Polisi wadaiwa kufanya unyama

Salum Bakari Muya anayedaiwa kuteswa kwa kukatwa ngozi kwa kisu kichwani na kisha kunyonyolewa nywele na baadhi ya vikosi vya ulinzi na usalama nchini ambapo alisema vikosi hao wakiwemo polisi ambao pia walikuwa na silaha.

MTU moja mkazi wa Mkele jana alinusurika kuuawa katika msako wa kuwakamata watu wanaotuhumiwa kusababisha vurugu zilizotokea wiki moja iliyopita mjini Zanzibar.
Vurugu hizo ziliibuka Oktoba 17 mwaka huu baada ya kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMUIKI) Sheikh Farid Ahmed Hadi kutoweka katika mazingira ya kutatanisha Oktoba 16, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa bahari mjini hapa jana, kijana aliyenusurika kuuawa, Salum Bakari Muya alidai aliteswa kwa kukatwa ngozi kwa kisu kichwani na kasha kunyonyolewa nywele polisi ambao pia walikuwa na silaha.

Sehemu ya ngozi aliyokatwa kijana huyo na jeshi la polisi

Alisema kabla ya kukutwa na tukio hilo alikuwa amekaa na wenzake wakiwa wanasubiri tenda ya mizigo ya kusafirisha kwa kutumia magari ya punda.
“Nilikuwa nabangaya – yaani kubangaiza –wakatokea polisi sita, walipofika nilipokaa wakanifunua kofia na kunikata kipande cha ngozi na nywele kichwani kwa kisu,” alisema Salum.
Alidai polisi waliomfanyia ukatili huo ni wa kikosi cha FFU na kwamba baada ya kitendo hicho waliamua kumpeleka kituo cha afya cha JKU kilichopoa Saateni kwa matibabu ya awali.
Salum alidai kuwa baada ya kupata matibabu katika kituo hicho cha JKU iliamriwa kwamba apelekwe Hospitali Kuu ya Mnazimoja kwa vile alikuwa anavuja damu nyingi.
Hata hivyo alisema alishangaa kabla ya kufika Mnazimoja polisi hao waliamua kumtekeleza katika eneo la kwa Abbas Hussein, kilometa chache kutoka walipomtoa hospitali ya JKU.
“Hawakunifikisha Manazimoja, wakaniacha na kuondoka huku wakisema ubaya ubaya mtakoma waambie na wenzio,” alisimulia Salum akiwa na bandeji aliyofungwa wakati anapata huduma ya kwanza.
Alisema baada ya kutelekezwa na polisi aliamua kwenda Welesi huko Kikwajini kwa lengo la kuzungumza na waandishi wa habari juu ya mkasa uliompata.
Baada ya kusimulia mkasa huo, Salum ambaye alifuatana na kaka zake walioomba wasiandikwe majina baadae alipelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.
Alipoulizwa juu ya tukio hilo, Kamishana wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema bado hajapopewa taarifa na kwamba iwapo mwathirika atalalamika kituoni polisi watachukua hatua ya kucunguza.
“Tumezoea kulalamikiwa, kama mtu amefanyiwa ukatili kwanini asiripoti kituo cha polisi, hapo ujue kuna jambo anaficha,” alisema Kamishna Mussa.
Lakini baada ya kuelezwa na mwamdishi wa habari hizi kwamba kijana huyo amepelekwa hospitali na kaka zake, Mussa alisema aliahidi kufuatilia tukio hilo.
Kitendo cha Salum kufanyiwa ukatili na watu wanaodaiwa kuwa polisi kimetanguliwa na matukio ya vijana wenguine wawili kuuawa wakati wa utekelezaji wa zoezi la msako huo mjini Zanzibar mwezi Oktoba mwaka huu.
Imedaiwa kuwa Hamad Ali Kaimu aliuawa Ijumaa iliyopitama wakati akiwa mikononi kuwa polisi katika eneo la Magomeni na Salum Hassan Mahanju alikufa baada ya kupigwa risasi katika maeneo ya Amani Fresh na watu waliotajwa kuwa maofisa ulinzi na usalama.

Mbali na vijana hao, askari mmoja Koplo Said Abdulrahman aliuawa na watu wasiojulikana huko Bububu baada ya tukio la kutoweka Sheikh Farid.

Tokea kuanza kwa vurugu hapa Zanzibar jumla ya watu watatu wamefariki ikiwa mmoja ameuwa na watu wenye hasira huku jeshi la polisi likidaiwa kuwauwa vijana wawili hali sio shuwari kufuatia unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na jeshi la polisi kwa kisingizio cha kuwatafuta wahahalifu.Wakati jeshi la Polisi visiwani Zanzibar likiendelea kuwasaka wahalifu, baadhi ya wananchi wamejitokeza kulalamikia juu ya operesheni hiyo ikiwemo ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi hilo uliosababisha kifo cha kijana mmoja akiwa mikononi mwa polisi. Bonyeza hapa kupata taarifa hiyo. 

Kufuatia kadhia hiyo DW ilimtafuta Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa na alikuwa na haya ya kusema Bonyeza hapa Tafadhali. 

Lakini Pia alitafutwa Kamishna wa Haki za Binaadamu Zanzibar, Bw. Zahor Juma Khamis ambaye naye alikuwa na haya ya kuiambia DW. Bofya hapa tafadhali.   

Mwili wa Marehemu Hamad Ali Kaimu anayedaiwa kupigwa risasi ya vikosi na kupata majeraha makubwa hadi kufa awali familia ya Marehemu iliususia mwili huo kutokana na kuwa walimchukua kijana wao akiwa hao na kumrejesha maiti

 

8 Replies to “Polisi wadaiwa kufanya unyama”

  1. Kila lenye mwanzo halikos kua na mwisho na hakika ya kila mtu atalipwa kwa alilo lifanya (kama tadinu tudani) ukiwa unatumia cheo chako kwa kunyanyasa hakika na wewe utanyanyaswa M/Mungu atulinde wazanzibar dhid ya hawa awnafik au wahafidhina pamoja na watanganyika yaarab kila ajae kwa shari ivunje yake dhamiri asiweze kusimama aaaaaaamin

  2. huyo kamishna kweli mpumbavu eti analalamika kwanini hajaripote polisi?mtu kapigwa na hao mapolisi halafu aende kituoni akaripoti nn?acheni mambo yenu hayo na nyinyi ni binaadamu leo kwa mwenzio kesho kwako,kwa maana hiyo kila ataekamatwa anakhusika na machafuko moja kwa moja?nyinyi ndio wavunjaji sheria halafu mnataka mtu aende wapi?tunajua zanzibar hakuna sheria mnafanya mnavyotaka nyinyi,umekuwa kituko sasa ngoja hao ma askari waje wampige mtoto wa yeyote ambae kiongozi au askari mwenzenu ndipo mtaanza kuuwana wenyewe kwa wenyewe maana zanzibar ndogo hiyo piga piga yenu iko siku mtampiga mtoto wa askari mwenzenu ambae nae ana silaha hapo atakapolipiza kisasi ndio mchezo utaanza,hamuwezi kuwabagua huyu nani na huyu nani si tunaendeleza chuki huo ndio utakuwa mwisho wake siasa za chuki tu.eti kapigwa na polisi halafu akimbilie polisi we kamishna umefika darasa la ngapi ki elimu?jichukulie wewe ungekuwa mwananchi umepigwa na polisi bila ya hatia je ungekimbilia polisi?kweli huyu jamaa katunukiwa cheti cha ujinga kweli hawajakosea,hata common sense huna?huyo aliepigwa na polisi?halafu akimbilie huko huko polisi wakammalize au vp?llaaanaaa tuuu lllah mapolisi wote wanaowapiga wananchi ovyo bila ya hatia,mwenyezi mungu akulipeni kwa hayo.

  3. Bw. Mussa Ali Umefeli na unaendelea kufeli kama ulivyofeli darasa la ……., unaonyesha ujinga wa hali ya juu kabisa kila unapotoa statment zako, bora huyo Bw. Aziz statment zake zimeenda shule. aibu kwako na unalitia jeshi zima aibu, noma mwanangu noma si mimi ni kauli zako zenye kujipinga, mara kundi limeona polisi likakimbia mbele imebadilika imekua kibaka anapigwa, na watu polisi wakamuokoa kumpeleka kumuua. kijana huyo huyo ukamwita ubaya ubaya, hebu namimi nikuulize kama wenzangu bwana mkubwa twambie umesoma hadi darasa langapi? hivi jeshi zima la polisi hakuna officer smart? marafiki zangu wasio wazanzibari wananicheka na kunifanyia inda, hebu mapolisi niokoweni.

  4. it is heart breaking tunapokwenda kubaya kwa hali hii nchi inatisha lakini polisi wakumbuke mkuki kwa nguruwe dooh…………..

  5. ndio faida ya muungano hiyo maafa yote hayo ni kupitia mkono wa taasisi za muungano halafu watanganyika wanafurahia lakini tupo hapa hapa kwani mtenda wema anaifanyia nafsi yake na mtenda maovu pia anaitendea nafsi yake .yaani ukiangalia hapa jamii forum watanganyika wanaonyesha chuki yao dhahiri kwa zanzibar hawa si wenzetu hawa tuachane nao.wanatamani tuangamie ndio lngo lao ila wkumbuke tu they will pay the price yatawarudia tu haya .watu wako kwenye nchi yao waliojaaliwa na mola wao hawataki kuburuzwa na nchi nyengine kwa kauli zao bila ya kushawishiwa na kutoka nje ya nchi yao nyie bado mnawahiliki na kuwauwa ivo nyinyi watanganyika kweli mna utu nyie.washenzi kweli nyie sisi hatutorudi nyuma bora mtuuwe sote halafu mje muishi nyie si ndo mnavotaka mbona sisi hatuhoji kuhusu mambo yenu huko tanganyika na wala hayatuhusu .hakuna hata siku moja mkaitakia mazuri zanzibar hatutaki nchi yetu nanyie si mna yenu chuki za nini .hamtosheki ,nyie wenyewe mnashindwa kujiongoza hatutaki ya nini kulazimishana .kwani lazima huu muungano si unganeni na burundi au ruanda nazo ni ndogo kama mikoa yenu.

  6. kuwapora wazanzibar nchi yao huo ndio uunjaji mkubwa wa haki zao tusiwe wanafiki sisi waafrika Zanzibar ni nchi waachie wazanzibari nchi yao mnawadhulumu halafu waafrika wote wamekaa kimya mnaendeleza ubaguzi, kunyimana haki,kunyanyasana na kuuwana wenyewe kwa wenyewe imefika pahali wanatanganyika kwa midomo yao wanatamka hasa ohhh Zanzibar si nchi oooo Zanzibar mkoa wetu mara nyinyi waanzibari tunakutawaleni kweli huu ni upendo kati yetu waafrika au kukebehiaana hii yote inadhihiri chuki yao kwa Zanzibar .tumechoka hatutaki tena muungano na watanganyika ya nini tena kulazimishana.kuna vijiinchi tele tu duniani vidogo kuliko Zanzibar na vina mamlakazao na kila kitu chao.huu si muungano ni hila tu za kuinakamisha Zanzibar.mfano Mauritius ni visiwa kama Zanzibar na wana mamlaka yao na wamepiga hatua kuliko hiyo Tanzania kwa ujumla sarafu yao ina thamani kuliko tsh na maisha yao yanatizamika ,twende Lesotho na Swaziland wamo ndani ya South Afrika na hakila kitu wanategemea South Afrika na hatujasikia hata siku moja kaburu au Madiba si Mbeki wala Zuma kusema Lesotho na Swazi ni mikoa ya South Afrika mjue kuwa nyinyi watanganyika hii dhambi ya kuikandamiza Zanzibar haitopita hivi hivi iko siku na haiko mbali itawarudia biidhnillah hilo mlijuwe.Kuna nchi ndogo sana europe inaitwa Andorra ,hii nchi ipo kwenye mpaka baina ya Spain na Ufaransa na ina mamlaka yake kamili ni mwanachama wa E.U, UEFA ,FIFA na IOC,U eneo lake la mraba Zanzibar ni kubwa ,raia wake ni kama laki tano isitoshe katika nchii hii wanaishi watu kutoka nchi mbalimbali kama waspain ,wareno,wafaransa.waingereza ,wabrazil,wamoroko n.k mamlaka ya nchi hii ipo mikononi mwa kanisa katoliki la nchi hii hakuna msikiti ila wamoroko ambao ni waislamu wameomba kujenga msikiti na maombi yao yanafanyiwa kazi.ukitaka kuingia nchi hii ni lazima upitie SPAIN ,Barcelona au FRANCE kwa sababu haina uwanja wa ndege ni lazima upitie mipakani na wala huulizwi mipaka iko wazi wapo askari wanakagua magendo n,k mimi binafsi sijawahi hata kuulizwa passport wala viza na napita kila siku.nchi hii ina raisi wake vyama vya siasa na uchaguzi mkuu na wanaopiga kura ni waandorra sio waspain si wafaransa wala wareno hawa wao ni wahamiaji tu kwa kufuata sheria zilokuwepo wa kuomba uhamiaji kwa kuwasilisha data zako zote za unakotokea na kupimwa afya yako kama ni nzuri ili usiambukize maradhi unalipa euro 21 unapewa kitambulisho cha ukaazi kwa sababu wao wenyewe wana vyeti vyao vya kuzaliwa na wakifika miaka 18 wanapeana passport moja kwa moja.kwa waspain upo mpaka ubalozi wa SPAIN kwa ajili ya raia zao. Tukija kwenye masuala ya kufanya kazi kama ni mgeni na tayari una ukaazi hapa, uhamiaji wanakupa fomu unaijaza wewe na alokuajiri unalipa euro21 na unafanya kazi.Andorra inanunua umeme SPAIN inatumia gati na uwanjandege Barcelona ,SPAIN ,uchumi wake ni utalii kwenye milima vya pyrenees wakati wa kiangazi na wakati wa baridi pia na biashara ya maduka kuuza bidhaa za electronic ,manukato,saa.nguo na mikahawa na mahoteli,mifugo na kilimo cha small scale mbogamboga na tumbaku kwa kutengeneza sigara na lugha yao official ni kikatalan ,lakini pia kinatumika sana kispain na kifaransa kumbuka kuwa katalani ni sehemu yote kutoka Toulose ya Ufaransa kupitia Andorra ,Barcelona yote hadi Valencia.France ndio mdau mkubwa wa maendeleo ya nchii hii.sio sisi waafiriti kazi kuuwana njaa tu na siasa uchwara hatuna maana pesa mbili ukienda zanzibar bampo la taka ukienda Dar utatapika uchafu mtupu kipindupindu tu faidaya raia wetu roho mbaya kwenda mbele tanganyika inaizibia zanzibar huku yenyewe raia wake wanasulubika kwa njaa maradhiya kila aina na umasikini wa kuoza wakati eneo hili la afrika ya mashariki lina kila ya aina ya rasilimali .tujue hizi zote ni laana kutoka kwa mungu dhidi ya chuki .fitna.na ufisadi tunaoufanya kwenye ardhi yake.MWENYE MACHO HAAMBIWI TIZAMA.
    WASSALAMU ALAIKUM .BWANA ASIFIWE .TUAMKE SISI WAFRIKA.

  7. Hivi nyinyi Mi CCM, ati kumeunguzwa maskani yenu ya kisonge,ndio mupoteze maisha ya watu wasio na hatia na wewe mshenzi kamishna wa Polisi Mussa jiandae kama hukulipata hapa duniani basi utalipata kesho Akhera inshaalah dhalimu mkubwa weeee!!!!

  8. Haya yote yanayotokea zanzibar huwenda ni mambo yaliyopangwa na serikali na sasa yanatekelezwa. Sababu ya kusema hayo ni kauli ambayo imetolewa ya kupigwa marufuku kwa vyombo vya habari kutotoa habari yoyo inayohusu muamsho au machafuko hayo. Hatujakaa vizuri serikali ikatangaza imekwisha uvumilivu kwa wanaohatarisha amani. kinacho tokea hatuoni kukamatwa kwa makundi yanayodhaniwa kuwa yapo ya ubaya ubaya na mengineo lakini ni kupigwa watu na kadhalika.
    ila haya serikali itambue si suluhisho la matatizo serikali iwasikilize wananchi wake na kuwatekelezea kile wanacho taka. kwa pampja tujenge zanzibar yetu.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.