Siasa

Tumechoka mgombea urais kuchaguliwa Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar, kimeeleza nia yake ya kutaka kuachiwa mamlaka ya kumchagua mgombea urais wa visiwa hivyo, badala ya utaratibu wa sasa unaoshirikisha wenzao wa Tanzania Bara. Pamoja na hatua hiyo, chama hicho pia kinafikiria kurejea mtindo wa kupokezana kiti cha urais wa Tanzania kati ya bara na visiwani kama ilivyokuwa awali, ili kuweka usawa katika Muungano. Hatua hiyo inaelezwa kuwa huenda ikazua mpasuko na malumbano mapya kuhusu suala la urais ndani ya CCM, ambako harakati za baadhi ya wanachama wake wameanza kupiga mbio za kuutaka urais katika uchaguzi mkuu wa 2015. Akizungumza katika mahojiano maalumu visiwani humo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, alisema kwa sasa suala hilo linajadiliwa na kwamba ana matumaini kuwa litapatiwa ufumbuzi. Endelea kusoma habari hii

Natarajia ZEC ijayo itajiamini – Maalim

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Sharif ameelezea matarajio yake kuwa tume mpya ya uchaguzi itakayoundwa Zanzibar itafanya kazi kwa kujiamini zaidi ili kukidhi matakwa ya wananchi.Amesema iwapo Tume ya uchaguzi itafanya kazi kwa kujiamini na kuacha kufuata matakwa ya wanasiasa, itajenga imani kwa wananchi juu ya uwezekano wa kuwepo kwa chaguzi huru na za haki. Maalim Seif ameeleza hayo leo nyumbani kwake Mbweni Zanzibar, wakati akizungumza na wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC waliofika kwa ajili ya kumkabidhi ripoti ya utendaji wa tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano, pamoja na kumuaga baada ya kumaliza muda wao wa utumishi ndani ya tume hiyo. Amesema kazi iliyofanywa na tume hiyo ni nzuri, lakini tume inayokuja inapaswa kujifunza kutokana na tume hiyo ili kufanya kazi zake kwa kufuata misingi ya sheria na kuongeza ufanisi wa Tume.Ameelezea haja kwa tume hiyo kuanzisha  mfuko wake, ili mapato ya tume yaingie moja kwa moja katika mfuko huo na kupunguza usumbufu wakati tume inapohitaji fedha kwa ajili ya matumizi yake ya kawaida. Endelea kusoma habari hii 

Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar wamaliza muda wao

Joto la Uchaguzi miongoni mwa Viongozi wa vyama vya siasa sambamba na wanachama pamoja na wapenzi wa vyama vya siasa litapungua au kuondoka kabisa endapo Tume ya Uchaguzi itaendelea kuwa karibu na washirika wake. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar { ZEC } Ndugu Khatibu Mwinchande alisema hayo wakati yeye na wajumbe wa Tume hiyo walipokuwa wakimuaga rasmi  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakikaribia kumaliza muda wao wa utumishi wa miaka mitano unaomalizika  Januari Mosi 2013. Ndugu Khatib Mwinchande ambae katika mazungumzo hayo akimkabidhi Balozi Seif  Ripoti kamili ya Utumishi wao wa Miaka Mitano alisema ukaribu wa Tume ya Uchaguzi kwa washirika wake ndio njia pekee ya kuondosha malalamiko au dhana potovu ya wadau hao dhidi ya Tume hiyo. “ Ni mara ya kwanza katika Historia ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kutoa fursa  kwa Vyama vya Siasa kupatiwa fursa ya kulikaguwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Hii ni ishara kwa Tume hii kuwa karibu na wadau wake ili kupunguza  joto la Uchaguzi”. Alifafanua Ndugu Khatib Mwinchande. Endelea kusoma habari hii

Wazanzibari wametumia fursa yao vizuri- Jussa

Mwakilishi wa Jimbo la Mjimkongwe Ismail Jussa Ladhu, amesewa Wazanzibar wameitumia vyema fursa yao ya kutoa maoni, tofauti na ilivyoelezwa na baadhi ya wajumbe wa Tume wa kukusanya maoni. Jussa ametoa kauli hiyo mwishoni jana wakati akihutubia mkutano maalum wa hadhara wa Chama hicho kwa ajili ya kuuaga mwaka 2012, uliofanyika viwanja vya Kibanda Maiti Zanzibar. Amefahamisha kuwa maoni waliyoyatoa Wazanzibari ni sahihi na wala hawakupoteza fursa hiyo kama ilivyodaiwa, ikizingatiwa kuwa suala la msingi kwa Zanzibar ndani ya Muungano ni “Muungano wenyewe” kwa vile Zanzibar ina katiba yake ambayo imeweka wazi juu ya masuala yote yanayohusu nchi ya Zanzibar. Mwakilishi huyo amewaambia wanachama wa chama hicho kwamba wazanzibari ni watu wenye upeo mkubwa katika masuala ya siasa na ni watu wenye kufahamu ya nchi yao na ndio sababu ya kudai nchi yao kwa kuwa wanajua Zanzibar imenyimwa mamlaka yake tokea kuingia katika muungano. Naye kwa upande wake mgeni rasmi katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema mwaka 2012 umekuwa na umuhimu wa kipekee katika historia ya kisiasa Tanzania. Amesema ndani ya mwaka huu unaomalizika Watanzania katika mikoa yote wamepata fursa ya kutoa maoni yao juu ya uundwaji wa katiba mpya ya Tanzania ambayo yatatoa mwelekeo imara wa mustakbali wa nchi. Endelea kusoma habari hii

Tanzania inahitaji mikakati ya kuendeleza kilimo- Lipumba

Tanzania inahitaji mabadiliko kwa kuwekeza katika kilimo cha kisasa sambamba na kutoa elimu na huduma bora kwa wakulima ili waweze kuendeleza kilimo chenye tija. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhra wa chama hicho uliofanyika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutba inayokubali kuotesha mazao mbali mbali, lakini bado hakujakuwepo na mikakati imara ya kuendeleza kilimo, jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi kwa maslahi ya wananchi.Prof. Lipumba amefahamisha kuwa Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa Mikoa inayoweza kufanya vizuri katika kilimo kutokana na kuwepo kwa maziwa na mito ya kudumu ambayo inaweza kutumika kwa kilimo cha mboga mboga na umwagiliaji, na kusaidia kukuza kipato cha wakulima.Sambamba na hilo Prof. Lipumba amewataka wakulima kutilia mkazo mazao ya nafaka yakiwemo mahindi na maharage, kutoka na kuongezeka kwa bei  ya mazao hayo katika soko la dunia. Mwenyekiti huyo wa CUF Taifa pia amesisitiza haja ya kuwepo kwa mikakati ya makusudi ya kuongeza ajira kwa vijana ili kuwanusuru kujiingiza katika vitendo viovu. Endelea kusoma habari hii

Nitautetea mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa -Dk Shein

RAIS wa Zanzibar Dk Ali Mohamed amesema ataendelea kuutetea na kuulinda mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa wenye lengo la kuondosha ubaguzi wa aina zote kwa wananchi wa Zanzibar. Amesema mfumo huo ni mzuri na upo kisheria na hakuna haja ya kuuvunja kwa kuwa lengo lake ni kuleta umoja na mshikamano jambo ambalo ndio miongoni mwa malengo ya mapinduzi. Dk Shein ameyasema hayo katika mkutano wa CCM uliofanyika jana katika viwanja vya Kibanda Maiti Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni sherehe za kumkabirisha baada ya kumaliza mchakato wa uchaguzi wa chama hicho uliofanyika huko Dodoma wiki hii. “Serikali ya mapinduzi zanzibar ina muundo wa kitaifa nataka nikuhakikishie kwamba serikali hii tutaiendeleza kwa mustakabali wa wanzanzibari wakiwa wamoja na hili ndio lengo la mapinduzi yetu na hili la umoja, mapenzi na mshikamano alilianzisha Mzee Karume yeye alisaini mkataba watu kuishi kwa umoja na mshikamano kwa hivyo hili sio jambo jipya madhumuni ni kuleta maendeleo katika nchi yetu tukiwa pamoja na mashikamano, vyama vya siasa vinafanya siasa lakini sio kutukanana sio kugombana sio kushutumiana” alisema Dk Shein. Endelea kusoma habari hii

Nipo tayari kunyanganywa kadi- Moyo

MUASISI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mzee Hassan Nassor Moyo amesema yuko tayari kurejesha kadi ya chama chake iwapo atalazimika kufanya hivyo huku akisisitiza kuunga mkono Muungano wa Mkataba. Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Zanzibar Moyo amesema ataendelea kuutetea msimamo wake wa kutaka Muungano wa mkataba kwa kuwa muungano uliopo kwa miaka 48 sasa umeshindwa kutatua kero zilizopo na kuleta matumaoni kwa wazanzibari. “Jambo kubwa ni nchi chama lilikuwa jambo la pili na kama viongozi wetu wa chama wanataka kutupeleka huko tukaeleze msimamo wa chama, mimi nasema muungano umekuja kwanza na hivyo ndio ninavyojua mimi na huo ndio msimamo wangu lakini ikiwa wanatwambia turejesha kadi mimi nitakuwa tayari lakini siwezi kuacha nchi yangu …nchi ilikuwa jambo la mwanzo” alisiitiza Mzee Moyo. Endelea kusoma habari hii

Muungano huu sebu! asema Mansoor

Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid amesema yupo tayari kunyanganywa kadi ya chama hicho lakini hataregeza msimamo wake juu ya kuitetea Zanzibar katika Muungano. Kauli ya Mansoor imekuja siku chache baada ya chama hicho wilaya ya mjini kutoa maamuzi ya kuwataka viongozi wenye kupingana na msimamo wa chama kurejesha kadi za chama hicho au kuacha tabia hiyo mra moja. Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Ujerumani (DW) jana Mansoor alisema kamwe hawezi kuogopa vitisho vinavyotolewa na watu wenye kujipa madaraka na udikteta ambao hawataki mabadiliko wala mawazo tofauti. Mansoor aliahidi kuendelea na msimamo wake katika kudai mabadiliko katika muundo wa Muungano na kusema kwamba msimamo wake hautabadilika licha ya vitisho vya baadhi ya Viongozi wa Chama hicho. Endelea kusoma habari hii

Kuna ‘Mamluki’ ndani ya CCM-UVCCM

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umewatuhumu baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaotoka Chama Cha CCM na kutishia kuwanyanganya kadi za uanachama kutokana na kuwa sawa na ‘Mamluki’ katika matendo yao. Kauli hiyo imetolewa juzi katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho uliofanyika viwanja vya Komba wapya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ambapo Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mjini, Mohammed Ali Khalfan alisema CCM inaweza kuwanyanganya kadi za chama hicho viongozi hao. Alisema viongozi hao ambao ni wajumbe wa baraza la wawakilishi zanzibar wameonekana kuwa na mtazamo tofauti na chama chao na hivyo kutaka wachukuliwa hatua ikiwemo kunyanganywa kadi za chama hicho cha CCM. Katibu huyo alisema wapo Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaokwenda kinyume na maadili ya chama hicho ambao amewafananisha kutokuwa na tofauti na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (JUMIKI). Endelea kusoma habari hii

Chama cha ADC chapata matumiani

CHAMA kipya cha Alliance for Democratic Change (ADC) jana kilipata matumaini mapya baada ya Msajiri wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa kusema chama hicho kinaendelea vizuri. Tenda alitoa matumaini hayo katika hutuba yake aliyotoa kabla ya kuanza kuhakiki wanachama 200 wa chama hicho Mjini Zanzibar. Katika hutuba yake fupi aliyoitoa nje ya ofisi ya ADC mtaa wa Bububu nje kidogo ya mji Zanzibar, msajili huyo alisema tangu chama hicho kpata usajili wa muda mapema mwaka huu kimekuwa kinafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria. “Nakupongezeni kwa juhudi mnazofanya lengo la chama ni kushika dola lakini kwa mwendo wenu inaonekana azma hiyo mnayo” alisema Tendwa. Hata hivyo alisema baada ya uhakiki wa chama hicho katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Pemba alitaka juhudi hizo ziendelea katika miko iliyobaki ili kutimiza masharti ya kupata usajili wa kudumu. Endelea kusoma habari hii

CCM yalalamikia rafu katika utoaji wa maoni ya katiba

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeitaka tume ya katiba kuchukua hatua dhidi ya watu wanaofanya vitendo vya udanganyifu kwa kuwasilisha barua za maoni kwa tume hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari huko Dunga Mkoa wa kusini Unguja Katibu wa CCM wa mkoa huo, Zainab Shomari alisema kumeanza kujitokeza vitendo vya udanganyifu wa watoaji maoni kwa kutumia majina bandia kwa wawasilishaji. “Kuna jina la Said Mwema limejitokeza katika barua na baada ya barua hizo tume ilitaka kumjua huyo mtu anayeitwa Said Mwema lakini matokeo yake hakuna aliyejitokeza,  kwa hivyo sisi tuna mashaka na hao watu wanaokwenda kupeleka maoni kwa njia ya barua tukiamini kuwa zinaandaliwa na baadhi ya wanasiasa” alisema Zainab. Akivitaja vitendo vyengine  vinavyofanywa katika mchakato huo, Zainab alisema ni pamoja na kuzomeazomea vilivyofanywa na vyama tofauti vya siasa, kuwatumia wanafunzi kutoa maoni baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa walimu wao pamoja na baadhi ya wanasiasa kuwaongoza wafuasi wao na kuwaelekeza maneno ya kwenda kutoa katika tume hiyo. Endelea kusoma habari hii 

Kukimbia kutoa maoni ni kujitia kitanzi

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imewahakikishia wazanzibari kuwa maoni yao hayatatupwa kapuni na badala yake yatafanyiwa kazi na serikali na kuonya kuwa kukimbia kutoa maoni ni sawa na kujitoa kitanzi. Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Sheria ya Katiba Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari huko Mapofu Wingwi, Mkoa wa Kaskazini Pemba. “Wananchi nakutoweni wasi wasi, maoni yenu hayatachakachuliwa, tume ya kukusanya maoni ina wajumbe sawa kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, kamwe wajumbe wetu hawataisaliti Zanzibar”, alisema Bakari ambaye ni Mwakilishi wa jimbo la Mgogoni. Bakari alisema anafahamu mawazo ya wazanzibari yalivyo hivi sasa yalivyo juu ya suala la Muungano na namna hisia zao zilivyo lakini aliwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kutoa maoni yao kwani ili yafanyiwe kazi na kuahidi kwamba hakutakuwa na njia yoyote ya kufanyika udanganyifu. “Nawasihi Wazanzibari tuitumie fursa hii kutoa maoni yetu, ili Zanzibar iwe na uwezo wa kufanya mambo yake kwa maslahi ya Wazanzibari, kukimbia kutoa maoni yetu ni sawa na kujitia kitanzi”, alionya Waziri huyo ambaye kitaalumu ni mwanasheria. Endelea kusoma habari hii

Mawaziri wa Serikali ya Zanzibar na sababu ya ubunifu

Maelekezo ya kiongozi wa nchi ni muhimu sana. Na mara nyingi kiongozi mwenye busara hutoa maelekezo na kutaraji wafuasi wake au walio chini yake watekeleze maagizio hayo bila visingizio vyovyote vile. Kiongozi wa nchi hutoa maelekezo hayo pia akiruhusu ubunifu na hata utekelezaji kwa mujibu wa hali ilivyo na sio kutekeleza maagizo kwa njia ya kulazimisha kwa kuwa tu ni kutekeleza maagizo. Endelea kusoma habari hii

Watanzania watakiwa kutoa maoni katika katiba

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba amewataka watanzania kusimama imara na kujipanga katika kutoa maoni ya katiba mpya, ili kuhakikisha kuwa katiba inaweka wazi suala la maliasili kuwa rasilimali za Watanzania. Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na maliasili nyingi zikiwemo dhahabu, almasi, Tanzanite, copper na madini mengine kadhaa, lakini bado rasilimali hizo hazijawanufaisha wananchi kutokana na kutokuwepo utaratibu unaoeleweka juu ya mgawano wa rasilimali hizo. Endelea kusoma habari hii

CCM waanza kupanga safu za uongozi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimekiri kupata uvamizi katika jumuiya zake na kuahidi kitendo hicho kutorejewa tena ili kupanga safu nzuri za uongozi bora wa chama hicho. Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Balozi Seif Ali Iddi jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Umoja Wapanda Mapikipiki wa CCM katika Ukumbi wa Chama hicho Mkoa Amani Mjini Zanzibar ambapo alisema kusitolewe mwanya wa watu wenye lengo la kuharibu.Endelea kusoma habari hii

Hamad Rashid atangaza kuunda chama chake mwezi Machi

Mahakama Kuu nchini Tanzania imetoa muda zaidi kwa chama cha upinzani nchini Tanzania, CUF, kuzipitia hoja za waliowafukuza kutoka chama chao, akiwemo Mbunge wa Wawi, kisiwani Pemba, Hamad Rashid. Shauri hili lilipangwa kusikilizwa leo, na sasa linatarajiwa kusikilizwa Machi 17. Hamad Rashid, kama mtuhumu, alikuwepo mahakamani  na Sudi Mnette wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle alizungumza naye baada ya Jaji Augostino Shango wa mahakama hiyo kuliahirisha shauri hilo, ambapo Rashid amedai kuwa chama chake cha CUF kimepasuka na akatangaza rasmi kuunda chama kipya hapo Machi. Kusikiliza mahojiano hayo, tafadhali bonyeza hapa.

Hatima ya Hamad Rashid katika CUF ni leo

HATIMA ya uanachama ya Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed inatarajiwa kujulikana leo atakapojieleza mbele ya Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho. Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila kuvuliwa uanachama na chama chake hicho kwa madai ya kukiuka maadili na katiba ya chama ambayo kwa kiasi kikubwa yanafanana na yale yanayomkabili Hamad.Hamad hivi karibuni amejikuta katika mgogoro na baadhi ya viongozi wa makao makuu ya CUF baada ya kutangaza kuwania nafasi ya katibu mkuu wa chama inayoshikiliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad na kuanza kupita kwenye matawi akigawa misaada, hatua ambayo ilisababisha vurugu katika matawi aliyopita huku tukio katika Tawi la Chechnya lililopo Manzese, likisababisha umwagaji damu baada ya wanachama wanaomuunga mkono kupambana na walinzi wa Blue Guard. Endelea kusoma habari hii

Rais Kikwete ateuwa mabalozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Mabalozi. Endelea kusoma habari hii

Mapalala’ haweshi ndani ya CUF

Kama CUF iliweza kukaa pamoja na CCM iliyodaiwa kutumia vyombo vya dola kuwafanyia ukatili, uovu na idhilali ya kutisha wanachama wake, hasa kila unapoingia uchaguzi mkuu, vipi ishindwe kutumia vikao vyake kusawazisha sintofahamu iliyo katika safu yake ya uongozi?.Endelea kusoma habari hii

Maalim Seif akana kumuandaa Jussa

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) amesema yeye binafsi hana chama bali anayetaka kuwania nafasi yeyote ya uongozi ndani ya chama afuate utaratibu wa chama unavyoelekeza. Sambamba na hilo amekanusha kumuandaa Ismail Jussa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho kwa siku za baadae. Endelea kusoma habari hii

JUSSA ANGARA MBELE YA MARANDO NA NAPE

MVUTANO mkali wa hoja uliibuka katika mdahalo uliopewa jina la Itikadi za vyama vya siasa na Tanzaniatunayoitaka, ambao mwakilishi wa Chama cha Wananchi (CUF), Jussa Ismail Ladhu aling’ara kutokana na hoja zake kuonekana kuwazidi nguvu wenzake, Mabere Marando wa Chadema na Nape Nnauye wa CCM.Endelea kusoma habari hii

MATUNDA YA SUK

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad amesema kupandishwa kwa bei za karafuu na ongezeko la mishahara kwa asilimia 25 ni moja ya mafanikio yaliopatikana baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa (SUK).Endelea kusoma habari hii

 

FUATENI SHERIA

MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka viongozi wanaosimamia sheria pamoja na wananchi kwa ujumla kuzingatia utawala wa sheria, kwa kigezo kuwa ndio msingi mkuu wa haki za binaadamu.Maalim Seif ametoa changamoto hiyo leo katika viwanja vya Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, ziliopo Miembeni Mjini hapa, katika hafla ya maadhimisho ya siku ya ‘Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar’, ambayo imetimiza miaka tisa tangu kuanzishwa kwake Julai 10, 2002.Endelea kusoma habari hii

KILA MZANZIBARI ATAPATA HAKI YAKE

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema maridhiano yaliofanyika baina ya vyama vya CCM na CUF na hatimae kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, yalilenga kuhakikisha kila mzanzibari anapata haki zake za msingi bila kubaguliwa.Endelea kusoma habari hii

FANYENI KAZI KWA MASHIRIKIANO

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amwewataka Mawaziri wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya kazi kwa mashirikiano ili kujenga Jumuiya yenye nguvu Barani Afrika.Endelea kusoma habari hii

 

JUSSA AMSHUSHUA PINDA

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu amemtaka Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda, kuwaaacha wazanzibari kutoe hisia zao kwa mustakabali wa nchi yaona kuacha kutoa vitisho dhidi yaovisivyo na lazima.Endelea kusoma habari hii

CUF YAPATA PIGO MTWARA

CHAMA cha CUF kimepata pigo mkoani Mtwara, baada ya wananchama wake 154 kutangaza kukihama chama hicho na kukabidhi kadi zao kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi mjini hapa.Endelea kusoma habari hii

MVUA YASITISHA SHEREHE ZA MUUNGANO

MVUA kubwa iliyoanza ghafla jana ilisitisha sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya muungano wa Tanganyikana Zanzibarkatika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar. Sherehe hizo zilizoanza majira ya saa 3:00 asubuhi ziliingia dosari hiyo huku tayari mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshakagua gwaride na kujumuika na viongozi wenzake katika jukwaa kuu.Endelea kusoma habari hii

CCM KUJIVUA GAMBA

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Pius Msekwa amesema chama chao kimezaliwa upya kwa mara ya pili kutokana na mabadiliko ya kujivua gamba yaliofanyika hivi karibuni.Endelea kusoma habari hii

MAZINGIRA NI URITHI WA WATOTO WETU

Wazazi wameshauriwa kuelimishana juu ya suala la utunzaji wa mazingira ili jamii ifaidike na maisha bora na kuwaachia watoto wao urithi wa mazingira bora ya kuishi.Ushauri huo umetolewa na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Seif Iddi alipokuwa akizundua rasmi maadhimisho ya Juma la wiki ya Wazazi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja yaliofanyika Bumbwini Makoba Wilaya Kaskazini B.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN AWAAPISHA WATEULE WAKE

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi mbali mbali ambao ni watendaji wa serikali ikiwa ni hatua ya kupanga safu yake ya uongozi.Walioapisha ni pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Katibu wa Rais wa Zanzibar, Haroub Shaibu Mussa, Naibu Katibu wa Rais wa Zanzibar Mariam Haji Mrisho na Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji ya Zanzibar, Chande Omar Omar. Endelea kusoma habari hii

BALOZI SEIF AWATAKA ZEC KUBADILIKA

16 02 2011

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetaka matokeo ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baada ya miaka mitano ijayo matokeo yake yatolewe kwa wakati ili kuondosha dhana mbyana na kuwatia khofu wananchi.Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd alipokuwa na mazungumzo na watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) huko ofisini kwao Chake Chake Mkoa wa Kusini Kisiwani Pemba.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN AWAREJESHA WAKURUGENZI WALE WALE

15 02 2011

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein jana amefanya uteuzi wa wakuu wa mbali mbali katika baadhi ya wizara za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Waliotuliwa kushika nafasi hizo katika Wizara ya Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Mashaka Hassan Mwita ambaye atakuwa Mkurugenzi Idara ya Mipango, Sera na Utafiti.Endelea kusoma habari hii

CCM WATAKIWA KUJIPANGA KWA USHINDI

14 02 2011

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi CCM Zanzibar wametakiwa kuwaweka pembeni viongozi wataotaka nafasi za uongozi kwa kuangalia vigezo vya udugu, urafiki na watoto wa vigogo ili kukiwezesha chama hicho kuwa na viongozi bora.Hali bora imeelezwa ndio itakayosaidia kukiwezesha chama hicho kupata ushindi mkubwa mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao ambapo ushindani wa vyama utakuwa umeongezeka kutokana na kuwepo viongozi wa wa upinzani serikalini.Endelea kusoma habari hii

UTEUZI WA WAKURUGENZI WENGINE WAFANYWA

29 01 2011

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa wakuu wa taasisi mbali mbali katika baadhi ya wizara.Kwa mujibu wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee amesema uteuzi wa wakuu hao umeanza rasmi jana.Walioteuliwa kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ni Yassin Ameir Juma, ambapo Ali Vuai Ali anakuwa Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi.Endelea kusoma habari hii

UTEUZI WA WAKURUGENZI WENGINE WAFANYWA

29 01 2011

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa wakuu wa taasisi mbali mbali katika baadhi ya wizara.Kwa mujibu wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee amesema uteuzi wa wakuu hao umeanza rasmi jana.Walioteuliwa kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ni Yassin Ameir Juma, ambapo Ali Vuai Ali anakuwa Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi.Endelea kusoma habari hii

CUF KUADHIMISHA MAUAJI KIMYA KIMYA

27 01 2011

CHAMA Cha Wanachi (CUF) jana kimeadhimisha miaka 10 ya maombolezo ya vifo vya wananchi vilivyotokea Januari 26-27 mwaka 2001 katika maandamano ya amani yaliyofanyika Zanzibar huku kikiwa na ujumbe wa kutaka suala kama hilo la aibu lisitokee tena nchini.Mkurugenzi wa habari uenezi mawasiliano ya umma na Haki za binadamu wa chama hicho, Salim Bimani alisema Tanzania kwa mara ya kwanza ilipata aibu kubwa ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu uliofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama jambo ambalo linapaswa kuepushwa na lisitokee tena kwa kuwa kitendo hicho kimeitia doa Tanzania katika sura za kimataifa.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN ATEUWA WAKURUGENZI WA TAASISI MBALI MBALI

25 01 2011

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein jana amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa taasisi mbali mbali serikalini ikiwa ni sehemu ya kuupanga serikali yake ya awamu ya saba.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, iliezea kuwa uteuzi wa watendaji hao umeanza rasmi jana.Endelea kusoma habari hii

VIONGOZI WA MJI MKONGWE WATIMIZA AHADI ZAO

15 01 2011

CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimewataka wananchi wote kushirikiana na serikali yao ya Mapinduzi Zanzibar iliyo chini ya mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa kwa lengo la kusaidia juhudi za kuleta maendeleo nchini.Agizo hilo limetolewa jana na Mbunge wa jimbo la Mji Mkongwe, Ibrahim Mohammed Sanya alipokuwa akikabidhi wananchi wa Mwembetanga kisima na na tangi la maji lenye ujazo wa lita 5,000 eneo la Mapembeani ikiwa ni moja ya ahadi za viongozi wa jimbo hilo walizozitoa wakati wa kampeni za kuwania kuingia madarakani.Endelea kusoma habari hii

KILELE CHA MAPINDUZI DK SALMIN AWALIZA WANA CCM

12 01 2011

MAADHIMISHO ya sherehe za miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanyika jana huku kivutio kikubwa kikiwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya tano, Dk Salmin Amour Juma alipowasili uwanjani hapo na kuamsha hisia za mamia ya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumshangiria kwa nguvu zote huku baadhi yao wakitokwa na machozi walipomuona akipanda jukwaani mwenyewe.Dk Salmini anayejulikana kama Komandoo aliingia uwanjani hapo majira ya saa 3:15 na kuchukua muda wa dakika fulani hivi kushuka ndani ya gari lake na kutembea na kupanda juu ya jukwaa ambapo alikataa kushikwa mkono na wasaidizi wake na maafisa wa usalama waliofika kumpokea na kutaka kumkamata mkono hadi jukwaani.Endelea kusoma habari hii

TUNAUNGA MKONO MCHAKATO WA KATIBA MPYA-CUF

2 01 2011

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amesema kwamba chama chake kinaunga mkono hatua ya Rais Jakaya Kikwete kuanzisha mchakato utakaoiwezesha Tanzania kuwa na Katiba mpya. Maalim Seif amesema kuundwa kwa Tume itakayowashirikisha wajumbe wa Zanzibar na Tanzania bara kuendesha shughuli za mchakato huo ni hatua nzuri ya kuanzia katika kufikia utekelezaji wa dhamira hiyo.Endelea kusoma habari hi

VIGOGO ZANZIBAR WAFUTIWA VIBALI VYA ARDHI

26 12 2010

WAKATI mtandao maarufu wa WikiLeaks ukionesha harufu ya rushwa kwenye ugawaji wa ardhi ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baadhi ya mawaziri na vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameanza kufutiwa vibali vyao vya kumiliki ardhi katika maeneo mbali mbali visiwani hapa.Tayari zaidi ya mawaziri watano ambao miongoni mwao wanaendelea na nyadhifa hizo ambao wanadaiwa kujimilikisha maeneo ya ardhi katika eneo mbali mbali wamefutiwa vibali vyao kutokana na kutofuata taratibu za umiliki wa ardhi hizo.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR YAHIMIZA KERO ZA MUUNGANO KUSHUGHULIKIWA

24 12 2010

24 12 2010

SERIKALI ya umoja wa kitaifa Zanzibar imetaka suala la kero za Muungano kushughuulikiwa kwa dhati kwa kuzingatia sheria na taratibu wakati wa kutoa maamuzi pamoja na utekelezaji wake, kwa kuwa uzoefu unaonesha kumekuwepo na maamuzi yasio na utekelezaji wa jambo hilo.Hayo yamebainika katika ya kikazi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu Hassan wakati akionana na viongozi wa wizara kadhaa wakati alipokwenda kujitambulisha hapa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN APEWA AGIZO NA WAZEE WA CCM

12 12 2010

WAZEE wa CHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wamemtaka Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein kuwa muumini na muendelezaji mzuri wa Mapinduzi ya Januari 12, 1984. Wazee hao walieleza matumaini yao kwa Dk. Shein kuwa atakuwa mtendaji bora zaidi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na kuwa muumini mzuri wa kuendeleza Mapinduzi ya Januari 12 1964. katika ziara yake iliyoanza jana katika mikoa ya Kusini Unguja.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR INAHITAJI KATIBA MPYA-PRO. SHIVJI

4 12 2010

Professa Issa Shivji

MHADHIRI Mtaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Professa Issa Shivji amesema ni wakati mwafaka wa kutaka katiba mpya Zanzibar umefika hasa kwa kuzingatia wakati huu ambao hali ya kisiasa inaridhisha kufuatia mabadiliko ya mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa.“Ni wakati mwafaka wa kuangalia upya katiba ya Zanzibar….turekebishe sheria zetu na katiba zetu na hasa kwa kuwa Zanzibar hali hivi sasa imetulia basi ndio wakati wa kudai mabadiliko hayo ya katiba lakini pia sheria ya kura ya maoni lazima ifanyiwe marekebisho” alisema Msomi huyo.Endelea kusoma habari hii

ZLS WAMPINGA DK SHEIN

1 12 2010

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein

CHAMA Cha Mawakilishi Zanzibar (ZLS) kimepinga uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein Novemba 29 mwaka huu wa 2010 na kuhoji uhalali wa uwepo wa Jaji Mkuu wa Zanzibar.Kwa mujibu wa barua ya Novemba 30 mwaka huu yenye kumbukumbu namba ZLS/IKULU/001 aliyopelekewa Dk Shein ambapo gazeti hili imepata nakala imeeleza kwamba chama hicho hakijarishishwa kabisa na uteuzi huo kutokana na kuwa haujazingatia vigezo na kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa sheria katika uteuzi huo.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN ATEUWA MAJAJI ZANZIBAR

29 11 2010

RAIS wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein jana amewateuwa majaji wanne wa mahakama ya mkoa Vuga kuwa majaji wa mahakama kuu ya Zanzibar .Kwa mujibu wa kifungu cha 94 (2) cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kimempa uwezo rais wa Zanzibar kuwateuwa, Fatma Hamid Mahmoud, Rabia Hussein Mohammed, Mkusa Isaac Sepetu na Abdul Hamid Ameir Issa.Endelea kusma habari hii

ZANZIBAR IWE NI MFANO MZURI DUNIANI -JESHI LA POLISI

29 11 2010

JESHI la Polisi Zanzibar limesema jukumu linalowakabili kwa sasa baada ya uchaguzi mkuu kumalizika ni kuendelea kuimarisha ulinzi ili Zanzibar izidi kuendelea kuwa sehemu ya amani yenye kupigiwa mfano duniani. Kauli hiyo imetolewa na Waziri Machano Othman Said kwa niaba ya Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud Mohammed wakati akifungua mafunzo ya sita tano ya uimarishaji wa mashirikiano kati ya polisi na mamlaka za serikali za mitaa katika kuzuia uhalifu kwa kutumia polisi jamii na ulinzi shirikishi.Endelea kusoma habari hii

PEMBA YAFURIKA KUMPOKEA MAALIM SEIF

Makamu wa kwanza wa rais

28 11 2010

WANANCHI mbali mbali wa Kisiwani Pemba wamejitokeza kwa wingi kumlaki Makamu wa kwanza wa rais, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye kwa mara ya kwanza amefanya ziara yake jana kisiwani humo tangu kuchaguliwa kushika wadhifa huo na rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein.Kuwasili kwa Maalim Seif kumewafurahisha mamia ya wananchi wa kisiwa hicho ambao wamekwenda kumpokea uwanja wa ndege wa Karume na kujipanga barabarani kama ishara ya kumuunga mkono kiongozi huyo kuchaguliwa katika serikali ya umoja wa kitaifa ambayo wazanzibari wana matumaini makubwa na serikali hiyo.Endelea kusoma habari hii

MAKATIBU WAKUU WAAPISHWA IKULU UNGUJA

26 11 2010

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein jana amewaapisha makatibu wakuu 17 manaibu 20 ambao watakuwa ni watendaji wakuu wa serikali ya umoja wa kitaifa.Makatibu wakuu hao wamekula kiapo cha uaminifu kwa serikali katika hafla iliyofanyika Ikulu Zanzibar, Mkoa wa Mjini Magharibi na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali na waandishi wa habari.Endelea kusoma habari hii

UTEUZI WA JK WAKOSOLEWA

25 11 2010

UTEUZI wa baraza la mawaziri Tanzania umepokewa kwa maoni tofauti na wananchi na wakaazi wa Zanzibar huku wengine wakipongeza na wengine wakikosoa uteuzi huo.Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini hapa wananchi hao wamesema uteuzi huo haujazingatia maslahi ya nchi bali umetizama zaidi kulindana na kukilinda Chama Cha Mapinduzi (CCM).Endelea kusoma habari hii

WANANCHI WATAKIWA KUTAMBUA SERIKALI YA UMOJA

23 11 2010

Balozi Seif Ali Idd

WANANCHI wa jimbo la Kitope wametakiwa kutambua wamo katika serikali ya umoja wa kitaifa inayolenga kukuza maendeleo na uchumi wa nchi na ni vyema washiriki kutoa mchango wao katika shughuli hizo. Wito huo aliutoa jana kwa nyakati tofauti na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, wakati akizungumza na Wazee, wanafunzi na viongozi wa Chama wa Jimbo hilo pamoja na Wilaya ya Kaskazini “B’ Unguja.Endelea kusoma habari hii

UCHAGUZI UMEMALIZIKA-BALOZI SEIF

23 11 2010

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutambua kwamba uchaguzi mkuu umemalizika na kukubaliana na viongozi waliopo madarakani kwa sasa.Akizungumza na wanachama wa CCM jimboni kwake Kitope mkoa wa kaskazini Unguja, Balozi Seif alisema kinachotakiwa kwa wanachama hao ni kuelezea matatizo yao kwa uwazi kwa viongozi wao ili kuijenga Zanzibar mpya itayokuwa na maendeleo na yenye kusonga mbele katika utekelezaji wa ahadi zake.Endelea kusoma habari hii

MSIBWETEKE KWA KUWA TUPO SERIKALINI-MAALIM

20 11 2010

MARA baada ya rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein kumaliza kazi ya kupanga safu yake ya uongozi kwa kuunda Baraza la Mawaziri, Makatibu wakuu wa SMZ wamekuwa wakihaha kusubiri uteuzi mpya wa muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.Wakati wowote kuanzia sasa Dk Sheni anatarajiwa kumaliza kazi ya kuunda muundo wa Serikali katika Wizara mbali mbali kwa kuteuwa makatibu wakuu na wakurugenzi ambao ndio watendaji na wasimamizi wa wizara husika.Endelea kusoma habari hii

WATENDAJI WATAKIWA KUFUATA KANUNI NA UTUMISHI

17 11 2010

SIKU MOJA tu baada ya mawaziri wapya wa kuapishwa,Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamamed Shein amewataka mawaziri hao kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni za utumishi na taratibu zilizowekwa katika nchi pamoja na kuwataka wahubiri amani kwa vitendo.Juzi Dk Shein aliwaapisha mawaziri 25 watakaounda wizara 16 chini ya serikali ya umoja wa kitaifa ambayo imewashirikisha wajumbe kutoka vyama vya CCM na CUF kutokana na mabadiliko ya 10 ya katiba ya Zanzibar ambayo yanasubiriwa kwa hamu kubwa kuonekana na wazanzibari wengi utekelezaji wake.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN APANGA SAFU YAKE YA UONGOZI

16 11 2010

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein ameteua Baraza la Mawaziri la serikali ya umoja wa kitaifa lenye mawaziri 25 kutoka vyama viwili vikuu visiwani humo vikiunda serikali hiyoTaarifa iliyotolewa na Ikulu ya Zanzibar jana ilieleza kuwa uteuzi wa mawaziri hao 15 kutoka CCM na 10 kutoka CUF unaanza mara moja na kwamba wataapishwa leo jioni katika Viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

UCHAGUZI ZANZIBAR WAKOSOLEWA

4 11 2010

MKUU wa kundi la waangalizi wa Umoja wa Ulaya, David Martin, jana ametoa taarifa yake ya awali kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu ulivyokwenda visiwani Zanzibar. Wakati huo huo Kamati ya waangalizi wa uchaguzi Tanzania TEMCO, nayo pia imetoa ripoti juu ya uchaguzi huo.Katika taarifa yake kuhusu uchaguzi, mkuu wa waangalizi wa Umioja wa Ulaya David Martin, alisema kwa ujumla uchaguzi ulifanyika katika hali ya amani na utulivu, lakini akataja dosari zilizotokeza na ambazo zinatia wasiwasi katika mchakato mzima.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN AKABIDHIWA MADARAKA YA URAIS

3 11 2010

RAIS mpya wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, ameingia rasmi madarakani huku akiahidi kutumia nguvu na uwezo wake wote, kutekeleza na kusimamia majukumu yanayomkabili na yenye maslahi kwa Wazanzibari wote.Dk Shein alitoa kauli hiyo jana katika hotuba yake, muda mfupi baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo katika sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN AMIMINIWA PONGEZI

3 11 2010

SALAMU z a pongezi kutoka ndani na nje ya Tanzania zinaendelea kutolewa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar wa awamu ya saba.Salamu hizo za pongezi zinatoka kwa Jumuiya, Vyama vya Siasa, Mashirika, Wizara, Taasisi za serikali na zisizo za serikali, afisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo nchi za nje, watu binafsi na wananchi mbali mbali.Endelea kusoma habari hii

RAIS MPYA KUAPISHWA KESHO ZANZIBAR

2 11 2010

Dk Shein, Juma Kassim Tindwa na Mama Mwema

RAIS Mteule Dk Ali Mohammed Shein aliyeshinda urais wa Zanzibar kwa asilimia 50.1 na kumshinda mpinzani wake Maalim Seif Sharif Hamad aliyepata asilimia 49.1 anatarajiwa kuapishwa kesho katika uwanja wa Amaani Mjini Zanzibar.Katika sherehe hizo ambazo zitafanyika asubuhi mapema zitahudhuriwa na wageni mbali mbali wa kitaifa na nchi majirani watahudhuria katika sherehe hizo wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa na serikali.Endelea kusoma habari hii

MSIVUNJIKE MOYO MTAKAOSHINDWA-KARUME

31 10 2010

Amani Karume

RAIS wa Zanzibar, Amani Abeid Karume jana alikuwa wa kwanza kushiriki zoezi la upigaji kura na kuwataka wazanzibari kutokata tamaa kwa wale ambao watashindwa katika uchaguzi huo.Alisema hayo muda mfupi baada ya kupiga kura yake akiwa amefuatana na Mama Shadya Karume ambapo wote kwa pamoja wamepiga kura katika kituo cha shule ya Kiembesamaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.Endelea kusoma habari hii

NITAKUBALI MATOKEO YOYOTE-MAALIM SEIF

30 10 2010

MaaliM Seif na Mohammed Abdulrahman

WANANCHI wa Zanzibar kesho wanapiga kura huku mgombea Urais wa visiwa hivi kupitia tiketi ya CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, akisema atakayakubali matokeo yoyote ya uchaguzi huo.Hata hivyo Maalim Seif ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa kuhitimisha kampeni zake, uliofanyika katika viwanja vya Maisara mjini Unguja, alimshauri mgombea wa nafasi hiyo kupitia tiketi ya CCM, Dk Ali Mohamed Shein, naye akubali matokeo.Endelea kusoma habari hii

UCHAGUZI WA WADI NNE WAAKHIRISHWA ZNZ

30 10 2010

Salim Kassim Ali

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema italazimika kurejea uchaguzi katika wadi nne za Mji Magharibi kutokana na hitilafu zilizotokea katika karatasi za kupigia kura.Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kupokelea matokeo ya uchaguzi ndani ya ukumbi wa hoteli ya Bwawani Mjini Unguja, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Khatib Mwinyichande alisema kuakhirishwa kwa uchaguzi huo kunatokana na kasoro zilizojitokeza dakika za mwisho.Endelea kusoma habari hii

UCHAGUZI WA AMANI NI MATUNDA YA MARIDHIANO

29 10 2010

Abdallah Mwinyi Khamis

KUMALIZIKA kwa uchaguzi mkuu mwishoni wiki hii kuwe ni mwanzo wa kazi ya vijana kuanza kutekeleza jukumu la kulinda amani, ambayo ni matunda ya maridhiano baina ya CUF na CCM, serikali iliema mjini hapa jana.Mkuu wa mkoa wa Mjini MagharibI, Abdallah Mwinyi Khamis alitoa changamoto hiyo wakati anafunguma semina ya siku moja ilioandaliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.Endelea kusoma habari hii

ASIYEKUBALI KUSHINDWA SIO MSHINDANI-SHEIN

28 10 2010

Dk Shein Nyumbani kwake Bosnia Kikwajuni

MGOMBEA urais kwa tiketi ya chma tawala CCM, Dk Ali Mohammed Shein amesema anaamini yeye na chama chake ndiyo watakaoshinda uchaguzi mkuu Jumapili ijayo.Dr Shein aliyasema hayo katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) mjini Zanzibar ambayo yalitangazwa jana jioni na Idhaa hiyo.Endelea kusoma habari hii

MASHEHA HAWANA JUKUMU VITUONI -ZEC

28 10 2010

Khatib Mwinyichande

TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) jana ilisema wakuu wa mikoa na masheha hawana jukumu lolote katika shughuli za uchagzuzi, kwa hatua iliyobaki kuelekea upigaji kura.Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa ZEC, Khatib Mwinyinchande katika mkutano na waangalizi wa uchaguzi kutoka ndani na nje ya nchi waliokuja kushuhudia uchaguzi wa mwaka huu, katika Hoteli ya Bwawani mjini hapa.Endelea kusoma habari hii

WANASIASA WAPOKEE MATOKEO KWA AMANI

27 10 2010

wanafunzi wa Fidel Castro wakisikiliza elimu ya upigaji kura

MWANASHERIA mstaafu wa serikali amesema kuna umuhimu kwa wanasiasa kuanzisha mpago wa kuwajenga wafuasi wao kuyapokea matokeo ya uchaguzi kwa njia ya amani. Hamid Mbwezeleni alikuwa anazungumza katika semina iliyogharamiwa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP kuzungumzia “mazingira ya usalama siku ya uchaguzi na katika kipindi cha kusherehekea matokeo.”Endelea kusoma habari hii

MSIWE NA KHOFU NA JESHI-MAALIM

27 10 2010

MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad amewatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuwa jeshi la ulinzi litaheshimu maamuzi ya wananchi wakishapiga kura.Akihutubia mikutano ya kampeni majimbo kadhaa tangu alipowasili kisiwani Pemba kumalizia kampeni yake, Maalim Seif amesema jeshi la ulinzi ni jeshi la wananchi wa Tanzania ambalo lina jukumu la kulinda amani ya nchi.Endelea kusoma habari hii

CCM WACHELEWESHA MAFUTA ZNZ

25 10 2010

Dk Slaa

MGOMBEA Urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chadema, Dk Wilbrod Slaam, amesema ubinafsi wa viongozi wa Serikali ya CCM, umekwamisha uchimbaji wa mafuta katika visiwa vya Zanzibar.Kwa mujibu wa Dk Slaam, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), liliwahi kuwasilisha bungeni, sampuli ya mafuta yaliyotafitiwa katika visiwa vya Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

SERIKALI YAKIRI MAKOSA YAKE KWENYE UCHAGUZI

24 10 2010

Dadi Faki Dadi

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekiri kwamba imeandikisha watu katika daftari la kudumu la wapiga kura wasiokuwa na sifa za kuandikishwa katika daftari hilo kutokana na sababu mbali mbali.Mbali na kukiri hilo, pia serikali imekiri kuwaajiri waafisa wasaidizi wasimamizi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) waliokuwa hawana sifa za kuajiriwa.Endelea kusoma habari hii

KAMPENI ZAFANYWA VIJIWENI PEMBA

Said Soud Akifanya Kampeni kwa kutumia Vespa

MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha wakulima (AFP) Said Soud Said ameanza utaratibu mpya wa kufanya kampeni kila penye mikusanyiko hadi kwa wakulima wakiwa mashambani mwao.Hatua hiyo imekuja kufuatia mgombea huyo kubakiza mikutano minne tu ya hadhara iliyoidhinishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kabla kufanyika uchaguzi mkuu disemba 31 mwaka huu.Endelea kusoma habari hii

WENYE VIRUSI WAHITAJI KUSAIDIWA

22 10 2010

Happy Birthday

NCHI za Afrika zimetakiwa kuangalia zinavyoweza kugharamia dawa za kupunguza machungu ya athari za virusi vya ukimwi kwa kuwa mashirika ya hisani yanazidi kupunguza misaada.Katika mkutano wa kubadilishana mawazo na timu ya kampeni ya mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad viongozi wa Jumuiya ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Zanzibar (ZAPHA+) waliopo Vuga Mkoa wa Mjini Magharibi walisema wanasema misaada ya wahisani inazidi kupungua mwaka hadi mwaka.Endelea kusoma habari hii

HAKI IKITENDEKA HATA SISIMIZI HAULIWI-WANANCHI

21 10 2010

Baadhi ya viongozi wa dini wa Micheweni wakisikiliza kongamano

VIONGOZI wa dini katika wilaya ya Micheweni wamesema iwapo haki itatendekea katika uchaguzi mkuu na aliyeshinda kukabidhiwa ushindi wake hakuna umwagikaji damu utakaotokea Zanzibar. Akichangia mada katika kongamano la kutafuta amani kwa viongozi wa dini wanasiasa makamanda na taasisi zisizo za kiserikali lililofanyika Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, Sheikh Kombo Faki Kombo, alisema hakuna umwagikaji wa damu utakaotokea iwapo haki itatendeka kwani tatizo kubw alinalotokea ni kunyimwa haki wanaohusika.Endelea kusoma habari hii

WALIOJIUNGA NA CCM WANATAFUTA VYEO

19 10 2010

WANANCHI wa Kisiwani Pemba katika maeneo mbali mbali wametoa maoni yao juu ya uamuzi wa vigogo wawili wa Chama Cha Wananchi CUF walioamua kujiengua na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM juzi.Wakizungungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kwamba kitendo walichokifanya Mbunge wa zamani Fatma Maghimbi na mjumbe wa mkutano mkuu wa CUF taifa, Othman Juma Othman ni cha aibu kisiasa na ni cha fedheha ambacho kimewashushia hadhi nchi nzima.Endelea kusoma habari hii

OFISI ZA MUUNGANO KUJENGWA UNGUJA NA PEMBA

18 10 2010

RAIS Amani Abeid Karume ametoa wito kwa taasisi za Serikali ya Muungano kuendelea kujenga ofisi Unguja na Pemba ikiwa ni hatua ya kuboresha utendaji wa serikali hiyo visiwani Zanzibar . Amesema mbali na kuboresha utendaji, ujenzi wa ofisi hizo, unachangia kuongeza nuru katika sura ya maendeleo visiwani. Endelea kusoma habari hii

NITAMALIZA YALIOBAKISHWA -CCM

18 10 2010

Dk Ali Mohammed Shein Mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM amesema akipata ridhaa ya kuongoza serikali kazi yake ya awali itakuwa ni kumalizia mipango yote iliyoanza kutekelezwa na uongozi wa rais Amani Karume kwa maendeleo ya wananchi.Dk Shein alikuwa akizungumza katika mkutano wa kampeni uliohudhuriw ana umati mkubwa katika uwanja wa shule ya Konde mkoa wa kaskazini Pemba.Endelea kusoma habari hii

NINA HAKIKA CCM ITASHINDA-DK SHEIN

18 10 2010

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohammed Shein amesema ingawa kazi ya kutangaza matokea ya uchaguzi sio ya chama hicho ana hakika CCM itashinda. Akizungumza katika uwanja wa Pujini jimbo la Chonga Dk Shein alisema ana imani hiyo kwa sababu wananchi wanajua kwamba CCM ina uzoefu wa kuongoza na pia njia ya kuingia ikulu viongozi wake wanaijua.Endelea kusoma habari hii

SADEC YATOA ONYO KWENYE UCHAGUZI

17 10 2010

John Tendwa

JUMUIYA ya Mashirikiano ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC imeonya kuwa itakuwa vigumu kuepuka migogoro ya kisiasa iwapo uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu nchini Tanzania hautosimamiwa vizuri. Onyo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa kitengo cha siasa, ulinzi, na usalama kutoka SADC, Tanki Mothae katika mkutano na wadau wa uchaguzi visiwani Zanzibar uliofanyika Zanzibar Beach Resort.Endelea kusoma habari hii

CUF WAFUTA MKUTANO DONGE KWA SHAMHUNA

15 10 2010

Ismail Jussa

HATIMAE Chama Cha Wananchi (CUF) kimeamua kutofanya tena mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika leo katika jimbo la Donge kutokana na kuhofia kuharibu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.Jimbo la Donge liliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja ndipo jimbo pekee ambalo halijawahi kufanyika mikutano ya siasa ya vyama vya upinzani usipokuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai kwamba wananchi wa Jimbo hilo hawataki kusikia sera za vyama vyengine.Endelea kusoma habari hii

NI KUFA NA KUPONA KULINDA MARIDHIANO-SEIF

13 10 2010

Maalim Seif

MAALIM Seif Sharif Hamad, amesema kwamba kulinda maridhiano ni suala la kufa na kupona kwa kuwa kiini cha amani iliyopo hivi sasa kinatokana na maridhiano hayo ambayo yameleta faraja kubwa miongoni mwa wananchi wengi.Maalim aliyasema katika mkutano wake wa kampeni za kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF) zinazoendelea mjini na vijijini katika mkutano uliofanyika Manzese Kiboje wilaya ya kati Unguja, Jimbo la Uzini.Endelea kusoma habari hii

MASAUNI AZINDUA KAMPENI KWA SHANGWE

13 10 2010

Hamad Masauni

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Hamad Masauni Yussuf amezindua kampeni za kuwania ubunge katika jimbo la Kikwajuni kwa kishindo baada ya mkutano huo kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.Masauni anagombea ubunge katika jimbo hilo baada ya kumuangusha katika kura za maoni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Paramuk Singa.Endelea kusoma habari hii

WATAKAOVUJISHA MITIHANI MAHAKAMANI-MAALIM

12 10 2010

MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema atahakikisha anaweka mazingira mazuri katika elimu na nguvu zaidi zitaelekezwa katika kupambana na wimbi la uvujaji wa mitihani nchini.Tatizo kubwa linaloikabili sekta ya elimu ni kuvuja kwa mitihani ambapo baadhi ya walimu wanashutumiwa kuvujisha kutokana na kukosekana maadili mema na uwajibikaji kwa wafanyakazi wa wizara za elimu nchini.Endelea kusoma habari hii

SITAMFUKUZA MTU-MAALIM SEIF

12 10 2010

MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kupitia chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wananchi wenye asili ya Tanzania Bara kuondosha wasiwasi wa kufukuzwa Zanzibar kama wengine wanavyodai. Alisema kwamba kuna watu wamekuwa wakisema kwamba Maalim Seif yeye ni kibaraka tu na iwapo akipata serikali itaongozwa na waarabu na watu wenye kutoka Tanzania bara wanaoishi Zanzibar watafukuzwa jambo ambalo Maalim Seif alilikanusha vikali.Endelea kusoma habari hii

VIBAKA WOTE TUTAWATAFUTIA KAZI-JAHAZI ASILIA

11 10 2010

CHAMA Cha Jahazi Asilia kimeahidi kuwasaka vibaka wote wazururaji kwa kuwakamata na kuwatafutia kazi za kufanya kwa kuwa wanafanya hivyo kutokana na kukosa kazi zinazopaswa kufanywa na vijana hao.Ahadi hiyo imetolewa na Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi kwa tiketi ya chama hicho katika jimbo la Kwamtipura, Ali Mwadini Faki wakati akinadi sera za chama chake ili achaguliwe kuwawakilisha wananchi katika jimbo hilo.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN AAHIDI UMEME WA MAWIMBI YA BAHARI

11 10 2010

Dk Ali Shein

MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Ali Mohammed Shein amesema kama atashinda uchaguzi serikali atakayounda itatilia mkazo utekelezaji wa mpango wa kuboresha huduma ya umeme unaotokana na upepo na mawimbi ya bahari.Dk Shein alitoa ahadi hiyo wakati akinadi sera za CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika Paje katika Mkoa wa Kusini, kilometa 48 kutoka mjini hapa.Endelea kusoma habari hii

AMANI HII NI MATUNDA YA MARIDHIANO-SPIKA

10 10 2010

Spika Kificho

SPIKA WA Baraza laWawakilishi, Pandu Ameir Kificho amesema hali ya utulivu unaoendelea Zanzibar ni matunda ya maridhiano ya kisiasa baina ya CUF na CCM, lakini ameonya hali hiyo itakosa uendelevu iwapo uchaguzi mkuu wa mwezi huu hautasimamiwa kikamilifu.Kificho alitoa mwelekeo huo juzi mjini hapa wakati anafungua kongamano lililoitishwa na “kamati ya pamoja ya viongozi wa dini” na kuwashirikisha wadau mbali mbali kuzungumzia umuhimu wa amani wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwezi huu.Endelea kusoma habari hii

MCHAGUWENI DK SHEIN- SAID SOUD

10 10 2010

Said Soud Said

MGOMBEA wa Chama Cha Wakulima (AFP) Said Soud Said amewataka wazanzibari wote wakiwemo wanachama wake kumpigia kura mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Ali Mohammed Shein kutokana na kuwa hana majungu.“Wanaomba wazanzibari yule bwana msimpe ushindi wa pili kama alivyokwambiaeni naomba kama hamkunipigia mimi basi mchagueni nyote Shein kwa sababu hatuwezi kuwa na rais mwenye majungu, hatuwezi kuwa na rais ana makundi na hatuwezi kuwa na rais hatosheki” alisema huku akishangiriwa na wanachanma wachache katika mkutano wake.Endelea kusoma habari hii

TUKOPESHENI KURA ZENU-CUF

8 10 2010

Maalim Seif

WANANCHI wa jimbo la Tumbatu wameombwa kuwakopesha kura zao wagombea waliojitokeza kuwania nafasi mbali mbali za uongozi jimboni humo, ili waweze kuwalipa maendeleo.Wito huo ulitolewa juzi na Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad katika mkutano wa kampeni uliofanyika ndani ya jimbo hilo katika Kiwanja cha Mpira cha Misuka kilichopo Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.Endelea kusoma habari hii

CCM YASIKITISHWA NA VIJANA WAKE

8 10 2010

CHAMA Cha Mapinduzi jimbo la Dole kimesema kwamba kinasikitishwa na vijana wa chama hicho ambao wameacha kukiunga mkono chama chao na kuhamia kwa wapinzani.Kauli hiyo imetolewa na Mgombea wa udiwani wa jimbo hilo wadi wa Mwera Bi Shani Omar Mbene katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye tawi la CCM Dole Wilaya ya Magharibi Unguja.Endelea kusoma habari hii

LEO HII CCM WANAWAOMBA WAPEMBA? CUF

8 10 2010

Jakaya Kikwete

MAKAMO Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF, Machano Khamis Ali, amesema kuwa ameshangazwa na kauli ya Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya ya Mrisho Kikwete ya kuwaomba wananchi wa Kisiwa cha Pemba wawape kura ili kuijaribu CCM.Hayo ameyaeleza jana katika uzinduzi wa Kadi za Uwanachama wa Vijana wa CUF uliofanyika katika Ukumbi wa Jamatkhan mjini hapa.Endelea kusoma habari hii

BADILIKENI FASTA-CCM

8 10 2010

Salim Turky

WAGOMBEA wa nafasi ya Ubunge na Uwakilishi katika jimbo la Mpendae kisiwani Unguja kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi wajinadi kuliletea jimbo hilo maendeleo ya Haraka endapo watachaguliwa na Wananchi kuliongoza katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu.Wana CCM hao Salim Hassan Turky anayegombea nafasi ya Ubunge na Mohamed Said Dimwa ,nafasi ya Uwakilishi wamekuja na kauli mbiu yao iitwayo ‘Mabadiliko Fasta’Endelea kusoma habari hii

TUTAKAMILISHA YALIOBAKI-KIKWETE

6 10 2010

Jakaya Kikwete

MGOMBEA wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema wananchi wakikichagua Chama Cha Mapinduzi kitakamilisha kazi iliyobaki ya kuwaletea maendeleo katika Visiwa vya Unguja na Pemba.Kikwete ameyasema hayo katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Demokrasia Kibanda Maiti Zanzibar uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wana CCM kutoka mikoa mitano ya Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

MUISLAMU HAKATI TAMAA -CUF

5 10 2010

WAZANZIBARI wameambiwa chini ya misingi ya Uislam ni kosa kwa mtu anayetafuta haki au kusaidia wengine kukata tamaa, kwani kufanya hivyo kunamkosesha kufikia malengo mbele ya Allah.Kauli hiyo imetolewa na Mzee Hassan Gharib ambapo alisema kwa kuzingatia misingi hiyo wananchi wa Dimani katika Wilaya ya Magharibi, wanapaswa kumuenzi kwa kumpa kura nyingi Maalim Seif Sharif Hamad anaewania nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR KUWA KITUO CHA UTALII

4 10 2010

MAALIM Seif Shariff Hamad ameahidi kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha Zanzibar inatangazwa vizuri kama kituo muhimu kwa shughuli za utalii.Maalim Seif alitoa ahadi hiyo wakati akifanya majumuisho ya mkutano wake na viongozi wa chama cha watembeza watalii Zanzibar (ZATO) uliofanyika ofisi za chama hicho, Hoteli ya Bwawani, mjini hapa juzi.Endelea kusoma habari hii

MICHEWENI ITAKUWA YA KISASA-DK SHEIN

3 10 2010

Dk Ali Mohammed Shein

CHAMA Cha Mapinduzi kimesema kama kitapata ridhaa ya wananchi kuongoza tena Zanzibar serikali itakayoiunda imekusudia kuibadili wilaya ya Micheweni kuwa wilaya yenye maendeleo ya kisasa yanayoendana na wakati uliopo na wakati ujao.Mgombea nafasi ya urais kupitia chama hicho Dk Ali Mohamed Shein aliwaambia wananchi wa Wilaya hiyo katika mkutano wa Kampeni uliofanyika jana kwenye kiwanja cha Shaame Matta kuwa mipango iliyoanishwa katika Ilani ya chama hicho inalenga kuifanya wilaya hiyo kuwa na maendeleo ya kisasa.Endelea kusoma habari hii

TAYARI TUMESHASHINDA -CUF

3 10 2010

Ismail Jussa

CHAMA Cha Wananchi CUF, kimesema kwamba tayari kina asilimia 62 ya kushinda kwa mgombea wao wa Urais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kushinda katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 31 mwezi huu nchini kote.Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya Urais wa chama hicho Ismail Jussa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye jimbo la Kiwakujuni mjini Zanzibar juzi.Endelea kusoma habari hii

MAALIM SEIF AWAAHIDI WAFANYABIASHARA

2 10 2010

Maalim Seif

MAALIM Seif Shariff Hamad jana ametembelea maeneo ya biashara ndogondogo mjini Zanzibar na kuahidi kuipa kipaumbele sekta ya biashara ambayo ni nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na watu wake. Katika ziara maalum aliyoifanya kama sehemu ya kampeni yake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa tarehe 31 Oktoba, mwaka huu, Maalim Seif alipokea kilio kikuu cha wafanyabiashara cha kuitaka serikali kupunguza viwango vya ushuru kwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi.Endelea kusoma habari hii

WANANCHI WATAKIWA KUWA MACHO

30 09 2010

WANANCHI wa Jimbo la Amani wametakiwa kuwa macho katika kipindi hichi cha kuelekea katika uchaguzi mkuu, na kutokubali kununuliwa na wagombea.Wito huo umetolewa na Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo. Seif Suleiman Kombo ‘Handingwa’, katika mkutano wa kampeni uliofanyika kiwanja cha SACCOS kilichopo ndani ya jimbo hilo.Endelea kusoma habari hii

MIKUTANO YA KAMPENI YAINGILIANA -ZEC

30 09 2010

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Wilaya ya Magharibi Unguja, imesema kwamba pamoja na kupanga ratiba za mikutano ya kampeni mapema lakini bado wanakabiliwa na changamoto za maingiliano ya mikutano kwa baadhi ya vyama.Hayo yameelezwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Suluhu Ali Rashid, huko Ofisini kwake wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kuhusiana na zoezi zima la mikutano ya kampeni, ambapo alisema kuwa marekebisho hayo hutokana na wengine kuahirisha na kuamuwa kufanya siku nyengine pamoja na wengine kupanga kufanya mikutano sehemu ambayo huona kwa siku ile hakuna ratiba ya mikutano.Endelea kusoma habari hii

NAHODHA AMSHANGAA MAALIM SEIF

29 09 2010

Shamsi Nahodha

MGOMBEA wa Uwakilishi wa CCM jimbo la Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi Unguja, Shamsi Vuai Nahodha amezindua mikutano ya kampeni kwa kusema ameshangazwa kiongozi wa upinzani kusema atashirikana na mgombea wa CCM Dk Ali Mohammed Shein.Shamsi amesema kauli ya Maalim Seif inaoneshwa kuwa anakiri kushindwa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.Endelea kusoma habari hii

VIJANA MJI MKONGWE KUWEZESHWA

28 09 2010

Ibrahim Sanya

VIJANA wa Mji Mkongwe Zanzibar wameahidiwa kupatiwa jumla ya shilingi millioni 81 za kununuliwa boti na mashine zake kwa matawi tisa ya mji huo na wagombea wa ubunge na uwakilishi muda mfupi baada ya kuapishwa endapo wataibuka washindi wa jimbo hilo. Fedha hizo zimeelezwa kukabidhiwa kwa wananchi hao katika mkutano wa hadhara utakaofanyika siku chache baada ya kutangazwa washindi wa jimbo, Ibrahim Mohammed Sanya (Mbunge) na Ismail Jussa Ladhu (Mwakilishi).Endelea kusoma habari hii

NITAINGARISHA ZANZIBAR-DK SHEIN

28 09 2010

MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohammed Shein amesema kama atachaguliwa atang’arisha zaidi maendeleo ya sura ya Zanzibar kwa kukamilisha miradi ya huduma za jamii, iliyoanzishwa na awamu zilizoangulia.“Kipindi cha miaka mitano ijayo, cha uongozi wa awamu ya saba,….Zanzibar itang’ara kwa maendeleo katika sekta nyingi, ikiwa CCM itarejeshwa madarakani”, alisema juzi katika mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya Unguja Ukuu, kilomita 45 kusini mwa mji wa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

KIKWETE TUTAMPA UWAZIRI-APPT-MAENDELEO

27 09 2010

CHAMA Cha siasa cha APPT Maendeleo kimeahidi kumpa unaibu Waziri wa Nishati na Madini mgombea urais wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete iwapo kama kitashinda katika uchguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.Ahadi hiyo imetolewa na mgombea mwenza wa chama hicho Rashid Yusuf Mshenga katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika juzi katika Jimbo la Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi Unguja.Endelea kusoma habari hii

TUTAWAKOMBOA WAKULIMA-NCCR-MAGEUZI

27 09 2010

Ambar Haji Khamis

CHAMA cha NCCR Mageuzi kimeahidi kuandaa sera itakayomkomboa mkulima na kuweka mazingira ya kumuwezesha mkulima kupata mikopo kwa dhamana ya maisha yao ili kujenga uchumi ulio imara.Ahadi hiyo imetolewa na mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama hicho Ali Omar juma katika uzinduzi wa mikutano ya kampeni kijiji cha Machui Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.Endelea kusoma habari hii

WAFUASI WA CCM NA CUF WAPIGWA MAWE

26 09 2010

umoja huu watu unawakera

WATU wasiojulikana juzi wamewarushia mawe wanachama wa chama cha wananchi (CUF) na siku ya pili Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika matukio mawili tofauti wakati wafuasi hao wakirejea kutoka katika mikutano ya hadhara iliyofanyika kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.Matukio hayo yote mawili yametokea majira ya saa 12 jioni eneo la Bububu nje kidogo ya mji wa Zanzibar ambapo baadhi ya watu waliokuwa wamejificha walirusha mawe katika msafara ulioongozwa na Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Sharif Hamad na siku ya pili msafara wa mgombea wa CCM Dk Ali Mohammed Shein.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN AAHIDI HUDUMA ZA KIJAMII KUPATIKANA

26 09 2010

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kwa tiketi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Ali Mohammed Shein amesema ikiwa atapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi kuongoza serikali atahakikisha huduma za jamii zinaiimarika zaidi hasa katika katika vijiji vya Unguja na Pemba.Dk Shein alitoa ahadi hiyo jana wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano uliofanyika kwenye uwanjwa wa Shule ya Nungwi Mkoa Kaskazini Unguja.Endelea kusoma habari hii

NICHAGUENI NIWE RAIS NISAIDIANE NA DK SHEIN-MAALIM

26 09 2010

MGOMBEA urais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewaomba wazanzibari wampe kura ya ndio katika uchaguzi wa Octoba 31 ili awe rais na makamu wa rais awe Dk Ali Mohammed Shein waweze kuwaletea maendeleo. Alisema ikiwa yeye rais na makamo wake atakuwa ni Dk Shein ambaye ana uzoefu mkubwa na ulio makini katika kazi yake hivyo nchi itapata mageuzi makubwa ya kimaendeleo kwa kuwa wote ni wachapa kazi na ni watu wenye kuipenda Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

BARABARA YA FUONI KUWEKWA LAMI

25 09 2010

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inakusudia kujenga kwa kiwango cha lami barabara kutoka Fuoni Kibondeni hadi Kombeni, pamoja na barabara inayokwenda katika njia ya Ijitimai.Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Mawasiliano na Uchukuzi Machano Othman Said, katika mkutano wa kampeni wa kuwanadi wagombea wa jimbo la Fuoni akiwemo Mbunge, Mwakilishi na Diwani.Endelea kusoma habari hii

WAWEKEZAJI WANUFAISHE NCHI- MAALIM

25 09 2010

MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kupitia chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema iwapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa rais wa Zanzibar, atahakikisha wawekezaji wanaoingia nchini wanakuwa na maslahi ya Wazanzibari na sio kwa manufaa yao.Maalim Seif aliyasema hayo jana katika mkutano na wajasiriamali uliofanyika kwenye ukumbi wa Skuli ya Sunni Madrassa Mkunazini Mjini Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

WAANDAAJI WA MIHAHALO WAADHIBIWE-NCCR

24 09 2010

Ali Omar

CHAMA Cha NCCR Mageuzi kimeitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwachukulia hatua waandaaji wa midahalo ya kisiasa kutokana na kukiuka sheria na taratibu zilizowekwa nchini.Kauli hiyo imetolewa na Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Omar wakati akihutubia mkutano wake wa kampeni katika jimbo la Koani eneo la Machui Mkoa wa Kusini Unguja.Endelea kusoma habari hii

NIPENI KURA NILETE MABADILIKO-SHEIN

23 09 2010

DK ALI Mohammed Sheni Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar amesema ndoto yake kwa wazanzibari ni kuwaletea mabadiliko makubwa ya maendeleo na kuwataka wampe kura ili wapate kushuhudia mabadiliko hayo.Mgombea huyo alikuwa akiwahutubia wanachama wa chama hicho katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika jimbo la Mkanyageni kijiji cha Chokocho Kisiwani Pemba ambako yeye mwenyewe anatokea kijijini hapo.Endelea kusoma habari hii

WAGOMBEA SITA WAKIMBIA MDAHALO

23 09 2010

Mgombea urais wa AFP Said Soud akimpakia mwenzake kuelekea kwenye kampeni

MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad, amelamizika katika mdahalo wa mahojiano akiwa peke yake baada ya wagombea wengine sita wanaowania nafasi kama hiyo kukataa kushiriki katika mdahalo huo.Mdahalo huo ulifanyika juzi katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View Mjini hapa, uliandaliwa na Jumuiya za Kiraia, kwa lengo la kuwawezesha wagombea kueleza namna watakavyoshughulikia mambo mbali mbali na muhimu ikiwa watachaguliwa na kuunda serikali baada ya kumalizika uchaguzi.Endelea kusoma habari hii

AHADI ZA CUF ZINATEKELEZEKA-DEDES

21 09 2010

Mohammed Dedes

MJUMBE wa Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF), Abdulrahman Mohammed Dedes, amewataka wazanzibari kutokubali kubabaishwa na maneno yanayotolewa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kueneza kampeni zake kuwa ahadi zinazotolewa na CUF hazitekelezeki.Dedes amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya baadhi ya viongozi wa CCM akiwemo Hafidh Ali Tahir kueleza katika kipindi kinachorushwa ya Televisheni Zanzibar (TVZ) kwamba ahadi zinazotolewa na Maalim Seif kamwe sio za kweli na haziwezi kutekelezeka hivyo amewataka wananchi kupuuza kampeni za chama hicho cha CUF.Endelea kusoma habari hii

NGOME ZA CCM TUMESHAZIVUNJA-LIPUMBA

21 09 2010

Professa Lipumba

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano Profesa Ibarahim Haroun Lipumba amesema tayari wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuziteka ngome za CCM na imebakia kujipanga kuzilinda kura.Hayo ameyasema wakati akihutubia mkutano wa kampeni uliogfanyika katika uwanja wa Demokrasia Kibanda maiti mjini Zanzibar, ambapo jumla ya wanachama wapya 37 aliwakabidhi kadi za chama hicho.Endelea kusoma habari hii

CCM WACHENI UCHOCHEZI-VYAMA VYA UPINZANI

21 09 2010

Said Soud Said

VYAMA Vitatu vya Upinzani Zanzibar vya AFP, TADEA na NCCR Mageuzi, vimeiomba Serikali kuifanyia marekebisho sheria ya Uchaguzi ili kutoa fursa kwa mahakama kutoa maamuzi wakati viongozi wa vyama vya upinzani vinapokwenda kuilalamikia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).Hayo wameyaeleza jana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi ya NCCR Mageuzi huko Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi Unguja.Endelea kusoma habari hii

TUTAPIGANIA GAO LETU BOT-MAALIM

20 09 2010

MGOMBEA urais wa Chama cha Wananchi (CUF) visiwani hapa, Maalim Seif Sharif Hamad amesema akichaguliwa kuingia Ikulu, atahakikisha Zanzibar inapewa mgawo wa asilimia 11.02 badala ya 4.5 inayopewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).Pia, amesema atafuatilia matatizo na malalamiko mengine ili kupata haki zote ambazo Zanzibar inastahili kuzipata kutoka BoT na kuhakikisha uadilifu wa utendaji wa benki kuu unatendeka.Endelea kusoma habari hii

HAKUNA MTU ATAKAYETIBIWA NJE-NRA

20 09 2010

Haji Khamis na Marshed

CHAMA Cha Siasa cha NRA Zanzibar, kimesema kwamba iwapo wananchi wa Zanzibar watakipa ridhaa ya kuongoza nchi itahakikisha hakuna mtu anaekwenda kutibiwa nje ya nchi kwa kuwa kitazingatia mfumo wa kuimarisha matibabu.Hayo yameelezwa na Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Haji Khamis katika mkutano wa kampeni za urais uliofanyika kwenye viwanja vya Ijitimai Mwanakwerekwe, wilaya ya Magharibi Unguja.Endelea kusoma habari hii

MIDAHALO YETU NI UWANJANI-CCM

19 09 2010

SHINIKIZO la kutakiwa kuruhusu wagombea wake kushiriki katika midaharo limezidi kuisumbua CCM, hadi kufikia katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba kuibuka katika mkutano wa hadhara na kuendelea kupiga marufuku kushiriki.Jana katika uzinduzi wa kampeni za CCM visiwani hapa, uliofanyika katika viwanja vya Demokrasia Kibandamaiti, Makamba alilazimika kutolea ufafanuzi zaidi juu ya uamuzi wa kuwasimamisha wagombea kushiriki midaharo akisema, wagombea wa CCM watafanya midaharo katika mikutano ya hadhara na si vinginevyo.Endelea kusoma habari hii

NITALETA MAGEUZI YA KIUCHUMI-NRA

19 09 2010

MGOMBEA Urais wa Chama cha Mwamko wa umma (NRA) Haji Khamis Haji alisema iwapo atapewa ridhaa ya kuwaongoza wazanzibari atafanya mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa kuanzisha viwanda vya usindikaji bidhaa na kuondosha kodi za kibishara zinazowabana wafanyabishara wadogo wadogo nchini.Alisema ili kuhakikisha uchumi unakua ataanzisha viwanda vya usindikaji wa bidhaa za matunda hasa wakati wa msimu wa matunda unapowadia kuweza ksuaidia na utatumika kuyasindika pamoja na kusindika samaki kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi ili kuimarisha uchumi.Endelea kusoma habari hii

VIONGOZI WA DINI WATETA NA WAGOMBEA

18 09 2010

MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad jana alikutana na ujumbe wa Kamati ya Amani Tanzania uliofika ofisi kwake Vuga, mjini Zanzibar. Ujumbe huo ulijumuisha masheikh kutoka Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) na Ofisi ya Mufti pamoja na maaskofu kutoka CCT (Kanisa Katoliki) na TEC (Baraza la Maaskofu Tanzania) na uliongozwa na Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa TEC.Endelea kusoma habari hii

CCM HAINA PICHA ZA WAGOMBEA MITAANI

18 09 2010

WAKATI kampeni Visiwani Zanzibar zikiwa zimezinduliwa rasmi jana, usiri mkubwa umegubikwa ndani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) visiwani hapa, huku chama hicho kikiwa bado hakijabandika picha yoyote ya mgombea urais, Dk Ali Mohamed Shein na ya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.Pia, hali kama hiyo imejitokeza kwa wagombea wa ubunge,uwakilishi na udiwani ikiwa ni tofauti na vyama vingine ambavyo tayari vimekwisha bandika picha za wagombea wao katika maeneo mbali mbali.Endelea kusoma habari hii

TUTAHIMIZA UWAJIBIKAJI-MAALIM SEIF

17 09 2010

CHAMA Cha Wananchi CUF, kimesema Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na Chama hicho, itatunga sheria mpya itakayodhibiti utumiaji mbaya wa madaraka ya umma na kwamba itaongoza kwa kufuata misingi ya utawala bora na sheria.Hayo yameelezwa na Mgombea wa Urais wa chama hicho Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya suala la uongozi mwema na maridhiano, huko katika Ukumbi wa Bait-alyamin Bwawani mjini Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

HATUNA HARAKA KUMTANGAZA MENEJA WETU-CCM

17 09 2010

Vua Ali Vuai

WAKATI leo Chama cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar kikiwa kinazindua kampeni zake rasmi katika Viwanja vya Demokrasia Mjini Unguja bado hakijamtangaza meneja kampeni wake hadi sasa.Hatua hiyo imeelezwa kusababishwa na mvutano wa chini kwa chini na kwamba imetokana na kutoaminia kati ya makundi yaliopo miongoni mwao.Endelea kusoma habari hii

KANSA YAWAMALIZA WAZANZIBARI-NCCR

17 09 2010

Haji Ambar na Ali Omar

MGOMBEA Mwenza wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Omar kupitia chama cha siasa cha NCCR Mageuzi amesema kwamba wazanzibari wengi wamekuwa wakiuguwa maradhi ya kansa kutokana na kula vyakula visivyokuwa na ubora.Hayo aliyaeleza jana katika uzinduzi wa kampeni wa chama hicho uliofanyika katika Kiwanja cha Komba wapya Mwembeladu Mkoa wa Mjini Unguja.Endelea kusoma habari hii

KAMPENI ZA CUF ZAZINDULIWA KWA NJIWA NA NYOKA

16 09 2010

NYOKA aina ya Chatu mwenye urefu wa mita 2.5 jana aliibuka katika uzinduzi wa kampeni za Chama cha Wananchi (CUF) na kuacha taharuki miongoni mwa mamia wa ya watu walioudhuria katika uzinduzi huo.Mbali na nyoka huyo ambaye hakuleta madhara yoyote, chama hicho kilizindua kampeni hizo kwa kupeperusha njiwa watatu weupe.Hayo yalitokea katika viwanja vya Demokrasia eneo la Kibanda Maiti visiwani Unguja ambapo kabla ya uzinduzi huo kulifanyika maandamano ya wanaCUF yaliyoanzia katika viwanja vya Mnazi Mmoja majira ya saa 4 asubuhi.Endelea kusoma habari hii

CUF WAZUWIWA KUFANYA MKUTANO

16 09 2010

CHAMA Cha Wananchi (CUF) katika jimbo la Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini Unguja, kimeshindwa kufanya mkutano uliopangwa kufanyika katika shehiya ya Muange baada ya wananchama na wananchi wa jimbo hilo kushindwa kupata tarifa kutokana na kuzuiliwa na sheha katika shehia hiyo.Mkutano huo ulikuwa wa uzinduzi wa kampeni wa kuwatambuliha wagombea wa Ubunge,Uwakilishi na Udiwani ulikuwa uhutubiwe na Makamo Mwenyekiti wa Chama hicho taifa Machano Kamis Ali.Endelea kusoma habari hiyo

MSIKUBALI KUBABAISHWA-MACHANO

15 09 2010

Machano Khamis Ali

MAKAMO Mwenyekiti wa CUF Taifa, Machano Khamis Ali amewataka wananchi kutosikiliza maneno ya baadhi ya viongozi wa dini wanaopita wakisema kwamba kushiriki katika uchaguzi ni dhambi hususan kwa wanawake.Makamo Mwenyekiti huyo alisema kwamba kumejitokeza baadhi ya makundi ya kidini ambayo yamekuwa yakihamasisha wananchi hasa wanawake watoshiriki kwenye uchaguzi kwa madai kuwa ni demokrasia ni haramu na inakwenda kinyume na maagizo ya dini.Endelea kusoma habari hii

VIJANA WA CCM WASHUTUMIWA

14 09 2010

IKIWA zimebaki siku chache kabla ya vyama vya kisiasa kuzindua kampeni zao Visiwani Zanzibar baadhi ya wagombea wa Chama Cha Wananchi (CUF) wamelalamikia tabia kubanduliwa picha za wagombea wao katika maeneo mbali mbali na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) visiwani hapa.Kwa mujibu wa maadili ya vyama vya siasa ambayo vyama vyote vimesaini maadili hayo ikiwemo CCM na CUF viongozi hao wamekubaliana kuendesha siasa za kistaarabu na kuvumiliana kisiasa bila ya kuchafuana kwa wagombea wala vyama ikiwa pamoja na kutochaniana picha za kampeni zinazobandikwa na vyama hivyo.Endelea kusoma habari hii

HAKIKISHENI MNALINDA KURA

13 09 2010

MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka mawakala wa chama chake kuhakikisha wanalinda kura zao kwa hali yoyote katika vituo vyao vya kupigia kura ili zisiibiwe.Akifungua mkutano wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Wananchi (CUF) lililofanyika Jamat-Khan eneo la Mji Mkongwe Maalim Seif alisema tabia ya mawakala kutoa nje kwenda kujisaidia kunatoa fursa ya baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kuiba kura za CUF.Endelea kusoma habari hii

MAALIM SEIF AZINDUA MTANDAO WAKE

12 09 2010

MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad jana amezindua mtandao wake ikiwa ni hatua ya kuwasiliana moja kwa moja na wananchi wanaotaka kuwasiliana naye.Mtandao huo uitwao http://www.maalimseifforpresident.net umezinduliwa pamoja na uzinduzi wa ilani ya uchaguzi ya chama hichi katika hafla iliyofanyika ukumbi wa juu wa hoteli ya Bwawani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Endelea kusoma habari hii

KARUME ATAKA KAMPENI ZA UTULIVU

10 09 2010

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume amewataka wazanzibari kushiriki katika uchaguzi kwa kuzingatia wanaendelea kuheshimu maridhiano yaliofikiwa na kuacha kutumia lugha za kejeli ili kuharibu maridhiano hayo. Karume aliyasema hayo wakati akitoa salamu zake za Eid El Fitri alipokuwa akihutubia baraza la Eid lililofanyika ukumbi wa Jumba la Wananchi (Peoples Palace) liliopo Forodhani Mjini Unguja.Endelea kusoma habari hii

MAAMUZI YA RUFAA YA NAHODHA KUTOLEWA

8 09 2010

TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imeahidi kutoa maamuzi ya rufaa ya mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Mwanakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha anayedaiwa kufanya kampeni kabla ya muda uliowekwa na tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).Vuai ambaye ni waziri kiongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar aliwekewa pingamizi na mgombea wa chama cha wananchi CUF, Idrissa Shaame Hamad wiki mbili zilizopita akidai Nahodha amekuwa akifanya kampeni katika jimbo hilo kinyume cha sheria kwa kuwa muda wa kampeni haujatangazwa rasmi lakini pingamizi hilo lilitupwa na msimamizi wa uchaguzi wilaya Suluhu Ali Suluhu.Endelea kusoma habari hii

VYAMA VYA SIASA VYASAINI MUONGOZO

7 09 2010

VIONGOZI wa vyama vya siasa 15 Zanzibar jana walitia saini rasimu ya muongozo wa maadili ya vyama vya siasa ikiwa ni kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Vyama hivyo vimekutana katika ofisi za tume ya uchaguzi na kushuhudiwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi pamoja na maafiasa wake kwa lengo la kuendesha kampeni za nidhamu zizizo na matuzi wala kejeli baina yao.Endelea kusoma habari hii

TEMCO YAMWAGA WAANGALIZI WA UCHAGUZI

6 09 2010

JUMLA ya waangalizi 7,210 wanatarajiwa kuangalia mwenendo wa uchaguzi mkuu katika maeneo yote ya Tanzania Bara na Zanzibar unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini.Mratibu wa kamati ya kuangalia uchaguzi Tanzania (TEMCO) Dk Benson Banna aliwaambia waandishi wa habari wakati akizungumza juu ya matayarisho ya uchaguzi mkuu katika ukumbi wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ) Rahaleo Mjini Unguja.Endelea kusoma habari hii.

SHERIA YA MABADILIKO YA KATIKA YATIWA SAINI

4 09 2010

SHERIA namba 9 ya mwaka 2010 ya marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya 1984 ambayo inaitambua Zanzibar kuwa ni nchi na muundo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa imetiwa saini rasmi na Rais Amani Abeid Karume, Agosti 13, 2010 mwaka huu. Sheria hiyo imekuja kufuatia kura ya maoni iliyopigwa Julai 31 mwaka huu na asilimia 66.4 ya waliopiga kura kukubali mfumo mpya wa muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ufanyike baada ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu.Endelea kusoma habari hii

NAHODHA AWEKEWA PINGAMIZI JIMBONI

4 09 2010

WAZIRI kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha

Msimamizi wa ZEC wilaya

amewekewa pingamizi na mgombea wa chama cha wananchi (CUF) Idrissa Shaame Hamad kwa kufanya kampeni kabla ya wakati na kutumia rasilimali za serikali katika kampeni zake.Hamadi alisema katika pingamizi lake kwamba Nahodha amekuwa akifanya kampeni katika jimbo la Mwanakwerekwe kabla ya muda rasmi kwa kampeni hizo kutangazwa kwa upande wa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

KURA ZENU NI SIRI-ZEC

2 09 2010

MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Khatib Mwinyichande amesema karatasi za kupigia kura zitakazotumika katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu, itabakia kuwa siri kwa mpigaji wa kura hiyo.Mwinyichende imekuja baada ya baadhi ya wananchi kutishana kwmaba mtu anayepiga kura katika chama atakuwa anajulikana iwapo atatafutwa amepigia chama gani kutokana na vishina vya vitabu vya kupigia kura kuwa na namba za pembeni.Endelea kusoma habari hii

SAU YASHINDWA KUREJESHA FOMU ZEC

30 08 2010

Mussa Haji Kitole

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Sauti ya Umma (SAU) Haji Mussa Kitole jana ameshindwa kurejesha fomu za kuwania nafasi hiyo kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambayo ni siku ya mwisho wa urejeshaji wa fomu hizo.Kitole awali alikataliwa kupewa fomu ya kuwania nafasi hiyo na ZEC kutokana na kuwa chama hicho kimetoa wagombea urais wawili wenye kutaka kuwania urais wa Zanzibar wakati sheria za ZEC zinaeleza chama kitowe mgombea mmoja wa nafasi hiyo.Endelea kusoma habari hii

NAHODHA AWASHANGAA WANA CCM

28 08 2010

WAZIRI Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuia Nahodha amewashangaa wanasiasa wenye kuhama vyama vyao na kuhamia vyama vyengine baada ya kukosa kuteuliwa katika kura ya maoni.Nahodha alisema tabia hiyo huwakuta wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwa hawana itikadi za chama chao na sio waumini wa kweli kutokana na kutawaliwa na tamaa za madaraka.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN WA PILI KUREJESHA FOMU

27 08 2010

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Ali Mohammed Shein jana maerudhisha fomu za kuwania nafasi hiyo kwa tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kukamilisha wadhamini katika mikoa mitano ya Unguja na Pemba.Akizungumza muda mfupi baada ya kupokewa na maandamano makubwa katika uwanja wa afisi kuu ya CCM Kisiwandui Dk Shein amesema ataingoza Zanzibar kwa kuweka maslahi ya wananchi mbele kwa mujibu wa katiba inavyosema.Endelea kusoma habari hii

WABUNGE KUMI WASHINDWA KUREJESHA FOMU

25 08 2010

JUMLA ya wagombea 10 waliochukua fomu za kuwania ubunge kutoka vyama tofauti wameshindwa kurejesha fomu zao kwa tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania (NEC). Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa tume hiyo imesema kwamba pamoja na wagombea wengi kujitokeza katika kuwania nafasi hiyo lakini baadhi yao wameshidwa kurejesha fomu hizo hadi siku ya mwisho ya urejeshaji wa fomu katika ofisi za wilaya.Endelea kusoma habari hii

NRA WAINGIA KATIKA KINYANYANYIRO CHA URAIS

24 08 2010

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha National Reconstruction Alliance (NRA) Haji Khamis Haji jana amechukua fomu kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).Haji mwenye umri wa miaka 60 ambaye ni kiongozi wa taasisi ya kidini inayojulikana kwa jina la Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) amekabidhiwa fomu hiyo majira ya saa 4:00 kamili asubuhi huku akitakiwa kufuata masharti yote yaliowekwa na tume hiyo kabla ya kurejesha fomu ya kuwania wadhifa huo.Endelea kusoma habari hii.

SIRI YA MARIDHIANO ZNZ YAWEKWA HADHARANI

24 08 2010

KATIBU mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad amesema kuwa sifa za maridhiano yaliyofikiwa Zanzibar hazipaswi kuelekezwa kwake wala kwa rais wa Zanzibar, Abedi Amani Karume na kwamba suala hilo lilifanywa kuwa siri kubwa kwa karibu miezi sita kuepuka kuvurugika kwa mpango wa muafaka.Karume na Seif wamekuwa wakisifiwa kuwa ndio walioasisi suala la maridhiano baada ya kukutana mara mbili Ikulu ya mjini hapa, mazungumzo yaliyofuatiwa na kitendo cha Maalim Seif kutangaza kuwa CUF imeamua kumtambua Karume kuwa rais wa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

MAALIM SEIF AREJESHA FOMU

23 08 2010

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amerudisha fomu za kuwania nafasi ya urais baada ya kukamilisha masharti ya kupata wadhamini.Maalim Seif ni mgombea wa kwanza kurejesha fomu za kuwania urais wa Zanzibar kati ya wagombea sita wanaowania nafasi hiyo ambao wamechukua fomu kwa tume ya uchaguzi Zanzibar iliyopo Maisara Mjini Unguja.Endelea kusoma habari hii.Endelea kusoma habari hii

UCHAGUZI UWE HURU NA HAKI-MAREKANI

23 08 2010

BALOZI wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt amesema matamaini yake makubwa ni kwamba uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba utakuwa wa huru na haki.Balozi huyo aliyasema hayo muda mfupi baada ya kukagua jingo jipya ya baraza la wawakilishi ambalo limefunguliwa hivi karibuni wakati akizungumza na kamati ya watu sita ya kusimamia maridhiano ya kisiasa na kura ya maoni visiwani Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

WABUNGE WATATU WAWEKEWA PINGAMIZI

22 08 2010

Salim Hassan Turky

BAADHI wa wabunge wa chama cha mapinduzi walioshutumiwa kutoa rushwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama chao wamejitetea kwamba hawawezi kushitakiwa kwa kuwa hakuna sheria ya kudhibiti rushwa Zanzibar.Wagombea hao ni pamoja na Turky Salum Hassan aliyegomeba ubunge katika jimbo la Mpendae Mkoa wa Mjini Magharibi anadaiwa kutoa fedha kwa ajili ya kuwapa wanachama wake ili wamchague katika kinyanyanyiro hicho ambacho kimemalizika hivi karibuni.Endelea kusoma habari hii

MGOMBEA WA JAHAZI ACHUKUA FOMU

19 08 2010

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha Jahazi Asilia,

Kassim Ali Bakari

Kassim Ali Bakari amesema watatumia sera ya uzanzibari katika kampeni kwa kukinadi chama chao katika uchaguzi mkuu unaitarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Mbali ya sera hiyo amesema chama chake kitafanya miujiza mikubwa ya kupata ushindi tofauti na watu wanavyofikiria ambao wanamaini kwamba jahazi asilia hakina wanachama wala hakina nguvu katika kuleta ushindi wa urais wa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN ACHUKUA FOMU YA URAIS ZANZIBAR

18 08 2010

Dk Ali Mohd Shein

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Ali Mohammed Shein jana amechukua fomu ya kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar kwa tiketi cha chama cha mapinduzi (CCM) na kujilabu kuwa CCM hakina mbadala katika ushindi nchini.Mara baada ya kuchukua fomu hizo Dk Shein akwenda aliongozana na msafara wake na kwend amoja kwa moja hadi ofisi ya chama cha mapinduzi Mkoa wa Mjini na kuzungumza na wadhamini wake ambao alipata fursa ya kuzungumza nayo.Endelea kusoma habari hii

SITAWAVUMILIA WENYE CHUKI-DK SHEIN

17 08 2010

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Ali Mohammed Shein amewataka wana CCM kusafisha nyoyo zao na kuondokana na chuki na ubinafsi kabla ya yeye kuingia madarakani.Dk Shein ameyasema hayo jana katika hoteli ya Bwawani wakati akizungumza na wagombea wa nafasi mbali mbali za ubunge, uwakilishi na udiwani walioshinda na walioshindwa katika mchakato wa upitiaji majina ya wagombea uliofanyika hivi karibuni Mjini Dodoma.Endelea kusoma habari hii

SAU YANYIMWA FOMU ZEC

16 08 2010

WAGOMBEA wawili jana wamechukua fomu za kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar na kufanya idadi ya wagombea hao kufikia wanne baada wa wengine wawili kujitokeza juzi kuchukua fomu hizo huku wengine wawili wakikataliwa kutokana na kujitokeza wagombea wawili wa chama kimoja.Wagombea walikwisha chukua fomu hizo ni pamoja na Juma Ali Khatib kutoka chama cha TADEA na Haji Ambar Khamis kutoka chama cha NCCR-Mageuzi ambapo jana waliochukua fomu ni Mwenyekiti wa chama cha Wakulima (AFP) Said Soud Said na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad.Endelea kusoma habari hii

WAGOMBEA WA URAIS ZANZIBAR WAONGEZEKA

15 08 2010

MBIO za kutaka kuwania kinyanganyiro cha urais wa Zanzibar zimeendelea

Juma Ali Khatib

kupamba moto baada ya kujitokeza wagombea saba wa vyama tofauti kutaka kunyakua nafasi hiyo.Tayari wagombea wawili wamechachukua fomu akiwemo mgombea wa urais kupitia tiketi ya TADEA, Juma Ali Khatib na mgombea wa NCCR-Mageuzi, Haji Ambar Khamis wamechachukua fomu zao Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) huku wakitakiwa kutimiza masharti ikiwa pamoja na kutafuta wadhamini 200 kwa mikoa mitano ya Unguja na Pemba.Endelea kusoma habari hii.

NCCR-MAGEUZI KUCHUKUA FOMU YA URAIS ZNZ

13 08 2010

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Zanzibar, Haji Ambar Khamis amejitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia chama hicho katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Khamis atakuwa ni mtu wa pili baada ya kutanguliwa na mgombea urais wa TADEA, Juma Ali Khatib aliyechukua fomu hizo juzi katika ofisi za tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) Maisara Mjini Zanzibar.Akimkabidhi fomu hiyo Mwenyekiti wa Tume hiyo, Khatib Mwinchande alimtaka kukamilisha taratibu zote zinazotakiwa ikiwa pamoja na kupata wadhamini wa miko mitano ya Unguja na Pemba.Endelea kusoma habari hii

KAMPENI YETU NI UMOJA-MAALIM SEIF

11 08 2010

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad Maalim Seif amesema chama chake hakitakuwa na kazi kubwa kufanya kampeni zaidi ya kuhimiza umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi wote wa Zanzibar.Maalim Seif alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika viwanja vya Mapembeani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.“Hatuna haja ya kufnaya kampeni sisi kampeni yetu kubwa itakuwa ni kuleta umoja na slogan yetu itakuwa ni umoja na mshikamano kwa wazanzibari wote bila ya ubaguzi” alisema Maalim Seif.Endelea kusoma habari hii

WASOMI WAJITAYARISHE KURUDI ZANZIBAR. MUWAZA

9 08 2010

Dk Yussuf Salim Mwenyekiti wa MUWAZA

SIKU chache baada ya maamuzi ya wazanzibari kutaka kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa wazanzibari wataalamu wote waishio nje ya nchi wametakiwa kujitayarisha kurejea kwao kwa lengo la kujenga nchi yao.Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa Jumuiya ya wazanzibari waishio nje ya nchi (MUWAZA) Dk Yussuf Salim anayeishi mji wa Copenhagen Denmark katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyosambazwa na Mwananchi kupata nakala na taarifa hiyo.Dk Salim amewataka wazanzibari wataalamu wa fani mbali mbali ambao kwa muda mrefu wamekwenda nje ya nchi kufuata masomo au kutokana na tofauti za kisiasa wajitayarishe kurejea nchini wakati wowote watakapohitajika kwa lengo la kuijenga Zanzibar mpya yenye matumaini mapya na maendeleo.Endelea kusoma habari hii

UMOJA WA MATAIFA WASIFU KURA YA MAONI

5 08 2010

Rais Karume na Asha Rose Migizo

UMOJA wa Mataifa umetoa pongezi zake kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume na wananchi wote wa Zanzibar kwa kufanikisha kura ya maoni kwa amani na utulivu.Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro aliyasema hayo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais Karume, Ikulu mjini Zanzibar.Dk. Migiro, alimueleza Rais Karume kuwa Umoja wa Mtaifa umeridhika na hatua iliyofikiwa katika kufanikisha zoezi zima la kura ya maoni kwa amani, utulivu na mafanikio makubwa.Endelea kusoma habari hii

HAROUN ASIKITISHWA NA MATOKEO YA KURA ZA MAONI

5 08 2010

Haroun Ali Suleiman

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali na Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi (CCM), Haroun Ali Suleiman amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika hilo kuyakubali matokeo ya kura za maoni kwa lengo la kuwaunganisha wazanzibari wote na mustakabali wa maendeleo ya Zanzibar.Kauli hiyo aumeitoa jana katika kikao maalum na wajumbe wa kamati ya siasa wanaowakilisha matawi 12 ya jimbo la Makunduchi liliopo Mkoa wa Kusini Unguja ambapo aliwataka wana CCM kuungana kwa sasa kwa kuwa matokeo ndio yameshatokea licha ya yao kutokubali kutia kura ya ndio kwa asilimia kubwa.Endelea kusoma habari hii

KARUME: PICHA YA KUMBUKUMBU IREJESHWE

4 08 2010

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume ameagiza kupatiwa picha yake aliyodai kuchukuliwa ndani ya afisi kuu ya chama cha mapinduzi CCM Kisiwandui Mjini Unguja na kupelekwa katika maskani ya Kisonge.Agizo hilo la Rais Karume amelitoa wakati wa kuzindua barabara ya kutulia na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar jana.Amesema picha hiyo ni ya marehemu baba yake mzee Abeid Amani Karume, na mkewe Bi Fatma Karume, Ali Karume na yeye mwenyewe ambayo walipiga uwanja wa ndege mara baada ya Mzee Karume kurejea safari yake kutoka nchini Ghana alipokwenda kwa ajili ya usuluhishi.Endelea kusoma habari hii

WAZANZIBARI WAENDELEA KUPONGEZWA

4 08 2010

NCHI za Uingereza na Ufaransa zimetoa pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume kwa kufanikisha kura ya maoni kwa amani na utulivu na kueleza matarajio yao makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii hapa Zanzibar.Balozi wa Uingereza Bi. Diane Corner na Balozi wa Ufaransa Bw Jacques Champagne de Labriolle, waliyasema hayo wakati walipokuwa na mazungumzo na Rais Karume, huko katika ukumbi wa uwanja mdogo wa ndege wa Zanzibar walipokutana kwa ajili ya sherehe za kuzindua uwanja huo ambayo umemaliza kufanyika matengenezo ya njia za ndege.Endelea kusoma habari hii

EU WAFURAHISHWA NA MATOKEO YA NDIO

3 08 2010

Rais Karume na Tim Clark

UMOJA wa nchi za Ulaya (EU) umetoa pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume kutokana na kufanikisha zoezi la Kura ya Maoni na kueleza kuwa Zanzibar imepata maendeleo ya kupigiwa mfano kidemokrasia.Mwakilishi wa Umoja wa nchi za Ulaya, Balozi Tim Clarke aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais Karume Ikulu mjini Zanzibar.Katika mazungumzo hayo ambapo Balozi Clarke akifuatana na baadhi ya Mabalozi wa nchi za Ulaya wanaofanyia kazi zao hapa Tanzania, alisema kuwa hatua iliyofikiwa Zanzib ar katika demokrasia ni kubwa na inapaswa kuungwa mkono.Endelea kusoma habari hii

WAWAKILISHI KUBADILISHA KATIBA WIKI IJAYO

3 08 2010

Wajumbe wa baraza la wawakilishi

MAREKEBISHO ya katiba yatakayoruhusu kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar yatari yemkamilika na yanatarajiwa kuwasilishwa Agosti 9 mwaka huu katika kikao cha baraza la wawakilishi Mjini Unguja. Kwa mujibu wa rasimu mswaada wa sheria ya marekebisho ya 10 ya katiba ya mwaka 1984 iwapo marekebsiho hayo yatapitishwa Zanzibar itaingia katika mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa. Marekebisho hayo ya katiba yamependekeza kifungu cha 39 cha katiba ya Zanzibar kufutwa na kuondoa nafasi ya waziri kiongozi na badala yake kutakuwa na makamu wawili wa rais ambao watajulikana kama makamu wa kwanza wa rais na makamu wa pili wa rais. Endelea kusoma habari hii

MAWAZIRI WA SMZ WATEMWA KURA ZA MAONI

2 08 2010

MAWAZIRI wawili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), manaibu waziri watatu na naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar ni miongoni mwa wagombea walioanguka katika kura za maoni zilizopigwa juzi nchi nzima.Wagombea wengine akiwemo Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Hamad Masauni Yussuf amepata ushindi kwa kupata kura 990 akimshinda Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz aliyepata kura 155 aliyetokea wa tatu katika mchakato huo na wa pili ni Mohamed Ahmed Mohamed aliyepata kura 511.Endelea kusoma habari hii

KATIKA HILI HAKUNA MSHINDI-KARUME

2 08 2010

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume amesema kufuatia kura ya maoni kupata ushindi na hatimae kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa hakuna mshindi kati ya walioshinda na walioshindwa bali ni wananchi wote wameshinda.“Bado tuna wajibu wa kuthibitisha kuwa mshindi wa zoezi hili ni Zanzibar na Wazanzibari wote, kwa kuhakikisha kwamba sote kwa pamoja tunaendesha uchaguzi mkuu ujao katika hali ya amani, salama na utulivu, tarehe 31 Oktoba mwaka huu. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kudumisha utulivu na ushirikiano tulionao hivi sasa” alisema na kuongeza kwamba.Endelea kusoma habari hii

CCM WAPIGA KURA ZA MAONI

1 08 2010

WANACHAMA wa CCM leo wameshiriki kupiga kura ya maoni kwa ajili ya kuwachagua wajumbe wa baraza la wawakilishi, wabunge na madiwani katika majimbo 50 ya Unguja na Pemba.Jumla ya wanachama wa CCM 735, wamepiga kura hiyo ya maoni baada ya kumalizika kwa mchakato wa kufanya kampeni zilizokuwa zikifanyika katika matawi ya CCM ya Unguja na Pemba.Baadhi ya makatibu wa wilaya walipozungumza waandishi wa habari na walieleza kukamilika kwa matayarisho ya maadalizi ya upigaji kura hizo ambapo katibu wa CCM wilaya magharibi, Mkongea Ali Pira, alisema jumla ya wagombea wanaoshiriki katika mchakato huo ni 165 ambapo wanaowania udiwani ni 53, uwakilishi 56 na ubunge 56.Endelea kusoma habari hii

WAZANZIBARI WAKUBALI KUUNDA SERIKALI YA UMOJA

1 08 2010

WAZANZIBARI wamekubali kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya kupiga kura ya ndio hapo jana na kushinda kwa asilimia 66.6 visiwani Zanzibar.Kura ya ndio, ilikuwa ikisubiriwa kuamua mfumo mpya wa kuundwa kwa serakali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ambapo imepata 66.4% dhidi ya kura za hapana zilizopata 33.6% kati ya kura zote halali 284,318 zilizopigwa katika mikoa yote mitano ya Unguja na Pemba.Endelea kusoma habari hii

KURA YA MAONI ITAPIGWA KWA SALAMA-KARUME

1 08 2010

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume, amesema zoezi la upigaji wa kura ya maoni lilivyoendeshwa ni dalili ya kuwepo mazingira bora ya maandalizi ya uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kutawaliwa na amani na utulivu.Rais Karume, alitoa matumani hayo jana asubuhi mbele ya waandishi wa habari baada ya kupiga kura ya maoni katika kituo cha Skuli ya Kiembesamaki, Magharibi Unguja.Kura hiyo ni suali wanaloulizwa Wazanzibari kama wanakubali kuwepo mfumo mpya wa serikali baada ya uchaguzi mkuu ujao..Endelea kusoma habari hii

KURA YA MAONI YAFANYIKA KWA UTULIVU

31 07 2010

Rais Karume akipiga kura kituo cha kiembe samaki

KURA ya maoni ya kuamua kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar imefanyika kwa amani jana kinyume na chaguzi zilizopita ambazo husababisha watu kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu.Wananchi walianza kujitokeza asubuhi kabla ya zoezi hilo kuanza kufanyika mnamo majira ya saa 2 asubuhi chini ya ulinzi wa kawaida wa askari polisi ambao walionekana makini wakiwa hawana silaha katika maeneo ya vituo vya wapiga kura. Katika mitaa ya mji wa Zanzibar doria ya askari ilikuwa imeimarishwa wakiwemo askari wa FFU ambao walionekana katika maeneo mbali mbali kuhakikisha zoezi hilo linafanyika katika kwa amani na utulivu.Endelea kusoma habari hii

MKUU WA WILAYA ATIMULIWA KAZI

31 07 2010

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume amemtimu kazi mkuu wa wilaya ya kati Ali Hassan Khamis akidaiwa kufanya kampeni chafu dhidi ya kura ya maoni ambayo itafanyika leo visiwani Zanzibar itakayoamua muundo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa.Taarifa kutoka ikulu zimesema rais karume ametmfukuza kazi mkuu wa wilaya hiyo kwa mujibu wa kifungu namba 53(b) cha sheria ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinachompa mamlaka rais kumfukuza mtu yeyote katika serikali yake.Hadi sasa hakuna sababu zilizotolewa kuhusiana na kufukuzwa kazi kwake lakini kwa mujibu wa tetesi ziliopo ni kwamba hatua ya rais karume imefuatia kauli yake ya juzi aliyoitoa katika hafla ya kuzindua majenereta ya umeme mtoni mjini Zanzibar amabpo alisema kuna baadhi ya viongozi wa serikali wamekuwa wakiwashawishi wananchi kupiga kura ya hapana.Endelea kusoma habari hii

MAALIM SEIF AKABIDHIWA ZAN ID MPYA

28 07 2010

Maalim Seif akikabidhiwa Zan ID na Hamid Haji Mwanasheria wa Idara ZanID

MGOMBEA wa rais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amesema ana matumaini ya kura ya maoni itakayoamua kuundwa kwa seirkali ya umoja wa kitaifa itafanikiwa kwa zaidi ya asilimia 52 kutokana na wananchi walio wengi wa zanzibar kuonekana kuunga mkono suala hilo.Maalim Seif aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa kitambulisho kipya cha Mzanzibari Mkaazi (Zan ID) chenye usajili namba namba ID 030114469 na mke wake Awena Sinani Masoud chenye usajili namba ID 199976376 na Mwanasheria wa Idara ya Ofisi ya Vitambuliho vya mzanzibari makazi Hamid Haji Machano Mtoni Mjini Unguja.Endelea kusoma habari hii

MSIKUBALI KUFITINISHWA-MWENYEKITI

27 07 2010

WANANCHI Kisiwani Pemba wamewatakiwa kutokubali kufitinishishwa kwa

Ali Mzee Ali

sababu za tofauti za kiitikadi kisiasa juu ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo inatarajiwa kufanyika Julai 31 mwaka huu.Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Watu sita ya Baraza la Wawakilishi inayofuatilia kura za maoni, Ali Mzee Ali alipokuwa akizungumza na wananchi mbali mbali katika kikao kilichoanza jana Kisiwani humo.Akizungumza katika mkutano wa pamoja wa Madiwani na Masheha wa Mkoa wa Kusini Pemba jana Ali Mzee alisema kwamba hivi sasa kumeundwa utaratibu moya wa kuzika siasa za fitina, chuki na hasama ambazo zinahitaji kuepukwa kabisa na badala yake kujenga mustakabali mpya wenye matumaini wenye kuzingatia umoja na mshikamano kwa jamii.Endelea kusoma habari hii

MASHEHA WA KASKAZINI WAKUBALI MARIDHIANO

26 07 2010

VIONGOZI wa Serikali za Mitaa Zanzibar (MASHEHA) wamesema kwa kuwa wao ndio waathirika wakubwa wa matukio ya vurugu katika chaguzi zote zinazofanyika visiwani Zanzibar wanahitaji mabadiliko makubwa ya kiserikali.Masheha hao wamesema hayo katika mkutano wa siku moja mbele ya kamati ya baraza la wawakilishi ya kusimamia maridhiano ya CCM na CUF ili chini ya Mwenyekiti wake Ali Mzee Ali katika kikao cha kutoa elimu juu ya kura ya maoni itakayoamua kuundwa au kutokuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

NDIO KWA KUINUSURU NCHI YETU-MAALIM

20 07 2010

KAMPENI za Kura ya Maoni zinaendelea kupata kasi hivi sasa, baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kutangaza rasmi msimamo wake wa kuwataka wananchi wa Zanzibar kupiga kura ya ndio ifikapo Julai 31 mwaka huu.Akitangaza msimamo huo uliotarajiwa wa chama chake, Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, alisema kwamba Zanzibar inahitaji serikali ya umoja wa kitaifa kwani ndio suluhisho pekee la kuimaliza miaka karibuni hamsini ya siasa za ubaguzi, uhasama na chuki.“Ukipiga kura ya HAPANA maana yake hutaki umoja, hutaki maelewano, hutaki amani. HAPANA maana yake unataka migogoro, magomvi, chuki na hasama viendelee..Endelea kusoma habari hii

WAPINGAJI WA KURA YA MAONI MAFICHONI

19 07 2010

Ubao unaotumiwa na CCM kwa kuandikia ujumbe

KAMPENI ya kuhamasisha wazanzibari kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura ya maoni itakayoamua kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar imeanza kwa kasi kubwa huku baadhi ya wanaopiga kura hiyo wakiwa mafichoni.Wakati kamati ya wajumbe sita wa baraza la wawakilishi ikiendelea kutoa elimu uchunguzi wa gazeti hili umegundua kwamba kumekuwepo na upotoshaji mkubwa wa wafanyao kampeni hiyo ambapo baadhi yao wamekuwa wakitoa elimu isiyo sahihi kwa wananchi mbali mbali katika maeneo ya mjini na vijijini kwa Unguja na Pemba.Baadhi ya wawakilishi, masheha na viongozi wa ngazi za juu wa serikali wamekuwa wakitajwa kuwa ni miongoni mwa wapotoshaji wakubwa ambao mbali ya kukataa kutoa misimamo yao juu ya kura ya maoni itakayotarajiwa kupigwa Julai 31 mwezi huu lakini pia wamekuwa wakiwataka wananchi kupiga kura ya hapana kwa maslahi yao binafsi.Endelea kusoma habari hii

MWAZIRI WAJITOKEZA KUTETEA NAFASI ZAO

19 07 2010

TAKRIBAN Mawaziri wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamechukuwa fomu kutaka kuwania ubunge na uwakilishi kupitia CCM katika zoezi la uchukuwaji fomu lililoaza kufanyika jana Visiwani Zanzibar.Hadi sasa mawaziri wawili tu ndio waliokuwa hawajachukua fomu akiwemo Ramadhan Abdallah Shaaban ambaye ni waziri wan chi afisi ya rais katiba na utawala bora na waziri wa mawasiliano Brigedia Mstaafu Adam Mwakanjuki ambaye kwa zaidi ya miaka mitatu sasa yupo kitandao baada ya kupata ajali mbaya alipokuwa anaelekea Dodoma mwaka juzi.Mbali na mawaziri hao 14 kati ya 16 waliochukua fomu pia naibu mawaziri wote sita wa SMZ wamechukua fomu kuwania uwakilishi na ubunge wa majimboni huku wengine wakichukua fomu za kuwania nafasi za viti maalumu kutokana na kukosa majimbo ya kugombania.Endelea kusoma habari hii

SPIKA ATANGAZA NDIO KURA YA MAONI

18 07 2010

Pandu Ameir Kificho

WAKATI wajumbe wengi wa Baraza la Wawakilishi wakiogopa kutangaza misimamo yao juu ya kura ya maoni, Spika wa baraza hilo, Pandu Ameir Kificho ametangaza msimamo wake kuwa atapiga kura ya ndio ili kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.“Mimi mkiniuliza nifanyeje nitasema weka ndio julai 31 katika kura ya maoni” alisema Spika huku akicheka na kupigiwa makofi wa vigeregere vya pongezi.Msimamo wa Spika iunakuja siku moja baada ya Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume kurudia kauli yake ya kuwataka wananchi wa Unguja na Pemba kupiga kura ya ndio ifikapo Julai 31 mwaka huu ili kutoa nafasi ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo ndio inayoonekana njia sahihi ya kumaliza migogoro ya kisiasa.Endelea kusoma habari hii

KATAA MALARIA SIO KURA YA MAONI-KARUME

17 07 2010

RAIS wa Zanzibar Aman Abeid Karume amewasisitiza wananchi wananchi wa Zanzibar kupiga kura ya ndio itakayofanyika Julai 31 mwaka huu itakayoamua kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi wa mwaka huu.Alisema atawashangaa sana wazanzibari watakapiga kura ya hapana kwa vile maridhianao yalofikiwa yamesaidia kujenga amani na mshikamano kwa wananchi wake hivyo kuna haja ya kuendelezwa ili kudumisha amani ambayo vizazi vijavyo vitakuja kurithi mazuri na hali ya amani inayoendelezwa hivi sasa.“Nasema lugha ya hapana inastahili kusikika katika sula la kataa malaria, kataa madawa na kulevya, kataa bangi lakini huwezi kukataa amani na utulivu ndo maana nitawashangaa wote watakao kataa suala la Serikali ya umoja wa kitaifa alisema rais Karume ambae ni muwasisi wa suala hilo.Endelea kusoma habari hii

MAMIA WAWAPOKEA SHEIN NA BILAL

17 07 2010

MAMIA ya wananchi wa kisiwani Pemba jana wamejitokeza kwa wingi kuwapokea wagombea wawili walioteuliwa huko Dodoma katika uteuzi uliofanyika hivi karibuni Dk Ali Mohammed Shein na Dk Mohammed Gharib Bilal.Wateule hao walipokelewa kwa shangwe na kutambulishwa na rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na kuwataka wananchi wa mikoa miwili ya Pemba kuwaunga mkono viongozi hao ambapo Dk Shein amechaguliwa kuwa mgombea wa urais wa Zanzibar na Dk Bilal kuwa mgombea mwenza wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Shangwe hizo na na furaha kubwa zilianzia katika mapokezi yalioanzia Kiwanja cha Ndege cha Karume Pemba hadi kiwanja cha Gombani ya kale ambapo palifanyika hafla hiyo ilioambatana na burdani mbali mbali za nyimbo za asili ambazo zilikuwa zikito wasifu wa viongozi hao kuwa ni waadilifu na wenye uwezo mkubwa wa uongozi.Endelea kusoma habari hii

KAMATI YA MARIDHIANO KUANZA KAZI

15 07 2010

KAMATI ya kusimamia uundwaji wa Serikali ya pamoja Zanzibar imeanza kazi ya kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa hatua zilizopendekezwa kwenye maamuzi ya Baraza la Wawakilishi kuhusu uanzishwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Akizungumza na waandishi mwenyekiti wa kamati hiyo, Ali Mzee Ali alisema kamati hiyo itamshauri Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi juu ya masuala yote yanayohusiana na Azimio la Baraza la Wawakilishi kuishauri Serikali yao. Ushauri huo ni juu ya mambo ambayo utekelezaji wake utahitaji kutungwa kwa sheria na kutoa mapendekezo katika hatua za mwanzo za utungaji wa sheria husika na kuelimisha wananchi katika masuala ya kura ya maoni kuhusiana na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.Endelea kusoma habari hii

NITAGOMBEA TENA UWAKILISHI-NAHODHA

15 07 2010

WAZIRI Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Shamsi Vuai Nahodha amesema atachukua fomu ya kuwania tena Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi katika Jimbo la Mwanakwerekwe Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Kwa sasa Nahodha ni Mwakilishi wa Jimbo hilo. “Wazee wangu na ndugu viongozi nimekuja hapa kuwashukuru kwa kuniunga mkono wakati ule nilipokuwa kwenye mchakato, lakini sasa tumeshapata mgombea nami ninawaelezeni kuwa nitagombea tena Uwakilishi” AlisemaWaziri Kiongozi alitoa matamshi hayo wakati akizungumza na Uongozi wa Chama cha Mapinduzi Jmbo la Mwanakwerekwe jana ikiwa ni siku chache kupita baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu maalum wa tisa Mjini Dodoma ambapo Dk. Ali Mohammed Shein alichaguliwa kuwa mgombea wa CCM kuwania Urais wa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

BILA YA CCM ZANZIBAR ITAYUMBA

15 07 2010

WAZIRI Kiongozi Mstaafu na Mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal amesema bila ya CCM Zanzibar itayumba.Hayo ameyasema katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Demokrasia jana ulioandaliwa kwa ajili yake pamoja na mgombea wa urais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein.“Ndugu zangu bila ya kuwa na CCM Zanzibar itayumba kwa hivyo kila juhudi zifanye ili kupata ushindi chama chetu” alisema Dk Bilal na kushangiriwa kwa vifijo na hoi hoi na wanachama waliomiminika katika uwanja huo.Endelea kusoma habari hii

SHEIN/BILAL WASUBIRI MAPOKEZI MAKUBWA ZNZ

14 07 2010

MAPOKEZI makubwa yanawasubiri wagombea wawili Dk Ali Mohammed Shein na Dk Mohammed Gharib Bilal ambao wameuteuliwa hivi karibuni katika vikao vya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) huko Dodoma.Viongozi hao wanatarajiwa kuja Zanzibar kwa kutumia boti maalumu wakifuatana na mashabiki wa chama hicho ambapo wanatarajiwa kufika Zanzibar majira ya saa 5:00 mchana na kupokelewa na umati mkubwa wa wananchi wa Zanzibar katika bandari ya Malindi.Mgombea wa urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Muungano Dk Mohamed Gharib Bilali wanatarajiwa kuja kwa pamoja.Endelea kusoma habari hii

KARUME AKAMILISHA NAFASI ZAKE ZILIZOBAKI

14 07 2010

IKIWA imebaki siku moja tu kabla ya kuakhirishwa kwa kikao cha baraza la

Saleh Ramadhan Ferouz

wawakilishi wajumbe wawili kutoka chama cha mapinduzi wameteulwia na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume kuwa wajumbe wa baraza hilo.Wajumbe hao ni Naibu Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz na aliyewahi kuwa waziri wa wanawake na watoto awamu ya utawala wa Dk Salmin Amour Juma, na Makamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania, Asha Bakari Makame .Kuteuliwa kwa wajumbe hao wapya wa Baraza la Wawakilishi watakuwa wamemaliza nafasi 10 za Rais ambazo kwa mujibu wa sheria ana mamlaka ya kuteuliwa wajumbe kumi kuingia katika baraza hilo kwa muda ataoona unafaa.Endelea kusoma habari hii

HATUJARIDHISHWA NA UTEUZI WA BILAL- WANA CCM

13 07 2010

LICHA ya kuteuliwa Dk Mohammed Gharib Bilal kuchukua nafasi ya kuwa mgombea mwenza wa rais Jakaya Kikwete baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi hawakuridhishwa na uamuzi huo huku maskani zote za CCM zikiwa kimya.Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili wanachama hao wamesema matarajio ya wana CCM Zanzibar kwa Dk Bilal ni kuwa rais na sio makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Baadhi ya mashabiki hao wengi wakikwepa kutajwa majina yao wakidai wao ni viongozi wenye nyadhifa kubwa ndani ya chama na maoni yao huenda yakaathiri maandalizi ya chama katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu lakini kwa ufupi hawajaridhika kabisa na uteuzi huo.Endelea kusoma habari hii

UTEUZI WA SHEIN VURUGU TUPU

10 07 2010

Dk Ali Mohammed Shein akipunga mkono mara baada ya kutangazwa

WANACHAMA wa chama cha mapinduzi (CCM) ambao walikuwa na matumaini makubwa ya wagombea wao kuchaguliwa kuwakilisha Zanzibar katika kinyanganyiro cha urais wa visiwani kupitia chama hicho waonekana dhahiri kuvunjika moyo mara baada ya kutangazwa Dk Ali Mohammed Shein juzi usiku.Hali hiyo imejitokeza mjini Zanzibar katika sehemu mbali mbali Unguja na Pemba ikiwemo maeneo ya starehe ikiwemo vilabu vya pombe ambapo baadhi ya watu waliamua kuvunja chupa ukutani kuonesha hasira zao juu ya kutochaguliwa kwa Dk Mohammed Gharib Bilal katika nafasi hiyo.Endelea kusoma habari hii

KUZUKA KWA DK SALMIN KWAZUSHA MJADALA

8 07 2010

Dk Salmin Amour Juma (Komandoo)SIKU moja baada ya kuibuka kwa rais mstaafu wa Zanzibar Dk Salmin Amour Juma katika harakati za kumtafuta mrithi wa rais Amani Abeid Karume kumeibuka hisia tofauti za kibaguzi juu ya kujitokeza kwake.Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani ni miongoni mwa waliotoa maoni yao yanayokosoa kujitokeza kwa ghafla Dk Salmin ambaye kwa miaka kadhaa hajaonekana katika ulingo wa kisiasa.Kauli kubwa ambao imetolewa na baadhi ya wanachama wa CCM Zanzibar hasa wenye msimamo wa maridhiano wa maridhiano ni kwamba Dk Salmin Maarufu Komandoo ana lengo la kurejesha nyuma juhudi zinazoendelea za kuwaunganisha ambazo zimefikiwa na viongozi wakuu wa vyama vya CCM na CUF.Endelea kusoma habari hii

SALMIN ATUA DODOMA NA SIRI YA MOYONI

8 07 2010

Dk Salmin Amour Juma

WAKATI hatima ya kumpata mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM inaelekea ukingoni mwishoni mwa wiki hii, makundi ya ushabiki yanahaha kuwapigia debe wagombea watatu ambao ni Dk Ali Mohamed Shein, Dk Ghalib Bilal na Shamsi Vuai Nahodha.Jana rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Salmin Amour (Komando) aliwasili mjini Dodoma akiwa katika ndege moja na Waziri wa Kiongozi Vuai Nahodha ambaye ni mmoja wa wagombea.Kwa muda mrefu sasa Dk Salmin haudhurii mikutana na vikao vya chama kutokana na kusumbuliwa na macho, hali inayoonyesha kuwa hatua ya sasa ya kumpata mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM ina unyeti wake.Endelea kusoma habari hii

8 07 2010

HARAKATI za kumpata Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi zimechukua sura mpya baada katika siku mbili zilizopita baada ya kuibuka kwa vitendo vya kampeni chafu dhidi ya Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye ameleta msisimko mkubwa tokea alipotangaza nia ya kugombea na kuchukua fomu mwezi uliopita.Katika kile kinachoonekana kama kurejea kwa siasa za kuandika makaratasi ya kukashifiana na kutukanana na kuyamwaga mitaani ambazo zilikuwa zimepamba moto katika miaka ya tisini, juzi na jana makaratasi ya aina mbili yalikuwa yamemwagwa katika mitaa mbali mbali ya mji wa Zanzibar.Sehemu ya makaratasi hayo yalionekana kumwagwa katika soko kuu la mjini Zanzibar na pia katika maeneo ya Michenzani, karibu na maskani ya Kisonge ambapo wiki iliopita mgombea mwengine, Waziri Kiongozi mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilal, ndipo alipoondokea na kurejea baada ya kurejesha fomu zake Ofisi Ndogo ya CCM, Kisiwandui.Endelea kusoma habari hii

4 07 2010

MDAHALO ulioandaliwa kwa ajili ya wagombea wanaowania urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) umekosa msisimko baada ya kujitokeza wagombea wawili tu kati ya 11 ambapo lengo lililokusudiwa limeshindwa kutimia kwa kukosa hata nusu robo ya waalikwa.Mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Habari ya Vox Media Centre Ltd na Kituo cha televisheni cha Star Tv na Kampuni ya ASAM ya Zanzibar kurushwa moja kwa moja katika vituo vya radio Fm ukiwa na lengo la kuwapa fursa wagombea hao ya kujieleza na kutangaza malengo yao kwa wananchi ambao ni wapiga kura wao Waliojitokeza katika mdahalo huo ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Abeid Karume na Mfanyabiashara Maarufu, Mohammed Raza Daramshi ambao pamoja na mambo megine walikubali kujibu maswali mbali mbali walioulizwa na waandishi wa habari katika halfa iliyofanyiwa Ocean View Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

KAMATI MAALUMU YAANZA MCHUJO WA WAGOMBEA

3 07 2010

KIKAO Cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM –Zanzibar kilifanyika jana

Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar
kimependekeza majina matano ya wagombea wa urais wa Zanzibar kati ya 11 ambayo yatapelekwa katika kikao cha kamati kuu (CC) kwa kujadiliwa zaidi na kutoa majina yasiozidi matatu.Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa wajumbe wote 11 waliomba nafasi hiyo walijadiliwa bila ya wao kuwepo baada ya kutakiwa watoke njia wakati majadiliano na pia hawakutakiwa kujieleza chochote katika kikao hicho.Kikao hicho kilichoanza majina saa asubuhi na kumalizika saa 10:30 jioni kiliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Amani Karume ambacho kilikwepa kutoa alama za viwango vya wagombea hao 11 na badala yake jina moja moja lilijadiliwa kwa kuangalia masharti na sifa za nafasi hiyo kabla ya kupelekwa majina hao katika kikao cha CC kinachotazamiwa kufanyika jumanne ijayo jijini Dar es Salaam.Endelea kusoma habari hii

WAGOMBEA WOTE WAREJESHA FOMU ZANZIBAR

1 07 2010

Haroun Ali Suleiman

WANACHAMA zaidi wa CCM wanaomba kuteuliwa kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, jana waliendelea kurudisha fomu zao katika ofisi kuu ya CCM mjini hapa huku baadhi yao wakiwa wamehamia Tanzania bara kufanya kampeni ya kimya kimya ili kuteuliwa. Waliyojesha fomu zao baada ya kupata wadhamini ni pamoja na Haroun Ali Suleiman, Mohamed Raza Dharamshi, Omar Sheha, na Ali Juma Shamuhuna ambao kama ilivyokuwa katika uchukuwaji, walikwenda bila ya kuwa na shamrashamra mitaani. Ni Dr Mohamed Gharib Bilali Pekee ambaye wafuasi wake waliamuwa kufanya sherehe mitaani baada ya kurudisha fomu, huku waliamuni kuwa mwaka huu ni zamu ya Bilali kugombea urais wa Zanzibar baada ya kukosa kupitishwa mara mbili mwaka 2000 na 2005.Endelea kusoma habari hii

WATANO WAREJESHA FOMU CCM

28 06 2010

JUMLA ya wagombea watano wanaomba kuteuliwa kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia CCM jana

Shamsi Vuai Nahodha

walirejesha fomu zao baada ya kukamlisha kazi ya kutafuta wadhamini, Unguja na Pemba . Dk Ali Mohammed Shein, alikuwa ni miongoni mwa waliyorejesha fomu katika ofisi kuu ya chama hicho Kisiwandui mjini hapa na kufuatiwa na waombaji wengine. Katibu wa Idara ya Oganazesheni ya Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar, Bi Asha Abdallah Juma alifanya kazi ya kupokea fomu hizo na kuzikaguwa kama zimejazwa kabla fomu hizo kuwasilishwa katika mkutano wa kamati maalum ya wajumbe 80 wa NEC Zanzibar siku ya jumamosi kuwajadili na kutoa mapendekezo yao.Endelea kusoma habari hii

WAGOMBEA WENGINE WAREJESHA FOMU

27 06 2010

Hamad Bakari Mshindo

WAGOMBEA wanne wanaomba kuwania urais wa zanzibar kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) wanatarajiwa kurejesha fomu zao leo kwa nyakati tofauti.Kwa mujibu wa katibu wa kamati maalumu ya CCM-NEC Zanzibar Vuai Ali Vuai aliwataja wagombea hao ni pamoja na Hamad Bakari Mshindo atakayerejesha fomu yake saa 6:00 mchana, Ali Abeid Karume saa 9:00 mchana.Wengine ni Mohammed Aboud Mohammed atakayerejesha fomu yake saa 10:30 na Shamsi Vuai Nahodha ambaye amepangiwa kurejesha saa 11:00 jioni.Wagombea hao wote walitakiwa kupata wadhamini 250 kutoka mikoa mitatu ya Unguja na Pemba jambo ambalo wengi wao wameshalikamilisha kabla ya siku ya mwisho wa urejeshaji wa fomu hizo Julai mosi.Endelea kusoma habari hii

BILAL AWA WA MWANZO KUREJESHA FOMU

26 06 2010

Mgombea wa uteuzi wa nafasi ya Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk Mohamed Gharib Bilal amekuwa wa kwanza kurejesha fomu baada ya kukamilisha mchakato wa kupata wadhamini 250 kwa mikoa mitano ya Zanzibar.Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Mbweni Matrekta mjini Zanzibar jana, Dk Bilal alisema walijotokeza wanachama wengi wa CCM waliotaka kumdhamini hadi ikabidi wengine wawarejeshe kutokana na idadi kuwa imeshapitiliza na kwamba hilo linaonyesha imani kubwa ya Wazanzibari kwake.Mara aliporudisha fomu Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Dk Bilal alikwenda Maskani Mama ya Mwembe Kisonge ambako wapenzi na wafuasi wake walikusanyika ili angalau awasalimie.Endelea kusoma habari hii

HAROUN, RAZA NA MSHAMBA WACHUKUA FOMU

24 06 2010

Haroun Ali Suleiman

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Haroun Ali Suleiman amechukua fomu ya kutafuta ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kugombea uraisi wa Zanzibar huku akitumia Qur-an kutetea maridhiano ya wazanzibari.Maridhiano hayo yaliasisiwa na Mashujaa wawili wa Zanzibar Rais Amani Karume na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) maalim Seif Sharif Hamad mwishioni mwa mwaka jana.Haroun alianzia safari yake katika jengo la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali jana kwenda katika Ofisi za CCM Kisiwa Ndui kuchukua fomu hiyo ya kugombea nafasi hiyo.Baada ya kufika katika ofisi za CCM Kisiwa Ndui, Haroun na msafara wake alienda moja kwa moja katika Kaburi la Hayati Mzee Abeid Amani Karume na kufanya dua fupi.Baada ya hapo msafara ulienda moja kwa moja katika chumba maalumu cha kuchukulia fomu ambapo alilipa sh1 milioni na kukabidhiwa fomu hiyo.Endelea kusoma habari hii

WATATU WAJITOKEZA KUTAKA URAIS ZNZ

22 06 2010

WATU watatu wengine wamejitokeza kutangaza nia ya kutaka kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar kwa tiketi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Mohammed Raza

imeelezwa.Kujitokeza kwa watu hao kutafanya idadi ya wagombea wa urais Zanzibar kufikia 11 ambapo tayari makada saba wa chama hicho wameshachukua fomu zao juzi aktika afisi kuu ya chama cha mapinduzi Kisiwandui Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Kwa mujibu wa taarifa kutoka afisi kuu ya CCM Kisiwandui iliyosambazwa kwa waandishi wa habari Mjini hapa imewataja watu hao ni Mfanyabiashara Zanzibar, Mohammed Raza Dharamshi, ambaye atachukua fomu juni 24 majira ya saa 4 asubuhi.Wengine ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, ambaye amepangiwa kuchukua fomu yake saa 6 mchana na Mohammed Yussuf Mshamba ambaye atachukua fomu saa 8 kamili mchana.Endelea kusoma habari hii

WAGOMBEA WA URAIS WACHUKUA FOMU

21 06 2010

WAGOMBEA wanane kutoka chama cha mapinduzi CCM leo wamechukua fomu za kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar baada ya rais aliyepo

Dk Ali Shein akikabidhiwa fomu ya urais

madarakani Amani Abeid Karume kumaliza vipindi vyake viwili vya uongozi kwa mujibu wa katiba.Takriban wagombea wote wanane wanaotaka kuwania kinyanganyiro hicho wamezungumzia suala la kudumisha amani na kuendeleza maridhiano yaliofikiwa na Rais wa Zanzibar Amani Karume na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad. iwapo watapata ridhaa ya wananchi ya kuiongoza Zanzibar.Sherehe hizo licha ya kuwa hazikuwa na shamrashamra za kuwasindikiza wagombea hapo afisi kuu ya CCM Kisiwandui lakini baadhi ya wapambe walikuwa pembezoni mwa wagombea hao na kukaa nje ya jingo hilo wakiwasubiri wagombea wao na kuwasinidiza kwa magari wakati walipomaliza kukabidhiwa fomu hizo.Endelea kusoma habari hii

DK BILAL AAKHIRISHA KUTANGAZA NIA

20 06 2010

Dk Mohammed Gharib Bilal

KIU ya wananchi ya kutaka kusikiliza maoni ya mgombea wa urais wa Zanzibar , Waziri Kiongozi Mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilali imezimika ghafla baada ya kuakhirisha kikao chake na waandishi wa habari jana kufuatia kifo cha kaka yake Bilal Gharib Bilal. Kwa mujibu wa taarifa za kifo hicho kilichotokea majira ya usiku na wakati huo huo kusambazwa ujumbe wa simu kwa sms kwamba mkutano wa waandishi wa habari umevunjika kutokana na kifo hicho cha kaka yake. “Innah lillah wainnah ilayhi rajiun. Tunasikitika kukuarifu kuhusu kuakhirishwa kwa tukio la press conference ya leo (jana) Zanzibar Ocean View kutokana na kifo cha kaka yake Dk. Bilal Mohammed Bilal hadi hapo itakapotolewa taarifa nyengine. Tunasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza, tafadhali muarifu na mwenzio” unasomeka ujumbe huo ambao umetumwa nyakati za usiku.Endelea kusoma habari hii

WATU SITA KUCHUKUA FOMU ZA URAIS ZNZ

18 06 2010

JUMLA wa wagombea sita watatarajiwa kuchukua fomu juni 21 mwaka huu katika kuwania kinyanganyiro cha kuwania nafasi ya kugombea urais wa Zanzibar kupitisha Chama Cha Mapinduzi (CCM).Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya

Omar Sheha Mussa

Uenezi na Itikadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar iliyosambazwa kwa vyombo vya habari Mjini hapa imesema kwamba wagombea hao watachukuwa fomu siku ya jumatatu katika nyakati tofauti.Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha na Waziri Kiongozi Mstaafu, Dk Mohammed Gharib Bilal wanatazamiwa kuwa ni watu wa kwanza kuingia katika jengo la afisi kuu Kisiwandui siku ya jumatatu majira ya asubuhi kwa ajili ya kukabidhiwa fomu hizo.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN ATAKA URAIS ZANZIBAR

9 06 2010

Dk Ali Mohammed Shein

MAKAMU wa Rais, Dk Ali Mohammed Shein ametajwa kuwa ni mmoja wa wanachama wa CCM wanaotarajiwa kuchukua fomu za kuwania urais Zanzibar Juni 21 mwaka huu.Kwa muda mrefu, Dk Shein amekuwa akiombwa na rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume achukue fomu ya kuwania nafasi hiyo kubwa ya kisiasa visiwani humo. Rais Karume anamaliza vipindi vyake viwili vya urais mwaka huu baada ya kuingia Ikulu mwaka 1995.Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jijini Dar es salaam na Zanzibar, Dk Shein alikuwepo visiwani humo na kufanya mazungumzo maalumu na Rais Karume na habari zinasema kuwa kiongozi huyo wa Zanzibar alimuomba Dk Shein kukubali kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo moto.Hamu ya Rais Karume kumtaka Dk Shein kuwa mrithi wake inatokana na makamu huyo wa rais kuonekana ana msimamo wa wastani katika siasa za Zanzibar zisizo na chuki za Upemba na Unguja, huku akionekana kuwa hana makundi kulinganisha na wagombea wengine.Endelea kusoma kusoma habari hii

KAZI YA KUBANDIKA MAJINA WIKI IJAYO-ZEC

8 06 2010

Salim Ali Kassim

TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imesema kwamba itaanza kazi ya kubandika ukutani majina ya wapiga kura wote waliosajiliwa katika daftari la kudumu la apiga kura kwa ajili ya uhakiki.Mara baada ya kubandikwa kwa majina hayo katika vituo vya kupiga kura wananchi watakuwa na fursa na nafasi ya kupinga majina ya wapiga kura ambao wanahisi kwamba hawana sifa na wameingizwa katika daftari hilo la kudumu la wapiga kura.Zoezi hilo la majina ya wapiga kura yote yanatarajiwa kubandikwa Juni 14 wiki jayo ambapo zoezi hilo linachukua muda wa wiki mbili mfululizo.Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, Salum Ali Kassim alisema hayo wakati alipokutana na wahariri wa vyombo vya habari nchini hapo katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort nje kidogo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii zaidi

MABADILIKO YA KATIBA NI MUHIMU-JAHAZI ASILIA

8 06 2010

CHAMA cha Siasa cha Jahazi Asili, kimesema ili hali ya siasa visiwani Zanzibar iwe katika hali ya amani na utulivu ni vyema kufanywa kwa marekebesho ya Katiba ya Uchaguzi ili yende sambamba na mahitaji ya vyama vyote vya siasa.Chama hicho kilisema kuwa katiba inayotumika hivi sasa ni ile ya mwaka 1984, ambayo ilikuwa ni ya chama kimoja pekee na sio ya vyama hivi jambo ambalo halitoa fursa nzuri kwa vyama vyengine vya Siasa na kufuata misingi ya demokrasi ya mfumo wa vyama vingi.Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Amour Rajab Amour, wakati akizungumza na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Habari Maelezo uliopo Rahaleo Mjini Zanzibar.Alisema kuwa wakati umefika kwa taasisi husika inayoshughulikia mambo ya katiba ya Uchaguzi kufanya marekebisho ya haraka juu ya Katiba hiyo ili iwe ya kisasa na kutoa fursa nzuri ya kushiriki katika ulingo wa siasa kwa vyma vyote ifikapo Oktobar mwaka huu.Endelea kusoma habari hii

NINA MATUMAINI MAKUBWA KUSHINDA- MAALIM SEIF

8 06 2010

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad amesema mwaka huu historia itakuwa nyengine

Maalim Seif Sharif

katika uchaguzi mkuu ujao kwani chama chake kingelikuwa madarakani tokea 1995 kama chaguzi zilizopita zingelikuwa za huru na haki. Alisema kwa uwezo wa subra ulionyeshwa na chama chake mwaka huu historia itakuwa vyengine, kwani wapo watu waliosema Maalim asigombe aligombea kwa kuwa huko nyuma wakati akiwa kiongozi katika chama cha CCM alitoa ahadi yakuwatumika Wazanzibari hadi mwisho wa maisha yake Akizungumza katika sherehe fupi ya kurejesha fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia CUF alisema amechukua fomu hiyo kwa vile wazanzibari bado wana imani naye angepata ushahidi kama wamemchoka asingechukua fomu ya kugombea tena urais lakini pamoja na kuwa amewania nfasi hiyo mara tatu lakini wanachama wake wamemuomba kuwania tena.Endelea kusoma habari hii

MAALIM SEIF ACHUKUA FOMU YA URAIS ZNZ

8 06 2010

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake kugombea urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.Hii itakuwa ni mara ya nne kwa Maalim Seif kuwania nafasi hiyo ya urais wa Zanzibar ambapo amesema katika uchaguzi huu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ana matumaini makubwa ya kushinda na kamwe hawezi kuvunjika moyo kwa kuwa amekosa fursa ya kuongoza mara tatu katika chaguzi zilizopita.Akizungumza katika Tawi la CUF, Mtoni mara baada ya kuchukua fomu alisema anamatumaini ya kushinda katika uchaguzi huo wa mwaka 2010 kutokana na mazingira mazuri ya kisiasa yaliofikiwa Zanzibar. Hamad alisema Zanzibar imefungua ukurasa mpya baada ya kufikia maridhiano ya kisiasa ya kusahau tofauti zilizopita na kuweka mbele maslahi ya nchi , na hivyo katibu mkuu huyo amesema hakuna mwanachama aliezuiliwa kugombea nafasi za urais wa Zanzibar na ile ya Muungano ambapo Juni 5 ndio iliyokuwa siku ya mwisho ya kurejesha fomu za nafasi hizo na hakuna aliyejitokeza kupambana naye katika kinyanganyiro hicho.Endelea kusoma habari hii

CCM WAZIMA MAANDAMANO YA VIJANA

22 05 2010

BAADHI ya Vigogo wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar wanahaha kuzima

viongozi wa CCM wilaya ya mjini

maandamano yaliyokuwa yafanyike wiki hii kushinikiza Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, kujiuzulu kutokana na kashfa ya kuhusishwa na sakata la UVCCM.Habari zilizopatikana Mjini hapa zinaeleza kwamba Vijana wa CCM wa Mikoa mitano ya Unguja na Pemba wanakusudia kufanya maandamano ambayo yatajumuisha mapokezi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM, Hamad Masauni Yussuf.Hata hivyo, wakati Vijana hao wakiandaa suala hilo, habari zimevuja na kuwafikia Viongozi wa CCM Zanzibar ambao jana Viongozi wa Wilaya ya Mjini ambao wanadaiwa kuwa upande wa Ferouz walikuwa na vikao kadhaa kujaribu kuzima mpango huo.“Jana usiku walikuwa na vikao hawa mabwana…pale Wilayani kuna watu wake Ferouz ndio wanaopinga maandamano yetu ambayo vijana wangebeba mabango ya kumtaka ajiuzulu” Alisema Kiongozi mmoja wa UVCCM ambaye hakutaja kutaja jina lake.Endelea kusoma habari hii

MASAUNI NI SHUJAA -VIJANA ZNZ

20 05 2010

MAMBO yanazidi kutokota ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) kufuatia kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Umoja huo Hamad Masauni Yussuf, Vijana Visiwani Zanzibar wamewasha moto, wanaandaa mapokezi makubwa kwa ajili ya Mwenyekiti wao wa zamani.Wenyeviti wa Umoja huo katika Majimbo mbalimbali ya hapa wamo katika maandalizi ya mwisho ya mapokezi hayo ambayo yatawahusisha vijana wenzao kutoka Kisiwani Pemba ambao wanatarajiwa kuwasili leo Mjini Unguja.Kwa mujibu wa waandaaji wa maandamano hayo wamesema yatawashirikisha vijana wa mikoa mitano miwili Kisiwani Pemba na mitatu ya Unguja.Chanzo chetu habari kinaeleza kuwa tayari fulana za “Masauni shujaa” zinatayarishwa kwa ajili ya kuvaliwa siku ya mapokezi hayo ambayo yataanzia katika bandari ya Malindi Unguja.Chanzo hicho ambacho akitaki kutajwa hadharani kimesema kuwa UVCCM Zanzibar umeamua kuandaa mapokezi hayo ili kuungana na Mwenyekiti wao wa zamani kumfariji na kuonesha mshikamano wao kuwa bado wanampenda na kumuamini na kilichotokea na bahati mbaya ambayo inaweza kumkuta mtu yeyote katika ulingo wa kisiasa.Endelea kusoma habari hii.

WAZANZIBARI MUAMKE-RAIS KARUME

19 05 2010

Rais Karume akikagua uwanja wa Amani

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume amewataka wazanzibari kuamka na kufuatilia mambo yanavyobadilika duniani juu ya mabadiliko ya kisiasa ambayo yanahimiza umoja na mshikamano.Alisema hakuna hata mtu mmoja aliyetarajia kwamba nchi kama uongereza kungetokea mabadiliko ya kisiasa kaam yanayotokea katika nchi za bara la Afrika kwa kuunda serikali za umoja baada ya vyama vilivyoshinda katika uchaguzi kuungana na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.Rais Karume alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waalikwa katika hafla ya makabidhiano ya uwanja wa mpira wa Amani uliokuwa ukifanyiwa matengenezo na serikali ya watu wa China jana Mjini Unguja, Katika hafla hiyo ilihudhuriwa na ujumbe wa chama cha wananchi CUF ulioongozwa na Katibu Mkuu wake Maaalim Seif Sharif Hamad na msaidizi wake Ismail Jussa, Mkurugenzi wa mawasiliano ya umma, Salim Bimani na wabunge na wawakilishi wa chama hicho.Endelea kusoma habari hii

TUTAREJESHA KADI ZA CCM- VIJANA

19 05 2010

Hamad Masauni

SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Hamad Masauni Yussuf kuachia ngazi wadhifa huo, baadhi ya vijana wa jimbo la Kikwajuni warejesha kadi za CCM kutokana na kutoridhishwa na suala hilo.Viongozi wa CCM Jimbo la Kikwajuni jana walikataa kusema lolote kwa madai kuwa wao hawajui kinachoendelea zaidi ya kupata taarifa hizo kwenye magazeti na walipotakiwa kuelezea uamuzi wa Vijana kurejesha kadi walisema “hatujawaona, lakini kwa vijana hilo linawezekana” Alisema Kiongozi Mmoja wa Jimbo hilo ambayer hakutaka kutajwa hata cheo chake.Baadhi ya viongozi hao walionekana wakisoma gazeti la Mwananchi na kusema kwamba ndio kwanza wamepata gazeti hivyo hawezi kutoa ufafanuzi wowote kuhusiana na suala hilo lakini wanachokijua huo ni uamuzi kutoka ngazi ya juu ya vijana.“Sasa hivi ndio nilikuwa na gazeti hapa lakini sijawahi hata kulisoma nimenyanganywa kuna vijana wanalisoma huko kwa hivyo hatujajua chochote hadi sasa lakini hata kama ndio amejiuzulu huo uamuzi ni wa vijana sisi kama chama hatujaletewa taarifa zozote zinazomhusu yeye ni mambo yao vijana” alisema Katibu wa jimbo hilo la kikwajuni.Endelea kusoma habari hii

WANASIASA WANAWAPOTOSHA WANANCHI-SHIVJI

17 05 2010

WAKATI Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) tayari imetangaza tarehe ya

Pro.Issa Shivji

kupiga kura ya maoni kuamuwa kama serikali ijayo baada ya uchaguzi mkuu iwe ya umoja wa kitaifa, msomi maarufu nchini Prof Issa Shivji amesema baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwa potosha wananchi. Akizungumza katika kongamano la kujadili mwelekeo wa Zanzibar katika kuunda serikali ya umoja wa kitaifa lililoandaliwa na chuo kikuu cha taifa cha Zanzibar, Professa Shivji alisema ni lazima juhudi zifanyike kuwaelimisha wananchi kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa, faida zake, na utofauti na serikali ya mseto. Alisema kwamba japokuwa serikali ya Zanzibar imo katika mandalizi ya kufanya kura ya maoni, wananchi wengi bado hawajaelimishwa vya kutosha kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa huku wanasiasa, wakitumia mwanya huo kupotosha mfumo huo wa serikali. Prof Shivji, mwanataaluma ya sheria na mhadiri mstaafu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam anaendelea na msimamo wake wa kupinga kura ya maoni Zanzibar kwa kusema kuwa serikali ya umoja wa kitaifa ingeweza kuundwa bila ya kura kwa sababu kwa hivi sasa wazanzibari wengi wanaunga mkono umoja na hawahitaji kuulizwa kama wanataka kuungana.Endelea kusoma habari hii

KARUME NA SEIF MEZA MOJA SIKU YA UZINDUZI

16 05 2010

Rais Karume alihudhuria ktka harusi ya bint wa Maalim Seif

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad wanatarajiwa kukaa meza moja siku ya ufunguzi wa utoaji wa elimu juu ya kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika Julai 31 mwaka huu Visiwani Zanzibar.Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Khatib Mwinyichande alisema hayo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari juzi ofisini kwake Maisara Mjini Unguja waliotaka ufafanuzi juu ya utoaji elimu utakaofanywa na tume yake.Alisema ingawa tume yake haijapanga ni lini uzinduzi huo utafanyika lakini alisema wanatazamia kuwaalikwa viongozi wakuu wa kisiasa ambao ni waanzilishi wa maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa Novemba 5 ili kuja kutoa maelezo yao kama ndio viongozi wakuu wa suala hilo.“Tunategemea kumualika katiak ufunguzi wa siku ya kutoa elimu ya kura ya maoni Mheshimiwa Rais wa Zanzibar aje kufungua na azungumze na pia Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif naye azungumze anachoona kinafaa kwa sababu wao ndio waanzilishi wa suala hili na watachosema watu watasikiliza” alisema Mwneyekiti huyo.Endelea kusoma habari hii.

KURA YA MAONI ZNZ NI JULAI 31 MWAKA HUU

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza rasmi Julai 31 mwaka huu kuwa ndio siku ya upigaji kura ya maoni ambayo yatategemea kuuundwa au kutokuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Visiwani Zanzibar.Akitangaza tarehe hiyo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Khatib Mwinyichande katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi alisema Julai 31 wazanzibari wanaamua kupitia kura za maoni.“Nikiwa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar nachukua nafasi hii kutangaza rasmi kupitia vyombo vya habari kuwa tarehe 31 julai mwaka 2010 ni siku ya kupiga kura ya maoni” alisema Mwenyekiti huyo.Katika kura hiyo wapiga kura watatakiwa kuweka alama katika chumba kidogo katika karatasi ya kupigia kura chenye neno NDIO au HAPANA kufuatia swali ambalo litaulizwa katika karatasi za kupigia kura hizo.Mwenyekiti huyo alisema katika karatasi hizo za kura kutakuwa na swali moja tu ambalo mwananchi atatakiwa kulijibu iwapo anataka au hataki na swali lenyewe litakuwa kama ifuatavyo “Je unakubali kuwepo kwa muundo mpya wa serikali mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2010?”. Endelea kusoma habari hii

ZEC YAKUBALI KUPUNGUZA VIWANGO VYA UDHAMINI

14 05 2010

HATIMAE Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesikiliza malalamiko ya vyama vya siasa kwa kupunguza viwango vya wadhamini wa wagombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu.Kwa mujibu wa ZEC nafasi ya urais awali ilitangazwa kudhaminiwa kwa shilingi millioni 3,000,000 lakini sasa itadhaminiwa kwa shilingi millioni 2 nafasi ya uwakilishi ilikuwa idhaminiwe kwa shilingi 300,000 lakini sasa itadhaminiwa kwa shilingi 200,000 na nafasi ya udiwani umepunguzwa hadi shilingi 30,000 kutoka shilingi 50,000.Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Khatib Mwinyichande alisema kutokana na kuzingatia viwango hivyo na kupokea malalamiko ya wadau wa uchaguzi ambao ni viongozi wa kisiasa wameona ipo haja ya kunguza viwango hivyo ili kwenda sambamba na hali halisi ya maisha.“Tumesikiliza kilio chao si unajua wanasiasa ni wadau wetu katika uchaguzi hivyo lazima tuwasikize na ndio tukaamua kuwapunguzia ili kwenda na hali ya maisha” alisema Mwenyekiti huyo akizungumza nje ya ofisi yake iliyopo Maisara Mjini Unguja.Alisema haki ya kushiriki katika uchaguzi ni ya kila mmoja hivyo ni vizuri wanaotaka kuwania nafasi hizo wapewe nafasi ya kuwania kutokana na uwezo na uzoefu wao wa uongozi lakini wasiwe na kikwazo cha kushiriki kutokana na kukosekana fedha.Endelea kusoma habari hii

EU YAIUNGA MKONO SMZ

12 05 2010

Ujumbe wa EU ukisalimiana na Rais Karume Ikulu

UMOJA wa nchi za Ulaya (EU) umeahidi kuendeleza ushirikiako wake na Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta za kimaendeleo, kiuchumi, kisiasa na kijamii.Ujumbe wa Babalozi wa EU hapa nchini wakiongozwa na Balozi wa Uingereza Bwana Tim Clarke walieleza hayo wakati walipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume, Ikulu mjini Zanzibar.Katika mazungumzo hayo Balozi Clarke alieleza kuwa EU imevutiwa na maendeleo yaliofikiwa Zanzibar na kuahidi kuyaunga mkono kwa hali na mali.Alieleza kuwa EU inatambua juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarishe sekta za maendeleo na ndio maana imevutiwa zaidi na kuahidi kuendelea kuunga mkono.Endelea kusoma habari hii

MABALOZI WAAHIDI KUISAIDIA ZANZIBAR

12 05 2010

MABALOZI wanane wa nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) wameahidi kufanya kila wawezalo ili kuhakikisha wanaisaidia Zanzibar katika kufikia demokrasia ya kweli katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu.Mabalozi hao wametoa ahadi hiyo baada ya kupokea maelezo kadhaa yaliotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad katika mazungumzo yao yaliofanyika Hoteli ya Serena Mkoa wa Mjini Magharibi jana asubuhi.Mkuu wa Jumuiya hiyo, Tim Clack amesema jumuiya ya Ulaya itatoa kila ushirikiano na watatumia uwezo wao kuwasaidia wazanzibari kutekeleza azma vyema kupitia maridhiano yaliofanyika kati ya Rais wa Zanzibar, Amani Karume na katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif inatekelezwa ipasavyo.Amesema wasingependa kuonekana wao ndio wanaokwamisha maridhiano hayo ambayo lengo lake ni kuiendeleza Zanzibar katika kufikia maridhiano ya kweli na yenye amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu ufanyike katika mazingira ya amani na utulivu.Tim Clack amesema msaada wa EU unahitajika kwa sasa katika kufikia demokrasia ya kweli hasa kwa kuzingatia dunia ya leo inahimiza sana demokrasia na misingi ya kuheshimu haki za binaadamu na utawala bora.Endelea kusoma habari hii.

MAMIA WAACHWA KUANDIKISHWA

12 05 2010

CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimesema pamoja na kumalizika kwa daftari la kudumu la wapiga kura bado limeacha kasoro zikiwemo wananchi kadhaa kuachwa kuandikishwa katika dafateri hilo licha ya kutimiza masharti yote yanayotakiwa.Zaidi ya wananchi wapatao 16,000 wenye haki na sifa za kuandikishwa hawakuandikishwa katiak daftari hilo kutoka Unguja na Pemba hadi jana.Mkurugenzi wa uchaguzi wa CUF, Juma Said Sanani alisema inagwa Tume ya Uchaguzi imesema imeshamaliza kazi ya uandikishaji na kinachofuata sasa ni matayarisho ya uchaguzi mku unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwaka huu lakini kuna kasoro nyingi ambazo zinahitaji kurekebishwa.Sanani aliyasema hayo akiwa ofisini kwake Vuga Mjini Unguja amesema pamoja na Tume kutangaza kukamilisha zoezi hilo bado kuna wananchi wengi wamekosa kuandikishwa kutokana na sababu za kutokuwa na vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi na wengine kukosa vyeti vya kuzaliwa pamoja na barua za masheha.Mkurugenzi Sanani alisema katika Majimbo 42 ya Unguja na Pemba watu ambao wamekosa kuandikishwa wengine wana sifa zote, lakini masheha wamewanyika haki zao za kuwa wapiga kura kwa kushirikiana naTume ya Uchauzi pamoja na Ofisi ya vitambulisho.Endelea kusoma habari hii

UANDIKISHAJI WAFUNGWA RASMI ZANZIBAR

11 05 2010

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema haitaweza kuwaandikisha wapiga kura ambao wamekosa kutokana na njia mbali mbali ikiwemo ugonjwa au kuwepo nje ya nchi kutokana na muda wa kazi hiyo kumalizika.Mwenyekiti wa Tume hiyo, Khatib Mwinyichande ameyasema hayo katika taarifa yake yenye kurasa nne iliyosambazwa kwa vyombo vya habari ambapo alisema ZEC inaelewa wazi kuwa katika kuendesha zoezi la uandikishaji wa wapiga kura na ubadilishaji wa shahada za kupigia kura kuna watu ambao kwa njia moja au nyengine wameshindwa kujiandikisha.Akizitaja sababu hizo ni pamoja na kusafiri, kuwa masomoni, kuuguliwa au kuugua ambapo hawakuweza kushiriki katika awamu zote mbili za uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.“Tunasikitika kuwa kwa kipindi hiki hatutaweza tena kuwashughulikia watu hao kwa kuwa zoezi hilo tayari limefungwa rasmi na mwelekeo wa sasa wa Tume ni wa maandalizi ya uchaguzi wenyewe ambao tayari ratiba yake tumeitangaza rasmi kwa vyama vya siasa na vyombo vya habari” ilisema taarifa hiyo ya Mwenyekiti.Endelea kusoma habari hii

KARUME AWAKEMEA WAPINGAJI WA UMOJA

2 05 2010

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Amani Abeid

Rais wa Zanzibar, Amani Karume

Karume amewataka viongozi wa Matawi ya CCM katika Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania kuitumia vyema elimu yao kwa kusimamia umoja, mshikamano amani na utulivu.Rais Karume pia amewabeza wanasiasa wenye kuendesha harakati za kisiasa zenye kutaka kuchafua hali ya utulivu ambao hupita mitaani na kuwataka wananchi kusitie kura ya ndio wakati ya kura ya maoni itakapoanza ambayo lengo lake ni kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar.Kauli hiyo aumeitoa juzi jioni katika ufunguzi wa Kongamano la viongozi wa Matawi ya CCM katika vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania, ufunguzi uliofanyika katika hoteli ya Bwawani mjini Unguja.Katika hotuma yake kwa wanavyuo hao, Rais Karume alisema kuwa CCM imeweza kujenga misingi madhubuti ya kusimamia umoja, amani,mshikamano na utulivu kwa lengo la kupata mafanikio zaidi hali ambayo vijana wanapaswa kuitekeleza kwa nguvu zote.Endelea kusoma habari hii

VIWANGO VYA ZEC VYALALAMIKIWA NA WADAU

29 04 2010

VIONGOZI wa vyama vya siasa wameilalamikia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kuweka viwango vikubwa vya wagombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu pamoja na kasoro zilizojitokeza katika zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura.Malalamiko hayo yametolewa jana katika mkutano wa pamoja kati ya viongozi wa vyama vya saisa na maafisa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar uliofadhiliwa na shirika la maendeleo ya UNDP uliofanyika Zanzibar Beach Resort. Hivi karibuni Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza viwango vipya vya nafasi za wagombea wa uchaguzi mkuu wa 2010 unaotarajiwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu.Kwa mujibu wa ZEC nafasi ya urais itadhaminiwa kwa shilingi millioni 3,000,000 badala ya shilingi millioni 1,000,000, nafasi ya uwakilishi utadhaminiwa kwa shilingi 300,000 badala ya shilingi 50,000 na nafasi ya udiwani itadhaminiwa kwa shilingi 50,000 badala ya bei za zamani shilingi 15,000 viwango ambavyo vimelelemikiwa na wadau wa uchaguzi.Akichangia katika mkutano huo, Naibu Katibu wa TADEA Zanzibar, Juma Ali Khatib amesema viwango vilivyowekwa na ZEC ni vikubwa na vinapaswa kupunguzwa kwa kuwa vyama vyengine vya siasa uwezo wake ni mdogo pamoja na kuwa vimesajiliwa kisheria lakini havina uwezo wa kumudu gharama hizo.Endelea kusoma habari hii.

WAZEE SASA WAITEGA SERIKALI YA KIKWETE

27 04 2010

WAKATI leo watanzania wanaadhimisha miaka 46 ya muungano wa

Mzee Hassan Nassor Moyo

Tanganyika na Zanzibar baadhi ya waasisi wa muungano wameibuka na kutaka mapendekezo ya tume ya Jaji Francis Nyalali yatekelezwe kwa vitendo. Moja ya mapendekezo ya wananachi katika tume ya Jaji Nyalali iliyoklusanya maoni ya wananchi wa Tanzania nzima ni kuundwa kwa mfumo wa serikali tatu ambao unaonekana utaimarisha muungano na kila serikali kuainisha majukumu yake. Maoni hayo ya watanzania yalikusanywa mwaka 1990-91 lakini mapendekezo ya tume hiyo yalitupiliwa mbali na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo hadi leo hayajafanyiwa kazi. Wanaotaka mfumo wa serikali tatu wanasema utaondosha malalamiko ya kila upande na pia yataimarisha muungano zaidi kuliko ilivyo sasa. Waziri wa kwanza wa sheria wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Hassan Nassoro Moyo aliwaambia waandishi wa habari kwamba sio dhambi kuwepo mfumo wa serikali tatu kwani maoni hayo hata katika tume zilizokusanya maoni ya watanzania yalibainisha kutakiwa jambo hilo.Endelea kusoma habari hii

MUUNGANO HUU NI BATILI-WAZANZIBARI

23 04 2010

Rashid Hemed (Joe)

JUMLA ya Wazanzibari 12 waliowahi kumshitaki mwanasheria mkuu wakidai kutaka hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar juzi wamekwenda ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) ziliyopo Zanzibar na kuwasilisha malalamiko yao hayo.Akizungumza na waandishi wa habari katiak ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) Mjini Unguja, Naibu Katibu wa kikundi hicho kiitwacho Zanzibar People of Representatives, Rashid Yusuf alisema suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar limegubikwa na utata mtupu na linafaa kushughulikiwa ipasavyo na sio kuandaa kamati ambazo hazina nguvu kisheria.Alisema hivi karibuni wamekwenda katika ofisi za UN na kuwasilisha malalamiko yao juu ya suala hilo na kutaka hatua za dharaura kuchukuliwa kwani Muungano uliopo haupo kisheria hasa kwa kuwa Mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar kusema mahakamani kwamba hana hati za makubaliano ya muungano huo.Naibu huyo alisema awali walikuwa wajumbe 10 na ambao wawawakilishi wazanzibari zaidi ya millioni moja katika kudai haki yao ya kutaka muungano uwepo kisheria alisema kikundi chake kilikwend amahakamani kumshitajki mwanasheria mkuu atoe hati ya muungano lakini bahati mbaya amesema hana hati hiyo.Endelea kusoma habari hii

UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR NI OCTOBA

23 04 2010

UCHAGUZI mkuu wa Zanzibar unatarajiwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu wa 2010 na matokeo ya uchaguzi huo yatatangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuanzia Octoba 31 hadi Novemba 2, 2010.Hayo yamemelezwa katika barua yake yenye kurasa nne iliyosambazwa kwa vyombo vya habari Mjini Zanzibar na kutiwa saini na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Khatib Mwinyichande.Katika barua hiyo imesema mchakato wa uandikishaji wa wapiga kura wapya ambao walihusisha uendeshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na ubadilishaji wa shahada za zamani za kupigia kura ambao umeanza tangu uchaguzi mdogo wa Magogoni mwezi Machi 2009 unatarajiwa kukamilika Mei 09, 2010 mwaka huu.Barua hiyo imesema kwamba kukamilika kwa zoezi hilo, kumetoa fursa kwa tume ya uchaguzi kupanga tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu na masuala mbali mbali ya yanayohusiana na kufanyika kwa uchaguzi huo kwa mujibu wa katiba na sheria za uchaguzi ya mwaka 1984.Sheira ya 1984, kifungu cha 45(1)(a) kinaeleza kuwa “endapo uchaguzi mkuu umepangwa kufanyika, siku ya uteuzi kwa jimbo lolote halitokuwa chini ya siku tano au zaidi ya siku ishirikini na tano baada ya kuvunjwa kwa baraza la wawakilishi” mwisho wa kunukuu.Endelea kusoma habari hii

MTOTO WA KOMANDOO ATAKA UWAKILISHI

18 04 2010

KWA mara nyengine tena wananchi wa Zanzibar wanaingia katika heka heka

Amin Salmin Amour Juma

za uchaguzi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2005 ambao ulitawaliwa na mizengwe kadhaa huku Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na vikosi vya serikali ya Zanzibar vikibebeshwa lawama ya kuwa ndio chanzo cha kuharibika kwa uchaguzi.Wagombea kadhaa wameonesha nia ya kutaka kuwania nafasi za udiwani uwakilishi na ubunge ambazo chama cha wananchi CUF wameshamaliza mchakato wa uchukuaji wa fomu hizo na kilichobali ni uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi za urais wa Zanzibar na muungano.Wagombea wanaotaka kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi wa mwaka huu ni wengi kutokana na kundi kubwa la vijana kujiingiza katika kinyanganyiro hicho ambacho kwa mara ya kwanza baadhi ya waoto wa viongozi wastaafu kujitokeza katika mchakato huo.Kilichovuta hisia za wau wengi ni kujitokeza kwa mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk Salim Amour Juma ambaye ameeleza nia yake ya kutaka kuwania kiti cha Magogoni katika uchaguzi mkuu wa 2010.Hii ni mara ya pili kwa Amini kutangaza nia yake hiyo ambapo mara ya kwanza aliingia katika mchakato huo wa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo hilo marehemu Daud Hassan Daud aliyefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.Endelea kusoma habari hii.

MUGHEIRY AMWAGA MILLIONI MBILI JIMBONI

12 04 2010

MWAKILISHI wa kuteuliwa na Rais wa Zanzibar, Sultani Mohammed Mugheiry ametoa shilingi millioni mbili kama mchango wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Mji Mkongwe.Mugheiry ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema kutoa fedha hizo ni kuitikia wito wa mwenyekiti wa chama chake Jakaya Mrisho Kikwete ili kukisaidia chama hicho katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.Akiwakabidhi fedha hizo viongozi wa tawi la Shangani liliopo Mji Mkongwe Mugheiry alisema kitendo cha Rais Kikwete kutoa fedha ni changamoto kwa wanachama na wapenzi wa CCM katika kuelekea uchaguzi mkuu.Akizungumza na wanachama pamoja na wajumbe wa halmashauri ya jimbo hilo alisema jimbo la Mji Mkongwe linapaswa kurudi mikononi mwa CCM katika uchaguzi ujao kwa kuwa wana CCM wa jimbo hilo wapo makini katika kukihudumia chama chao.”Chama cha Mapinduzi ni chama shupavu sana kwa hivyo mimi sioni sababu ya chama cha mapinduzi kushindwa kulichukua jimbo hili katika uchaguzi ujao nadhani tujipangeni vizuri ili hadhi ya chama chetu irudi mikononi mwetu na jimbo hili lisichukuliwe na wapinzani” alisema mwakilishi huyo.Endelea kusoma habari hii

MASHEHA WAILALAMIKIA ZEC

12 04 2010

TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imelalamikiwa na baadhi ya masheha kwa kuwapatia vitambulisho vya mzanzibari mkaazi (ZAN-ID) watu bila kupatiwa fomu kutoka kwa masheha.Malalamiko hayo yamejitokeza kwenye baadhi ya vituo vya uandikishaji Zanzibar baada ya badhi ya vijana kunyanganywa vitambulisho vyao na masheha kwa madai ya kuwa wamevipata kwa njia ya udanganyifu. “Walikuwa mwanzo wanakuja moja kwa moja kwa sheha na sasa hawapitii tena kwa sheha wanakwenda moja kwa moja tume ndipo tukiwagundua kuwa watu wanapata vitambulisho ambavyo wanapewa na Tume kwa hivyo sisi hatuwezi kuwaachia lazima tuwanyanganye”alisema sheha wa shehia ya Kwamtipura, Machano Salum Khamis.Baadhi ya wananchi kadhaa walinyanganywa vipande vyao vya uraiya bila sababu za msingi na kuvichukua vitambulisho hivyo kwa madai ya kuwa hawatambui katika shehia yake na wamevipata kwa kutumia njia ya udanganyifu.Zoezi la uandikishaji linaloendelea Zanzibar limekumbwa na malalmiko kadhaa ikiwemo kutakiwa vyeti vya ndoa, vyeti vya kuzaliwa na pamoja na baadhi ya wananchi kukataliwa kuandikishwa kwa madai ya kutokujua taratibu za ukaazi katika shehia zao.“Uelewa wa watu ni mdogo baadhi ya vitambulisho vyao kuwa na majina ya vitongoji visivyo rasmi pia kumechangia kukataliwa na kuwakosesha kuandikishwa katika buku la wapiga kura” amesema mkaazi mmoja ambaye alikosa kuandikishwa.Endelea kusoma habari hii

MILANGO YA MARIDHIANO YAFUNGULIWA ZNZ

MILANGO ya Maridhiano inaendelea kufunguka visiwani Zanzibar, ambapo katika tukio la jana, kwa mara ya kwanza Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad alishiriki kwenye dua maalum ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.Dua hiyo ilifanyika katika Ofisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kisiwandui, mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano, mabalozi, viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali.Hii ni mara ya kwanza kwa kipindi cha zaidi ya miaka ishirini, kwa Maalim Seif kuingia kwenye jengo la Ofisi ya CCM Kisiwandui, tangu alipofukuzwa uanachama wa CCM hapo mwaka 1988.Akizungumza na waandishi wa habari, muda mfupi baada ya dua hiyo, Katibu Mkuu huo wa CUF, alisema yeye na Chama chake wanautambua mchango mkubwa uliotolewa na mwasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 katika kuijenga Zanzibar imara na yenye umoja.Endelea kusoma habari hii

KIKWETE AKATA MIZIZI WA FITNA

6 04 2010

RAIS Jakaya Kikwete jana amekata mzizi wa fitna na kutoa msimamo wa chama cha mapinduzi juu ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar.Kauli ya Rais Kikwete imekuja siku chache baada ya baadhi ya wana CCM kupita matawini na kueneza uvumi kwamba msimamo wa chama cha mapinduzi juu ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa haujatolewa rasmi.Mbali ya wana CCM kupita matawini pia wajumbe wa baraza la wawakilishi wa upande wa CCM katika kikao kilichomalizika wiki hii waligomea kuuchangia mswaada wa kura ya maoni juu ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa wakidai kwamba hawajasikia msimamo wa chama juu ya suala hilo.Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya kifo cha marehemu Mzee Amani Abeid Karume yaliofanyika viwanja vya Maisara Mjini Unguja Rais Kikwete alisema msimamo wa chama ni kuunga mkono uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa.Hata hivyo aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi katika kupira kura ya maoni juu ya uundwaji wa serikali hiyo kwani faida zake ni nyingi kuliko hasara.Endelea kusoma habari hii.

ANAYEKATAA UMOJA SIO CCM HUYO-KARUME

2 04 2010

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume amesema mwanachama yeyote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayekataa umoja na mshikamano hapaswi kuwa katika chama hicho kwa kuwa sera na ilani ya chama hicho ni kudumisha amani nchini.Kauli ya Rais Karume imekuja siku chache baada ya kupitishwa mswaada wa kura ya maoni juu ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa katika kikao cha baraza la wawakilishi visiwani Zanzibar.Hayo ameyasema katika uzinduzi wa matembezi ya kumuenzi Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, miaka 38 baada ya kifo chake, yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) na kuwashirikisha vijana 150 wa Mikoa 26 ya Tanzania yaliofanyika Makunduchi Mkoa wa Kaskazini Unguja.Matembezi hayo ambayo yataendelea kutafanyika kwa mikoa mitatu ya Unguja kwa siku tano mfululizo yana lengo la kuwahamasisha vijana kufuata nyazo za Mzee Karume kwa vitendo.“Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) anayekataa Umoja na mshikamano, huyo atakuwa siye mwanachama halisi kwa sababu Chama cha mapinduzi katika sera na ilani zake zote zinaeleza kudumisha mshikamano na kuweka amani na utulivu nchini kwetu kwa hivyo kila mmoja lazima atekeleze umoja na mshikamano” alisema Rais Karume.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR NI YA WAZANZIBARI WOTE-KARUME

1 04 2010

ZANZIBAR haiwezi kujengwa bila ya kuwepo umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi na ushiriki wa viongozi wa Chama Cha CUF katika shughuli za miradi ya maendeleo ni mafanikio ya umoja huo.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume aliyasema hayo katika ufunguzi wa skuli mpya ya Mjini Kiuyu Shehia ya Kiuyu Minungwini katika Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo viongozi mbalimbali wa chama na serikali walihudhuria wakiwemo viongozi wa chama cha CUF.Katika hotuba yake aliyoitoa katika sherehe hiyo, Rais Karume alisema kuwa yeye mwenye binafsi amefarajika kuona ushiriki wa viongozi wa Chama Cha CUF katika sherehe hizo na kusisitiza kuwa huo ndio umoja na mshikamano ambao unajenga amani, utulivu na upendo na kuahidi kuusimamia.Alisema kuwa Wazanzibari wote ni wamoja hivyo kuna kila sababu ya kuishi kwa upendo na maelewano hatua ambayo itaipeleka mbali Zanzbar katika kuimarisha uchumi wake na miradi yake ya maendeleo sanjari na uimarishaji wa amani na utulivu.“Sisi Wazanzibari wote ni wamoja na wala wasitokee watu wakatudanganya tukajigawa na ili uwe Mzanzibari ni lazima utokee Unguja ama Pemba na hata ingekuwa si wamoja kwani ingekuwa vibaya kuungana, mbona leo Ulaya wameungana na kuunda (EU) ambapo ni nchi nyingi na watu wake ni wengi na wanaongea lugha tofauti”,alisisitiza Rais Karume.Endelea kusoma habari hii

RAIS KARUME AZUNGUMZA TENA NA MAALIM SEIF

5 03 2010

KATIKA kuendeleza maridhiano yalioasisiwa mwaka jana na viongozi wawili wa Zanzibar Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad leo wamekutana na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume Ikulu Mjini Zanzibar.Hii ni mara ya tatu tokea viongozi hao kukutana ambapo kwa mara ya kwanza walikutana mwezi Novemba mwaka jana na baadae kukutana tena kwa mara ya pili Desemba mwaka uliopita na kuzungumzia masuala mbali mbali ikiwemo kushirikiana na kuzika tofauti za kisiasa ambazo zimedumu kwa miongo kadhaa visiwani hapa.Mazungumzo ya wawili hayo yamechukua takriban sasa mbili ambapo lengo la ziara ya Maalim Seif Ikulu ni kujaribu kutafuta njia ya usuluhishi ambayo kwa miaka kadhaa hivi sasa wazanzibari wamekuwa katika malumbano yasiokwisha hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha maendeleo ya visiwa hivyo vya Unguja na Pemba.Awali Maalim Seif na Rais Karume walipokutana walisema lengo lao ni kuzika tofauti za kisiasa na kuchana na siasa chafu na kusistiza kwamba kukutana kwao huko hakuna lengo baya bali ni kuendeleza maelewano ambayo yamekosekana tokea kurudi kwa mfumo wa vyama vingi 1992.Endelea kusoma habari hii

UANDIKISHAJI UTAHATARISHA MARIDHIANO

2 03 2010

MAZUNGUMZO kati ya rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad huenda yakasambaratika wakati wowote kuanzia sasa kutokana na madai ya msingi yaliosababisha viongozi hao kukutana kurejea tena kwa kasi.Kukutana kwa viongozi hao kulitokana na mvutano wa muda mrefu wa vyama vikuu vya CCM na CUF pamoja na matatizo yaliojitokeza wakati wa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili mwaka jana ambalo ililazimika kusitishwa na kutafutwa ufumbuzi wa suala hilo baada ya matukio kadhaa kutokea katika uandikishaji wakati huo.Kati ya mambo yaliojitokeza ni pamoja na wafuasi wa vyama hivyo kuchomeana moto nyumba, mabanda ya kuku, wanyama kama punda kuchapwa mapanga, kutiana tindi kali machoni, kupigana wenyewe kwa wenyewe na mambo yanayofanana na hayo hali iliyosababisha jeshi la polisi kuingilia kati na kurusha mabomu ya machozi katika vituo vya uandikishaji baada ya wafuasi hao kurushiana mawe katika maeneo ya Unguja na Pemba.Jambo la msingi ambalo wananchi hao walikuwa wakilalamikia wakati huo na kusababisha vurugu ni baadhi ya wananchi kutokuwa na vitambulisho vya mzanzibari mkaazi ambavyo vimeingizwa kama ni sharti moja wapo la kuandikishwa katika daftari hilo ambapo idadi kubwa ya wananchi hawana vitambulisho hivyo jambo ambalo lilisababisha Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kusitisha zoezi hilo kutokana na vurugu zilizozuka katika uandikishaji huo.Endelea kusoma habari hii

WAKONGWE WAINGIA TENA KATIKA KINYANYANYIRO

26 02 2010

WAKATI zimebaki siku mbili za kumalizika uchukuaji fomu za ubunge, uwakilishi na udiwani kwa chama cha wananchi (CUF) takriban wabunge na wawakilishi wote wa zamani tayari wameonesha nia ya kutetea nafasi zao za majimbo wanayoyashikilia katika kinyanyanyiro cha uchaguzi mkuu ujao isipokuwa mwakilishi mmoja.Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umegundua kwamba hadi sasa Mwakilishi mmoja tu kutoka Kisiwani Pemba ndio ameonesha kutaka kupumzika na kuwaachia vijana nafasi hiyo ambapo baadhi ya vijana wameonesha nia ya kutaka kuchukua majimbo yote ya Unguja na Pemba.Mwakilishi huyo ni Mohammed Salim Mulla kutoka Jimbo la Mkoani ndio pekee hadi sasa aliyetangaza kutogombania nafasi hiyo kutokana na kutaka kupumzika katika uongozi wa kuwawakilisha wananchi wa jimbo hilo ambapo amesema ni vyema wanaotaka kuwania nafasi hiyo wakachukua fomu na kuomba ridhaa ya wananchi.Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Mkoani Pemba Mulla amesema ameiwacha nafasi hiyo kwa hiari yake kutokana na kuwa yeye ameshakuwa mwakilishi muda mrefu na pia anataka kuwaachia vijana kwani kubadilishana uongozi ni jambo la busara la lenye faida hasa kwa jimbo.Endelea kusoma habari hii

VIJANA WENGI WAJITOKEZA KUWANIA UONGOZI

26 02 2010

IDADI kubwa ya vijana imeonekana kujitokeza katika katika zoezi la uchukuwaji wa fomu za kuwania nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) katika maeneo mbali tokea kuanza kwa zoezi hilo Febuari 16 mwaka huu.Jimbo la Mji Mkongwe ambalo pekee kwa upande wa Unguja linashikiliwa na Mwanamke, Fatma Abdul-habib Ferej kutoka Chama Cha Wananchi (CUF) huku majimbo mengine 18 yakiwa ni ya Kisiwani Pemba ambayo yanashikiliwa na chama hicho.Tokea kutangaza kutolewa kwa fomu za kuwania nafasi hizo, jumla ya watu watano wametangaza kuwania nafasi za uwakilishi katika jimbo la Mji Mkongwe ambao ni vijana ambapo hadi sasa vijana watatu wameshachukua fomu akiwemo Goli kipa maarufu wa Mji Mkongwe, Othman Hamoud Dugheish (Abui), Mjumbe wa baraza kuu taifa, Abdallah Suleiman (Uhuru) na Khaleed Said Masoud (Gwiji). Miongoni mwa vijana hao waliojitokeza mara hii katika uchukuaji fomu ni pamoja na Mbunge mpya wa kuteuliwa na rais Jakaya Kikwete, Ismail Jussa Ladhu ambaye anatarajiwa kuchukua fomu yake leo asubuhi kuwania nafasi ya uwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe ambayo kwa sasa inashikiliwa na Fatma Abdul-habib Ferej.Endelea kusoma habari hii

BARAZA LA MAPINDUZI KUKUTANA

26 02 2010

KATIKA kuendeleza maridhiano yaliofikiwa Novemba 5 mwaka jana baraza la mawaziri linatarajiwa kukutana leo kujadili na kupitisha rasimu ya sheria ya kura ya maoni juu ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar.Wajumbe hao watakutana saa 3:00 asubuhi katika jumba la wananchi Forodhani mkoa wa mjini Magharibi na kuijadili kwa kina rasimu hiyo kabla ya kulepelekwa katika baraza la wawakilishi.Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Iddi Pandu Hassan aliwaeleza waandishi wa habari kwamba tayari ameshakamilisha taratibu zote zinazotakiwa na kilichobaki ni kuwasilishwa kwa wajumbe wa baraza la mapinduzi (baraza la mawaziri).Alisema ofisini yake imekuwa ikifanya kazi kutokana na maelekezo kutoka baraza la wawakilishi na sio kutoka kwa vyama vya siasa ambapo kazi aliyotakiwa kutayarisha ni rasimu ambayo imeshakamilika na leo itakwenda kuwasilishwa mbele ya wajumbe wa baraza la mapinduzi. Hassan alisema kukamilika kwa rasimu hiyo kutatoa nafasi kuwepo uwezekano wa kufanyika kura ya maoni kabla ya uchaguzi mkuu ambapo serikali ya mapinduzi Zanzibar itafanya maamuzi yake hasa kwa kuwa wao ndio wasimamizi wakuu wa shughuli hiyo.Endelea kusoma habari hii

MAALIM SEIF ATUNUKIWA ZAWADI LONDON

18 02 2010

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad ametunukiwa nishani na wazanzibari waishio nchini Uingereza kwa juhudi zake za kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya Zanzibar.Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari nishani hiyo alikabidhiwa juzi nchini Uingereza yenye kigae na alama ya visiwa viwili vya Unguja na Pemba ambapo watoto wadogo wanaojiita ‘New Generation’ kizazi kipya cha Zanzibar ndio waliomkabidhi kwa niaba ya wazanzibari wote.Kabla ya kuanza kwa mkutano uliondaliwa na jumuiya ya wazanzibari waishio London (ZAWA), Maalim Seif alipokewa na kuvishwa shada la mauwa katika mkutano huo uliofanyika Febuari 13, katika ukumbi wa Barking Abbey School Leisure Center ulioandaliwa na jumuiya ya wazanzibari (ZAWA) wanaoishi Jijini London.“Tumekabidhi tunzo hii maalim Seif kwa kuwa tunajua amejaribu sana kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya Zanzibar na amekuwa mstari wa mbele katika masuala kama hayo kwa hivyo sasa sisi kama wazanzibari tumefurahi sana kuwa ndoto na juhudi zake na kutaka kuijenga Zanzibar mpya yenye maridhiano na umoja sasa zimetimia Al-hamdulillah” kilisema chanzo chetu cha habari.Endelea kusoma habari hii

CCM YAWAPOZA WENYE MASHAKA NA MARIDHIANO

3 02 2010

KAMATI Maalumu ya Halmashauri Kuu ya taifa ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) imewataka watanzania kutokuwa na khofu na uamuzi wa wa baraza la wawakilishi juu ya kuudwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar.Maazimio hayo yametoka baada ya kikao cha kamati maalumu ya NEC ilifanya kikao chake jana Kisiwandui chini ya makamu mwenyekiti wake,rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.“Kikao kimewataka wazanzibari na watanzania kwa ujumla kutokuwa na wasiwasi kuhusiana na uamuzi huo uliopitishwa na wajumbe hao wa baraza la wawakilishi na kwamba wananchi waendelee kusimama imara na kujitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa baadae mwaka huu (2010), ili kukipatia ushindi wa kishindo chama chao” imesema taarifa ya NEC iliyotiwa saini na katibu wa kamati hiyo, Vuai Ali Vuai.Vuai kwa kuwa suala la kuundwa kwa serikali wa umoja wa kitaifa ni geni kwa wananchi na wananchi wengine ufahamu wao ni mdogo juu ya umuhimu wa kulinda amani nchini ipo haja ya kutolewa elimu juu ya umuhimu wa kuleta umoja na mshikamano ambayo unataka kuoneshwa hapa Zanzibar.Alisema kwa kuwa mfumo huo ni mpya haukuwepo awali lazima kila mmoja atakuwa na maoni yake tofauti lakini jambo la msingi kwa sasa ambalo viongozi wa kisiasa, dini na jamii kwa ujumla wanatakiwa kutumia vyema taalumu kwa kuwaelimisha wananchi na kusahau yaliopita na kujenga upya Zanzibar yenye amani na kuheshimiana.Endelea kusoma habari hii

MARIDHIANO YAWASILISHWA NEC ZANZIBAR

25 01 2010

RAIS wa Zanzibar na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM visiwani, Aman Abeid Karume ameyawasilisha rasmi maridhiano aliyofikia yeye na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambapo kimsingi suala la serikali ya mseto limekubaliwa.Rais Karume aliyasema hayo kwenye kikao kilichofanyika jana kuanzia saa nane mchana hadi saa moja usiku kikiwa chini uenyekiti wake na kuhudhuriwa na miongoni mwao, Makamu wa Rais, Dk Ali Mohammed Shein na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.Zanzibar imekuwa na matumaini ya kumalizika kwa siasa za chuki tangu Rais Karume afanye mazungumzo na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad Novemba 5, mazungumzo ambayo yalisababisha chama hicho kitangaze kumtambua Karume kuwa rais wa visiwa hivyo.Akizungumza na Waandishi wa Habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zbar, Saleh Ramadhani Feruzi alisema Rais Karume alikifahamisha kikao hicho kilichokuwa na ajenda kuu tatu, kuhusiana na mazungumzo yake na Maalim Seif akisema kuwa mazungumzo hayo yalikuwa na lengo la kuijenga Zanzibar mpya.Maridhiano hayo yaliyosababisha hoja binafsi ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar, yameishtua CCM ambayo ililazimika kukutana mara kwa mara ikiwamo mkutano wake uliofanyika Zanzibar jana.Alhamisi wiki hii kiongozi wa kambi ya upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Abubakar Khamis Bakari aliwasilisha hoja binafsi kutaka kutenguliwa kwa vifungu vya Katiba ya Zanzibar ili kuweka mazingira ya Zanzibar kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa.Endelea kusoma habari hii

SHAMHUNA AUNGA MKONO SERIKALI YA UMOJA

24 01 2010

NAIBU Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna, amesema anaunga mkono kwa dhati hatua iliyochukuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume, ya kukutana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, na kuzaa maridhiano ya kisiasa visiwani humo.Shamuhuna aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar kuzungumzia vuguvugu la kisiasa linaloendelea Zanzibar tokea viongozi hao wawili kuikutana Novemba 5, mwaka jana pamoja na hatua ya Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Abubakar Khamis Bakari, kuwasilisha hoja binafsi ya kutaka iundwe serikali ya umoja wa kitaifa baada ya wananchi kutoa ridhaa yao . Akizungumza kwa kujiamini na ufasaha mkubwa, Waziri Shamuhuna aliwashangaa wale wanaobeza hatua hiyo na kusema alichokifanya Rais Karume ni utekelezaji wa malengo yaliyoanzishwa na Chama cha Afro Shirazi (ASP) kupitia Rais wake, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na baadae kuendelezwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).Endelea kusoma habari hii

MANSOOR AJITOKEZA KUUNGA MKONO HOJA

24 01 2010

Waziri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid amekuwa mjumbe wa kwanza wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama cha Mapinduzi kutangaza nia yake ya kuiunga mkono hoja binafsi inayotaka kuundwa Serikali ya Pamoja Zanzibar.“Nina kila dhamira na nia kuiunga mkono hoja hiyo kwa sababu naamini inakwenda sambamba kabisa na mwelekeo na mtizamo wa Chama cha Mapinduzi”, Waziri huyo anaeshikilia Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, alisema katika mahojiano na Shirika la Habari la Uingereza (BBC) juzi.Mansoor amekuwa mtu wa kwanza kuvunja ukimya siku chache baada ya Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi Abubakar Khamis Bakari kupeleka Hoja Binafsi inayotaka kuundwa kwa Serikali ya Pamoja ambapo wengi wakiamini ni matunda ya yale yanayoitwa maridhiano yaliotokana na mkutano wa Rais wa Zanzibar Amani Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad uliofanyika Ikulu Novemba 5 mwaka jana.“Tuache khofu na kuishi kwa kutoaminiana, tuache kutishwa na vivuli vyetu, tuache kufungwa na historia, tuache kuishi kwa mazoea. Naamini wakati umefika, japo ni mgumu lakini mabadiliko lazima yatokezee,” alisema Mansoor ambaye pia Mwakilishi wa kuchaguliwa wa Jimbo la Kiembesamaki (CCM).Endelea kusoma habari hii

KARUME ALIARIFU BARAZA LAKE LA MAWAZIRI

20 01 2010

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume kwa mara ya kwanza ameliarifu rasmi Baraza lake la Mawaziri juu ya mazungumzo kati yake na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad yaliofanyika Ikulu Mjini Unguja.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika juzi majira ya 4:00 asubuhi na kumalizika sasa 6:00 mchana, Rais Karume aliwapa taarifa ya mazungumzo yake na Maalim Seif na kuwaeleza lengo la mazungumzo hayo yaliopewa jina la maridhiano ni kwa maslahi ya Wazanzibari wote.Rais Karume aliwaambiwa mawaziri hao kwamba mazungumzo hayo, yaligusia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na haja ya kudumisha amani na utulivu visiwani humo na maelewano na mashirikiano kati ya wananchi wote wa Unguja na Pemba.Alisema jambo la msingi walilozingatia katika mazungumzo yake ya Maalim Seif ni kuzika tofauti zilizopo ambazo zinachangia kuwatenganisha Wazanzibari na kutoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa jumla kushirikiana katika kujenga nchi bila ya kujali itikadi zao za kisiasa.Wakati wajumbe hao wa Baraza la Mawaziri wakiwa kimya wakimsikiliza Rais Karume anavyowaeleza juu ya mazungumzo hayo Rais alisema kwamba wananchi wakishirikiana na kujenga nchi kwa pamoja, watapiga hatua kubwa zaidi za maendeleo kuliko zilivyo hivi sasa.Rais Karume aliwataka wajumbe hao wazingatie maridhiano hayo kuwa yana faida kubwa kwao na kwa wananchi wote.Endelea kusoma habari hii

CCM WASHIRIKI MAANDAMANO YA CUF

18 01 2010

CHAMA cha Wananchi(CUF) jana kilifanya maandamano makubwa yaliyowashirikisha wanachama wa CCM mjini Zanzibar, kuunga mkono maridhiano yaliyofikiwa kati ya Rais wa Serikali ya Mapindizi (SMZ), Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad Novemba 5, mwaka jana. Maandamano hayo yalianza saa 2:00 asubuhi katika Viwanja vya Maisara na kuishia Uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Mkoa wa Mjini Magharibi, yalipambwa na rangi za bendera za vyama vya CCM na CUF pamoja na picha za Maalim Seif na Rais Karume. Katika maandamano hayo baadhi ya wanachama wa vyama hivyo walibeba mabango yenye ujumbe mbalimbali mengine yakisomeka “Ahsante Rais Karume, ahsante Maalim Seif, tumesamehe na tutasahau, kwa maslahi ya wazanzibari tupo tayari kwa lolote, asiyeitakia mema Zanzibar ni hasidi wa Wazanzibari.” Mengine yalikuwa na ujumbe uliosema: “Kujiamulia sio kuamuliwa, maslahi ya Zanzibar ni makubwa kuliko chama, Zanzibar ni moja ya Waunguja na Wapemba, Zanzibar ipo juu ya CCM na CUF, kuungana sio kutengana, hatima ya Wazanzibari itaamuliwa na Wazanzibari wenyewe zama za giza zimekwisha tukishirikiana, pasipo na mapenzi hakuna maendeleo na viongozi tusipoteze nafasi ya kuwaunganisha Wazanzibari.”.Endelea kusoma taarifa hizi

TUTAMSHAWISHI RAIS-WAZANZIBARI

14 01 2010

SIKU chache baada ya rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume kusema katiba haimpi nafasi kuwania uongozi kwa kipindi cha tatu baadhi ya wazanzibari wamesema wataendelea kumshawishi ili akubali kuendelea na wadhifa wake wa uongozi hata kwa kubadilisha katiba.Wamesema lengo la ushawishi huo ni kutoa nafasi na muda wa kurekebishwa baadhi ya kasoro zilizopo kabla ya kuingia katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika mwaka huu visiwani hapa kwa kuwa bila ya marekebisho mfumo uliopo wazanzibari wataingia katika uchaguzi usio salama.Hayo yameelezwa katika kongamano la siku moja la kujadilia maridhiano na mustakabali wa Zanzibar lililofanyika hoteli ya Bwawani mjini Unguja lililoandaliwa na CUF ambalo liliwashirikisha viongozi wa kisiasa, viongozi wa dini, masomi wa vyuo vikuu na wataalamu mbali mbali wa ndani na nje ya nchi. Wakitoa maoni yao muda mfupi baada ya kuwasilishwa mada na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wasomi hao wamesema hakuna haja ya kuingia katika uchaguzi wakati inafahamika kila uchaguzi unaofanyika Zanzibar hutawaliwa na vurugu na hatimae wananchi kupoteza maisha au kujeruhiwa jambo ambalo linachangia katika kurejesha nyuma nyuma juhudi za maendeleo.Naila Majid Jidawy ni mwanasiasa mkongwe ambaye amewahi kukamata nyadhifa kadhaa katika vyama tofauti amesema ipo haja ya kuongezwa muda kwa viongozi wawili Maalim Seif na rais Karume ili wamalize tofauti zao na mambo yaliokubaliana ili wazanzibari waingie katika uchaguzi wakiwa na hali ya usalama na amani.Endelea kusoma habari hii

KATIBA HAINIRUHUSU-KARUME

14 01 2010

Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume amezima ndoto za wananchi wenye kutaka aendelee na uongozi katika kipindi chagine cha urais kwa kuongezewa muda ambapo italazimika kubadilishwa katiba ili kumsogezea muda.Akihutubia wananchi katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 46 ya mapinduzi zilizofanyika Gombani Kisiwani Pemba, rais Karume alisema kipindi chake cha uongozi kimekomea hapo kwa mujibu na kwamba katiba hiyo haitoi nafasi kwa kipindi cha tatu cha uongozi.“Sherehe hizi za maadhimisho ya mapinduzi, leo januari 12, 2010, zina umuhimu wa pekee katika historia ya nchi yetu, maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika miezi 10 kabla ya uchaguzi mkuu na pia kumalizika kipindi cha pili kwa awamu ya sita ya serikali ya mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wangu na hakuna awamu nyengine ya tatu kikatiba” amesema rais karume.Hata hivyo hakufafanua kauli yake hiyo ambayo bado inawaacha watanzania katika giza zito kuhusiana na maoni ya wengi yanayomtaka yeye na katibu mkuu wa CUF Maalim Seif kuunda serikali ya umoja wa kitaifa katika kujenga misingi ya umoja unaoendelea miongoni mwa wazanzibari hivi sasa.Katika hutuba yake rais Karume ambayo imechukua takriban saa 1.30 alizungumza mambo mbali mbali ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa na kusisitiza misingi ya kuendeleza demokrasia nchini.Akizungumzia suala la daftari la kudumu la wapiga kura ambalo limengezewa sharti la vitambulisho vya mzanzibari mkaazi na kusababisha malalamiko makubwa kutoka kwa kambi ya upinzani huku chama cha wananchi CUF kikiwa kimelisusia daftari hilo kwa madai ya kukoseshwa kupatiwa vitambulisho hivyo.Endelea kusoma habari hii

LENGO NI KUDUMISHA AMANI-KARUME

11 01 2010

MAKAMO Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume amesema kuwa kukutana kwake na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad lengo lake kubwa llikuwa ni kuimarisha amani na utulivu kwa mustakabali wa kujenga nchi na ananchi wake.Rais Karume aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa huko Ndagoni Mkoa wa Kusini Pemba mara baada ya ziara yake ya kutembelea uendelezaji wa uwekaji wa waya wa umeme kutoka Tanga hadi Pemba na pia kupata nafasi ya kulikagua Tawi la CCM la Ndagoni ambalo limo katika ujenzi.Katika hotuba yake hiyo, Makamo Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar aliwaeleza wananchi waliohudhuria katika mkutano maalum ulioandaliwa mara baada ya kukagua Tawi hilo la CCM hapo Ndagoni, alisema kuwa mafanikio makubwa yaliopatikana nchini yameweza kudumisha amani, upendo na utulivu.Alisema kuwa wananchi walipomchagua mwaka 2000 malengo yao makubwa ilikuwa ni kuendeleza amani na utulivu sanjari na kuimarisha shughuli nyengine za kiuchumi, kisiasa na kijamii hali ambayo ameweza kuidumisha na hivi leo kupatikana matunda yake pamoja na mafanikio makubwa.Endelea kusoma habari hii

KARUME KUTOBOA SIRI LEO

11 01 2010

KILELE cha sherehe za miaka 46 ya mapinduzi Zanzibar zinatarajiwa kufanyika leo kisiwani Pemba huku hutuba ya rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi ambayo itatoa majibu ya hoja ya mazungumzo yake na katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad na kutoa muelekeo wa znz mpya.Sherehe hizi zitakazofanyika katika uwanja wa Gombani mkoa wa kusini Pemba zitakazotanguliwa ya maandamano ya wananchi, wafanyakazi mbali mbali na gwarinde la vikosi vya ulinzi na usalama kabla ya kusoma hutuba na mgeni rasmi wa shughuli hizo rais Karume.Akizungumza kwa nyakati tofauti katika uzinduzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo rais Karume aliwataka wananchi kusubiri kwa hamu kubwa mambo ya ziada ambayo aliwaahidi kuwatolea katika hutuba.“Hapa sina mengi ya kusema lakini nitakuwa na ya ziada huko katika kilele cha sherehe zenyewe …huko ndio yatasemwa mambo yote na mtafurahi nyie” alisisitiza rais Karume huku akipigiwa makofi.Endelea kusoma bahari hii

MUDA WA WA MSETO NI MDOGO-NAHODHA

11 01 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema uwezekano wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa hivi sasa sio rahisi kutokana na muda ulibaki ni mfupi.Hayo yameelezwa jana na Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio yaliopatikana katika kipindi cha miaka 46 ya mapinduzi katika ukumbi wa juu wa baraza la wawakilishi Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi.Nahodha alisema huu ni wakati wa kuangalia uwezekano wa kutengeneza Zanzibar mpya na sio wakati wa kujadiliana masuala hayo ya kuunda kwa serikali ya pamoja.Kauli hiyo ya Nahodha imefuatia maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua hatma ya mazungumzo ya viongozi wakuu wa vyama kati ya Rais Amani Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad ambayo yamewapa matumaini makubwa wananchi wa Zanzibar.Nahodha alisema mazungumzo ya viongozi hao yatasaidia zaidi katika kuinua nchi kimaendeleo pamoja na kuonesha njia nzuri ya kupita wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Endelea kusoma habari hii

LENGO LA MAPINDUZI LITAFIKIWA KARIBU

7 01 2010

WANANCHI wa Kisiwani Pemba wamesema mazungumzo ya rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambayo yana nia ya kutandika ukurasa mpya yataweza kufikia lengo la mapinduzi iwapo yatatekelezwa kwa vitendo.Wananchi hao wameyasema hayo kwa nyakati tofauti katika sehemu mbali mbali kisiwani Pemba wakati wakizungumza na gazeti hili kuhusiana na azma ya mazungumzo hayo yenye lengo la kusahau yaliopita na kuanza kuendesha siasa za kistaarabu katika visiwa vya Zanzibar.Wamesema ni vyema viongozi hao wakatekeleza kwa vitendo makubaliano hayo ili kufikia lengo la mapinduzi ya 1964 ambayo lengo lake yalikuwa ni kuwaunganisha wazanzibari kuwa kitu kimoja na kuondosha ubaguzi, chuki na uhasama wowote katika visiwa hivyo.Hata hivyo wananchi hao wamempongeza rais karume kwa kurudi nyuma na kufuata nyayo za baba yake ambaye alikuwa akiipenda sana nchi yake katika kuiletea maendeleo ambapo wamesema katika uhai wake hakuwa tayari kuona watu wake wakinyanyaswa kwa maslahi ya wengine. “Rais Karume na Maalim Seif ikiwa watatekeleza kwa vitendo azma yao ya mazungumzo basi watakuwa wametekeleza malengo ya mapinduzi kwa sababu mapinduzi ya 1964 yalikuwa na lengo la kuwaunganisha wazanzibari wote na hayo ndio malengo ya marehemu Mzee Karume” alisema Haji Sharif Ali mkaazi wa Kichungwani Chake Chake.Endelea kusoma habari hii

UANDIKISHAJI WAENDELEA CUF WAGOMEA BADO

3 01 2010

UANDIKISHAJI wa daftari la kudumu la wapiga kura unaendelea kwa utulivu licha ya chama cha wananchi CUF kuendelea na msimamo wake wa kutokwenda kujiandikisha katika daftari hilo kwa madai kwamba malalamiko yao ya msingi bado hayajapatiwa ufumbuzi wa kudumu.Wakati zoezi hilo likiwa linaendelea katika mkoa wa kusini katika majimbo ya Uzini na Mji Mkongwe mkoa wa mjini magharibi Unguja kwa upande wa Pemba uandikishaji huo unafanyika katika jimbo la Mkoani sehemu ambayo kuna kambi ya Jeshi la Kujenga Uchumi na (JKU) na Kikosi Maalumu cha Kuzuwia Magendo (KMKM).Kwa upande wa Unguja uandikishaji huo unaendelea katika jimbo linaloongozwa na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais (Muungano) Mohammed Seif Khatib, ambapo kuna jumla ya vituo vitatu ikiwemo Umbuji, Michamvi na Uzini. Huku Pemba kukiwa na vituo vya Chumbageni, Wambaa, Makoongwe, Makombeni na Mbuyuni.Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wamesema wataendelea kuligomea daftari hilo hadi hapo madai yao yatakapotekelezwa kwa vitendo kwa kupatiwa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi kila mwenye haki ya kupewa.Endelea kusoma habari hii

DAFTARI KUREJESHA NYUMA MAZUNGUMZO

24 12 2009

ZOEZI la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura huenda likayarudisha nyuma mazungumzo ya kumaliza tofauti za kisiasa yaliyofikiwa kati ya Rais Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad.Uchunguzi wa gazeti hili, umebaini kuwa baada ya kukutana kwa viongozi hao, wananchi wengi wakiwemo wafuasi wa vyama vya CCM na CUF waliamini kuwa matatizo ya kisiasa yaliyodumu zaidi ya miaka 17 yatakuwa yamepata suluhu ya kudumu.Hata hivyo, kumekuwepo na wasiwasi mkubwa hasa katika kipindi hiki ambacho daftari la kudumu la wapiga kura linaendelea kisiwani Pemba katika Wilaya ya Mkoani katika Mkoa wa Kusini Pemba ambako hali inaoenakana kuwa si shwari hasa baada ya wananchi kuendelea na mgomo wa kutojitokeza katika vituo vya uandikishaji.Mgomo huo unazidisha joto la kisiasa, ambako wakati zoezi hilo likianza siku yake ya kwanza jana katika jimbo la Mkanyageni anakotokea Makamu wa Rais Dk.Ali Mohamed Shein vituo vyote isipokuwa Chokocho vilikuwa na upungufu mkubwa wa watu.Kituo cha Chokocho huenda kikawa ni chanzo cha kutoaminika tena kwa maridhiano yaliyofikiwa, baada ya kuwepo kwa malalamiko ya kupandikizwa kwa watu wanaodaiwa kuwa ni askari wa Jeshi la Kujenga uchumi(JKU) wakiwa na barua za uhamisho zenye muhuri na nembo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Vijana hao licha ya kutokuwa na alama zozote zinazowaonesha kuwa ni askari, muda wote waliokuwepo kituoni hapo, walikuwa wakificha nyuso zao waume kwa wanawake kutopigwa picha na waandishi wa habari.Endelea kusoma habari hii

WADANGANYIFU TUTAWASHITAKI-ZEC

24 12 2009

MKURUGENZI wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Salum Ali Kassim ametegua kitendawili cha muda mrefu kuhusiana na vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watu kwa kujiandikisha zaidi ya mara moja jambo ambalo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria.Akiwasilisha mada katika kongamano la siku mbili la kujadili na kutathmini hali ya kisiasa Zanzibar lililoandaliwa na taasisi ya sayansi na utafiti wa siasa (REDET) ya chuo kikuu cha dar es salaam, Mkurugenzi huyo alisema vitendo hivyo vimebainika kujitokeza katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba.Alisema kwamba tume ya uchaguzi inajiandaa kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliofanya udanganyifu katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ambalo kwa sasa linaendelea katika jimbo la Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba.Aidha alivitaka vyama vya siasa viwahimize wanachama wao kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo kwa vile bila ya kufanya hivyo watakosa haki yao ya msingi na kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010.Kutokana na hali hiyo, mkurugenzi huyo aliwahimiza wananchi kufuata sheria na taratibu za uandikishaji ambapo ni kosa la jinai kujiandikisha zaidi ya mara moja.Endelea kusoma habari hii

KARUME AONGEZEWE MUDA- SOUD

23 12 2009

MWENYEKITI wa Chama kipya cha (AFP) Alience Former Part Said Soud amesema kuna kila sababu ya rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume kuongezewa muda wa kukaa madarakani kutokana na hali tete iliyopo visiwani Zanzibar.Soud alisema hayo wakati akichangia mada mbali mbali zilizowasilishwa katika kongamano la kitaifa la kujadili hali ya kisiasa Zanzibar katika hoteli ya bwawani lililoandaliwa na REDET.Soud alisema kutokana na hali ya kisiasa iliyopo hakuwezi kufanyika uchaguzi mkuu wa 2010 hivyo ni vyema katiba ikabadilishwa na rais kuongezewa muda wa kukaa kipindi chengine madarakani huku akisifu juhudi za viongozi wa kisiasa kukaa pamoja na kuzungumzia mustakabali wan chi yao.“ Hali hiyo ili ifanikiwe uzuri sana ni lazima Rais Amani aongezewe muda wa uongozi ili kuweza kukaa madarakani kwa muda wa miaka mitatu au mitano mengine hadi hapo nchi itakapokuwa katika hali ya ushuari” alishauri Soud ushauri ambao uliwahi kutolewa na vyama vyengine vya upinzani pamoja na wae wa chama cha mapinduzi.Mwenyekiti huyo alisema kuwa katika kuhakikisha hayo yanafanikiwa ni wazi kuwa ipo haja ya kufanyika kwa Serikali ya kitaifa haraka iwezekanavyo ili kuweza kuzima kauli mbaya zinazotolewa na baadhi ya viongozi hawafidhina.Endelea kusoma habari hii.

USIRI WA MAZUNGUMZO UONDOSHWE-KONGAMANO

23 12 2009

WASHIRIKI wa kongamano kuhusu hali ya kisiasa katika visiwa vya Zanzibar, wameshauri lengo na dhamira ya kweli ya mazungumzo kati ya Rais wa Zanzibar Amani Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, zikiwekwe hadharani.Washiriki hao walitoa rai hiyo jana katika kongamano hilo linalotarajiwa kumalizima leo mjini Zanzibar.Walikuwa wakichangia mawazo yao katika mjadala kuhusu hali ya kisiasa ya Zanzibar, mjadala ulioandaliwa na Taasisi ya Redet na kufanyika katika Hoteli ya Bwawani, iliyoko katika Mkoa wa Mjini Unguja.Washiriki hao walisema ingawa kuna dhamira ya kweli kuhusu mazungumzo ya viongozi hao, lakini kuna haja ya kuwaeleza wananchi kufahamu kilichozungumzwa.Walisema kukutana kwa Rais Karume na Maalim Seif na kuna faida kubwa katika kuleta maridhiano na kuondoa siasa za chuki na uhasama na kwamba kwa msingi huo, mazungumzo yao hayapaswi kuwa jambo la siri ya viongozi hao wawili.Mmoja wa washiriki, Mohamed Yussuf ambaye aliwahi kuwa ofisa wa kibalozi katika Umoja wa Mataifa, alisema ili Watanzania wafurahie matunda ya mazungumzo hayo, lazima yale yaliyojadiliwa, yawekwe hadharani.Endelea kusoma habari hii

KILA MTU ANAWEZA KUWA RAIS

18 12 2009

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume amesema hakuna kikwazo kwa mtu yeyote kutoka katika visiwa vya Unguja na Pemba mwenye kutaka kuwania nafasi ya kuwa rais wa Zanzibar.Hayo yameelezwa katika hafla ya sherehe za elimu bila ya malipo juzi jioni katika kijiji cha Vikunguni mkoa wa kusini Pemba ikiwa moja ya ziara yake ya siku mbili kisiwani Pemba.Alisema sio jambo la ajabu kwa mtu kutoka katika visiwa hivyo kupata fursa ya kuchaguliwa kuiongoza Zanzibar kwa kuwa suala la kuwa rais ni uamuzi wa wananchi wenyewe ambao huamua kutoa nafasi ya kutaka kuongozwa na nani.“Hakuna kikwazo kwa mtu yoyote kuwa rais wa nchi hii wala msidhanie kwamba eti fulani tu ndie anayepaswa kuwa rais wa Zanzibar hapana…mtu yeyote anaweza kuwa rais na mimi nakwambieni mnaweza mtu akaukwaa urais nyote mkashangaa hapa” alisema rais Karume.Kauli ya rais Karume imeonekana kuwakera baadhi ya viongozi ambao kwa muda mrefu wamekuwa na mawazo ya kwamba hawatakubali Zanzibar kuongozwa na mtu kutoka kisiwa cha Pemba hata akiwa anatoka katika chama cha mapinduzi.Endelea kusoma habari hii

TUTASHIRIKIANA KULETA MAENDELEO- KARUME

14 12 2009

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume amesema wazanzibari wataendelea kutofautiana kiitikadi lakini sio katika maendeleo.Kauli hiyo ya rais Karume ameitoa jana katika ufunguzi wa shule mpya iliyopewa jina la waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Haroun Ali Suleiman iliopo katika kijiji cha Ungi Msuka mkoa wa kaskazini Pemba .Rais Karume alisema hakuna chama hata kimoja cha siasa ambacho hakitaki maendeleo hivyo kwa kuwa kila chama kinadi maendeleo katika sera zake kuna kila sababu ya wananchi wa Zanzibar kukaa pamoja na kushirikiana katika kujiletea maendeleo katika vijiji vyao.Alisema sio vibaya kutofautiana katika itikadi za kisiasa kwa kuwa vyama vyote hunadi sera kwa wananchi wao ili kuingia madarakani katika uongozi na kila mgombea kutoka katika chama chake anajitangaza kwa wananchi lakini wisho wa siku mgombea huyo hutangazwa mshindi na analotakiwa ni kuleta maendeleo ya nchi na jimbo.“Tunatafautiana katika siasa lakini hatutafautiani katika maendeleo kwani kila chama kinajinadi kwa wananchi wake kutaka kuleta maendeleo ama katika nchi au kijiji anachotoka mgombea kwa hivyo kwa kuwa sote lengo letu ni moja la kujiletea maendeleo katika nchi yetu kwa nini tusishirikiane? Na kwa nini tugombane” alihoji rais Karume.Endelea kusoma habari hii

KARUME, MAALIM SEIF WAKUTANA TENA IKULU

14 12 2009

KATIKA kile kinachoonyesha kuimarika kwa uhusiano kati ya rais wa Zanzibar, Amani Karume na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, viongozi hao wawili jana walikutana tena faragha Ikulu ya Zanzibar.Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na mkurugenzi wa mambo ya nje wa CUF, zinasema kuwa kukutana kwa viongozi hao ni mwendelezo wa yale waliyozungumza walipokutana kwa mara ya kwanza Novemba 5 mwaka huu.“Ni kweli, katibu mkuu wa CUF amekwenda Ikulu na kukutana na Rais Karume. Walichozungumza bado ni siri. Lakini ni mwendelezo wa mazungumzo yao ya awali ya kutafuta maridhiano ya Wazanzibar na kuyaimarisha,” alisema Jussa.Jussa alisema kuwa kama walivyoeleza viongozi hao wakuu wa vyama vikuu vya siasa visiwani Zanzibar, mazungumzo hayo ni endelevu na kwamba hiyo ni hatua ya pili.Ingawa kilichozungumzwa na viongozi hao kimefanywa siri, taarifa za awali ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa pamoja na mambo mengine, Seif aliwakilisha kwa Karume majina mawili ya wanachama wa CUF ambao chama hicho kimewapendekeza kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa anayepaswa kuwasilisha majina hayo kwa Rais Karume ni kiongozi wa upinzani kwenye Baraza la Wawakilishi.Endelea kusoma habari hii.

RAIS KARUME ZIARANI PEMBA

14 12 2009

BAADA ya kukutana na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad mara mbili katika Ikulu yake, Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume leo anaanza ziara ya siku mbili kisiwani Pemba.Ingawa hakuna taarifa rasmi ya Ikulu kueleza rais Karume atazungumzia nini katika ziara hiyo, wananchi wengi wa Zanzibar hasa wakazi wa kisiwa hicho ambao wengi wao ni wapenzi na wanachama wa CUF, wanatarajia rais Karume kuzungumzia kilichojiri kwenye mkutano wake wa mwisho na Hamad siku ya Ijumaa iliyopita.Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, kisiwani Pemba, baadhi ya wakazi wa kisiwa hicho walisema wana hamu ya kumsikia Karume akieleza kuhusu mazungumzo yenye lengo la kuondoa chuki za kisiasa Zanzibar, zilizojengwa kutokana na mfumo mbaya uliopo.“Tunamsubiri Rais Karume aje na tumsikie, maana mwenzake Maalim Seif alikuja kutufanyia mkutano akatuambia kuwa Chama chetu kimemtambua rais, lakini kauli ya Rais Karume bado hatujaisikia,” alisema mmoja wa wakazi wa kisiwa hicho.“Nini kitafuata baada ya kusikia kauli ya Karume hilo ndio jambo la msingi kwetu, kwa sababu tumechoka na matatizo ya kisiasa yanayokuja kila wakati wa uchaguzi.”alisema mkazi mwingine wa ene hilo. Endelea kusoma habari hii.

WANAOBEZA MSETO ZANZIBAR NI ‘MASHETANI’

9 12 2009

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakuna tatizo kwa chama hicho, kuungana na CUF na kuunda serikali ya mseto na kueleza kwamba wanaobeza jitihada hizo ni mashetani. Akizungumza na gazeti hili, katika mahojiano maalum ofisini kwake Kisiwandui, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Saleh Ramadhan Ferouz alisema wanaofanya hivyo, pia wana mawazo ya kikoloni.“Mimi naweza kumwita ibilisi mkubwa au ni shetani yeyote ambaye hataki kuyaunga mkono mazungumzo haya kwa sababu ninaamini huyo, atakuwa hatutakii mema Zanzibar na anataka sisi tugombane miaka yote mtu huyo atakuwa ananufaika na migogoro inayotokea Zanzibar,”alisema. Ferouz alisema awali uamuzi wa rais Karume kukutana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif ulikuwa wake mwenyewe lakini, sasa umekuwa uamuzi wa Wazanzibari wote kwa kuwa kila kiongozi amewaambia wanachama wake na wasiokuwa na vyama pia wameelezwa.Mkutano ulifanyika Novemba 22, mwaka huu, ulitayarishwa na Chama Cha Mapinduzi na haukuwa wa serikali na pale rais alipokuja kuhutubia alikuja pale kama Makamu mwenyekiti wa CCM, hakuja kama rais na wananchi walikuja kusikiliza maelekezo ya chama. Kwa nini tuseme uamuzi ni wa rais Karume?. Sasa hivi tatuwezi tena kuita mazungumzo ya rais Karume na Maalim Seif sasa tunayaita maridhiano ya Wazanzibari kwa sababu viongozi wetu wote wamewasilisha mazungumzo hayo kupitia mikutano ya vyama vyao,”alisema Ferouz.Endelea kusoma habari hii

HATUHITAJI NAFASI ZA VITI MAALUMU-TAMWA

9 12 2009

MKURUGENZI Mtendaji wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Ananilea Nkya amesema watanzania hawahitaji tena viti maalumu vya wanawake katika uchaguzi mkuu ujao wa 2010.Nkya aliyasema hayo katika mafunzo ya wiki moja juu ya namna ya kuripoti habari zinazohusu masuala ya udhalilishaji wa kijinsia iliyoandaliwa na wizara ya kazi, maendeleo ya vijana, wanawake na watoto Zanzibar kwa kushirikiana na TAMWA katika chuo elimu mbadala visiwani Zanzibar. Alisema wanawake wa Tanzania hivi sasa wamehamasika vizuri na wamekuwa na uwezo mkubwa katika uongozi hivyo hawahitaji nafasi za kugaiwa kama ilivyotokea vipindi vya uchaguzi vilivyopita ambapo wanawake walikuwa wakifikiriwa zaidi kwa nafasi za upendeleo.“Wanawake wa Tanzania hatuhitaji tena viti maalumu kwa sababu wanawake wamehamasiaka na wana akili sana za kuwashinda wanaume na mimi nasema hivi kwa sababu nimeshawaona wanawake wanavyopanda juu katika uongozi na wakishindanishwa na wanaume wao wamepanda sana kwa nini tume tunagaiwa nafasi za upendeleo wakati uwezo tunao” alihoji mkurugenzi huyo.Alisema katika chaguzi zilizofanyika mwaka 2005 Tanzania wanawake waliingia katika kinyanyanyiro cha kugombea ubunge lakini kati ya wanawake wote walioteuliwa na vyama vyao walishindwa kupitia majimbo isipokuwa mmoja kutokana na mfumo dume kulitawala taifa la Tanzania lakini hivi sasa hali ni tofauti.Endelea kusoma habari hii

TUTAENDELEZA UMOJA WETU-KARUME

7 12 2009

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume amesema kuwa wananchi wa Zanzibar wana historia kubwa ya kuimarisha umoja, mshikamano na maelewano hivyo suala la kukaa pamoja kwa viongozi na kujadili mustakabali wa nchi ni utamaduni wa Kizanzibari. Alieleza kuwa Wazanzibari wote ni ndugu na hakuna kitu ambacho kinaweza kuwatenganisha katika umoja na ushirikiano wao, hivyo tofauti za kisiasa si sababu ya kuwagawa Wazanzibari ambao ni wamoja kwa miaka kadhaa. Rais Karume ameyasema hayo leo wakati wa mazungumzo na balozi wa Canada nchini Tanzania Bw. Robert Orr, Ikulu mjini Zanzibar ambako alifika kwa ajili ya kujitambulisha. Rais Karume alimueleza Balozi huyo kuwa mbali ya yeye mwenyewe binafsi kukutana na Katibu Mkuu wa chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad tayari hapo siku za nyuma wananchi walikuwa wakishirikiana kwa pamoja kupitia miradi yao ya maendeleo kwenye Kamati zao bila ya kujali itikadi zao za siasa. Alisema kuwa mbali ya mashirikiano ya wananchi hao wa mjini na vijijini Wawakilishi wa Majimbo ndani ya Baraza la Wawakilishi ambao wanawawakilisha wananchi wao nao wamekuwa na mashirikiano makubwa katika maendeleo ya Zanzibar. Kutokana na hatua hiyo, Rais Karume alieleza kuwa umoja, mshikamano na maelewano yapo kwa wananchi wote na hatua ya kukutana kwa viongozi wakuu imeendeleza na kuimarisha na kujenga mustakabali mzuri kwa maendeleo ya wote.Endelea kusoma habari hii.

MARIDHIANO YALELEWE-ALI KARUME

3 12 2009

BALOZI wa Tanzania nchini Italy, Ali Abeid Karume amesema mazungumzo kati ya rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad hayana tofauti na mtoto mchanga aliyezaliwa ambaye atahitaji malezi mema ya wazazi wake.Alisema mazungumzo hayo ni mazuri na yanafaa kuendelezwa na kila mmoja hadi kufikia kikomo chake kwani mtoto anapozaliwa na akaachwa bila ya kupewa malezi mazuri kutoka kwa wazazi wema ukuaji wake hauwezi kuwa mzuri na huenda huko mbele akaharibika kwa kufuata yabia za watu wengine ambao hawana maadili mema.Akizungumza na Mwananchi balozi Karume amelinganisha mazungumzo hayo na mtoto anayezaliwa ambaye anahitaji malezi mema kutoka kwa wazazi wake ili apate kukuwa vyema katika ulimwengu wenye mazonge mengi na kila aina ya mitihani ndani yake.Alisisitiza lazima kuwepo kwa kiongozi mwengine ambaye ataweza kuyaendeleza mazungumzo hayo kwani hivi sasa ndio kwanza yameanzishwa na muda wa rais Karume wa kuondoka madarakani unakaribia hivyo ni vyema wazanzibari wakatafuta mtu ambaye ataridhi mazuri yaliachwa na kiongozi anayemaliza muda wake.Alisema jambo zuri linahitaji kuendelezwa lakini kwa kuwa mazungumzo hayo ndio yameanza yanapaswa kupatiwa kiongozi mzuri ambaye ni jasiri na atakayeweza kuchukua nafasi kama hiyo ya kuyasogeza mbele mazungumzo hayo ambayo yana dhamira ya dhati ya kumaliza mgogoro uliopewa jina la mpasuko wa kisiasa.Endelea kusoma habari hii

MAREKANI YARIDHISHWA NA UTAALAMU WA DAFTARI

3 12 2009

SERIKALI ya Marekani imeridhishwa na utaalamu unaotumika katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea visiwani Zanzibar.Hayo yameelezwa na balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt, jana alipowasili Ikulu Mjini Zanzibar alipofika kwa ajili ya kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume.Balozi huyo alisifu jinsi zoezi hilo linavyoendelea kwa amani na utulivu katika maeneo mbali mbali katika vituo kadhaa alivyovitembelea alipowasili visiwani Unguja kabla ya kwenda ikulu kuonana na rais.Katika maelezo yake Balozi Lenhardt alimueleza Rais Karume kuwa hatua iliyochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuwapatia wananchi vitambulisho vya Ukaazi ni muhimu sana katika maendeleo yao.Alieleza kuwa ameweza kushuhudia yeye mwenyewe jinsi ya zoezi la uandikishaji linavyoendela na kuona jinsi amani, utulivu uliopo na jinsi teknolojia ya kileo inavyotumika katika zoezi hilo la uandikishaji.Balozi Lenhardt alieleza kuwa kabla ya kuonana na Rais Karume alitembelea katika kituo cha Uandikishaji cha skuli ya Jangombe ambapo amejionea hali nzima ya zoezi hilo linavyoendelea.Endelea kusoma habari hii

MAALIM SEIF AANIKA MKAKATI WAKE KARUME

30 11 2009

SIRI zaidi za mkutano wa rais wa Zanzibar, Abeid Amani Karume na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad zinazidi kuwekwa bayana baada ya Maalim Seif kusema lengo kubwa la faragha yao ilikuwa ni kuunganisha nguvu katika kutetea mambo yanayoihusu Zanzibar kwenye Muungano. Seif alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wananchi kwenye sherehe maalum za Baraza la Eid El-Hajj zilizoandaliwa na CUF kwenye ukumbi wa Jamat-khan ulio Mkunazini Mjini Unguja. Seif, ambaye aliwahi kuwa waziri kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ), alisema, Zanzibar iliyoungana itazaa Tanzania iliyoungana. Alisema kuungana kwa Wazanzibari kutasaidia kuimarisha muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar kuliko kugawanyika kwa Wanzibari kwa kuwa pande zote mbili zina malalamiko kuhusu suala hilo. “Wazanzibari wakiungana wataweza kudai haki zao na kuuimarisha muungano kuliko wakigawanyika,” alisema. Zanzibar imekuwa na madai kadhaa kwenye Muungano, ikidai kurejeshewa utaifa wao ili iweze kushiriki katika masuala ya kimataifa; inadai pia kuwa kuna baadhi ya mambo yameingizwa kinyemela katika mambo ya Muungano, likiwemo suala la mafuta na baadhi wanataka rais wa Zanzibar arejeshewe hadhi yake ya kuwa makamu wa rais.Endelea kusoma habari hii.

TUMEDHAMIRIA KWA DHATI-KARUME

28 11 2009

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume amesema yeye na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad wamesafisha nyoyo na kusameheana kwa dhati kama maadili yao yanavyowaelekeza.Akihutubia katika hafla ya baraza la Eid El-Hajj lilifanyika katika ukumbi wa Jumba la Wananchi Forodhani Mjini hapa, Rais Karume amesema walikutana na Maalim Seif kwa kuelezana ulazima wa kuleta amani na utulivu kwa nia ya kujenga misingi ya kuleta maendeleo makubwa zaidi ya wananchi na nchi yao.“Tumesafisha nyoyo na kusameheana kwa dhati kama itikadi na maadili yetu yanavyotufundisha. Zaidi ni kuwa tumejenga msingi wa kuaminiana.” amesema Rais Karume na kupigiwa makofi mengi na hadhara iliyokuwa ikimsikiliza. Alisema msimamo huo ni kwa niaba ya wananchi wote ambao wanaamini kuwa umoja, masikilizano, mshikamano,amani na utilivu ni mambo muhimu zaidi kuliko kuzingatia mengine kwa ajili ya mustakabali wa Zanzibar na watu wake.Katika hutuba yake hiyo alisema lengo ni kuishi aktika umoja daima ili kupatikane mafanikio ya kila jambo hivyo kila siku zinavyokwenda hali izidi kuimarika zaidi kuliko ilipotoka “Namuomba Mwenyeenzi Mungu ajaalie siku zetu zote za umri wetu ziwe ni furaha ili tuishi katika umoja, upendo na tupate mafanikio ya kila jambo. Lengo letu liwe, leo iwe bora kupita jana na kesho kuliko leo.Hakika Mwenyeenzi Mungu yeye ni Msikivu, Yu karibu na wenye kukubali dua za waja wake” alisema Rais huyo.Endelea kusoma habari hii

SHAMHUNA NI MBINAFSI-MAONI

25 11 2009

WASOMI na wana siasa kadhaa wameleza wasiwasi wao juu ya matamhsi yaliotolewa na Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Juma Shamhuna kukataa uwezekano wa kuwepo serikali ya pamoja Zanzibar.Shamhuna alinukuliwa na vyombo vya habari juzi akisema kuwa kinachotakiwa zanzibari ni kile alichokiita kuwepo na utamaduni wa kukubali matokeo ya uchaguzi na kuwa wenye kushinda wapewe fursa ya kuunda serikali kadri watavyooona inafaa.Alisema Zanzibar haina haja ya kuwa na serikali ya mseto wala ya pamoja ila kinachotakkiwa kuwa na kile alichokiita kuwa na “Meneja Mzuri” ambaye ataweza kutatua matatizo ya nchi moja baada ya jengine.Akionekana kutaka kujijengea mazingira mazuri Shamhuna alisema hakuna haja ya kusema kuwepo na zamu za Unguja na Pemba kuwania nafasi ya urais, wala kuwa mtu anaefaa kuwa rais ni kijana au mzee. Watu waliotoa maoni yao kwa gazeti hili ni pamoja na waziri mmoja wa muda mrefu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar alisema anamuona Shamuna kuwa ni kama mtu mwenye tabia ya kudandia fursa za kisiasa mara zinapojitokeza.Alisema kuwa haikumuwajibikia kabisa Shamhuna kutoa kauli zinazoendelea kugawa wazanzibari wakati rais karume ambaye ni mkuu wake wa kazi tayari ameshatoa msimamo unaohimiza ujenzi wa umoja na mshikamano huku rais mwenyewe akisisitiza kuwa milango ya mazungumzo ipo wazi.Endelea kusoma habari hii

MAWAZIRI WACHAFUA HALI YA HEWA ZNZ

25 11 2009

WAKATI Zanzibar ikiendelea kushangilia maafikiano ya kihistoria baina ya Rais Amani Abeid Karume na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, juu ya uwezekano wa kuwepo kwa Serikali ya Mseto, mawaziri wawili wamejitokeza hadharani kutia doa shangwe hizo. Viongozi hao wameeleza bayana kuwa Serikali ya Mseto si muhimu visiwani hapa. Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Ali Juma Shamhuna na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Muungano), Mohammed Seif Khatib, wametofautiana na msimamo wa Karume ambaye alisema kuwa uamuzi wa kuwa na Serikali ya Mseto ni wa Wazanzibari wenyewe. Tamko hilo la Karume alilitoa siku chache baada ya kukutana kwa faragha na Maalim Seif, ambaye baadaye aliitisha mkutano wa hadhara na kueleza kuwa CUF imeamua kumtambua rais huyo kwa kuwa kufanya hivyo kutarahisisha mazungumzo ya kutafuta muafaka. Lakini Shamhuna, ambaye pia ni Waziri wa Habari wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ), alisema Zanzibar haihitaji Serikali ya Mseto wala Serikali ya Umoja wa Kitaifa, bali kinachotakiwa ni kujenga utamaduni wa kukubali matokeo ya uchaguzi ya kushinda na kushindwa. Alisema hayo katika kipindi cha Harakati za Kisiasa kinachorushwa hewani kila siku ya Jumanne na kituo cha redio cha Zenji FM, ambacho kinamilikiwa na Waziri Mohammed Seif Khatib.Endelea kusoma habari hii.

WANANCHI WARIDHISHWA NA MAZUNGUMZO

23 11 2009

BAADHI ya wazanzibari wamesema wamerajirika sana na kufurahishwa lakini wana wasi wasi wa utelelezaji wa kauli iliyotolewa juzi na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume ya kuutangazia umma kwamba amani ya kudumu hivi sasa imepatikana Visiwani Zanzibar.Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao wakiwemo wasomi masuhuri amabo hawakutaka kutajwa majina yao gazetini wamesema kauli ni jambao moja na utekelezaji ni jambo jengine lakini hawana shaka iwapo kuna dhamira ya kweli ya kumaliza tofauti za kisiasa zikifikiwa. Wamesema kwa sasa wanachokiomba ni dua za amani na kuwataka viongozi hao wawe wakweli katika kauli zao ikiwa pamoja na kutekeleza kwa vitendo maneno yao waliokuwa wameyatoa kwa nyakati tofauti katika mikutano yao ya hadhara iliyofanyika katika viwanja vya Demokrasia Kibanda Maiti Mjini Unguja.Wananchi hao wamesema licha ya kwamba miafaka mingi inayofikiwa na pande mbili hizo hasimu za CCM na CUF lakini ikiwa kuna dhamira ya kweli ambayo itaoneshwa kwa vitendo wao hawana pingamizi na wapo tayari kuunga mkono mazungumzo hayo amabyo yana maslahi na manufaa kwa wazanzibari.“Sisi hatuna matatizo na mazungumzo ya Mwafaka au maridhiano kama yalivyoitwa sasa.umesikia bwana tatizo letu kubwa ambalo tuna wasiwasi nalo ni utekelezaji mama lakini ikiwa sasa wenyewe wameshakubaliana kusuluhishana bila ya kuwepo umoja wa mataifa wala Rais Mkapa au Rais Kikwete basi tunawaombea dua sana tu maridhiano hayo yawe salama” alisema Amour Said Mansoor Mkaaji wa Kikwajuni Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR YATANGAZWA AMANI YA KUDUMU

23 11 2009

RAIS wa Zanzibar, Amani Abeid Karume ametangaza rasmi kuzika uhasama wa kisiasa uliokuwepo kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), akisema suala la serikali ya mseto liko mikononi mwa wananchi. Tamko hilo la Rais Karume limekuja siku chache baada ya katibu mkuu wa CUF, Seif Hamad Rashid kwenda Ikulu ya Zanzibar kuzungumza naye na baadaye kufanya kitendo cha kijasiri cha kuwatangazia wafuasi wake kuwa chama hicho kimeamua kumtambua Karume kuwa rais wa visiwa hivyo. Tayari CUF imeshafanya mikutano miwili ya kuwataarifu wafuasi wake kuhusu uamuzi huo wa kumtambua Karume, ukiwemo mkutano wa kwanza ambao Maalim Seif alipingwa hadharani na jana ilikuwa zamu ya rais huyo kuwaeleza wafuasi wake wa CCM mjini hapa. Akihutubia maelfu ya Wazanzibari waliofurika kwenye viwanja vya Demokrasia vilivyo mkoa wa Mjini Magharibi jana, Rais Karume alitangaza kwamba amani ya kudumu Zanzibar sasa imepatikana. “Zamani magazeti yalikuwa yakiandika Zanzibar kunawaka moto, hakukaliki¦ sasa ndugu zangu amani ya kudumu imefika Zanzibar. Na hili tulikuwa tunalitafuta kwa muda mrefu sana,” alisema Karume huku akishangiliwa na umati wa watu.Endelea kusoma habari hii

RAIS KARUME KUUTANGAZIA UMMA KESHO

21 11 2009

MAKAMO Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Rais Amani Abeid Karume leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkubwa ulionadaliwa na chama hicho kwa lengo kuelezea mazungumzo ya kisiasa yaliyofikiwa kati yake na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad.Mkutano huo ambao utakuwa ni wa mwanzo wa chama hicho kuzungumzia mazungumzo ya viongozi hao yaliobatizwa jina la ‘Maridhiano’ unatarajiwa kuwa wa aina yake katika viwanja vya Demokrasia Kibanda Maiti ambapo imeelezwa kwamba utapambwa kwa vikundi mbali mbali vya burudani kabla ya kuanza kwa mkutano huo.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Umoja wa Wazazi wa Jumuiya ya CCM na kusainiwa na Naibu Katibu Mkuu wake, Yasmin Aloo na kusambazwa kwa vyombo vya habari imewataka wanachama na wafuasi pamoja na wakereketwa wa chama hicho wa mikoa yote mitatu ya Unguja kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo.Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikitarajiwa kuwatangazia wanachama wake suala la mazungumzo ya Rais Karume na Malim Seif tayari Chama Cha Wananchi (CUF) kimeshawaelezwa wanachama wake suala hilo na kuwaomba wanachama wote wa CUF na wazanzibari kuunga mkono mazungumzo hayo ambayo yana azma ya kuleta umoja na maridhiano kwa wazanzibari wote bila ya kujali itikadi za kisiasa walizonazo wanachama hao.Endelea kusoma habari hii

TUNA IMANI NA MAZUNGUMZO-EU

19 11 2009

UMOJA wa Ulaya (EU) umesema kwamba una imani kwamba Rais wa Zanzibar, Amani Karume, na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, wamejitolea kwa dhati kuumaliza mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar. Kauli hiyo imetolewa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, ambaye kwa sasa anaongoza timu maalum ya Umoja huo, Staffan Herrstroem, alipofanya mazungumzo mafupi na waandishi wa habari katika Hoteli ya Serena, Mjini Zanzibar, mara baada ya kukutana na Rais Karume na Maalim Seif kwa nyakati tofauti.“Tumekwenda kuongea na Rais Karume na Katibu Mkuu Hamad na tumetiwa moyo sana na namna wawili hao wanavyoonesha dhamira ya dhati kuelekea ufumbuzi wa mgogoro huu wa kisiasa.” Alisema Balozi Herrstroem.Balozi Herrstroem alisema kwamba Umoja wa Ulaya hauna sababu yoyote ya kutilia shaka dhamira ya viongozi hao wa Zanzibar, kwani kumaliza mgogoro wa Zanzibar na kuimarisha demorasia ni jambo lenye maslahi kwa kila mtu na kwa hivyo ni suala la kuungwa mkono.Akijibu swali kuhusu msimamo wa EU juu ya uhusiano uliopo baina ya matukio ya uandikishaji wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na msimamo huu mpya wa viongozi hawa wawili wa Zanzibar, Balozi Herrstroem alisisitiza kwamba EU inaona kuwa hatua za kumaliza mgogoro wa Zanzibar zinahusiana moja kwa moja na haja ya kuwepo kwa uchaguzi wa huru, wazi na wa haki na kwamba hiyo ndiyo sera ya Umoja huo.Endelea kusoma habari hii

TUSAMEHE MAALIM – WANAWAKE CUF

15 11 2009

zaha ali hamadJUMUIYA ya Wanawake wa Chama Cha Wananchi (CUF) imeomba radhi kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kutokana na kitendo cha kumpinga hadharani na kuangusha vilio baada ya kutolewa kauli ya kutambuliwa Rais Amani Karume.Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanawake, Zahra Ali Hamad katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Demokrasia na kuhudhuriwa na maelfu ya wanawake wa mikoa mitano ya Unguja. Wiki iliyopita Katibu Mkuu wa chama hicho, aliwaambia wanachama na wapenzi wa CUF kwamba chama chake kimemtambua Rais Karume kuwa rais halali wa Zanzibar jambo kauli amabyo ilipingwa vikali wa wanachama hao na baadhi yao kuangua vilio wakisema Maalim Seif amekisaliti chama chake na hivyo hawakubaliani na uamuzi huo wa kumtambua Rais Karume.“Tunakuomba utusamehe kwa hisia kali tulizozionesha wiki iliyopita katika viwanja hivi hivi. Tulikuwa hatujakuelewa. Sasa tumekuelewa na kutoka kwetu tegemea mashirikiano yasiyo masharti katika hili. Kwako ujumbe wetu ni mmoja tu, nao ni kwamba tulikupenda, tunakupenda na tutaendelea kukupenda maana nawe daima umekuwa ukitupenda!” alisema Zahra huku akiungwa mkono wa wanawake wenzake. Amesema ni jambo la fakhari kuwa wanawake ndio ambao wamekuwa jumuiya ya mwanzo kuuona umuhimu wa maamuzi hayo yaliyofanywa na uongozi za CUF na, hivyo, kuamua kuingia barabarani kuthibitisha uungaji mkono wa kufanya kila lililo ndani ya uwezo wao ambapo dhamira ya pamoja itaweza kutimia.Endelea kusoma habari hii

UCHAGUZI UTAKUWA SALAMA-KARUME

15 11 2009

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume, amesema uchaguzi hauwezi kufanyika iwapo watu wenye haki ya kupiga kura wakiwa wameachwa kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.Rais Karume amesema itakuwa ni kichekesho kufanyika kwa uchaguzi wakati kuna wananchi wengi hawajaandikishwa katika daftari kama wapiga kura halali ambao wanapaswa kushiriki katika uchaguzi kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.Kauli hiyo ameitoa katika mazungumzo yake na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasilia Zanzibar katika Uwanja wa Ndege akitokea Dar es Salaam, alipotunukiwa Shahada ya Heshima ya Falsafa ya Udaktari wa Sayansi na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.Wakati Rais Karume akiyasema hayo kuna mamia ya wananchi wa Unguja na Pemba ambao hawajaandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura baada ya kukosa kuwa na vitambulisho vya mzanzibari mkaazi vitambaulisho ambavyo vimefanywa kuwa ni sharti muhimu la kuandikishwa katika daftari hilo.Mara kadhaa Rais Karume ametoa agizo kwa idara ya vitambulisho vya mzanzibari mkaazi (ZAN-ID) kuhakikisha wanampatia kitambulisho kila mzanzibari mwenye haki ya kupewa kitambulisho hicho pamoja na kuhakikisha kila mwenye haki ya kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura aandikishwe agizo ambalo halijatekelezwa ipasavyo hadi sasa.Endelea kusoma habari hii

NORWAY YAAHIDI MISAADA ZAIDI ZNZ

12 11 2009

NORWAY imeahidi kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuendeleza normiradi ya mandeleo na kupongeza mazungumzo yaliofanywa kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad hivi karibuni.Balozi wa Norway nchini Tanzania Bw. Jon Lomoy aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais Karume Ikulu mjini Zanzibar.Katika maelezo yake Balozi Lomoy alimueleza Rais Karume kuwa Norway imefarajika kwa kiasi kikubwa kwa mazungumzo hayo yaliyofanyika kati ya viongozi hao na kueleza kuwa hatua hiyo itafungua ukurasa mpya wa mafahamianoLomoy alieleza kuwa Norway imefurahishwa na hatua hiyo na kutoa pongezi zake za dhati kwa Rais Karume na kueleza kuwa hatua hiyo ni historia kwa Zanzibar.Balozi huyo alieleza kuwa mazungumo hayo yatasadia katika juhudi za Zanzibar katika kupga hatua za maendeleo.Alisema kuwa hatua ya kukaa kwa pamoja kati ya viongozi hao wawili na kuzungumza juu ya mustakabala mwema wa nchi.Alieleza kuwa changamoto iliyopo hivi sasa ni kuendeleza sera za kujiletea maendeleo endelevu na kuahidi kuwa nchi yake itaendelea kuunga mkono.Endelea kusoma habari hii

WAZANZIBARI WOTE WAPONGEZANA

12 11 2009

seif&karumeUmoja wa Wazanzibari Wanaoishi Nje ya Nchi (MUWAZA) wametoa tamko la kufurahishwa kwao kutokana na hatua ya viongozi hao wawili kukutana kwa ajili ya mazungumzo na kuzika tofauti zao za kisiasa ambazo zimedumu kwa miongo kadhaa hivi sasa.Tamko hilo limetolwa na kutiwa saini na Mwneyekiti wake wa muda Dkt. Yussuf Saleh Salim limesema kukutana kwa viongozi hao kutasaidia kutetea mustakbal wa Zanzibar pamoja na kuwaunganisha wazanzibari wote bila ya kujali tofauti zao za kisiasa.Tamko hilo limesema mazungumzo hayo yataweza kuzaa Zanzibar mpya kwa wazanzibari kuishi kitu kimoja, kuondosha uhasama na chuki baina ya wazanzibari wote na pia kuwashajiisha wazanzibari kwa pamoja kuleta maendeleo katika visiwani za Unguja na Pemba.“Rais Amani Abeid Karume na Maalim Seif Shariff Hamad kukutaka MUWAZA imefurahishwa kwa msimamo wa viongozi hao wawili na kupongeza kwa hatua waliochukua ya kuweza kuka pamoja na kuzungumza” lilisema tamko hilo ambalo lililosambazwa kwa vyombo vya habari ambali limesainiwa na Mwenyekiti wa muda Dk.Yussuf Saleh Salim.Kwa mujibu wa tamko hilo lililosambazwa kupitia njia ya mtandao, MUWAZA inaunga mkono kwa kutetewa kwa Nchi, Taifa na Dola la Zanzibar ambapo kutetewa maslahi ya kiuchumi yakiwemo mafuta na gesi aslilia ya Visiwani Zanzibar.“Kukutana kwao kuleta maendeleo ya kijamii – siha, elimu na utamaduni wa Zanzibar na kutetea haki za kidemokrasia bila ya kujali itikadi pamoja na kuruhusu kila mzanzibari kuwa na uhuru wa kupiga kura,kutetea mihimili halali ya utawala ya Zanzibar,kurejesha cheo cha makamu wa Rais Zanzibar,kurejesha mambo asili kumi na moja ya Muungano na hatimae kuyajadili upya,kulipa baraza la wawakilishi heshima sawa na bunge la Muungano” amesema taarifa hiyo yenye kurasa moja kutoka Makao Mkuu wa ofisi hiyo Copenhagen Denmark.Endelea kusoma habari hii

UNDP YARIDHISHWA NA ZANZIBAR

12 11 2009

SHIRIKA la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limeeleza tnkuridhishwa kwake na hatua za uendelezaji wa miradi ya maendeleo Zanzibar na kuahidi kuendelea kuunga mkono hatua hizo.Akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume, Mwakilishi Mkaazi mpya wa UNDP nchini Tanzania ambaye pia ni Mratibu wa shughuli za Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Dk. Alberic Kacou, alisema kuwa hatua hizo ni za kuungwa mkono kwani zimeleta faraja kwa UNDP.Dk. Kacou ambaye alikuja kujitambulisha kwa Rais Karume, alisema kuwa UNDP itaendeleza miradi yake iliyopo na kuanzisha mengineyo kwa ajili ya maendeleo.Katika maelezo yake, Mwakilishi Mkaazi huiyo alieleza kuwa UNDP imefarajika zaidi kutokana na Zanzibar kuendesha vizuri miradi inayofadhiliwa na Shirika hilo.Alisema kuwa anamatumani makubwa ya kuzidi kupata mafanikio katika miradi ya maeendeleo kutokana na uongozi mzuri uliopo chini ya Rais Karume.Alieleza kuwa mafanikio katika maendeleo hayawezi kupatikana iwapo hapatakuwa na uongozi bora hatua ambayo Zanzibar imeweza kufanikiwa na kuwa kigezo kwa nchi nyengine za Bara la Afrika.Endelea kusoma habari hii.

AFRIKA KUSINI YAFURAHIA MAZUNGUMZO

10 11 2009

kusAFRIKA Kusini imeeleza kuridhishwa na mazungumzo yaliofanywa kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamadi na kueleza kuwa ni changamoto kwa nchi za bara la Afrika na hatua hiyo imeonesha kukua kwa demokrasia Zanzibar.Balozi wa Afrika ya Kusini anaemaliza muda wake wa kazi nchini, Sindiso Mfenyana aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais Karume Ikulu mjini Zanzibar.Katika maelezo yake Balozi Mfenyana alimueleza Rais Karume kuwa hatua hiyo ni somo kubwa kwa nchi za Bara la Afika ikiwemo nchi yake ya Afrika ya Kusini kwani kilichozingatiwa zaidi ni maslahi ya wananchi na nchi yao.Mfenyana alieleza kuwa Afrika Kusini itaendelea kuimarisha uhusiano na udugu wake na Zanzibar na kusisitiza kuwa hatua hiyo ina matarajio makubwa ya kupiga hatua kisiasa, kiuchumi na kijamii.Alieleza kuwa mazungumo hayo yanatoa faraja kubwa na ni imani ya kwamba Zanzibar itaendelea kupiga hatua kubwa ya katika maendeleo yake ikiwa ni pamoja na miradi ya maendeleo sanjari na kuimarisha amani na utulivu uliopo.Alisema kuwa hatua ya kukaa kwa pamoja kati ya viongozi hao imeudhiirishia ulimwengu kuwa Wazanzibari wote ni wamoja na tofauti zao za kisiasa si jambo la kuwatenganisha.Endelea kusoma habari hii

CUF KUMTAMBUA RAIS AMANI KARUME

8 11 2009

Chama Cha Wananchi (CUF) kimeregeza msimamo wake na kutangaza rasmi DSC05290kumtambua Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume.Kauli hiyo imeonekana kuwa ni mwiba kwa wanachama wa chama hicho, imetangazwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad ambapo baada ya kutangaza kauli hiyo kulizuka tafrani katika mkutano mkubwa uliofanyika Kibanda Maiti Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo mkutano huo ulikuwa umeandaliwa kwa lengo la kuelezea mazungumzo ya hivi karibuni yaliofanyika Ikulu Mjini Unguja baina yake na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume.Baada ya muda mfupi Katibu Mkuu huyo alilazimika kuteremka jukwaani ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za Zanzibar Maalim Seif alipingwa hadharani na wanachama wake ambao walikuwa na jazba na hasira kubwa.Maalim Seif amesema kutokana na hali ya kisiasa ilivyo tete hivi sasa hakuna haja ya kuendelea na msimamo wa kutomtambua Rais Karume hivyo uongozi wa baraza kuu umeamua kumtambua ili kuondosha matatizo yanayoweza kujitokeza siku za mbele katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao mwakani.“Leo asubuhi tulikuwa na baraza kuu la uongozi wa CUF na tumeona kuwa kutomtambua Mheshimiwa Karume ni zaidi nadharia kuliko hali halisi kwa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kwa maana hiyo kwa maslahi ya wazanzibari baraza kuu limeamua kumtambua Mheshimiwa Karume” alisema Maalim Seif. Huku akipigiwa kelele na wananchi hatutaki.Endelea kusoma habari hii

ZEC YASHAURIWA KUACHA KUTUMIA ZAN-ID

20 10 2009

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imeshauriwa kuachana na kitendo cha kutumia kitambulisho cha mzanzibari mkaazi katika daftari la kupigia kura ili kuweza kuepusha kutokea kwa vurugu zisizo za lazaima. Ushauri huo umetolewa jana na Katibu wa Chama UPDP, Abdallah Nassor Ali, wakati akizungumza na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa habari Maelezo Mjini Unguja, Alisema kuwa ipo haja kubwa kwa Tume kufuata utaratibu huo ambao unaonesha dhahiri kuwa ndio sababu kuu ya kuweza kuondoka kasoro ziliopo hivi sasa katika hatua za kujiandikisha katika daftari la kupigia kura visiwani Zanzibar.Hivyo alisema kuwa pindi Tume ikiacha utaratibu huo ni wazi kuwa inawezeka kuwepo na kuzidisha kwa ghasia na malalamiko ya kujiandikisha kutoka kwa wananchi pamaoja na viongzi wa vyama vya siasa. “Utaratibu wa kutumia kitambulisho cha ukaazi ZAN ID, kwa kiasi kikubwa unachangia kuwepo kwa uhasama baina ya wanasisa na hata wananchi wenyewe kwa wenyewe ambao wao ndio wahusika wakuu katika chaguzi”alisema Katibu huyo. “Vitendo hivyo vinakuja kufuatia wananchama hao pindi wakiwa hawana kitambulisho cha Uzanzibar, hivyo hulaziaka kukosa ahakia ya kujiandikisha katika daftari”alisema.Endelea kusoma habari hii

KAMATI YA MWINYI YAANZA VIBAYA ZNZ

20 10 2009

mwinyiKAMATI ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ya kuchunguza mwenendo wa vikao vya baraza la wawakilishi na mpasuko katika bunge imeanza vibaya baada ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kugomea kuhojiwa mtu mmoja mmoja na kutaka wahojiwe kwa pamoja.Uamuzi huo wa kuhojiwa mtu mmoja mmoja unaelezwa kuja ghafla wakati awali viongozi wa kamati hiyo walisema watawahoji wajumbe hao wa baraza la wawakilishi kwa pamoja na sio mtu mmoja mmojaWajumbe hao ambao wote ni kutoka Chama Cha Mapinduzi wamekutana na kamati hiyo kwa lengo la kutoa maoni yao juu ya kauli kali zilizokuwa vimetolewa katika vikao vya baraza la wawakilishi ambapo lugha kali na jazba zilitumika katika vikao hivyo.“Tumegoma kuhojiwa mmoja mmoja kwa nini watufanyie hivyo kama wanataka kutuhoji au kuchukua maoni yetu basi ni vyema watuhoji tukiwa kwa pamoja kwa sababu tabia ya kumwita mtu mmoja mmoja inaleta fitna na inaweza kusababisha tofauti kubwa kati yetu maana kwa wale woga lazima watatetereka wanapofika huko ndani wataanza kubabaika na ndio maana tukaamua tuwepo sote kama ni kutusulubu basi iwe kwa sote” alisema Mjumbe mmoja wa baraza la wawakilishi.Kamati hiyo iliwasili juzi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuwahoji wajumbe wa baraza la wawakilishi na baadhi ya viongozi wa serikali kufuatia kauli kali zilizojitokeza dhidi ya viongozi wa serikali ya muungano hasa baada ya kuelezwa kuwa zanzibar sio nchi na uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuliondosha suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano.Endelea kusoma habari hii

KHATIB AFANANISHWA NA NYERERE

18 10 2009

KIONGOZI wa Dini Padri Lucian Malamsha wa Kanisa Katoliki Zanzibar mohammed-seifamemfananisha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Rais (Muungano) Mohamme Seif Khatib na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Padri huyo amesema Khatib ndiye kiongozi hasa anayefuata muongozo na nyayo za baba wa taifa, Mwalimu Nyerere katika utumishi wake wa kulitumikia taifa la Tanzania.Tamko hilo amelitoa jana katika mkutano wa hadara alipokuwa akihutubia wananchi katika hafla ya kukabidhi nguzo za umeme zinazotarajiwa kutumika kusambaza huduma hiyo katika vijiji vya wilaya ya kati katika Jimbo la Uzi Kisiwani Unguja.Padri Malamsha alisema Waziri Khatib ametoa mchango mkubwa katika kutumikia taifa la Tanzania na ni miongoni mwa viongozi wachache walioonesha uadilifu wa kujiepusha na vitendo vya ufisadi katika jamii na hasa wakati huu ambao viongozi wengi wamekubwa na kashfa hiyo.Alisema kwamba viongozi wengi wamekuwa wakitoa ahadi, lakini baadaye hushindwa kuzitekeleza, kitendo ambacho hakileti sura nzuri na kusema kitendo cha kukabidhi nguvu za umeme ni ukombozi mkubwa katika kuwasogezea maendeleo wananchi katika vijiji hivyo.Padri huyo alimsifia Waziri Khatib ambapo alisema ameanza kumfahamu miaka mingi tokea alipokuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM taifa na ni miongoni mwa viongozi waliotoa mchango mkubwa katika kulitumikia taifa na kudumisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

KAMATI YA MWINYI KUANZA KAZI ZNZ

17 10 2009

Ally-Mwinyi-300x234KAMATI ya Kuchunguza viongozi inayodaiwa kwenda kinyume na maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo baadhi ya wawakilishi na mawaziri imeanza kazi yake zanzibar chini ya mwenyekiti wake Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.Kamati hiyo iliwasili juzi zanzibar kwa ajili ya kuwahoji wajumbe wa wawakilishi na baadhi ya viongozi wa serikali kufuatia kauli kali zilizojitokeza dhidi ya viongozi wa serikali hasa baada ya kuelezwa kuwa zanzibar sio nchi na uamuzi wa seirkali ya mapinduzi zanizbar kuliondosha suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya muungano.Timu ya Kamati hiyo ilikutana na kamati ya uongozi wa baraza la wawakilishi chini ya mwenyekiti wake waziri kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha ikiwa na wajumbe sita kutoa hali halisi ya mambo yalivyojitokeza wakati wa mjadala wa masuala hayo yalipokuwa yakijadiliwa katika baraza la wawakilishi.Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM) Zanzibar , Vuai Ali Vuai amethibitisha kamati hiyo kuwa tayari imeanza kukutana na viongozi wakiwemo wajumbe wa baraza la wawakilishi.“Kweli kamati ipo na kama walivyosema wenyewe walipokutana na waandishi wa habari wamekuja kutekeleza majukumu waliopewa na chama na watakutana na wajumbe wa baraza la wawakilishi baada ya kukutana na kamati ya uongozi wa chama”alisema Vuai.Endelea kusoma habari hii

MWAKILISHI ASEMEA KAZI YA ZAN-ID

MWAKILISHI wa Jimbo la Gando (CUF), Said Ali Mbarouk amesema kazi ya usajili wa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi hivi sasa inakwenda vizuri Said Ali Mbarouk(CUF)Gandokatika Mkoa wa Kaskazini Pemba.Hayo yameelezwa katika kikao cha pamoja kati ya viongozi wa vyama vya siasa vya CCM na CUF na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili wa Vitambulisho , Mohammed Juma Ame ambaye kwa siku ya pili hivi sasa yupo kisiwani Pemba kufanya tathmini ya kazi ya usajili wa vitambulisho hivyo ambavyo tokea kuanza kwake kumekuwepo na malalamiko makubwa miongoni mwa wananchi mbali mbali Unguja na Pemba.“Kwa kweli vitambulisho hivi vina matumizi mengi na kwa kutambua hilo mimi mwenyewe nilifanya mikutano minane ya hadhara kuwafafanulia wananchi umuhimu wa ZAN-ID na kwa ujumla mambo yanakwenda vizuri hakuna matatizo” Alisema Mwakilishi huyo.Mwakilishi huyo amesema kwamba hakubaliani na suala la kukiukwa sheria ili kuruhusu watu wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa kuweza kuandikishwa na badala yake alitilia mkazo utawala bora na kufuata misingi ya sheria ili kila mwenye haki ya kuandikishwa katika daftari aandikishwe na pia kila mwenye sifa apatiwe kitambulisho.Endelea kusoma habari hii.

CUF YATAKA GWARIDE

Salim BimaniCHAMA Cha Wananchi (CUF) kimeomba kuandaa gwaride la utambulisho la watu wasiokuwa na vitambulisho vya mzanzibari mkaazi ili kuondosha malalamiko ya usajili wa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi katika wilaya ya chake chake.Akizungumza katika mkutano wa pamoja baina ya Mkurugenzi wa Msajili wa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi, Mohammed Juma Ame na viongozi wa vyama vya siasa, katibu wa CUF wilaya ya Chake Chake, Saleh Juma, alisema kuwa ni muhimu kuwepo kwa gwaride hilo.Mkutano huo uliofanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa kusini Pemba uliokuwa chini ya uwenyekiti wa mkuu wa wilaya ya Mkoani, Jabu Khamis Mbwana viongozi wa CUF walitaka kuwepo kwa suala hilo kwa kuwa wanaamini wapo wazanzibari wengi hawana viotambulisho tofauti na takwimu zilizoendelezwa na afisa mwenye dhamana ya ZAN-ID Pemba. Walisema kwamba masheha wamekuwa vikwazo katika utoaji wa fomu na hivyo kusababisha kuwepo na idadi kubwa ya watu wasiokuwa na vitambulisho wakati kazi ya uendelezaji wa daftari la kudumu ikiendelea kuanza katika mkoa wa kusini Pemba hali inayoweza kusababisha kukosa haki ya kuandikishwa katiak daftari hilo.Endelea kusoma habari hii.

GNRC WATOTO WASITIWE KHOFU

Taasisi ya Mtandao wa Ulimwengu wa Dini kwa Ajili ya Watoto (GNRC) WATOTO KANGAGANIimesema hali ya kuwepo vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo ya shule ni khatari kwa kuwa yanaweza kuwasababishia watoto hali ya khofu na kuwakosesha amani katika masomo yao.Hayo yameelezwa na Mkurugenzi GNRC, Zameer Noorali katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyosambazwa na mara baada ya kukamilisha ziara yake yeye na ujumbe wa taasisi hiyo kisiwani Pemba kukagua hali ya usalama wa watoto ilivyo katika kipindi hiki cha uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura.“Tulishuhudia katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, hususan Wilaya ya Wete katika vituo vya uandikishaji vya Skuli za Limbani na Jadida uwepo wa kutisha wa vyombo vya dola wakati wanafunzi wakiwa madarasani katika muda wote wa masomo ambao kwa hakika unakwenda na muda wa uandikishaji” alisema Noorali.Mkurugenzi huyo aliongeza kusema kwamba “Kuwepo kwa askari kwa njia ya kudumu, wakiwa na silaha zote kama vile bunduki, mabomu ya machozi na gari ambalo tayari limepachikwa bendera nyekundu kama kwamba fujo imeshatokea- hakuwezi kuwa kwa maslahi ya mtoto ambaye hatupendi ashuhudie mambo kama haya, seuze kuwekewa katika maeneo ambayo ni ya elimu” amesisitiza katika taarifa yake kwa waandishi. Endelea kusoma habari hii.

ZEC YAMGOMEA MGOMBEA URAIS

ALIYEKUWA Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Jahazi Asilia, Mussa Abdallah Kitole amekataliwa kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapigakura kwa madai ya kutokuwa na kitambulisho cha mzanzibari mkaazi.Tukio hilo limetokea juzi katika kituo cha uandikishaji wapiga kura katika Shule ya Gamba Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo Kitole alikwenda kujiandikisha kama mpigakura katika dafatari hilo lakini maafisa wa uandikishaji walimwambia hawezi kuandikwa kwa kuwa hana sifa za kuandikwa katika daftari hilo.Msimamizi wa Unadikishaji wa wilaya ya kaskazini Unguja A, Murshid Khamis alisema kwamba kutokana na kukosekana kwa kuwa na kitambulisho cha mzanzibari mkaazi hawezi kuandikishwa na sheria ni msumeno na hakuna aliyekuwa juu ya sheria.Kitole ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa chama cha Jahazi Asilia ambapo kwa sasa ni Katibu Mkuu wa chama hicho ambacho kimejijengea uaminifu mkubwa katika Mkoa wa Kaskazini alipozaliwa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour Juma (Komandoo).Endelea kusoma habari hii

CUF YAISHITAKI TANZANIA ULAYA

kapigwaCHAMA Cha Wananchi (CUF) kimeanza harakati za kuzishawishi nchi za Jumuiya za Ulaya kuweka vikwazo kwa Tanzania kutokana na matatizo yanayojitokeza katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura linaloendelea visiwani Zanzibar.Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho, Mhene Said Rashid ambaye yupo mji wa Stockholm nchini Sweden akijaribu kuzishawishi nchi za ulaya ya kaskazini kuweka mbinyo kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya zanzibar kwa kutoheshimu demokrasia.Mjumbe huyo ambaye anatarajiwa kutembelea katika nchi za Finland, Sweden na Denmark na kuonana na wajumbe mbali mbali kwa lengo la kuzishawishi nchi hizo ambazo zinaifadhili tanznaia katika suala zima la kusimamia demokrasia nchini.Akizungumza katika Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW) jana asubuhi Rashid alisema lengo la safari hiyo ni kuzishawishi nchi zinazoifadhili Tanzania ziwache kuisaidia kutokana na kutoheshimu misingi ya demokrasia kutokana na wananchi wa zanzibar kunyimwa haki yao ya kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapigakura linaloendelea hivi sasa ambapo kikwazo kikubwa na kukosekana kwa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi.Endelea kusoma habari hii.

MRIPUKO WATOKEA WETE

mabomuSIKU moja baada ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kuwahakikishia wananachi na wageni kuwa Zanzibar ni shuwari na atakayetaka kutembelea anakaribishwa mripuko mkubwa umetokea katika nyumba moja Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.Mripuko huo umetokea majira ya saa 4 usiku katika nyumba ya Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ramadhan Issa Kipaya Mtaa wa Mtemani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba na kusababisha nyumba hiyo kuharibika eneo la kuta zake lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.Juzi katika ziara yake ya ziku mbili Kisiwani Pemba Rais Amani Karume amewahakikishia wananchi na wageni wanaotaka kutembelea katika visiwa vya Zanzibar kuwa Zanzibar ni shuwari na hakuna matatizo yoyote kama inavyokuzwa na waandishi wa habari kwamba hakukaliki.Alisema kuwa Zanzibar imekuwa ni nchi ya amani na utulivu tokea miaka ya chuma hivyo mtindo uliojitokeza katika siku za karibuni wa kuchoma moto nyumba hauna maslahi kwa wananchi na badala yake aliwataka wanasiasa waliofilisika kufunga virago na kutafuta shughuli ya kufanya.“Zanzibar kuna amani tena utulivu wa kutosha watu wanafanya shughuli zao za kawaida na tunawalika wengine pia waje kutembelea visiwa hivi na wachane na wale watu wanaosema kuwa Zanzibar hakukaliki, nyumba zaripuliwa hayo ni maneno ya waandishi tu” alisema Rais Karume.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR NI SHUWARI-KARUME

RAIS wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Amani Abeid Karume amesema hali ni shuwari Zanzibar na kuwataka ZakarumeCCwanasiasa katika Kisiwa cha Pemba kupingana kwa hoja na wale wasioweza kujenga hoja waondoke katika ulingo wa siasa.Hayo ameyaeleza wakati akizungumza katika uzinduzi wa shule ya msingi ya Wingwi Mtemani katika Mkoa wa Kaskazini Pemba jana ambapo alisema kwamba kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa kutumia jukwaa la kisiasa kwa kueleza mambo ya vitisho kutokana na kushindwa kujenga hoja za maana.“Tupingane bila kupigana kwa maana tukipingana kwa hoja ndio demokrasia kama hoja zimeisha wewe tulia tu katafute mhogo na samaki wako wa tasi ule sio kuleta vitisho” alionya Rais Karume.Alisema kuwa Zanzibar imekuwa ni nchi ya amani na utulivu tokea miaka ya chuma hivyo mtindo uliojitokeza katika siku za karibuni wa kuchoma moto nyumba hauna maslahi kwa wananchi na badala yake aliwataka wanasiasa waliofilisika kufunga virago na kutafuta shughuli ya kufanya.“Zanzibar kuna amani tena utulivu wa kutosha wau wanafanya shughuli zao za kawaida na tunawalika wengine pia waje kutembelea visiwa hivi na wachane na wale watu wanaosema kuwa Zanzibar hakukaliki” alisema Rais Karume.Kaika hatua nyengine Rais Karume alivitaka vyombo vya habari hasa vya nje ya Zanzibar kuacha kuandika mambo ya uchochezi dhidi ya Zanzibar na badala yake vifanye kazi kwa mujibu wa maadili na taaluma ya habari.Endelea kusoma habari hizi

POLISI ITEKELEZE MAJUKUMU YAKE-MWEMA

IGP%20MwemaMKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali, Said Mwema amefanya ziara ya siku mbili katika Visiwa vya Unguja na Pemba kufuatia ghasia za uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura zinazoendelea katika visiwa hivyo.Awali Mwema alikutaka na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha na kufanya nao mazungumzo kabla ya kuonana na watendaji wa jeshi hilo, wanasiasa, viongozi wa dini na viongozi wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Wakati akizungumza na Rais Amani na Waziri Kiongozi Nahodha aliwaahidi kwamba jeshi lake litafanya kazi kwa misingi ya haki na kufuata sheria zote za jeshi hilo na kuwataka viongozi kushirikiana na jeshi lake katika kuweka hali ya amani katika visiwa vya Zanzibar.Alisema suala lililojitokeza ni malalamiko ya vitambulisho vya mzanzibari mkaazi hivyo aliwaomba viongozi hao kutatua kasoro zinazojitokeza katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuepusha nchi kuingia katika machafuko kwani ikumbukwe kuleta uvunjifu wa amani ni rahisi lakini kuirejeshs hali katika mani ni kazi kubwa..Katika ziara yake hiyo ya siku moja katika kila kisiwa Mwema alitaka kujua tatizo la uvunjifu wa amani litakabiliwa vipi hasa katika kipindi hiki ch akuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo hivi sasa alisema hali imeanza kuonesha kuwa na dalili mbaya kiusalama.Alisema inaonesha amani inaanza kuharibika na aliwataka viongozi hao kuwa makini na kuvunjika kwa amani kwani kupotea kwa amani katika nchi ni kazi nyepesi lakini kuirejesha amani ni kazi kubwa na ina gharama kubwa katika nchi yoyote.Endelea kusoma habari hii.

WAKAAZI WA KANGAGANI WAINGIA MWITUNI

Wakati uandikishaji wapiga kura ukiingia katika siku yake ya tatu kwenye majimbo ya Mtwambwe na Ole, kisiwani Pemba, hali ya shaka na khofu mzeeimeendelea kutawala vijiji vya Kangagani na Ole Skuli kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni vitisho dhidi ya wakaazi wa maeneo hayo katika nyakati za usiku. Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tafauti, wakaazi wa maeneo hayo wamesema kwamba wamekuwa wakiishi katika khofu kwa siku kadhaa sasa na kwamba hawana uhakika na usalama wa mali na maisha yao hasa katika nyakati za usiku, ambapo wanadai watu wanaowaita ‘Janjaweed’ wakifuatana na askari polisi hupita majumbani mwao kuwasaka, kuwapiga na wengine kukamatwa. “Miye mume wangu ana mosi (wiki) nzima hii hajalala nyumbani. Akimbia askari. Juzi walikuja wakanigongea wakanambia nifunguwe niwagaie maji ya kunywa, ila nilipojua kuwa ni wao, nikakataa kuwafungulia. Mwisho wakanitisha kwamba watauvunja mlango, au nimwambie mume wangu atoke. Nikawambia mume wangu hayumo!” Alisema Chumu Hamad Hamad (37) wa Kangagani, mmoja wa kinamama ambao waume zao hawalali majumbani mwao kwa khofu ya usalama wao.Naye Ali Msanifu (40) wa Kangagani, ambaye amekuwa akilala katika eneo linalojuilikana kwa jina la Makaani kwa takribani wiki nzima sasa, alimwambia mwandishi wa habari hizi kwamba yeye na wenzake wanaofikia kumi na mbili hawawezi kurudi majumbani mwao kwa sasa kwani kufanya hivyo ni sawa na kifo au kujiulisha.Endelea kusoma habari hii.

UNGUJA NAKO DAFTARI LADORORA

majikaliIDADI ya wananchi wanaojitokeza kuandikishwa kuwa daftari la wapigakura wapya katika Jimbo la Tumbatu na Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja imeongezeka kidogo huku baadhi ya vituo vikikosa watu kabisa.Kituo cha Tumbatu Jongowe hakuna mtu aliyejitokeza kutaka kuandikishwa tangu zoezi hilo lilipoanza juzi ambapo baadhi ya wananchi walisema wamesusia kujiandikisha na hawatakwenda kabisa katika vituo vya uandikishaji.Sababu kubwa ya wananchi hao kusususia uandikishaji huo imeelezwa na Maafisa wa Tume ya Uchaguzi baada ya kuwahoji wananchi wa kijiji hicho, ni kutokana na kuwapo mzozo wa mipaka kati ya kijiji hicho na shehia ya Tumbatu Gomani.Maafisa hao walifahamisha tangu wameanza uandikishaji huo hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza katika kituo hicho kulikotokana na msimamo uliowekwa na wananchi wa kijiji hicho kwa vile hakuna mwanachama wa chama chochote aliyeenda kujiandikisha.Wananchi hao waliwaambia maafisa wa tume ya uchaguzi Zanzibar kwamba kamwe hawatashiriki katika zoezi lolote la uandikishaji hadi hapo viongozi wa serikali watapokaa nao kwa lengo la kufanya nao mazungumzo.Suluhu Ali ni Msimamizi wa Uchaguzi alithibitisha kwa wananchi hao kususia kwenda vituoni ambapo alisema wananchi hao wamegoma kujiandikisha katika kituo cha Tumbatu Jongowe.“Tokea kazi ya uandikishaji imeanza hakuna hata mtu mmoja aliejitokeza kituoni kujiandikisha na hilo linathibitisha kuwa wananchi wamesusia zoezi hili la uandikishaji” alisema Msimamizi huyo.Wakati wananchi hao wakiwa wamegoma kwenda kituoni hapo kituo cha Tumbatu Uvivini kumetokea purukushani na jeshi la polisi kulazimika kurusha mabomu ya machozi baada ya wananchi kukirushia mawe kituo hicho.Endelea kusoma habari hii

PEMBA SIO CHUWARI TENA

jeshiWANANCHI wa Kisiwani Pemba hivi sasa wamelalamikia hatua ya kufuatwa majumbani mwao na jeshi la polisi nyakati za usiku wakiwa na silaha mikononi kwa madai ya kuwatafuta mavunjifu wa amani.Waandishi wa habari walishuhudia idadi kubwa ya wanakijiji hao wakiwa ni wanawake na watoto ambapo walisema waume zao ndio waliokimbilia maporini kwa kuhofia usalama wao kwa kuogopa kukamatwa na jeshi hilo.“Hivi sasa waume zetu wanalala mwituni, wanakimbia majumbani mwao, waume zetu wanadhalilishwa hivi serikali inataka nini kwa waume zetu? Kwa nini sisi tu ndio tunaodhalilishwa kiasi hiki leo tunakimbiw amajumbani na waume zetu eti wanawasaka wahalifu na wavunjifu wa amani hii kweli ni haki? Alihoji Siti Omar Suleiman Mkaazi wa Kangagani.Wanawake hao wamesema wamekuwa wakilala na khofu kwa kuwa wana watoto wadogo na hawajui kitu gani kitatokea katika kijiji hicho kutokana na matumaini ya usalama kutoweka katika siku za hivi karibuni katika kijiji hicho.“Tuligongewa mlango usiku sana na tukaambiwa tufungue mlango tulipouliza tukaambiwa nyinyi funguweni huo mlango na kama hamjafungua mtakiona lakini hapo kila mmoja alikuwa akiogopa” alisema Mama mmoja Salama Mohammed akiwa amebeba mtoto wake mgongoni.Baadhi ya wanakijiji waliotoweka katika kijiji hicho ni pamoja na Hassan Abdallah, Jamal Juma, Mussa Bakari, Ali Msanifu Hassan Ali na Said Nyange.Wananchi hao walimshutumu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kuhusika na matukio ya kamatakamata kutokana na kutoa amri kwa jeshi la polisi la kutafutwa baadhi ya wafuasi wa upinzani na kukamatwa.Endelea kusoma habari hii

CCM NA CUF WAHUJUMIANA PEMBA

tumbatuTABIA ya Wafuasi wa Vyama vya siasa Kisiwani Pemba kufanyiana vitendo vya hujuma bado inaendelea ambapo sasa imehamia katika kuhujumu mifugo.Katika matukio mawili yaliyotokea juzi na jana katika Jimbo la Ole, Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Kombo Hamad Yussuf, banda lake la kuku zaidi ya 100 wamechomwa moto na watu wasiojulikana.Tukio kama hilo pia limemkumba Kiongozi wa Chama Cha Wananchi (CUF) Ali Salim Mussa ambaye kama ilivyo kwa Kiongozi wa CCM naye kuku wake wameteketezwa kwa moto katika banda lake la kuku.Akizungumzia matukio hayo, Mkuu wa Wilaya ya Wete, Omar Khamis Othman alisema hujuma hizo zimetokea usiku wa manane eneo la Makaani nje kidogo ya Kijiji cha Kangagani katika Jimbo la Ole ambapo kazi ya uboreshaji wa daftari la kudumu linaendelea kwa kusua sua.Mkuu huyo wa Wilaya amesema kwamba matukio yote mawili ni ya kisiasa hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa Jimbo la Ole uandikishaji wapigakura katika daftari la kudumu bado unaendelea.Endelea kusoma habari hii

CCM YAIPONGEZA ZEC

ferouzCHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kusimamia sheria kwa kuendelea na kazi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura katika Mikoa ya Kaskazini Pemba na Kaskazini Unguja.Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz ameyasema hayo katika ziara yake ya siku moja ya kuwapa pole wana CCM waliofika na matatizo yanayotokana na kuchomewa nyumba zao na kushambuliwa.Alisema licha ya kuwepo kwa shinikizo kutoka kwa Chama cha CUF kutaka Tume ya Uchaguzi kusitisha kazi ya uandikishaji, lakini ZEC wanaendelea na kazi kama kawaida kwa sababu suala la kujiandikisha ni la mtu binafsi.“Kwa hili tunawapongeza sana ZEC kwa kutowasilikiza wale wanaotaka kusitishwa kwa kazi ya uandikishaji hatuoni kama kuna sababu za msingi za kukataa shughuli hiyo isiendelee” alisema Ferouz.Alisema kwamba daftari la kudumu la wapigakura limeanzisha kwa mujibu wa sheria ambapo tume kulingana na tariba iliyojipangia ya uboreshaji wa daftari hilo halitakuwa rahisi kukubaliana na hoja za kambi ya upinzani kwa sababu uandikishaji unahusu mambo mengi ikiwemo uhamishaji wa taarifa za vifo kwa wapigakura ambao walikuwepo katika daftari.Endelea kusoma habari hii

UANDIKISHAJI WAENDA POLE POLE

KAZI ya kuandikisha wananchi katika daftari la wapiga kura linaendelea FFU Pembahuku idadi ndogo ya wananchi wanaojitokeza katika vituo vya uandikishaji vilivyopo Mkoa wa Kaskazini Pemba.Wananchi hao waliojitokeza majira ya asubuhi baada ya vituo hivyo kufunguliwa jana huku idadi yao ikiwa ndogo ambapo wameanza kutumia mbinu mpya ya kufika katika vituo hivyo kwa kutumia gari za daladala na kuteremka katika vituo vya uandikishaji tofauti na siku za nyuma ambapo wakiteremshwa na magari maalumu chini ya ulinzi mkali.Mwananchi imeshuhudia wafanyakazi wa kike wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) wakiwa wamekaa nje ya vituo hivyo na kushina kofia wakidadi kukosa kazi za kufanya kutokana na kukosekana watu wanaofika kujiandikisha.Kwa mujibu wa maafisa wa ZEC wamesema wamekuwa wakitumia muda mwingi kukaa bila ya kazi kuliko muda wanaofanya kazi katika vituo hivyo na kulalamikia zoezi hilo ambalo lmedorora tokea kuanza kwa awamu hii ya pili 12 mwezi huu.“Hatuna kazi za kufanya tusiposhona kofia tufanye nini wakati hali ya masiaha katika kisiwa chetu mnaoina watu wanashindwa hata kununua futari, hapa masiaha magumu sana lazima mjue hilo” amesema mwandishi mmoja wa tume hiyo nje ya kituo hicho.Tokea kuaza kwa zoezi hilo katika kituo cha Kiuyu Minungwini watu waliojiandikisha ni 75, Kituo cha Kambini jumla ya watu 112 huku idadi kamili ya vituo vyengine ikiwa haijapatikana kutokana na maafisa wa tume hiyo kukataa kutoa kwa wanadishi wa habari.Endelea kusoma habari hii.Endelea kusoma habari hii

TUMEVUKA MALENGO –MKURUGENZI

MKURUGENZI wa usajili wa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi, Mohammed Juma Ame amesema ofisi yake hivi sasa imevuka lengo kwa kutoa jumla ya vitambulisho 156,301 karika Kisiwa cha Pemba.Akizungumza kwa njia ya simu Mkurugenzi huyo amesema watu waliondikishwa hadi sasa ikiwa ni zaidi ya malengo yaliowekwa ya kuandikisha watu 155,000 hadi kufikia mwaka 2010.Amesema kwamba idadi hiyo ya watu ni kubwa na kuwa suala la vitambulisho upatikanaji wake sio tatizo kwa sababu wananchi wanaendelea kusajiliwa katika ofisi za wilaya na kwa masheha kwa kufuata utaratibu zilizowekwa.Wakati Mkurugenzi akitoa takwimu hizo Kisiwani Pemba Mwananchi imeshuhudia mamia ya watu wakiwemo vijana na wazee wenye umri mkubwa wakiwa nje ya ofisi ya vitambulisho iliyopo Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba wakilamikia kukoseshwa vitambulisho hivyo licha ya kufuata masharti yote yanayotakiwa.“Sisi tunachofanyiwa hapa ni dhulma kwa sababu hakuna sababu yoyote ya sisi kunyimwa nyinyi waandishi hebu tizameni hivi vyeti vyetu vya kuzaliwa vina kasoro gani, lakini tumekwend atunaambiwa vyeti hivi havifai wakati tumepewa huko katika ofisi ya usajili wa vizazi na vifo sisi kosa letu lipo wapi? Wamesema wananchi hao ambao walikuwa wamezongea katika ofisi ya vitambulisho mkaazi.Idadi kubwa ya vijana imekuwa ikilalamikia zoezi hilo la utoaji wa vitambulisho wakidadi kuna mbinu za kisiasa zinazofanywa na serikali kwa kuwakosesha kuwapatia vitambulisho licha ya kufuata taratibu zote zilizowekwa.Endelea kusoma habari hii

UANDIKISHAJI WAPWAYA KASKAZINI PEMBA

daftariZOEZI la kuandikisha wananchi katika daftari la wapiga kura linaendelea huku idadi ndogo ya wananchi wanaojitokeza katika vituo vya uandikishaji vilivyopo Mkoa wa Kaskazini Pemba.Wananchi hao waliojitokeza majira ya asabuhi baada ya vituo hivyo kufunguliwa jana huku idadi yao ikiwa ndogo ambapo wameanza kutumia mbinu mpya ya kufika katika vituo hivyo kwa kutumia gari za daladala na kuteremka katika vituo vya uandikishaji tofauti na siku za nyuma ambapo wakiteremshwa na magari maalumu chini ya ulinzi mkali.Mwananchi imeshuhudia wafanyakazi wa kike wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) wakiwa wamekaa nje ya vituo hivyo na kushina kofia wakidadi kukosa kazi za kufanya kutokana na kukosekana watu wanaofika kujiandikisha.Kwa mujibu wa maafisa wa ZEC wamesema wamekuwa wakitumia muda mwingi kukaa bila ya kazi kuliko muda wanaofanya kazi katika vituo hivyo na kulalamikia zoezi hilo ambalo lmedorora tokea kuanza kwa awamu hii ya pili 12 mwezi huu.“Hatuna kazi za kufanya tusiposhona kofia tufanye nini wakati hali ya masiaha katika kisiwa chetu mnaoina watu wanashindwa hata kununua futari, hapa masiaha magumu sana lazima mjue hilo” amesema mwandishi mmoja wa tume hiyo nje ya kituo hicho.Tokea kuaza kwa zoezi hilo katika kituo cha Kiuyu Minungwini watu waliojiandikisha ni 75, Kituo cha Kambini jumla ya watu 112 huku idadi kamili ya vituo vyengine ikiwa haijapatikana kutokan ana maafisa wa tume hiyo kukataa kutoa kwa wanadishi wa habari.Endelea kusoma habari hii

MAREKANI INA MKONO WA VURUGU-SMZ

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imedai fujo zinazoendelea hivi Hamza Hassan Juma(CCM)sasa kisiwani Pemba ni mpango maalumu na wa muda mrefu wa serikali ya Marekani.Kauli hiyo ya kulishutumu taifa kubwa duniani imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya kituo cha uandikishaji cha shule ya Sizini mkoami Kaskazini Pemba.Mwishoni mwa mwezi uliopita, Marekani ilitoa taarifa kwa raia wake ikiwataka kuwa makini na safari za kisiwani Pemba ambako ilisema kuna vurugu zinazohusiana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.Marekani, ambayo ina tabia ya kutahadharisha raia wake kufanya ziara sehemu ambazo kuna ama kunaweza kutokea vurugu, ilieleza kuwa tangu kuanza kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura, kumekuwa na vurugu kubwa kisiwani Pemba na kuwaonya raia wake kuwa makini na mikusanyiko wawapo visiwani Zanzibar, huku ikiwataka wajiandikishe kwenye ubalozi wake mara watakapowasili Tanzania.Lakini SMZ ilijibu vikali taarifa hiyo ya tahadhari kwa raia wa Marekani na jana Waziri Juma alieleza msimamo wa serikali yake kuhusu kitendo hicho cha Marekani.“SMZ inaamini kwamba Marekani ilikuwa inajua nini kitatendeka katika kisiwa chaPemba na ndio maana ikaanza kutoa tahadhari kwa wananchi wake mapema,” alisema Waziri Juma ambaye alisema ametumwa na serikali kwenda Pemba kuangalia hali ya usalama.“Haiwezekani Marekani iwatake wananchi wake wasitembelee kisiwa cha Pemba halafu iwe haijui nini kitatokea katika kisiwa hicho.Endelea kusoma habari hii

HATUENDESHWI NA WANASIASA-POLISI

JESHI la Polisi kisiwani Pemba limejibu tuhuma za CCM kuwa linafanya kazi kwa kukipendelea chama cha upinzani cha CUF, ikisema kuwa inafuata misingi ya sheria.Mjumbe wa Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM, Zainab Khamis Shomari bugialiwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita akisema kuwa chama chake hakina imani tena na polisi wa kisiwani Pemba kwa kuwa idadi kubwa ya askari wamejiingiza katika siasa kwa kuishabikia CUF.Alisema kutokana na polisi wengi kujiingiza kwenye ushabiki wa vyama, inakuwa vigumu kwao kufanya kazi kwa haki na kwamba suala hilo si siri tena kwa kuwa liko wazi.Jana kwa nyakati tofauti, makamanda wa polisi wa mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba walisema taarifa ya kada huyo wa CCM ni potofu na imelenga kuchafua jina zuri la Jeshi la Polisi kisiwani Pemba ambalo alisema hivi sasa linafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na jamii.Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini, Said Salum Malekano alisema Shutuma zilizotolewa na mjumbe huyo wa CCM ambaye pia katibu wa chama hicho wilaya ya Chake Chake, hazina msingi.“Kama tunaonekana sisi ni mashabiki wa CUF kwa kuwa hatukutumia nguvu, huo ni mtazamo wake lakini sisi kama Jeshi la polisi hatutatumia nguvu mahali ambako hapastahili na badala yake tutatumia misingi ya kisheria katika kutekeleza majukumu yetu,” alisema Malekano.Endelea kusoma habari hii

POLISI YARUSHA MABOMU YA MACHOZI

polisi pbaJESHI la Polisi Kisiwani Pemba limelazimika kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwepo karibu ya eneo la vituo vya uandikishaji wapiga kura katika daftari la kudumu.Tukio hilo limetokea majira ya saa 6:00 asubuhi katika kituo cha Kambini Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya wananchi kujikusanya nje ya vituo ambapo walitakiwa kuondoka kwa kwenda katika vituo vya kujiandikisha au kuingia ndani ya nyumba zao na sio kukaa nje ya nyumba na kusubiri kinachotokea.Tokea kuanza kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura katika daftari la kudumu wananchi wananchi hao wamegoma kusogea katika vituo na kujiandikishia na badala yake wamekuwa wakikaa mbali na vituo hivyo kwa madai kwamba hawana vitambulisho vya mzanzibari mkaazi.Kwa mujibu wa wananchi walizungumza na Mwananchi wamesema hawawezi kujiandikisha katika daftari wakati wenziwao wengi hawana kadi za uzanzibari mkaazi jambo ambalo wamesema wataendelea kukaa nje ya vituo hivyo hadi hapo watakapopewa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi.Endelea kusoma habari hizi.

UANDIKISHAJI WADORORA PEMBA

daftariUandikishaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu katika Mkoa wa Kaskazini Pemba umeanza huku watu wachache wakijitokeza katika vituo hivyo kwa madai ya kuzuwiwa na watu wasiojulikana kwenda kujiandikisha.Mwananchi Jumapili imeshuhudia wananchi wachache mno wakiitikia wito wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) iliyowataka kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha katika vituo mbali mbali katika Jimbo la Ole wilaya ya Wete.Katika kituo cha uandikishaji cha Kiuyu Minungwini wananchi walikwenda kujiandikisha katika siku ya kwanza ya kusajili wapiga kura wapya kulingana na ratiba ya tume ya uchaguzi ambapo kesho na kesho kutwa ni siku ya kubadilisha vitambulisho vya kupigia kura kwa wapiga kura wa zamani.Ulinzi mkali umeimarishwa katika vituo vyote vya uandikishwaji huku wananchi wakiwa wamejikusanya vikundi kando ya mita 200 kutoka katika vituo hivyo huku vikosi vya serikali ya mapinduzi zanzibar vikiwa vimesimama na silaha nzito nje ya vituo hivyo.Katika kituoc ha Kiuyu Minungwini watu waliojiandikisha hadi saa 6 mchana walikuwa ni 18 huku kituo cha Kambini Mchanga Mdogo wakiwa wamejiandikisha watu saba huku matukio ya kurushiana mawe yakiwa wametanda lakini katika tukio hilo hakuna mtu aliyejeruhiwa.Endelea kusoma habari hizi

SERIKALI HAITAFUTA VITAMBULISHO

leoRAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume amesema Serikali haitafuta matumizi ya vitambulisho vya mzanzibari mkaazi kama kigezo moja wapo cha kuandikishwa kuwa mpiga kura kama ilivyopendkezwa na wapinzani visiwnai hapa.Kauli hiyo ya Rais Karume imekuja siku chache baada ya wapinzani kulamikia zoezi la utoaji wa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi kwa madai ya kutolewa kwa misingi ya kisiasa jambo ambalo baadhi ya wananchi hukoseshwa kupewa na kusababisha kukataliwa kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura lililoanza jana Kisiwani Pemba baada ya kuakhirishwa mwezi uliopita.Rais Karume ameyasema hayo katika mikutano yake na wazee wa Chama cha Mapinduzi wa Matawi na Maskani za Chama hicho katika Mkoa wa Kusini Pemba jana kabla ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili kisiwani hapa.Alisema watu wasiokuwa na sifa wasahau kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwani hatua ya Serikali ni kuondosha malalamiko katika Uchaguzi kwa kuwepo mamluki.Endelea kusoma habari hizi.

MAALIM SEIF NI MBINAFSI-MKUU WA MKOA

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi ametoboa siri kwamba suala la Chama cha CUF kupinga daftari la kudumu la wapigakura si la DADIChama hicho bali ni la ubinafsi wa Katibu Mkuu wake, Seif Shariff Hamad anayehofikia kushindwa Uchaguzi Mkuu kwa mara ya tano mfululilo akiwa ndani ya CCM na nje ya Chama hicho.Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake jana, Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba Wabunge wengi na Wawakilishi wa Chama hicho ambao hakuwa tayari kutaja majina yao alisema wamemkuwa wakichoshwa na msimamo huo wa kibinafsi wa Katibu Mkuu wao unaoangalia zaidi utashi wa kutaka Urais badala ya kujali maslahi ya walio wengi.“Wabunge na Wawakilishi wa CUF hawana matatizo, mie wamekuwa wakiniambia wazi wazi kwamba wao hawana wasi wasi na kutetea ushindi wao, lakini wamekuwa wakipata shinikizo kutoka kwa Maalim Seif anayekhofia kupata kura chache cha Urais wa Zanzibar” Alibainisha Mkuu huyo wa Mkoa.Dadi alisema ushindi wa Maalim Seif katika Uchaguzi Mkuu ujao ni ndoto na kwa kutambua hilo ndio maana amekuwa akishawishi Chama chake kipinge uendelezaji wa daftari la kudumu akiamini mwaka 2010 ndio mwaka wake wa mwisho wa kuwa mgombea asiyeshinda kwa vipindi tofauti.Endelea kusoma habari hii

CUF KUFANYA MAANDAMANO

PICT0078CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimeandaa maandamano makubwa kwa wafuasi wake katika kisiwa cha Pemba kwa lengo la kupinga kuanza tena kwa uandikishaji wapiga kura katika daftari la kudumu unaotarajiwa kufanyika kesho.Maandamano hayo yamekuja siku chache baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutanagza siku ya uandikishaji wapiga kura katika daftari kufanyika siku ya jumamisi ambapo CUF imesema maandamano hayo yatafanyika kwa wilaya zote nne na yanatarajiwa kuwashirikisha wananchi mbali mbali katika mikoa yote miwili ya kisiwa hicho.Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed aliwaambia waandishi wa habari kwamba chama chake kimekusudia kufanya maanadamano hayo kwa ajili ya kupinga uandikishaji huo wa watu katika daftari la kudumu.“Tumeamua kufanya maandamano siku ya Jumamosi kupinga uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuhusu kuanza tena kwa uandikishaji…kwani kuna watu wengi hawana vitambulisho na sisi hatujashirikishwa kufikia uamuzi huo tunaona bado mapema kuandikishwa watu wakati suala hili bado halijamalizwa” alisema Mohammed.Endelea kusoma habari hii.

TUME YA HAKI ZA BINADAMU KWENDA PEMBA

TUME ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora ikiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Ramadhan Manento inaanza ziara ya siku nne katika kisiwa cha Pemba kwa ajili ya kuchunguza na kujuwa kiini cha matatizo ambayo yamepelekea kusimama kwa shunguli za uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento amesema kutokana na taarifa kupitia vyombo vya habari wamelazimika kufanya ziara ili kubaini kama kuna viashiria vya uvunjaji na ukiukaji wa haki za binaadamu na utawala bora.Tayari ujumbe wa Tume hiyo umekutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi Hamza Juma Hassan Mkurugenzi wa ZEC Khatib Mwinchande na Mkuu wa Idara ya Vitambulisho Mohamed Juma Ame kwa lengo la kubaini kiini cha watu kutoandikishwa na kususuia zoezi hilo kisiwani Pemba.Jaji Manento alisema moja kati ya jukumu la Tume ni kulinda ,kuendeleza na kuhifadhi haki za binadamu katika kutekeleza majukumu hayo pia hutoa elimu,kushauri na kufanya na utafiti ikiwa ni pamoja na kuchunguza jambo lolote ambalo lipo katika mamlaka yake iwapo jambo lenyewe matokeo yake au moja kwa moja huvunja haki za binadamu na kukiuka misingi ya utawala bora.Endelea kusoma habari hii

SMZ KUMSHITAKI MAALIM SEIF

Seif%20SharrifSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imo katika mchakato wa kumshtaki Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF), Seif Shariff Hamad kwa kutoa madai ya kuandikishwa watu vitambulisho vya Uzanzibari Mkuranga na Mkoani Tanga.Akizungumza na waandishi wa habari Mjini hapa jana, Mkurugenzi wa Idara ya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari, Mohammed Juma Ame alisema shutuma hizo ni nzito na wanampata Kiongozi huyo kuthibitisha.“Kwa kweli ni madai mazito na kwa kuzingatia hilo tunamtaka athibitishe, vyenginezo tunampeleka Mahakamani…hivi sasa tumo katika mchakato wa kusubiri ushauri wa wanasheria, tutampeleka Mahakamani akathibitishe” Alisema Mkurugenzi Ame.Alisema Idara yake inafanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na kusisitiza madai yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad hayana usahihi wowote zaidi ya kuipaka matope Idara yake.Msimamo huo wa Serikalim umekuja siku chache baada ya Kiongozi huyo kudai kuwa kumekuwa na kazi inayofanyika katika maeneo ya Mkuranga Mkoani Pwani ya kusajili vitambulisho waytu wasiokuwa na sifa pamoja na Mkoa wa Tanga.Endelea kusoma habari hii

WANANE WAFIKISHWA MAHAKAMANI PEMBA

WATU wanane wakazi wa Kijiji cha Kiuyu Minungwini Mkoa wa Kaskazini Pemba wamefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kukutwa na fomu za vitambulishokughushi za Idara ya usajili Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.Watu hao walifikishwa Mahakamani jana mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mkoa Kaskazini Pemba, Makame Khamis wakituhumiwa kujipatia usajili huo kinyume na kifungu 312 cha sheria ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya mwaka 2004.Mwendesha mashtaka kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, Abdallah Issa Mgongo ameiambia Mahakama kwamba watuhumiwa hao Agosti 18 wakiwa katika Afisi ya Usajili wa Vitambulisho ya Wilaya ya Wete waliwasilisha fomu za kughushi kwa nia ya kutaka kupewa kitambulisho.Walishtakiwa ni Shamte Hamad(19), Bakar Khamis Haji(18), Bakar Hamad Ali(20), Fatma Ali Nassor(20), Fatma Malik Bakar(20), Saada Ali Pandu(22), Fatma Mohammed Ali(18) na Sophia Said Salum(18).Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande hadi Septemba 2 wakati kesi hiyo itakapotajwa tena ambapo Mahakama itazingatia pia ombi la upande wa utetezi la kutaka watuhumiwa hao kupewa dhamana.Endelea kusoma habari hii

HATUNA IMANI NA POLISI-CCM

nmbwiziWAKATI Tume ya Uchaguzi Zanzibar, ikitangaza kuanza tena kwa kazi ya uendelezaji wa daftari la kudumu la wapigakura katika Mikoa ya Kaskazini Pemba na Unguja, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa shutuma nzito kwa Jeshi la Polisi kwa askari wake wengi Kisiwani Pemba kushabikia Chama cha CUF.Akizungumza Mjini Chake Chake jana, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ta CCM Taifa kupitia Mkoa wa Kusini Pemba, Zainab Khamis Shomari alisema kwamba hakina imani na askari Polisi kwa sababu kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakifanya kazi kwa misin gi ya itikadi za kisiasa.“Hakuna siri tena ni jambo ambalo kila aliyeko Pemba analijuwa, askari Polisi wamekuwa washabiki wakubwa wa CUF na ndio maana utendaji wa kazi zao unakuwa mgumu kwa kuingiza ushabiki wa kisiasa katika kazi” Alisema Mjumbe huyo wa NEC mbaye pia ni Katibu wa CCM, Wilaya ya Chake Chake katika Mkoa wa Kusini Pemba.Katibu huyo alisema kwamba ni jambo la kusononesha kuona watumishi wa Jeshi la Polisi kutingwa na siasa huku wakitelekeza majukumu yao ambayo kimsingi hawapaswi kujiingiza katika masuala hayo na kumtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema kuichukulia hali hiyo kwa umakini wa hali ya juu.Endelea kusoma habari hii

VYAMA VYAJIANDAA KUISHITAKI ZEC

BAADHI ya Vyama vya siasa vimepanga kufungua kesi chini ya hati ya dharura kuishtaki Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) kwa kuvikumbatia Vyama vya CCM na CUF kiasi cha kuvunja misingi ya demokrasia kwa IMG_0386kitendo cha Tume hiyo kusitisha uandikishaji wapigakura katika daftari la kudumu Kisiwani Pemba.Wakizungumza Mjini Chake Chake jana, Viongozi hao wa vyama vya Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), National League for Democracy(NLD), Chama cha Muungano wa Wakulima Tanzania(AFP) wamesema maandalizi yote muhimu yameshakamilika na wakati wowote kuanzia wiki hii watafungua kesi hiyo.Hatua hiyo inaweza ikauingiza Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2010 katika dosari kubwa ikiwa kesi hiyo itaanza kuunguruma ambapo kikawaida huchukua muda mrefu.Wakati hatua hiyo ikijitokeza, Viongozi wa Serikali Kisiwani Pemba wameilalamikia ZEC kwa kushindwa kuendelea na kazi ya uendelezaji wa daftari la kudumu bila kuwepo kwa sababu za msingi.Uamuzi huo wa vyama hivyo umechukuwa ikiwa ni siku kadhaa kupita tangu ZEC kutoa tamko la haitaendelea na kazi ya uandikishaji hadi vyama vya CCM na CUF vitakapokubaliana juu ya uandikishaji huo ambao ulisimama katika Jimbo la Ole Mkoa wa Kaskazini Pemba.Endelea kusoma habari hii

MWAKILISHI AKATAA KUTOA MAELEZO POLISI

MWAKILISHI wa Jimbo la Chonga, Abdalla Juma Abdalla (CUF) amegoma kutoa maelezo Polisi juu ya tuhuma za kumshambulia kwa matusi ya nguoni, Sheha wa Shehia ya Pujini, Khamis Uledi Kombo mbele ya hadhara ya watu katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Kisiwani Pemba., “Niliitwa Polisi siku ya Jumatano, nikakutana na RCO(Mkuu wa Upelelelezi Mkoa) akinitaka nitoea maelezo…mimi nikamwambia sitoe, maelezo yangu nitayatoa Mahakamani” Alisema Mwakilishi huyo alipokuwa akizungumza jana akiwa Jimboni kwake Pujini.Mwakilishi huyo alisema tuhuma anazodaiwa kufanya hazina ukweli wowote na anadhani kuwa Sheha anachuki naye kwani imekuwa ni kawaida kila unapokaribia Uchaguzi kumzulia jambo “ Sheha huyu mimi simfahamu hasa anataka nini kwangu, huyu mwaka 2000 alinizushia jambo ambalo mimi sikulifanya” Aliongeza.Alisema maelezo ya Sheha Kombo ni ya uongo na atathibitisha Mahakamani kuwa hayakuwa sahihi kwani tuhuma hizo ni mwendelezo wa kile alichodai kuwa ni ajenda binafsi dhidi yake “Hii ni kesi ya tatu inayofanana na hiyo ambazo zote zinamuhusisha yeye pamoja na Sheha huyu wa Pujini” Alisema Mwakilishi huyo.Alisema kwamba Sheha huyo amekuwa akimfuata fuata na akijinasibu mbele za watu kwamba atahakikisha anamfunga jela hivyo alisisitiza kuwa ataendelea kutetea haki za watu bila kuogopa vitisho vya Sheha.Endelea kusoma habari hii

MWAKILISHI WA CUF KUBURUZWA MAHAKAMANI

Abdallah Juma Abdallah(CUF)ChongaMWAKILISHI wa Jimbo la Chonga(CUF), Abdallah Juma Abdallah, anatarajiwa kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumshambulia matusi ya nguoni Sheha waShehia ya Pujini, Khamis Uledi Kombo katika Wilaya ya Chake Chake wakati wa kazi ya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi Kisiwani Pemba. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Said Salum Malekano alisema jana Mjini hapa kwamba kimsingi taratibu zote zimekamilika ikiwa pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutokuwa na pingamizi dhidi ya mashtaka ya Mwakilishi huyo.Mwakilishi huyo ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar anatuhumiwa kumtukana matusi ya nguoni Sheha Kombo ambaye baada ya tukio hilo alikwenda kutoa ripoti Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.“Sheha baada ya kushambuliwa kwa matusi ya nguoni na Mheshimiwa Mwakilishi aliamua kuja Polisi kutoa ripoti hiyo na sisiTulipokwenda katika eneo la tukio katika Afisi za Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake mtuhumiwa alikuwa ametoweka” Alisema Kamanda Malekano.Kamanda Malekano alisema kwamba tukio hilo limetokea Agosti 18 mwaka huu katika Afisi za Wilaya za Usajili wa Vitambulisho ambapo Mwakilishi huyo alidaiwa kutaka kupewa fomu mtu ambaye Sheha alikuwa akiamini kutokuwa na sifa za kupatiwa kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.Endelea kusoma habari hii

WATOTO WATUMIWA KATIKA UANDIKISHAJI

MBINU mpya ya kuwatumia watoto wadogo kupata Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi imeibuka Kisiwani Pemba ambapo saini za Wakuu wa GetAttachmentWilaya na mihuri ya Serikali inatumika.Hali hiyo imefanya mwanafunzi wa kidato cha tatu, Nuru Nassor Ali kuhukumiwa na Mahakama ya Mkoa wa Kaskazini kwenda jela kwa muda wa wiki mbili baada ya kupatikana na hatia ya kughushi cheti cha kuzaliwa.Wakizungumza kwa nyakati tofauti Kisiwani hapa juzi, Wakuu wa Wilaya ya Chake Chake na Wete walisema kuna mtindo mpya umebuniwa wa kuwatumia watoto wadogo kuwatengenezea vyeti vya kughushi kwa lengo la kuongeza wapigakura.Mkuu wa Wilaya ya Wete, Omar Khamis Othman aliwaambia waandishi wa habari Afisini kwake kuwa hadi jana walifanikiwa kugundua vyeti 70 vya watu mbalimbali walioghushi tarehe na mwaka wa kuzaliwa, sahihi yake huku ikionesha alisaini mwaka 1986 mwaka ambao yeye hakuwa Mkuu wa Wilaya.Mkuu huyo wa Wilaya aliteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Amani Abeid Karume mwaka 2006, lakini idadi kubwa ya watoto waligundulika na vyeti vya kughushi vikionesha wamezaliwa kati ya mwaka 1987, 1988,1989 na kuendelea huku vikiwa na saini yake.Endelea kusoma habari hii

WANANCHI WAKUSANYIKA KWA MKUU WA WILAYA

umatiWANANCHI mbali mbali jana asubuhi walikusanyika na kuvamia Afisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Idara ya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari wakishinikiza kusajili kupatiwa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.Wafuasi hao wa CUF walianza kujikusanya majira ya saa 1:00 asubuhi wakitokea Vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Chake Chake hukun wengine wakishushwa katika magari aina ya Fuso ambao wengi wao walikusanyika Afisi ya Wilaya ya CUF kabla ya kuelekea Afisi ya Vitambulisho. Katika Afisi ya Mkuu wa Wilaya, makundi ya watu hao idadi kubwa wakiwa vijana walisikika wakisema kuwa hawataondoka hadi Serikali itakaposikiliza na kutekeleza madai yao ya kupatiwa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.Hali hiyo ilisababisha askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kuimarisha ulinzi katika maeneo ya Mji wa Chake Chake.Wakati wakifanya maandamano, mitaani kulionekana magari yaliyokuwa na askari wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Ghasia (FFU) na yale ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yakiimarisha doria kuhakikisha hakuna madhara yatakayotokea.Endelea kusoma habari hii

MSIWE NA WASI WASI -KARUME

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume amewatoa wasi wasi Mabalozi wa Umoja wa nchi za Ulaya, amani karumeMarekani, Canada na wengineo juu ya zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya ukaazi pamoja na Daftari la Kudumu la Wapiga kura.Rais Karume aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Mabalozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Canada, Marekani na wengineo.Rais Karume aliwahakikishia Mabalozi hao kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendeleza juhudi za kuhakikisha kuwa wananchi katika Majimbo yote ya Pemba yaliyoanza uandikishaji wanaandikishwa kwa mujibu wa Sheria na taratibu zilizopo.Katika maelezo hayo Rais Karume aliwaondoa hofu na wasiwasi waliokuwa nao Mabalozi hao juu ya zoezi la uandikishaji wa Daftari la Kudumu lililokuwa likiendelea kisiwani Pemba sanjari na zoezi endelevu la uandikishaji na upatikanaji wa vitambulisho vya ukaazi.Wakizungumza katika Mkutano huo Mabalozi hao walieleza kuridhishwa kwao na maelezo waliyopewa sanjari na elimu walioipata kutoka kwa Rais Karume.Rais Karume, alieleza kuwa taratibu za kuwepo kitambulisho cha ukaazi pamoja na matumizi yake zimewekwa kisheria na kukubaliwa na pande zote mbili katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Endelea kusoma habari hii.

VIPEPERUSHI VYASAMBAZWA PEMBA

raisikikweteWATU wasiojulikana wamesambaza vipeperushi katika maeneo mbali mbali kisiwani Pemba vyenye ujumbe wa kuwataka watu wenye kuweka vikwazo kwa wananchi kujiandikisha wajitayarishe mwaka 2010 utakuwa ni wenye mateso kwao ikiwa wataendelea kuwapinga watu wanaotaka vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.Afisa Tawala wa Wilaya ya Wete, Khamis Juma Silima alisema tayari wamepokea taarifa za kuwepo kwa kundi hilo lenye kusambaza vipeperushi ambapo vyombo vinavyohusika vinalifanyia kazi suala hilo.Alisema kwamba uchunguzi wa kina unafanyika kuhusiana na kundi hilo kabla ya hatua kuchukuliwa na watakaopatikana na hatia watachukuliwa sheria kali dhidi yao kwa kuendesha vitisho dhidi ya wananchi ambapo lengo alisema ni masheha.Afisa huyo alisema kwamba kundi hilo limeundwa kwa dhamira ya kufanya vitendo vya hujuma ambapo tayari wameanza kuwatisha baaadhi ya Masheha kutokana na msimamo wa viongozi hao katika kusimamia sheria ya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.Amesema Afisa Tawala huyo alisema kuwa kundi hilo ndilo linalohusishwa na kumwagia tindikali Sheha Mussa Kombo Omar ambaye ilibidi apelekwe kwa matibabu zaidi Unguja.Mbali ya hatua hiyo, kundi hilo linahusishwa na kufanya vitendo vya kutaka kuhujumu kazi ya usajili na utoaji vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi na hivi karibuni limetoa vitisho kwa kumwandikia vipeperushi Sheha wa Shehia ya Kambini, Ali Said Ali.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Saleh Bugi alisema kwamba Polisi inatoa onyo kali kwa mtu yeyote au kikundi kinachotaka kufanya vitendo vya uvunjifu wa sheria na kwamba wanafuatilia suala hilo.Endelea kusoma habari hii.

ULINZI MKALI WAIMARISHWA PEMBA

JESHI la Polisi Kisiwani Pemba limelazimika kuimarisha ulinzi kutokana na mamia ya wananchi kukusanyika nje ya Afisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chake p12Chake, Idara ya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari wakishinikiza kupatiwa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.Wananchi hao walianza kujikusanya majira ya saa 1:00 asubuhi jana wakitokea mitaa mbali mbali ya Wilaya ya Chake Chake huku kadiri saa zinavyozidi ndivyo wananchi hao wanavyoongezeka kuteremka katika malori aina ya Fuso ambao wengi wao walikusanyika barabarani kabla ya kuelekea Afisi ya Vitambulisho ambako ndio kulipokuwa kumefurika. Jeshi la Polisi kwa kusaidiana na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha wanaimarisha ulinzi katika maeneo ya Mji wa Chake Chake huku wakitoa tahadhari ya kutosababisha fujo yoyote katika sehemu za hizo.Wakati wananchi wakitembea mitaani magari ya vikosi yalionekana wakitembea sambamba na wananchi hao huku askari wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Ghasia (FFU) na yale ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yakiimarisha doria kuhakikisha hakuna madhara yatakayotokea.Wananchi hao walikusanyika katika ofisi za CUF kabla ya Maofisa wa Polisi na JWTZ kufika katika ofisi hizo na kutaka wananchi hao kutawanyika huku wakitoa agizo la kuwataka kwenda kwa masheha kuchukua fomu kwa ajili ya kusajili baad aya kuzungumza na viongozi wa ngazi za juu katika wilaya hiyo.Katika Afisi ya Mkuu wa Wilaya, makundi ya watu hao idadi kubwa wakiwa vijana walisikika wakisema kuwa hawataondoka hadi Serikali itakaposikiliza na kutekeleza madai yao ya kupatiwa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.Endelea kusoma habari hii.

SMZ KUWAALIKA MABALOZI

808[1]SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imewaalika Mabalozi na Jumuiya ya Nchi za Ulaya kupitia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje kuzuru visiwani wiki ijayo ili kuzungumza na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume ili kuwafahamisha taratibu za upigaji kura zilivyo kwa mujibu wa sheria.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi Hamza Hassan Juma amyesema hayo wakati alipokuwa na mazungumzo na waandishi wa habari ofisini kwake Vuga Mkoa wa Mjini Magharibi kwa lengo la kutoa ufafanuzi zaidi juu ya suala hilo ambalo limegusa vichwa mbali mbali magazeti nchini.Waziri Juma alisema SMZ imestushwa na tamko lililotolewa na mabalozi na nchi za Jumuiya ya Ulaya na kusambwazwa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ilivyo Pemba katika zoezi la uandikishaji na upatikanaji wa vitambulisho linapaswa kuangaliwa kwa kina.“SMZ imeshtushwa na tamko la Balozi wa Canada, Japan, Norway, Marekani na nchi wanachama wa Jumuiya ya Ulaya-EU- iliyotolewa Agosti 13 na kusambazwa katika vyombo vya habari juzi” alisema Waziri huyo.Akililaumu tamko hilo alisema kuhusu uandikishaji na uendelezaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura huko Pemba limetolewa bila ya kutilia maanani hali halisi ilivyo huku SMZ ikiamini kujiandikisha ni haki ya msingi ya kila mwananchi.Alisema tamko hilo la baadhi ya mabalozi na washirika wa maendeleo Zanzibar linaonekana kuwa na upungufu kwa vile limetayarishwa na kuzingatia maoni ya upande mmoja na kutotilia maanani juhudi zilizochukuliwa na SMZ katika kuhakikisha zoezi linafanyika kwa utulivu.Endelea kusoma habari hii.

SMZ HAIJAFURAHISHWA NA TAARIFA YA EU

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeionya Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU) na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania kutoiingilia kabisa Hamza Hassan Juma (CCM) Kwamtipuramambo yake ya ndani na pia imeuponda utafiti wa kisiasa kuhusu mbio za urais wa Zanzibar mwaka 2010 uliofanywa na kampuni ya the Steadman Group kwa kuuita ni wa kitapeli.Onyo hilo kwa EU na kupondwa kwa utafiti ulioonyesha kubashiri kukubalika kwa wagombea wa urais huku Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad na Waziri Kiongozi wa awamu ya tano Dk Mohamed Gharib Bilal wakikabana koo, limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi Hamza Hassan Juma katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake Vuga Mjini hapa jana. Juma alisema Zanzibar ina mamlaka yake kamili ya kikatiba na kisheria na hivyo haiongozwi kwa shinikizo la mtu au jumuiya yeyote kutoka nje au ndani ya nchi.Alisema kampuni ya Steadman Group juni 18 mwaka huu iliiomba ofisi ya Waziri Kiongozi ifanye utafiti juu ya masuala ya kiutamaduni na kiuchumi lakini kwa makusudi wamekiuka taratibu na kufanya utafiti wa kisiasa kinyume na ombi lao la msingi.“SMZ haiongozwi kwa kumuogopa mtu au kwa shinikizo lolote,ina katiba yakae,sheria zinayosimamia masuala mbalimbali na upana mkubwa wa maendeleo ya demokrasia ‘AlisemaWaziri huyo wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi alisisitiza kuwa SMZ ina utawala wake kamili ikiwemo pia na sheria inayosimamia uchaguzi ambayo iliyopitishwa na BLW kama chombo cha kutungia sheria.Endelea kusoma habari hii.

CCM ZNZ WAPONDA UTAFITI WA SYNOVATE

KARUMEBAADHI ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) wameshtushwa na ripoti za utafiti zilizotolewa na Kampuni ya Synovate ambayo imempa nafasi kubwa ya uongozi katika uchaguzi mkuu wa 2010 Maalim Seif Sharif Hamad na kufuatiwa na Dk Mohammed Gharib Bilal na kusema kuwa hawakubaliani na utafiti huo.Kwa mujibu wa utafiti huo uliowajumuisha na kuwahoji wananchi 2000 Tanzania nzima juu ya viongozi waliopo madarakani na wengine wanaotarajiwa kuingia katika kinyanganyiro cha urais katika uchaguzi mkuu ujao imetoa matokeo kwamba kwa upande wa Zanzibar Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad anaongoza katika kinyanganyiro hicho kwa kupata asilimia 28.Pia utafiti huo umempa nafasi ya pili Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Waziri Kiongozi Mstaafu, Dk. Mohammed Gharib Bilal kwa kupata asilimia 24 Wakati Waziri Kiongozi wa sasaShamsi Vuai Nahodha akipata asilimia 10 na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein akipata asilimia 2.Wakizungumza nje ya ukumbi wa mkutano wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui jana wajumbe hao kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini wamesema utafiti uliofanywa haukuzingatia vigezo halisi vinavyohitajika na hivyo hawawezi kuuamini.Endelea kusoma habari hizi.

TULIKHOFIA KUTOKEA VURUMAI -TUME

MKURUGENZI wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Salum Kassim amesema zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura nanilimesitishwa kisiwani Pemba kwa sababu wananchi wa jimbo la Ole na jimbo la Tumbe walijitokeza katika vituo vya kujiandikisha kwa wingi kinyume cha matarajio hivyo Tume kwa kuhofia kutokea matatizo katika vituo walilazimika kusitisha zoezi.Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake jana, Kassim alisema katika vituo vya uandikishaji walifika hata watoto wadogo wa umri wa miaka minane mpaka kumi, wakidai kuwa hawakuandikishwa na wanahitaji vyeti vya Mzanzibari Mkaazi. “Kutokana na hali ilivyokuwa ilikuwa lazima tusitishe zoezi lile ili tusije tukasababisha madhara, kwani mazingira yalikuwa yanaonyesha kutokea tatizo la uandikishaji, hivyo tukaona kuwa ni bora tusitishe,” alieleza Kassim.Alisema matarajio ya awali ilikuwa ni kuandikisha wapigakura wapya wachache tu wale ambao ni vijana waliofikisha miaka 18 na wale ambao kwa sababu moja au nyingine hawakuwahi kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapigakura lakini walishangaa kuona kuwa waliojitokeza kuandikishwa walikuwa wengi na wengine hawakuwa hata na sifa ya kuandikishwa kutokana na kutotimiza umri.Endelea kusoma habari hii

MAALIM SEIF ACHUNGUZWE-CCM

sChama Cha Mapinduzi (CCM) kimeitolea wito Serikali zote mbili na jumuiya za kimataifa kuanza kumtazama kwa maakini Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad kama ni tishio jipya la uvurugaji wa ustawi wa amani katika nchi za Maziwa Makuu.Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Itikadi na Uenezi CCM Vuai Ali Vuai ametoa tamko hilo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliuofanyika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Unguja.Vuai alisema Maalim Seif ndiye anayechochea wafuasi wake wafanye fujo huko Pemba na kuvunja sheria huku akiwalazimisha waandikishwe wakiwa hawana vitambulisho vya ukaazi wa miaka mitatu vinavyotolewa chini ya sheria Namb 7/2005 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.Alisema kuwa bila shaka ana agenda ya mpya tete iliyojificha ikiwa dhamira mbaya ya kudumaza misingi ya demokrasia ili isifuate mkondo wake Zanzibar.Alisema kiongozi yeyote anayetoa matamshi yasiyo na tahadhari yenye kuchochea ili kuharibu misingi ya amani kunakoambatana na ukiukaji wa katiba na sheria ni tishio kwa usalama na amani ya nchi na mustakabali wake.“CCM tunaziomba serikali mbili za SMT na SMZ kuzifuatilia kwa karibu kauli za Maalim Seif,lakini pia tunaitolea wito jumuiya ya kimataifa,mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania na Taasisi za kimataifa kumtahadhari kiongozi huyu kama ni tishio jipya”.Endelea kusoma habari hii

TUTAENDELEA KUDAI HAKI-MAALIM SEIF

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi- CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema ikiwa kuwaambia watu wasimamie na kudai haki zao ni uchochezi basi ataendelea kuchochea mara kwa mara na yuko tayari kwa lolote.maalimseifAkihutubia mamia ya wafuasi wa CUF, wakazi wa Mji Mkongwe, Zanzibar katika viwanja vya Vuga jana, Maalim Seif alisema wananchi wa Pemba wenyewe walipoona kuwa Tume ya Uchaguzi haiwatendei haki katika zoezi la uandikishaji katika daftari la wapigakura ndipo walipoamua kusimama kidete na kusema kuwa kama watu wanaostahili kupewa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi hawapewi, basi hakuna atakayeandikishwa.“Kama watu wakisimama kidete kudai haki zao ndio kuchochea, basi mimi nitachochea, chochea, chochea…,” alisisitiza Maalim Seif.Alisema kama SMZ wasipotoa haki za wananchi, litakalotokea lolote serikali itabeba lawama. “Haki za watu watazitoa kwenye tundu za pua zao.” “Wananchi wenyewe walisema kama hawapewi vitambulisho vya uzanzibari hakuna atakayeandikishwa kwa kuwa jambo hilo limeingizwa katika sheria za uchaguzi isivyo halali kwamba ikiwa huna kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, huna haki ya kuandikishwa kupiga kura. Hayo ni makosa kwani ni kinyume cha Katiba. Katiba inasema mwenye haki ya kupiga kura Zanzibar ni Mzanzibari, mwenye akili, aliyetimia umri wa miaka 18. Sasa inakuwaje mtu mwenye umri wa miaka 70 ambaye amezaliwa, amekulia, amezaa na amejukuu Zanzibar aambiwe kuwa kama hana cheti cha kuzaliwa hapewi kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi na haandikishwi katika daftari la kupiga kura?” Alihoji Maalim Seif.Endelea kusoma habari hii

MUUNGANO HAUWEZI KUVUNJIKA-MOYO

WAZIRI wa zamani katika awamu ya kwanza na ya pili katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar DSC04996Hassan Nassor Moyo amesema kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauwezi kuvunjika kwa sababu ya mafuta kwa kuwa haukuundwa kwa sababu hiyo.Akizungumza na Mwananchi Jumapili nyumbani kwake, Fuoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar jana, Moyo alisema; “Huu ulikuwa ni muungano wa makubaliano, mimi nilikuwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, tulishirikishwa katika majadiliano na tukakubaliana na wenzetu wa Tanganyika kwa kuwa zilikuwapo sababu nyingi za kijamii, kiuchumi na hata za kisiasa kwa nchi hizi mbili kuungana, hivyo tuliungana kwa mapenzi na nia njema.”Hivi karibuni Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitoa onyo kuwa kutokana na chokochoko zilizopo kuhusu Muungano ipo siku utavunjika na ukivunjika upo upande utakaoumia zaidi, kuhusu kauli hiyo Mzee Moyo alisema “Yule aliyejibu hivyo hajui kitu, kwa nini wanafikiria kama Muungano huu utavunjika kwa sababu kuna vitu watu wanavihoji, ile kufikiria kwamba Muungano utavunjika ni makosa, kwanini wanafikiria hivyo? Unafikiri huu Muungano umeundwa kwa sababu ya mafuta? Huu si Muungano wa mafuta, mtu yeyote anayefikiria kuwa kwa sababu tunataka mafuta tuyatoe katika Muungano tunataka kuvunja Muungano hivyo sivyo kwa sababu huu Muungano si wa mafuta bali ni wa nchi mbili, hivyo kusema kuwa utavunjika kwa sababu ya mafuta na gesi si kweli.Endelea kusoma habari hii

SHEHA AMWAGIWA TINDI KALI PEMBA

SHEHA wa Shehia ya Ole Muhogoni Mkoa wa Kaskazini Pemba Mussa Ali Kombo amemwagiwa tindikali usoni na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.Kamanda wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Bugi amethibitisha kutokea tukio hilo majira ya saa mbili usiku na kuahidi kuwatafuta wote waliohusika na kuwachukulia hatua kali za SHEHAkisheria.Alisema jeshi la polisi bado linafanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ili kuweza kujua zaidi chanzo cha tukio hilo pamoja na kuwatia mikononi watu waliofanya kitendo hicho cha kikatili.Chanzo cha tukio hilo inasadikiwa ni kufuatia zoezi la daftari la uendelezaji kastika daftari la kudumu la wapiga kura katika kisiwa cha Pemba,ambalo linaratibu wapiga kura wapya na wale wa zamani kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu mwakani.Chama cha mapinduzi Mkoa wa Mjini Magharibi kimetoa taarifa kwa vyombo vya habari leo hii mjini Unguja huku kikilaani kutokea kwa tukio hilo linalotishia amaniAidha CCM Katibu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ramadhan Abdallah Ali imeelezea kusikitishwa kwake na tukio hilo kupitia taarifa hiyo kwa vyombo vya habari. Endelea kusoma habari hii

HAANDIKISHWI MTU KWA KUWA ANA MVI

DSC_8657WAKUU wa Mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba wamesema hakuna mwananchi atakayendikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kigezo cha kuangalia mvi katika kichwa chake.“Hakuna mtu atakayeandikishwa kwa kuangalia kigezo cha mvi lazima awe na kitambulisho cha mzanziabri mkaazi kama sheria inavyosema na hakuna atakayepewa kitambulisho cha mzanzibari mkaazi bila ya kuwa na cheti cha kuzaliwa” alisema Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi.Tamko hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia malalamiko ya kuwepo wananchi wengi waliokwama kuandikishwa tangu kuanza kwa zoezi hilo kutokana na kukosa vitambulisho vya uzanzibari ukaazi.Dadi alisema kwamba ni kweli kuna idadi kubwa ya watu waliokwama kuandikishwa kwa vile hawana vyeti vya kuzaliwa ambavyo ndivyo vinavyowawezesha kupata kitambulisho cha mzanzibari mkaazi kubla ya kuandikishwa katika daftari hilo.Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba wapo wazee wenye umri kati ya miaka 70 na wanafahamika kisiwani pemba lakini wameshindwa kuonesha vyeti vya kuzaliwa wakiwemo na vijana waliotimiza umri wa miaka 18 kabla ya kupewa kitambulisho cha mzanzibari mkaazi na kusajiliwa kama mpiga kura katika uchaguzi ujao wa 2010.Endelea kusoma habari hii.

UANDIKISHAJI UTASABABISHA MACHAFUKO ZNZ

SASA kuna kila dalili kwamba zoezi la uandikishaji wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) ndio litakaloiingiza nchi katika DSC01016machafuko makubwa kutokana na kuzuiwa kwa watu wengi kuingizwa kwenye Daftari hilo.Hayo yamebainishwa jana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kiwanja cha Herous Mkwajuni Kibeni,Mkoa wa Kaskazini Unguja.Katika mkutano huo uliokusudiwa kuhitimisha ziara za Katibu Mkuu huyo katika wilaya ya Kaskazini ‘A’, Maalim Seif aliwaambia wananchi kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ikishirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Idara ya Vitambulisho imeandaa mpango maalumu unaokusudiwa kuwaengua katika zoezi la uandikishaji kiasi ya Wazanzibari 80,000 kufikia mwakani ambapo zoezi hilo litakuwa limekamilika.“Hawa jamaa wana mpango maalum wa kuwanyima Wazanzibari haki yao ya kupiga kura. Wanajuwa kwamba bila ya kufanya hivyo, hawana uwezo wa kushinda Zanzibar. Lakini tunasema kwamba, mara hii hatukubali, hatukubali, hatukubali. Wanavyotaka tunataka. Wakitaka iwe noma, itakuwa noma kwenye nchi hii mara hii,” Alisema Maalim Seif kwa hasira huku akishangiliwa na wafuasi wake.Endelea kusoma habari hii.

MPANGO WA KUSHINDA UCHAGUZI UJAO

PICT0323CHAMA cha wananchi (CUF) kimezindua mkakati mpya unaolenga kushinda uchaguzi mkuu ujao, huku ikitoa tuhuma dhidi ya serikali na Chama cha mapinduzi (CCM) kuhusu undanganyifu. Katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliyofanyika katika viwanja vya Kibanda-maiti mjini hapa mwishoini mwa wiki iliyopita, viongozi wa chama hicho walizindua “mkakati wa kuelekea Ikulu, na mkakati wa zinduka.” Katibu mkuu wa CUF maalim Seif Sharif Hamad, Naibu wake Juma Duni Haji, na Mkurugenzi wa uenezi Salum Bimani, kwa nyakati tofauti, waliwataka wafuasi wao kuunga mkono mikakati hiyo kwa kujinadkisha. “CCM chini ya Rais Kikwete, wamepanga mkakati wa kufanya uchaguzi bila fujo, ili uonekane kuwa wa huru na haki. Lakini ukweli ni kwamba wamepanga mikakati ya kuwanyika haki wazanzbari wengi fursa ya kupiga kura kwa kuwanyika vitambulisho vya mzanzibari,” alisema Maalim Seif. Endelea kusoma habari hii.

UMOJA WA VIJANA WATAKA ILANI ITANGAZWE

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa CCM -UVCCM -nchini imesema vijana p21wake wanatakiwa kuifafanua ilani ya uchaguzi kwa kutaja faida na maslahi ya utekekezaji wa kila sekta. Naibu Katibu MKuu wa (UVCCM) Zanzibar Mohammed Hassan Moyo alitoa ufafanuzi huo jana katika hafla ya kumpongeza Mwakilishi wa Jimbo la Magogoni Asha Mohamed Hilal zilizofanyika katika ukumbi wa Gymkana. Moyo alisema kuwa haitoshi kusema ilani ya uchaguzi imetekelezeka bila ya kutoa ufafanuzi na kuainisha manufaa halisi ya kimaslahi wanayofaidika wakulima, wavuvi,wafanyabiashara na wafugaji hasa katika maeneo ya vijijini. Endelea kusoma habari hii.

CCM WAIBUKA MSHINDI JIMBO LA MAGOGONI

Bi Asha Mohammed Hilal (CCM) alieyeshinda katika jimbo la Magogoni
Bi Asha Mohammed Hilal (CCM) alieyeshinda katika jimbo la Magogoni

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemtangaza Mgombea wa CCM, Asha Mohammed Hilal kuwa mshindi baada ya kuibuka na kura 2874 dhidi ya upinzani wake wa CUF Hamad Ali Hamad aliyepata kura 1974 huku Khamis Mselem Omar wa SAU aliyepata kura 22. Akitangaza matokeo hayo katika kituo cha Mwanakwerekwe, Msimamizi wa ZEC, Suluhu Ali Rashid alisema watu 5494 waliandikishwa kupiga kura ambapo kura zilizopigwa ni 4917 huku kura 48 zikiwa zimeharibika katika uchaguzi huo ambao umemalizikwa kwa salama bila ya vurugu wowote. Katika hatua nyengine zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Magogoni umefanyika katika vituo 16 ukiwa umetawaliwa na mabishano ya mawakala na baadhi ya vijana kutaka wapige kura bila ya kuwa na shahada ya kupigia kura. Endelea kusoma habari hii.

CCM NA CUF WAHITIMISHA KAMPENI ZAO

Mgombea wa CUF, Hamad Ali Hamad

Chama Cha Wananchi (CUF) kimewataka vijana kukikataa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa hakioneshi kuwajali katika kuwaisaidia na kuwakomboa. Akizungumza na umati mkubwa uliokuja kusikiliza mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa CUF, Hamad Ali Hamad uliofanyika katika viwanja vya Mabata, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad amesema wakati umefika vijana kubadilika na kuikataa CCM. Amesema vijana wawe ndio wa mwanzo kubadilika na kwa kuwa nguvu kubwa katika nchi yoyote inatokana na vijana kutokana na wazee wao huwa wasindikizaji baada ya vijana wao kuongoza mapambano ya mabadiliko.Endelea kusoma habari hii.

NI AIBU KUIPIGIA KURA UPINZANI -UVCCM

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi –UVCCM- umesema vijana MSANIIwazalendo nchini kwao iwe ni aibu kuvipigia kura vyama vya wapinzani kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kuyasaliti Mapinduzi ya 1964 na Uhuru wa Tanganyika 1961.Naibu katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Mohamed Hassan Moyo jana aliwaeleza wana CCM waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi mgombea wake Asha Mohamed Hilal. Moyo alisema kuwa Mapinduzi ya 1964 na juhudi za kuleta uhuru wa 1961 mikakati yake iliandaliwa na kutekelezwa na kundi la vijana hivyo ni lazima heshima ya vijana wa ASP na TANU zilindwe na kuthaminiwa na wote. Endelea kusoma habari hii.

MWAKILISHI WA WAWI (CUF) AFARIKI DUNIA

Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Pemba, Marehemu Soud Yussuf Mgeni
Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Pemba, Marehemu Soud Yussuf Mgeni

WAKATI leo ni siku ya Uchaguzi mdogo katika Jimbo la Magogoni, Mwakilishi wa Jimbo la Wawi na Mnadhimu wa Chama cha Wananchi (CUF) katika Baraza la Wawakilishi, Soud Yussuf Mgeni (61) amefariki dunia jana na atazikwa leo Kijijini kwao Vitongoji Mkoa wa Kusini Pemba. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Umma wa Chama cha CUF, Salim Rashid Biman alisema marehemu Soud alikuwa amelazwa katika wodi ya wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalum (ICU) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. “Kwa sasa Soud hatunaye katika dunia hii ndiyo kazi ya Mwenyezi Mungu, mipango ya mazishi inafanywa na tunatarajia kesho (leo) Inshaallah tutakwenda kumzika nyumbani kwao Kisiwani Pemba” Alisema Bimani. Endelea kusoma habari hii.

JESHI LA POLISI LAONYA

JESHI la Polisi limewatahadharisha wapiga kura katika Jimbo la Magogoni kuhakikisha wanaweka amani wakati zoezi la upigajikura litapofanyika hapo kesho na wananchi waondoe wasiwasi katika ushiriki wa zoezi polisihilo.Kamanda wa Mkoa wa Mjini Magharib, Bakari Khatib Shaaban alitoa tahadhari hiyo jana wakati akizungumza na Zanzibar Leo Mjini Zanzibar.Tahadhari hiyo inakuja kutokana na kesho asubuhi kuanza kwa zoezi la upigajikura katika Jimbo hilo baada ya kampeni zake kufungwa rasmi leo jioni.Hadi sasa, wagombea wanaotarajiwa kuwania uchaguzi huo ni kutoka vyama vitatu, kikiwemo cha CCM, ambapo Mgombea wake ni Asha Mohammed Hilal, CUF, Hamad Ali Hamad na Chama cha SAU ni Khamis Msele Omar. Endelea kusoma habari hii.

ZEC ENDESHENI CHAGUZI KWA UWAZI-CUF

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad

Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuendesha uchaguzi kwa uhuru, haki na uwazi ili kila chama kiridhike na matokeo yatakayotangazwa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Magogoni unaotarajiwa kufanyika Mei 23 mwaka huu. Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa Jimbo la Magogoni Mkoa wa Mjini Magahribi uliofanyika katika viwanja wa Daraja Bovu. “Mizengwe imeshafanyika wakati wa uandikishaji sasa nasema katika uchaguzi huu sitarajii kufnayika kwa mizengwe yeyote tena tunaomba uchaguzi huu ufanyike kwa haki ili kila mmoja aridhike kama ameshinda au ameshindwa kila mmoja afurahi na kukubali matokeo tunaomba sana sana” alisisitiza Maalim Seif. Endelea kusoma habari hii.

UN HAWATASIMAMIA UCHAGUZI-SMZ

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Nchi za Ulaya (EU)hazitahusika katika kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Zanzibar . Waziri Kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha mabaloziamebainisha hilo jana kwenye mkutano wa kampeni wa kumdani mgombea wa CCM jimbo la Magogoni,Asha Mohamed Hilal uliofanyika katika viwanja vya Diwani. Nahodha alisema Zanzibar ni nchi huru na Umoja wa Mataifa unaheshimu uhuru wa kila Taifa hivyo hauhusiki na hautahusika na jukumu la kusimamia shughuli za ndani za nchi yeyote iliyo huru. “ninawapasha viongozi wa CUF wasianze kuwaghilibu wananchi kwa kusema ati uchaguzi mkuu wa 2010 Zanzibar utasimamiwa na Umoja wa Mataifa,hiyo si kazi ya UN kuingilia mambo ya ndani ya nchi ”Alisema Nohodha. Endelea kusoma habari hii.

CUF -TUTAENDELEA KUDAI UN WASIMAMIE

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kitaendelea kudai uchaguzi wa mwaka 2010 kusimamiwa na Umoja wa Mataifa licha ya kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema watasimamia wenyewe kwa mujibu wa katiba.

Hamad Rashid Moh'd, Kiongozi wa upinzani Bungeni
Hamad Rashid Mohd, Kiongozi wa upinzani Bungeni

Akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo katika jimbo la Magogoni uliofanyika katika viwanja vya Greenneti Mkoa wa Mjini Magharibi, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed amesema CUF inaposema jambo huwa haina mzaha na hilo watalisimamia hadi pumzi za mwisho. “Tumemsikia Mkurugenzi akisema kuwa UN haitasimamia uchaguzi wa Zanzibar lakini sisi tutaendelea kufuatilai suala hilo kwa sababu tupo serious na hata CCM hilo wanalijua kuwa tukisema jambo tunalifuatilai mpaka hatua za mwisho ili uchaguzi mkuu kusimamiwa na UN” alisema Mohammed huku akishangiriwa na wanachama hao. Endelea kusoma habari hii.

CCM- MAFUTA SIO YA MUUNGANO

Chama Cha Mapinduzi –CCM- Zanzibar kimesisitiza kuwa mafuta na gesi asilia si suala la Muungano bali liliomo kwenye orodha ya mambo ya muungano ni suala la uagizaji na uingizaji wa mafuta ya taa, dizeli na petroli. Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mjini Magharibi Yusuf Mohamed Yusuf amewaeleza wananchi jana 028waliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguizi mdogo jimbo la magogoni uliofanyika eneo la welezo tangi la maji. Yusuf amewataka wananchi wa zanzibar kulipuuza suala hilo na kusema mafuta na gesi asilia si suala katika orodha ya mambo ya Muungano bali mafuta yanayoelezwa ni yale ya uagizaji na uingizaji lakini si katika utafutaji na uchimbaji wake nishati hiyo. Akiwashangaza hata baadhi ya wanasiasa wenziwe waliokuwepo mkutanoni alisema”ndugu zangu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Juma Duni ameibeza CCM ati kwa kuridhia mafuta na gesi liwe suala la muungano, si kweli mafuta si suala la Muungano asiwadanganye asilan” alisema Mgombea huyo. Endelea kusoma habari hii.

UMOJA WA VIJANA CCM WAWAKEMEA WAPINZANI

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa (UVCCM) Hamad Yussuf Masauni amewakemea wapinzani wanaowatisha na kuwazomea viongozi wa Chama Cha Mapinduzi katika kampeni zinazoendelea katika uchaguzi wa mdogo Busanda. PICT0546Akihutubia wanachama wa CCM katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Magogoni Visiwani Zanzibar, Masauni alisema chama cha CHADEMA kinaendesha kampeni chafu huko Busanda jambo ambalo linakwenda kinyume na demokrasia ya mfumo wa vyama vingi. Alisema mbali ya kuendesha kampeni za fujo na lakini pia wapinzania wamekuwa wakitumia njia za kuwatisha wanachama wa CCM katika kampeni hizo vitendo ambavyo haziwezi kuvumiliwa katika uendeshaji wa siasa za Tanzania kwa kuwa kunawanyima baadhi ya wananchi kushiriki katika kampeni hizo. Endelea kusoma habari hii

ZEC-UN HAIWEZI KUSIMAMIA UCHAGUZI ZNZ

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema haiwezekani uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kusimamiwa na Umoja wa Mataifa (UN) kwa vile ni kwenda balozikinyume na katiba ya Zanzibar. Tamko hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Tume hiyo, Salim Kassim Ali alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Maisara Mjini Zanzibar kuhusiana na matayarisho ya uchaguzi mdogo katika Jimbo la Magogoni unaotarajiwa kufanyika Mei 23 mwaka huu. Alisema kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar uchaguzi wa Rais, Wawakilishi na Madiwani unatakiwa kusimamiwa na tume ya uchaguzi pekee na hakuna chombo chochote chenye mamlaka ya kufanya kazi hivyo zaidi ya tume. “Umoja wa Mataifa hawana mamlaka ya kikatiba ya kusimamia uchaguzi wa Zanzibar na hakuna nchi yoyote ambayo imewahi kusimamia uchaguzi wake na UN duniani sina kumbukumbu hizo” alisema Mkurugenzi huyo. Endelea kusoma habari hii.

UMOJA WA ULAYA WAAHIDI UCHAGUZI HURU

Mabalozi 12 wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) wametahadharisha kwamba Zanzibar haiwezi kumudu kufanya uchaguzi mwengine wenye ulalamishi na kutaka hatua zichukuliwe kuhakikisha wazanzibari wanapewa nafasi ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu wa wa 2010.Wakizungumza na viongozi wa vyama vya siasa vya CCM na CUF na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mjini Zanzibar mabalozi hao walisema jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa umakini mkubwa uchaguzi utakaofanyika Zanzibar. Mabalozi hayo wameahidi kuyachukua maoni mbali mbali yaliotolewa na kuvihakikishia vyama hivyo kuyafanyia kazi maoni yote yaliotolewa na vyama viwili hivyo kwa lengo la kuhakikisha uchaguzi mkuu wa 2010 unafanya katika misingi ya haki na uwazi. Endelea kusoma habari hii.

CCM NA CUF WATOA MISAADA

Fatma Ferej Mwakilishi wa Mji Mkongwe
Fatma Ferej Mwakilishi wa Mji Mkongwe

MWAKILISHI wa Jimbo la Mji Mkongwe Fatma Fereji, (CUF) amekabidhi Cheki ya shilingi 700,000, kwa Shule ya serkondari Vikokotoni Mkoa wa Mjini Magharibi kwa lengo la kusaidia uboreshaji wa Maabara katika shule hiyo. Cheki hiyo imekabidhiwa kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Hashim Abdalla Muhammed, ambapo alisema ametoa msaada huo kufuati kupata maombi kutoka shuleni hapo ambayo ina upungufu mkubwa wa vifaa ufundishaji wa wanafunzi, hasa katika masomo ya sayansi. Akizungumza katika makabidhiano hayo Mwakilishi huyo alisema kwamba kutoa kwa msaada huo hakuna maana kuwa ni wa mwisho bali, ameahidi kusaidia kila hali itakaporuhusu . “Nina ahidi kusaidi vifaa mbali mbali Skulini hapa kila hali itakaporusu ili kuhakikisha elimu inapatikana bila ya usumbufu hasa kwa kuwa mimi nimesoma pia katika skuli hii ya darajani”alisema. Endelea kusoma habari hii.

CCM NA TUME WAMEANDAA MIZENGWE

Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF

Katibu Mkuu wa Chama wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema tayari kumeandaliwa mizengwe ya kuiwezesha CCM iweze kushinda katika uchaguzi mdogo wa magogoni mjini Zanzibar. Hayo ameyaeleza alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni uliofnayika katika viwanja vya shule Kinuni mkoa wa mjini magharibi unguja na kuhudhuriwa na mwenyekiti wa chama hicho professa Ibrahim Lipumba. Amesema Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) tayari imeandaa mazingira ya kuwanyima haki wapiga kura wakati wa zoezi hilo utakapofika mei 23 mwaka huu kujaza nafasi ya Mwakilishi kufuatia kifo cha Daud Hassan Daud aliyefariki desemba kmwaka jana. Amesema tayari kuna mipango ya orodha ya wapiga kura kubandikwqa nje ya vituo majina yao lakini majina hayo hayataonekana ndani vituo vya wapiga kura. Endelea kusoma habari hii.

POLISI HAITOVUMILIA SIASA CHAFU

JESHI la Polisi nchini limeonya kuwa halitawavumilia wanasiasa salma14watakachochea vurugu wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo katika jimbo la magogoni mkoa wa mjini magharibi unguja unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Madema, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakari Khatib Shaaban, alisema hawategemei kuwepo kwa matamshi ya uchochezi na kashfa katika kipindi cha kampeni hivyo amewahimiza wafuasi wa vyama na viongozi wao kuzingatia sheria na taratibu za nchi. Alisema kwamba uchaguzi ni njia mojawapo ya kidemokrasia hivyo ni imani ya jeshi lake kuona vyama vya siasa vinaheshimu utawala bora ili kuona Zanzibar inasonga mbele katika kuimarisha utawala wa sheria. Kamanda Bakari alisema kutokana na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) katika Wilaya ya Magharib imeshafanya vikao vyake na vyama vya siasa juu ya mwenendo mzima juu ya maadili ya uchaguzi hivyo ni muhimu kuzingatia maadili hayo. Endelea kusoma habari hii.

TUME YATUPILIA MBALI PINGAMIZI ZA VYAMA

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetupilia mbali pingamizi za Vyama vitatu vya siasa vya CCM, CUF na SAU vinavyoshiriki Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Magogoni kutokana na madai yaliotolewa na vyama hivyo hayana hoja za msingi kisheria. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Magogoni, Suluhu Ali Rashid amesema wameamua kuyapitisha majina matatu ya wagombea wa Vyama hivyo,Asha Mohammed Hilal kutoka (CCM), Khamis Mselem Omar(SAU) na Hamad Ali Hamad(CUF). “Tumeyapitia kwa umakini mkubwa madai ya Vyama vyote vya siasa yaliyotufika ofisini kwetu na uamuzi wetu ni kwamba wagombea wote wana haki ya kugombea kwani hatukuona katika pingamizi zao kama zina msingi wa kisheria kuwazuia waliolalamikiwa kutogombea katika uchaguzi wa magogoni” Alisema Rashid. Endelea kusoma habari hii.

TADEA WAJITOA UCHAGUZI MDOGO

CHAMA Cha TADEA nchini kimetangaza kumuondoa mgombea wake Ali Mohammed Ali kushiriki uchaguzi mdogo katika jimbo la Magogoni kwa DSC04932madai zoezi la uandikishaji limetawaliwa na ukiukwaji wa sheria. Tamko hilo limetolewa jana na katibu mkuu wa chama hicho Juma Ali Khatib alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Idara ya Habari maelezo mjini Zanzibar jana. Alisema baada ya zoezi la uandikishaji kumalizika chama hicho kilifanya tathmini ya zoezi hilo na kubaini zaidi ya watu 1000 wamenyimwa haki ya kuandikishwa katika daftari la wapiga kura na viongozi wa serikali za mitaa (masheha) kwa kushirikiana na baadhi ya watendaji wa tume hiyo. Alisema kwamba lengo la uandikishaji limetangazwa na tume ilikuwa ni kuandikisha watu 10000 lakini hadi zoezi hilo linakamilika ni watu 5000 tu ndio walioandikishwa sawa na asilimia 50 ya watu walioshiriki uchaguzi wa mwaka 2005. Endelea kusoma habari hii.

KIKWETE AONGOZA DUA ZNZ

bagamoyo_DSC09957Rais Jakaya Kikwete amewaongoza viongozi wakuu wa serikali na waumini wa dini mbali mbali katika sala na dua ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume aliyefariki dunia baada ya kupigwa risasi visiwani Zanzibar. Ibada hiyo iliyowashirikisha viongozi mbali mbali imefanyika wakiwemo viongozi wa madhehebu ya dini ya kikatoliki na anglikan ambapo awali yalianza na maandamano ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka alipozaliwa kiongozi huyo hadi Ofisi Kuu ya Chama hicho Kisiwandui kwenye kaburi la Mzee Karume. Tarehe 7 April mwaka 1972 kundi linalodaiwa ni la mahaini na wapinga Mapinduzi walifanikiwa kumpiga risasi na kumuua Rais wa Kwanza wa Zanzibar hayati Mzee Abeid Karume katika jengo la Makao Makuu ya ASP Kisiwandui majira ya jioni. Endelea kusoma habari hii.

HAKUNA HAJA YA TUME YA MARIDHIANO-SMZ

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema haioni haja ya kuundwa kwa Tume ya upatanishi maridhiano na ukweli ili kusahau na kufunika yaliofanyika kabla na baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi Hamza Hassan Juma amewaeleza waandishi wa habari ofisini kwake Vuga Mjini hapa wakati akielezea siku maandalizi ya April 7 kila mwaka kuwa ni siku ya maadhimisho ya kuwakumbuka mashujaa wa Zanzibar. Juma alisema SMZ kwa kiasi kikubwa tayari imekwishachukua juhudi za kuleta upatanishi na usuluhishi katika jamii kuhusu masuala kadhaa yaliopita wakati wa ukoloni na baada ya Mapinduzi ya 1964 ikiwa ni pamoja na kuwahimiza watu kuchanganya damu kupitia ndoa. Endelea kusoma habari hii.

MHUNZI ASHUTUMIWA KWA WIZI

Abass Juma Mhunzi
Abass Juma Mhunzi

Mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza mahesabu ya fedha na uchumi ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika baraza la wawakilishi (PAC) Abass Juma Mhunzi ameangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake huo. Kujiuzulu kwa Mhunzi ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Chambani Kisiwani Pemba kumekuja siku chache baada ya baraza kuu la uongozi la chama chake cha CUF kumbwaga katika nafasi yake na mjumbe wa baraza hilo uchaguzi ambazo umefanyika wiki hii jijini Dar es Salaam.

MUASISI WA CUF AFARIKI DUNIA

MWASISI wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaaban Khamis Mloo amefariki dunia katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar ambako alikuwa akitibiwa maradhi ya moyo. Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha CUF, Salim Biman amesema marahemu Mloo atazikwa Shambani kwake katika Kijiji cha Mfenesini Mkoa wa Mjini

Mzee Shaaban Mloo
Mzee Shaaban Mloo

Magharibi Unguja. Biman alisema marehemu Mloo mwishoni mwaka jana alilazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya moyo, alipata nafuu, lakini mwanzoni mwa wiki hii alilimbizwa Hospitali ya Mnazi Mmoja na kulazwa (ICU). Endelea kusoma habari hii.

MTOTO WA DK. SALMIN CHINI

salminMatokeo ya kura za maoni katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Magogoni Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Mei 23 zinaonesha kuwa baadhi ya vigogo waliotegemwa kuongoza wamepigwa na chini katika kura za maoni. Katika watu waliotemwa ni mwanasiasa chipukizi ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Salmin Amour Juma, Amin Salmin ambaye ameambuliwa kura tano katika kura za maoni. Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Elimu, Uchumi na Malezi wa Wilaya ya Magharibi, Ali Yussuf Machano alisema katika kura hizo zinaonesha Abbasi Hassan Juma ambaye ni ndugu wa waziri wan chi ofisi ya waziri kiongozi Hamza Hassan Juma amepata kura 29 wakati Khamis Yahya Machano amepata kura 27 huku vigogo maarufu waliopata kushika nafasi mbali mbali wakibwagwa bila ya kutegemewa. Endelea kusoma habari hii.

CUF- TUTACHEZA NGOMA ITAKAVYOPIGWA

jkKatibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amesema wanachama wa chama chake wataingia katika uchaguzi mkuu wa 2010 wakiwa wamejitayaridha kupambana na mazingira yoyote yatakayojitokeza. Hayo ameyaeleza walipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya kibanda maiti mkoa wa mjini magharibi na kutumia muda mwingi kujibu hoja zilizotolewa na Rais Jakaya Mricho Kikwete katika ziara yake ya miko mitano ya Zanzibar. Alisema kauli zilizotolewa na Rais Kikwete haziashirii kuwepo uchaguzi huru na wa haki Zanzibar kwa vile wapinzani wasitarajie kukamata madaraka ya dola na wengine wataishia kutafuta nafasi hiyo hadi mwisho wa maisha yao. Endelea kusoma habari hii.

KIKWETE HANA UBAVU WA KULINDA MAPINDUZI

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Machano Khamis Ali amesema Rais Kikwete hana uwezo wa wowote wa kuyalinda mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na kama ana uwezo huo basi angeonesha kwa kuwalinda walemavu wa ngozi (Albino) wanaouwa kinyama.

Makamu Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali
Makamu Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali

Akihutubia mkutano wa hadhara ulioitishwa na chama hicho kwa lengo la kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya januari 26 na 27 mwaka 2001 katika Uwanja wa Demokrasia Mkoa wa Mjini Magharibi Ali alisema kama kweli Kikwete ana ubavu huo azuwie kwa vitendo mambo yanayofanyika hivi sasa dhidi ya mauaji hayo. “Kikwete hana ubavu wa kuyalinda mapinduzi na kama ana uwezo huo basi angewalinda maalbino wanaokufa ovyo wala, kama Kikwete ana uwezo huo wa kuyalinda mapinduzi basi atuoneshe tuone” alisema Makamu huyo. Endelea kusoma habari hii.

CCM – MAALIM SEIF AOMBE RADHI

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimemtaka Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amuombe radhi Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete baada ya kumtaka aache JKkuwagawa wazanzibari. Hayo yameelezwa katika tamko maalumu lililotolewa na Katibu Mwenezi wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai ambapo pia Maalim Seif ametakiwa awaombe radhi wananchi wa Zanzibar na chama hicho. Vuai amesema wakati Maalim Seif akihutibia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara alitoa maneno yasiofaa dhidi ya Rais Kikwete kufuatia ziara yake aliyoifanya katika maeneo mbali mbali ya mikoa mitano ya Zanzibar. Endelea kusoma habari hii.

NCHI WANACHAMA ZIWE MAKINI

Shamsi Vuai Nahodha(CCM)Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kabla nchi wanachama hawajaazisha rasmi Soko la Pamoja la Afrika Mashariki zinapaswa kuwa makini katika umiliki wa ardhi na pasi za kusafiria. Hayo yalilezwa na Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha wakati akifunga kikao cha 14 cha baraza la wawakilishi kilichoketi kwa wiki mbili Maisara Mjini Zanzibar. “Nawaomba wananchi wa Zanzibar waendelee kutoa maoni yao bila ya khofu kila fursa ya kufanya hivyo inapopatikana kujadili masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, narejeo wito wangu kuwa watanzania tunapaswa kuwa makini sana katika kuilinda ardhi yetu na kuwasomesha vijana wetu ili waweze kushindana katika soko la ajira” alisema Nahodha.Endelea kusoma habari hii

SMZ YALIFUNGIA TAIFA HURU

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imelipiga marufuku rasmi gazeti ya la TAIFA HURU linalotolewa na Kampuni ya Zanzibar Media Cooperation kuingia katika Visiwani vya Zanzibar. Kwa mujibu wa barua ya serikali ya Janauri 22 mwaka huu yenye kumbukumbu namba IHM/UBM/1/VOLUME/1 iliyotumwa kwa Meneja wa Kampuni ya Zanzibar Media Cooperation ambayo inamilikiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mohammed Seif Khatib iliyosainiwa na Afisa wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jamila Mahmoud imeeleza sababu ya kupigwa marufuku kwa gazeti hilo. Barua hiyo imesema hatua ya kulifungia gazeti hilo inatokana na Kampuni hiyo kukiuka kifungu cha 11(1) sheria No 5 ya mwaka 1988 ambapo kwa mujibu wa sheria mwenye mamlaka ya kusajili magazeti Zanzibar ni msajili na sio taasisi nyengine. Endelea kusoma habari hii.

PEMBA BAADA YA SHEREHE ZA MAPINDUZI

PICT0578Kisiwa cha Pemba kimeanza kurudi katika hali yake ya kawaida baada ya watu waliokuja kwa wingi kutoka Unguja na Tanzania Bara kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya miaka 45 ya Mapinduzi wote kurejea makwao. Shamra shamra zilizokuwa katika mitaa mbali mbali pamoja na mapambo ya bendera za rangi ya kijani na njano zimeanza kupachuliwa katika maofisi ya serikali pamoja na majumbani huku biashara zikiwa zimeanza kudorora kwa kasi kubwa kwa kukosa wateja ambao walionekana kwa wingi wakijinunulia bidhaa kadhaa katika soko kuu la Mji wa Chake Chake na maeneo mengine ya miji ya kisiwa hicho. “Waswahili wanasema mgeni njoo mwenyeji apone sasa biashara zilikuwa zimeimarika katika kipindi cha siku mbili tatu tmeuza sana hasa vinywaji na vyakula lakini sasa zimeanza kurudi katika hali yake ya kawaida si unajua bwana” alisema mfanyabiashara wa Mji wa Chake Chake, Khamis Hamad Ali. Endelea kusoma habari hii

Advertisements

24 Replies to “Siasa”

 1. I have seen your very nice website and, I have gone through that. In there, I have seen so many news that gives me green light, especialy political story. you know very wellabout my side is CCM but, I ‘m well educated and I know which is right and wrong. I have to say that, your site is very productive for those who look for Zanzibar Development. It seems that, after a very shot period of time, your going to emprove more, and lastly I have to thank you for your good contribution on this, and I have to congratulate for your effort. May Allah will be with you.
  thank you sister.
  your class mate.

 2. Bwana haji machano.
  habari yako rafiki.
  Ahsante kwa kumpa pongezi mwanzilishi wa blog hii.ni blog nzuri tu.

  Bwana haji machano,ningependa kutoa dukuduku langu binafsi kuhusiana na kauli yako hapo juu uliyoitowa kuwa “my side is CCM”
  Maelezo yako yanaweka wazi kuwa wewe ni mwana CCM. Hongera kwa kutumia haki yako ambayo inakupa fursa ya kujiunga na chama chochote cha kisiasa ukipendacho kati ya vyama vilivyo sajiliwa kisheria hapa nchini.

  Binafsi nimekuwa nikipata tabu kubwa ya kutafakari ni vipi Kijana wa Kizanzibari halisi ataweza kujikita kwa hali na mali kukisapoti chama cha CCM.
  Sina Mzanzibari niliyeongea naye amabaye hana malalamiko yanayoonyesha kudhalilishwa,kudharauliwa na kufedheheshwa kwa Zanzibar na hii CCM pamoja na serikali ya muungano.

  Kila kukicha tumekuwa tukiwashuhudia wawakilishi na wabunge wa Zanzibar (ccm na cuf) wakitowa msururu wa malalamiko na kero wanazozipata kutoka kwa hao Wakuu wao wa ccm na serikali ya muungano.licha ya makelele ya wawakilishi na wabunge hawa ya kutaka kuikwamua Zanzibar kutoka katika makucha ya watawala hawa.Genge la CCM pamoja na wakuu wa serikali ya muungano ikiongozwa na Pinda tayari washatowa kauli zao kuwa hakuna lolote lile litakalokuwa. wakimaanisha kuwa ZANZIBAR haina maamuzi yeyote yakufanya kuhusiana na kero hizo wanazozitowa.kwa lugha nyengine ni kusema kuwa wao ndio watawala na waamuzi wa mambo yote ya ZANZIBAR.

  Hapa kinachoonekana ni kuwa kwa Mzanzibari aitakiaye mema nchi yake ya ZANZIBAR basi nilazima atafute mbinu mpya zitakazoIwezesha kuinusuru ZANZIBAR . na hakika kuwa pamoja na ccm haitosaidia. maana Matatizo haya yote yanayotajwa yameletwa na hiyo ccm,aidha ccm wanashindwa kuyatatuwa matatizo hayo amabayo yashadumu kwa miaka mingi sasa.na siku hadi siku mambo yanazidi kuwa mabaya kwa upande wa ZANZIBAR.

  Mimi binafsi nimezungukwa na CCM damu lakini bila ya kukuficha kwa sasa hawana tena imani na CCM pamoja na serikali ya muungano.maana kwa maelezo yao wanakiri kuwa iwapo wanaitaka nchi yao ya ZANZIBAR basi ni lazima waikimbie CCM. miongoni mwao wanasisitiza kuwa ,kuwa CCM ni sawa na kuwa mjumbe wa kuingamiza ZANZIBAR..( hawa ninao wazungumzia hapa ni watu wangu wa damu halisa,miongoni mwao wapo wanaoshikilia Elimu za juu kabisa na wapo wasio na chochote kielimu )
  Point yangu hapa ni kuonyesha wasiwasi tuliokuwa nao wazanzibari wengi kuwa CCM na serikali ya muungano haiitakii mema ZANZIBAR. (FACT)

  Ndugu Rajab haji Machano. maelezo yako hapo juu yanaonesha kuwa u mtu muungwana halisi na mtu mwenye elimu na hikima.
  Kama haitokuwa tabu na kama sitokupa usumbufu ningelipenda unieleweshe ni kwa misingi gani ndugu yangu unaendelea kujinasibu na kuisapoti CCM,hasa ukizingatia hali ya zanzibar kisiasa,kiuchumi na kijamii ilipofikia sasa?
  Ahsante.

 3. Wewe SEDOUF unamuuliza mwenzio akupe misingi ya kuisapot CCM ili iweje? nawe utajiunga na ccm ama?maelezo yako yanajitosheleza umesema kuwa unamshkuru kwa kuitumia hgaki yake ya vizuri na ndio maana amejinasibu kuwa yeye ni mwana ccm, so muache mwenyewe ana sababu zake za msingi zio lazma akupe wewe..tuache siasa za chuki9 na kijinga ndio maana hatuendelei kwa upumbavu kama hbuu ungeambiwa ukasaidie kujenmgs nyumba za michenzani au any where ungeanza kuuliza wewe si ungekimbia tu..kila mtu na maisha yake cha msingi kaza buti kwa upande wako iusaidie nchi yako unajua kama tupo nyuma kiuchumi na maendeleo ingeneral so just mind ur business n plz jenga taifa la Zasnzibar kwa moyo wote mengine ya vyama waachie wenyewe wanaokereketwa na vyama vyao abaaaaaaaa!!

 4. Hivi hizi fyokonyoko za kisiasa huku CUF hazipo? Mbona tuna taarifa nyingi tu kutoka Pemba kuhusu misigano ya CUF lakini hairipotiwi katika ukurasa huu uliopewa jina la siasa za Zanzibar? Ni bora sasa uwe ‘Siasa za Unguja/CCM’ Hii biasing ya nini? Objectivity katika utoaji taarifa iko wapi? Au ndio propagating weapon ya CUF na nyinyi ndio maboi wa kuiwezesha??

 5. Sedouf anadai eti Kijana wa Kizanzibari halisi hawezi kuisapoti CCM!! Huu ni ulemavu wa fikra! Kama tunaangalia asili toka hapo kale kubwa basi ni wazi kuwa CUF tutaigundua kuwa ndio chama cha watu wageni hasa wale wenye asili ya ukoloni wa Kiarabu na vibaraka vyao! Ndio, huo ndio uhalisia. Sasa kitendo cha wazalendo halisi kuiunga mkono CCM ambacho kiasilia ndio chama chao cha ukombozi kina athari gani kwao?

 6. I know that you’re in the process of eliminating my thoughts, but since you’ve already gone through it I’m very much satisfied and not necesarily to be viewed by your general audience!

  1. WAZANZIBAR KUENDELEA KWENU HAKUHITAJI CHAMA CHA SIASA BALI NI UMOJA NA MATUMIZI BORA YA RASILIMALI ALIZO WAPA MUNGU BAHARI ,VIVUTIO VYA UTALII , FUNGUENI VIWANDA VYA KISASA BADALA YA KUNUNUA MAGOROFA TANZANIA BARA KESHO NA KESHO KUTWA HAMWEZI KUYAPAKIA KWENYE MELI KURUDI NAYO UNGUJA AU PEMBA WATU WA BARA WAME KUBALI KILA KITU WACHUKUWE WAGENI MUNGU WANGU JARIBUNI KUAMKA MUWE MFANO KWETU SISI WATU WA BARA MPO WACHACHE RAHISI KUSIKILIZANA MSIINGIE KWENYE MITEGO YA BARA POLENI SANA AMKENI SASA

 7. kwamtizamo wangu habarizenu hazipatikani kwa wakati mutambuwe wasomaji wenu wengi wako nje yanchi baada ya miezi mitatu ndo tunapata habari hiyo si sawa haturidhiki na utowaji wenu wa habari mikonyuma sana sana.

 8. CCM NA CUF NI VYAMA IMARA NA MAKINI NA VINA NIA YA KUWALETEA WAZANZIBARI UMOJA, MSHIKAMANO NA MENDELEO. MUNGU VIBARIKI.
  ANAESEMA HATUHITAJI VYAMA KUPATA MAENDELEO MIMI NAHISI NI MVIVU WA KUFIKIRI . HII NI KWASABABU KUPITIA VYAMA NDIO MADARAKA YA NCHI YANAPATIKANA NA UONGOZI HATA YA MATUMIZI YA RASILIMALI UNAANZIA HAPO.

 9. DUNIA HII HAIJA ANZA LEO SASA, TOKA HUKO NYUMA ENZI ZA UKOLONI,USULTANI HADI UHURU NI CHAMA GANI KIMELETA MAENDELEO TANZANIA KAMA SIO WA TANZANIA WENYEWE NDIYO MAANA TUNA TAKA WAGUMBEA BINAFSI HII NI KWA MUJIBU WA KATIBA YA NCHI LAKINI VIONGOZI WENGI WA VYAMA VYA SIASA NI WAOGA WA HILO, HESABU YA KARIBU WANA CHAMA WA VYAMA VYA SIASA HAWA FIKI MILLON SITA. SASA NDUGU YANGU SISI WAPENDA MAENDELEO TUNA FIKA MILLION AROBAINI, SI LAZIMA CHAMA HAPA, ILA UTARATIBU TUU ULIOZOELEKA NDIYO UANKUTISHA. MKOLONI ALIKUWA NA GAVANA MOJA TU ,LAKINI KILA KITU KIKWENDA SAWA KAMA MALIKIA ALVYO AGIZA. TUNATAKA SERIKALI YENYE MALENGO YA KISASA BILA KUTOA VISINGIZIO
  ASANTE -HAJI RASHID AMANI

 10. What it a first thing you are looking at when is situated on internet shop? Of course it is the variety of goods and prices. Assa.biz is the one of the biggest shops of electronic products, which can give their visitors qualitative goods and attractive prices. We offer to our customers magnificent service and fast delivery at any point of the country. And it means that your mood never will be bad because of any similar internet shop. All our clients remain happy after their every buy. So if you want to buy something for your home or to surprise your native with a good gift, just look through our internet shop and choose anything you want.store high-quality and inexpensive electronics
  Netbooks
  LG 47LW5600 47 Inch 3D 1080p 120Hz Smart TV LED
  ASUS Eee PC Seashell 1018P-PU27-WT 10.1-Inch Netbook (White)
  Gateway/Acer Retail, Dual-ScreenTouch-GorillaGlass
  Tablets
  Blu-ray Players

 11. Somebody essentially help to make seriously articles I would state. That is the very first time I frequented your web page and to this point? I surprised with the research you made to make this particular put up incredible. Great activity!

 12. I am not sure where you’re getting your info, but great topic.
  I needs to spend some time learning much more or understanding more.
  Thanks for magnificent info I was looking for this information for
  my mission.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s