Maadhimisho ya Taasisi ya Sayansi ya Bahari

Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari Zanzibar (IMS) Dkt. Yohana Shaghudi akisoma risala wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya utafiti yaliyofanyika Ofisi za Taasisi hiyo Mlindi Mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknologia Tanzania Dkt Hassan Mshinda alisema Taasisi ya Utafiti wa Sayansi za Bahari Zanzibar (IMS) imetoa mchango mkubwa katika kuimarisha Uchumi wa Zanzibar.

Amesema Utafiti wa zao la mwani ambao umefanywa na Taasisi hiyo umekuwa mkombozi kwa wanawake wengi wa Zanzibar hasa wanaoishi kando kando ya bahari ya Visiwa hivyo.

Dkt Mshinda aliaeleza hayo alipokuwa akifungua maadhimisho ya wiki ya utafiti katika Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar-es-salam iliopo Malindi Mjini Zanzibar .

Amesema zao la mwani hivi sasa linashika nafasi ya tatu katika kuingiza fedha za kigeni Zanzibar, ikitanguliwa na zao la karafuu na sekta ya utalii, na iwapo juhudi zitaendelezwa kunadalili miaka michache ijayo mwani ukachukua nafasi ya kwanza.

Ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kwa mwamko wake wa kuanzisha vitengo vya utafiti katika Wizara zote ikiwa na lengo la kushajiisha kufanyika tafiti mbali mbali na matokeo ya tafiti hizo kutumika katika kutekeleza sera kwa ajili ya maendeleo yake.

Alisema kuwa tafiti nyingi zinazofanyika nchini huchangia kukuza uchumi wa nchi na kupunguza umasikini kwa kuzalisha ajira nyingi zisizo rasmi hasa kwa vijana.
Alifahamisha kuwa lengo la Vyuo Vikuu pamoja na kufundisha wanafunzi pia vinajukumu la kufanya tafiti mbali mbali ambazo matokeo ya tafiti hizo yatatumika vizuri yananafasi kubwa yakuleta mabadiliko.

Dkt Mshinda aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taasisi ya hiyo ikiwemo kuwapatia eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 125 katika kijiji cha Buyu na hatua ya kuliendeleza eneo hilo zinaendelea.

Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari Dkt. Yohana Shaghude alisema Taasisi hiyo imepewa majukumu makubwa ya kufanya utafiti wa sayansi katika fani zote za bahari pamoja na kutowa ushauri bora wa matumizi ya bahari

Alisema lengo la kufanya tafiti za aina hiyo ni kutoa elimu pamoja na ushauri kwa wananchi jinsi ya njia bora ya matumizi endelevu ya rasilimali zilzopo.

Aliongeza kuwa tafiti zilizofanywa na Taasisi zimesaidia kudhibiti maeneo ya mwambao wa bahari , uimarishaji na ubunifu wa uendelezaji wa ufugaji wa chaza pamoja na uhifadhi wa matumbawe na mikoko.

“Taasisi ya sayansi ya bahari inajitahidi kulinda vizuri mazingira ya bahari na uendelezaji mzuri wa nishati katika bahari kama vile Mwani, Chaza,Samaki na Matumbawe” alisema Dkt Yohana.

Taasisi ya Sayansi za Bahari Zanzibar ilanzishwa Octoba 17 mwaka 78 ikiwa imeanza na wanataaluma sita na hivi sasa inatoa shahada za uzamivu na uzamili ikiwa chini ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Chanzo: Idara ya Habari Maelezo Zanzibar

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s