TATHIBITISHA KUSHIRIKI KAGAME CUP

TIMU ya Soka ya Miembeni ‘FC’ imetoa uthibitisho wake rasmi kwa Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA) wa kushiriki katika michuano ya nchi za Afrika burundi%20440[1]Mashariki na kati, yatambulikayo kwa jina la Kombe Rais Kagame (Kagame Cup). Uthibisho wa timu huo umekuja baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar mwaka jana 2008. Akizungumza na gazeti hili katibu wa timu hiyo Adam Kessi Said, huko Mjini Unguja, alisema timu yake imeamua kutoa uthibitisho huo kutokana hivi sasa tayari wameshajipanga vyema katika ushiriki huo. Matumani makubwa kuondoka nchini Zanzibar ifikapo Juni 24, ya mwaka huu kuelekea nchini Sudan kwa ngarambe hizo. Hata hivyo alifahamisha kuwa kikosi chake hivi sasa kipo katika matayarisho ya kufanya mazoezi zaidi ya kuhakikisha ubingwa mwaka huu unaingia ndani ya nchi ya Zanzibar. Endelea kusoma habari hii.

BAUSI AFUNGIWA MAISHA WADAU WASHANGIRIA

zanteCHAMA cha soka Zanzibar (ZFA), kimepongezwa kwa uamuzi wake wa kumfungia maisha Kocha Mkuu wa timu ya Soka ya JKU, Salum Bausi Nassor kufuatia kufanya shambulizi la hatari kwa muamuzi. Pongezi hizo zimetolewa na baadhi ya wadau na wapenzi wa soka hapa visiwani wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti.Walisema umamuzi wa chama hicho kwa kocha huyo ni mzuri sana na ni njia moja ya kuonesha mikakati yake katika utendaji wao wa kazi katika msimu huu wa ligi kuu ya Zanzibar, lakini pia uamuzi wake huo inawezekana ukawa funzo kwa Makocha wengine. Mmoja wa Wadau hao Abduraman Is-haka alisema chama hicho kinastahiki pongezi kubwa kufuatia adhabu waliyoitoa kwa kocha huyo ikionesha kuwa haina upendeleo wowote kwa kuwa anastahiki kwa alichofanyiwa na itatoa funzo kwa wengine. Endelea kusoma habari hii.

WADAU WACHENI LAWAMA-AHMADA

WADAU wa Soka nchini wametakiwa kuacha tabia ya kuwatupia lawama Wakufuzi wa mchezo huo, kutokana na kasoro za waamuzi. Ushauri huo umetolwa jana na Mkufunzi Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Issa Ahmada, wakati akizungumza na gazeti hili alisema baada ya kutokea vitendo mbali mbali vya kuwalaumu viongozi wa soka. Ahmada alisema ni vyema kwa wadau hao kuacha tabia mbaya hiyo ya kuwapaka matope wakufuzi, tabia ambayo inakwenda kinyume na maadili ya mchezo huo nchini. Ahmada alisema kuwa tabia ya muamuzi kuwa na koroso binafsi wakati wa uchezashaji huwa hazitokani na mkufuzi, bali tabia hiyo huwa ni yake mwenye muamuzi.Endelea kusoma habari hii.

CHABAZA YAAKHIRISHA UCHAGUZI

P1030935UCHAGUZI wa Chama Cha Mchezo wa Netiboli Zanzibar (CHABAZA), umeakhirika kufuatia kukosekana kwa mgombea wa nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho kujitokeza kuchukua fomu ya nafasi hiyo. Kwa mujibu wa habari kutoka kwa Katibu Mkuu wa Baraza taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), Khamis Ali Mzee zinasema uchaguzi huo ulikuwa ufanyike mapema mwezi ujao lakini kutokana na nafasi hiyo kukosa mgombea hivyo imeamuliwa na baraza hilo kuahirishwa kwa muda usiojulikana hadi hapo atakapopatikana mgombea wa nafasi hiyo. Hata hivyo Katibu huyo alizidi kufahamisha kuwa wameamua kuchukua uamuzi huo ili kuweza kuwapa changamoto wale ambao wanataka kugombea nafasi hiyo ambayo muhimu katika utekeleza wa mambo ya chama hicho. Endelea kusoma habari hii.

VURUGU ZATAWALA KIWANJANI PEMBA

Bullfight_znzTIMU ya soka ya Konde Kisiwani Pemba imefanikiwa kwa tabu kupata nafasi ya kushiriki katika michuano ya ligi kuu mwakani baada ya kutoka sare ya goli 1-1, na timu ya Shaba ya kisiwani humo.Katika mchezo huo ulichezwa uwanja wa Gombani Pemba ambapo timu ya Konde walijihakikishia kupanda daraja hilo huku vurugu kali zikitanda kiwanjani hapo wakati mchezo huo ukiendelea.Vurugu hizo zilianza kutokea mwanzoni mwa mchezo huo ambapo kocha wa timu ya Shaba Issa, alilivamia benchi la waamuzi na kuanza kumtwanga makonde Kamisaa Salum Abbas baada ya kutofautiana ambapo kipigo hicho kikiendelea muamuzi wa mchezo huo Asaa Ali alisimamisha mchezo huo kwa dakika chache kwa lengo la kutoa msaada wake kwa mwenziwe huyo.Endelea kusoma habari hii.

MASHINDANO YA COPA COCA COLA YAWADIA

znzJUMLA ya wanasoka ishirini na mbili (22) wameteuliwa kuunda timu ya vijana ya Wilaya ya Kati kwa ajili ya mashindano ya Copa Coca Cola yatakayofanyika jijini Dar es Salaam baadae mwaka huu. Taarifa za Chama cha Soka (ZFA) wilayani humo, zinaeleza kuwa kupatikana kwa wachezaji hao kumetokana na ligi ndogo iliyoshirikisha klabu zote zilizomo ndani ya wilaya hiyo. Endelea kusoma habari hii.

SKWASH YAUNGAMA NA WENZAO DUNIANI

michezCHAMA cha Mchezo wa Skwash Zanzibar kimeungana na vyama vyengine duniani kote kuunga mkono mchezo huo kuingizwa katika mashindano ya Olympic kama michezo mengine inavyofanywa. Chama hicho kimeonesha ushirikiano wao huo kwa kufanya mchezo mdogo uliochezwa na wachezaji wa timu ya Zanzibar Shwash huko katika kiwanja cha Bwawani MjiniMkoa wa Mjini Unguja ambapo katika mchezo huo Omar Yussuf, alimbwaga Bakar Omar kwa seti 3-2, huku Sale beat alimlaza Sebastian kwa seti 3-0 katika pambano la mwisho.Naye kepten wa timu hiyo Nadir Mahfudh mara baada ya kumaliza kwa pambano hilo alisema, mchezo huo walioundaa ni njia moja ya kuonesha umoja na mshikamamo na vilabu mbali mbali vya Skwash duniani kote. Endelea kusoma habari hii.

ZANZIBAR MWENYEJI MPIRA WA MIKONO

Serena na kombe la AustraliaZANZIBAR imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya mchezo wa mpira wa mikono (hand ball) maarufu kwa jina la ‘Urafiki Cup International Open Championship’. Katibu wa Chama cha mchezo huo Zanzibar (ZAHA) Mussa Abdurabbi amesema kuwa michuano hiyo imepangwa kufanyika Oktoba 22-25 mwaka huu. Abdul-Rabbi amesema Zanzibar imepewa nafasi hiyo ili kuwapa fursa mashabiki na wananchi wake kuweza kuishuhudia michuano hiyo mikubwa ya kimataifa. Alizitaja nchi zitakazoshiriki katika mshikemshike huo kuwa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Tanzania Bara, na wenyeji Zanzibar pamoja na Kenya itakayoshiriki kama timu mualikwa. Endelea kusoma habari hii.

 

POLISI WASHINDWA KUTAMBA MBELE YA MALINDI

TIMU ya Soka ya Polisi imeshindwa kuwatambia masarahange wa Malindi baada ya kuoka sare ya goli 1-1 katika michuano ya ligi kuu ya Zanzibar DSC04699inayoendelea visiwani hapa. Masarahange hao walishindwa utambiwa huko katika uwanja wa Maotse tung, baada ya kuonesha kipaj chao cha mchezo katika mchezo o ambao ulihudhuriwa na mashabiki wengi wa soka kutoka kona mbali mbali zaUnguja wakiwa na lengo la ubudisha nyoyo zao. Masarahange hao waliweza kuonesha soka safi wakati wa kipindi cha kwanza na kuwawacha mashabiki kutoamini kama ni wao wakongwe wa ligi hiyo, na kupelekea kupata bao la kwanza katika dakika ya 44, kupitia mchezaji Fadhili Ibrahim ambapo mchezo huo ulikuwa umebakisha dakika moja tu kwenda mapumziko.Endelea kusoma habari hii.

FC NUNGWI YAICHARAZA HARD ROCK 1-0

TIMU ya soka ya Nungwi ‘FC’ imeicharaza Hard Rock ya Pemba goli 1-0, katika michuano ya ligi kuu ya Zanzibar inayoendelea kutimua vumbi. Katika pambano hilo ambalo lilikuwa na upinzani mkubwa kwa timu hote mbili kila moja ikiwa na matumaini ya kutaka kuondoka uwanjani hapo ikiwa kifua mbele dhidi ya mwenzake. Lakini huku kiwanjani hapo kukiwa na uhaba wa mashabiki waliofika kwa ajili ya kungalia soka hili na kuzipa moyo timu hizo za kongeza bidii za mchezo. Mkumange huo uliendelea kuchezwa kwa kasi katika kipindi hicho cha kwanza kwa timu zote mbili kushambuliana kwa zamu. Endelea kusoma habari hii.

MIEMBENI YAICHAPA JAMHURI 1-0

TIMU ya Soka ya Miembeni imeendelea kutoa kipigo cha mbwa kwa Eto'o akibebwa kwa macherakuicharaza Jamhuri ya Kisiwani Pemba bao 1-0 katika michuano ya ligi kuu ya Zanzibar inayoendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar. Mabingwa hao wa soka Zanzibar timu ya Miembeni walitoa kipigo hicho kwa tabu sana huko katika mchezo uliochezwa uwanja wa Mao tse tung Mkoa wa Mjini Unguja. Katika mchezo huo ambao ulikuwa na matumaini makubwa kwa mashabiki wa waliohudhuria ya kuwa hadi kumalizika dakika 90, timu zote zikatoka kiwanjani bila ya kufungana. Matumainia hayo ya mashabiki yalianza toakea kuanza kwa mchezo huo kuafuatia wanandinga hao wote kuweza kumiliki mpira vyema. Endelea kusoma makala hii.

VIJANA ELFU SABA KUWASHA MISHUMAA ZNZ

JUMLA ya zaidi ya Vijana 7,000, kutoka Mkoa ya Mjini Unguja audience_best_by_Masoud_Khamis_DSC01201wanatarajiwa kushiriki katika maadhimisho ya uwashaji wa Mshumaa mweupe yanayotarajiwa kufanyika leo (Jumapili) nchini hapa. Ambao vijana hao watakuwa kati ya umri wa miaka 10 hadi 24 ambao hivi sasa inaonesha kuwa ndio wanaoathirika zaidi la janga hilo. Akizungumza na Wandishi wa habari Afisa mtendaji kitengo cha Familiy Heath International, Nyasingo Emmanuel jana huko ukumbi wa Hoteli ya Mjini Unguja.Alisema maadhimisho hayo ya uwashaji wa mshumaa, yanalengo la kuwakumbuka ndugu na jamaa waliofariki kutokana na janga hatari la ukimwi. Ambao kati yao walifariki kwa walifariki kwa ngono na wenine walifariki kwa kuambukizwa kwa njia zisizo kuwa za mgono.Endelea kusoma habari hii.

MAFUNZO YATOKA SARE YA 2-2 NA POLISI

TIMU ya Soka ya Maafande wa Mafunzo imeshindwa kuitambia timu ya Saviola kuihama Barcelona yayumkinikaPolisi baada ya kutoka sare ya 2-2 katika mashindano ya ligi kuu ya Zanzibar , inayoendelea kisiwani hapa. Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake kwa timu zote mbili kila moja ikionesha ubabe dhidi ya mwenzake, na kuwawacha mashabiki wa soka kiwanjani hapo kukaa midomo wazi. Harambee hizo zikiendelea mafande wa Mafunzo katika waliweza kuwazidi wenzao hao katika kipindi cha kwanza ingwa nao walikuwa hawakubali kuonesha udhaifu wao. Mchezo huo uliendelea kwa kuwaburudisha watazamaji kwa vinara hao wa Mafunzo kwa kuzitikisha nyavu za wenzao kupitia mchezaji wao Sadiki Habib mnamo dakika ya 18, ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo.Endelea kusoma habari hii.

MIEMBENI YAONESHA UBABE

MABINGWA watetezi wa Soka Zanzibar Miembeni FC, imeonesha ubabe wake baada ya kuitwanga timu ya Kizimbani ya Pemba mabao 2-0 katika mashindano ya ligi kuu ya Zanzibar yanayoendelea nchini hapa. Watetezi hao waliwanyanyasa vibaya wachuma karafuu hao wa Pemba huko katika uwanja wa Mao Mjini ungunja.Manyanayaso hayo yalianza mapema kwa timu ya Miembeni kwani mnamo dakika ya 19, ya kipindi cha kwanza waliweza kuwazawadia bao la kwa lililofungwa na mchezaji Issa Othman, na kuwafanya wapemba hao kuchachawa kwa kipigo hicho. Bao hilo liliweza kuwafanya Mashabiki wa Miembeni kuzidisha kidedea cha kasi kiwanjani hapo wakiwa na lengo la kuwatia moyo wachezaji wao na kuwafanya wapinzani wao kukosa uhuru wa kutawala mchezo huo kiwanjani hapo. Endelea kusoma habari hii.

ZFA IFANYE UCHUNGUZI

CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimetakiwa kufanya utaratibu wa kuandaa kikosi maalum cha uchunguzi wa matatizo viwanjani wakati michezo inapoendelea ili kuweza kuepusha kati ya waamuzi na vilabu. Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wadau wa soka nchini hapa wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti hivi karibuni. Walisema ipo haja kubwa kwa chama cha soka kuangalia uwezekano kwa kuandaa kikosi cha ufuatiliaji wa matatizo ya soka ili kuweza kuondosha hali ya tupiana lawama baina ya chama na vilabuh ambayo hivi sasa imekuwa ikizidi. “Ni vyema kuandaliwa kikosi maalum ambacho kitaweza kuangalia makosa yanayokea kiwanajani hapo katyi ya waamuzi na vilabu na baadaye kuweza kutafuta njia sasa ya kuyatatua”walisema. Endelea kusoma habari hii.

MBIO ZA BAISKELI ZAANZA ZNZ

CHAMA cha Mbio za Baiskeli Zanzibar (CHABAZA) kimeanza mashindano madogo ya kuwasaka wakimbiaji bora ambao wataweza kuunda timu ya Taifa ya Zanzibar. Kwa mujibu wa habari kutoka kwa Katibu wa mashindano hayo Wilaya ya kati Unguja, Abdalla Bodi zinasema kuwa chama chake kimeamua kufanya mashindano madogo hayo ili kuweza kuibua kwa wakimbiaji wenye vipaji bora ambao wataweza kuunda timu ya taifa. Aidha alifahamsha kuwa katika mashindano hayo madogo wameanza kufanya zoezi hilo la kutafuta wakimbiaji bora katika Mikoa mitatu ya Unguja tu, na baadae kwenda kisiwani Pemba. Hata hivyo katibu huyo alifahamisha kuwa mara baada ya kupatika kwa vijana bora kutoka Unguja na Pemba wataweza kuunda timu moja ambayo itatambulika kwa jina la timu ya taifa ya Zanzibar. Endelea kusoma habari hii.

WANAMICHEZO MSILAUMIANE

WANAMICHEZO wa Soka nchini wametakiwa kuacha vitendo cha kutupiana lawama zisizokuwa za msingi na badala yake kuzidisha gushirikiano baina yao ili kuweza kukuza vipaji vyao vya michezo. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afisi ya Waziri kiongozi Zanzibar, Hamza Hassan Juma, wakati akikabidhi vifaa mbali mbali vya michezo kwa timu za Jimbo kwake ikiwa ni moja ya ahadi alizotoa.Hamza alisema ni vyema kwa wanamichezo wote kuacha tabia hiyo mbaya ambayo kama itaendelea ni wazi kuwa inaweza kuleta madhara makubwa michezoni na katika jamii. Aidha alifahamisha kuwa mifarakano mingi katika timu inatokea kufuatia kutowepo kwa umoja wa uhakika kati ya viongozi na wanamichezo jambo ambalo si zuri hata kidogo. Endelea kusoma habari hii.

VODA KUZIPIGA JEKI TIMU ZNZ

Kampuni ya simu za mikono ya Vodadacom Tanzania jana, imemkabidhi Naibu Waziri wa habari ,Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo jezi kwa ajili ya timu za soka ziliopo Zanzibar. Meneja Mauzo wa Kampuni ya Vodacom, Macfadyne Minja alimkabidhi Naibu Waziri huyo seti 18 za jezi za mpira wa miguu katika hafla iliofanyika katika ofisi ya Vodacom iliopo Mkoa a Mjini Unguja Minja alisema msaada huo utaleta mashirikiano mazuri ,baina ya Kampuni yake na vilabu vya soka visiwani Zanzibar kasa katika dhana nzima ya kuinua vipaji vya michezo ambazo vinaonekana kuzorota kwa muda mrefu visiwani hapa. Endelea kusoma habari hii.

ZFA KUISHAURI SMZ

CHAMA Cha Soka Zanzibar (ZFA) kiakusudiwa kuishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kubadilisha utaratibu wa kuzipa msaada mapema timu zinazowakilisha nchi katika michuano ya kimataifa baada ya kubainika kuwa misaada hiyo hutumika kwa malengo yasiyokusudiwa. ZFA imesema kwa kawaida serikali huzipa msaada wa shilingi milioni kumi kwa kila timu kwa ajili ya kuzisadia katika michuano hiyo hasa pale wanapokaribia kucheza mechi za nyumbani dhidi ya timu ngeni. Alisema msaada huo unalenga zaidi kuzisaidia timu hizo kwa ajili ya kuzisaidia huduma za chakula na malazi timu ngeni katika hoteli zinazochaguliwa kifikia,lakini imebainika msaada huo hutumika kinyume na mtazamo wa serikali. Endelea kusoma habari hii.

ZFA YANG’OA MABANGO YA WADHAMINI

 

AmbaniTimu ya Soka ya Taifa ya Tanzania, juzi ilianza mazoezi katika uwanja wa Mwenyekiti Mao-Tsetung Mjini Unguja, idadi ya wamashabiki ilikuwa imesheheni katika kila kona ya uwanja huo. Kama inavyoofahamika, Timu hiyo inadhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, ZFA Iliamuru kuondolewa kwa mabango yaliyowekwa na Taifa Stars ya Mdhamini wao kikidai kuwa matangazo ya ulevi hayaruhusiwi Visiwani Zanzibar. Maswali mengi yalinijia huku majibu yake yakiwa yenye utata, kwanza ni lini Baraza la Wawakilishi lilipitisha sheria ya kukataza matangazo ya ulevi? na kama sio Baraza ni tangazo namba ngapi la Serikali lililopiga marufuku? Endelea kusoma habari hii.

 

WADHAMINI WACHACHE

naibuSerikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema katika mashindano ya fainali ya Thabit Kombo Cup baadhi ya wafadhili wachache wamejitokeza watakaochangia katika kudhamini kikombe hicho ambapo Future Century wamechangia fedha taslim shilingi millioni 1.1 Hayo yameeleza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mahmoud Thabit Kombo wakati akijibu maswali mbali mbali katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Zanzibar. Kombo alisema fedha hizo zilizotolewa ni za washindi watakaonyakua nafasi za kwanza, wapili na watatu katika mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika leo Kisiwani Pemba. Endelea kusoma habari hii.

UFAHAMU MDOGO WALETA MIGOGORO

CHAMA Cha Soka Zanzibar (ZFA) kimesema uelewa mdogo miongoni mwa wadau wa soka visiwani hapa juu ya suala la udhamini wa ligi kuu visiwani linachangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa migogoro kati ya vilabu na chama hicho. Hivi karibuni vilabu vya soka vya Zanzibar vilitishia kususia vifaa vilivyotolewa na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mikononi ya ZANTEL na kufikia hatua ya kugomea ligi hiyo. Hatua hiyo ya vilabu imedaiwa ni kutokana na imani yao kuwa ZFA imeficha mkataba ambao vilabu walitaka wauone kwanza huku ZFA ikijitetea kuwa mkataba huo ulikuwa haujawasilishwa kwao na ZANTEL. Endelea kusoma habari hii.

ZFA, VILABU WAPATANA

HATIMAE mvutano uliojitokeza kati ya umoja wa vilabu na Chama Cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) umekwisha baada ya pande mbili hizo kufanya kikao cha pamoja na kupitia mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya Zanzibar. Awali vilabu vya soka viliishutumu ZFA kuwa imeficha mkataba wa udhamini wa Kampuni ya simu za mkononi ZANTEL kwa dhana ya kutozingatiwa maslahi yao kiasi cha kutishia kususia ligi kuu ya Zanzibar kutofanyika au kuahirishwa. Habari zinasema Meneja wa matukio na udhamini wa mdhamini wa ligi hiyo (ZANTEL) June Warioba ndiye aliyeviridhisha vilabu kwa kusema mkataba huo waliowasilisha ZFA hapo juzi na hakuna ubabaishaji wowote uliotokea kati yake na Chama Cha Soka Zanzibar. Endelea kusoma habari hii.

SAUTI ZA BUSARA ZAANZA

DSC04895Tamasha la Sita la Sauti za Busara Zanzibar limepangwa kufanyika Febuari 12 hadi 17 litawakusanya wasanii mbali mbali kutoka ndani na nje ya Tanzania ambapo baadhi yao ni wasanii mashuhuri ulimwenguni hasa katika fani ya sanaa za muziki. Tamasha hilo ambalo litarajiwa kuwavutia wasanii wengi wakiwemo wageni litafanyika katika ukumbi wa Ngome Kongwe uliopo eneo la Mji Mkongwe ambao mbali ya kuwa ni kivuti kwa watalii wengi kutokana na majengo yake lakini pia Mji Mkongwe umo katika urithi wa kimataifa. Endelea kusoma habari hii

ZFA YAIJIA JUU TFF

Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA) kimelitahadharisha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya kuidhinisha wachezaji kutoka Zanzibar kucheza ligi Tanzania Bara wakati wachezaji hao hawajakamilisha taratibu za kikanuni. Baadhi ya wachezaji kutoka timu za Zanzibar wameidhinishwa kucheza ligi kuu ya Vodacom bila ya kufuata kanuni hizo ambazo si ngeni kwani wale wanaokuja kucheza Zanzibar Chama Cha Soka Visiwani hapa huzingatia kuwa wamehama kwa mujibu wa kanuni za TFF. Endelea kusoma habari hii

ZFA YAWAJIA JUU WATANGANYIKA

Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA) kimetoa tahadhari kwa baadhi ya vilabu vya Tanzania Bara ambavyo vimesajili wachezaji kutoka Visiwani Zanzibar bila ya kufuata taratibu za uhamisho zinazohusika. Msemaji wa Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA) Maulid Hamad Maulid, amewaambia waandishi wa habari kwamba kwa mujibu wa kanuni za ZFA uhamisho unapaswa kufanyika kwa kufuata taratibu na sio kusajili bila ya kuzingatia sheria zilizowekwa. Endelea kusoma habari hii

Advertisements

5 Replies to “Michezo”

  1. Viwanja vya znz havina kaz maalumu mara sherehe za muungano.mara mashindani ya punda na ng’ombe.viwanja vya soka znz bado hamna.wachenzaji wapo lakin viwanja ndo hamna@sijui lini michezo itakua waziri wa michezo kawa waziri wa wariba@

  2. I need to say, as very much as I enjoyed reading what you had to express, I couldnt support but lose interest following a while. Its as should you had a good grasp on the subject matter matter, but you forgot to include your readers. Perhaps you should think about this from more than one angle. Or perhaps you shouldnt generalise so much. Its far better if you take into consideration what others may have to say rather than just going for the gut reaction for the theme. Consider adjusting your own thought procedure and giving other people who may study this the benefit of the doubt.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s