Matangazo ya TBC yakatika ghafla

Ni kweli hali ya bunge leo ilichafuka ghafla na kukazuka kelele Kutokana na kukatika kwa matangazo ya Televisheni ya Taifa (TBC) kulikotokana na sababu za kiufundi, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu amelazimika kuakhirisha kikao hadi Jumatatu ambapo kabla ya kusikilizwa taarifa za kamati nyengine itabidi Mjumbe wa Bunge hilo Tundu Lisu ataendelea na kutoa ufafanuzi waka ambao aliouanza leo kabla ya kukatika kwa matangazo hayo. Mwenyekiti wa Bunge Samwel Sitta alilazimika kusitisha shughuli hizo baada ya Mjumbe Freeman Mboe kutoa taarifa za kupokea kwa kukatika kwa matangazo huku baadhi ya wajumbe wengi wakiwa wametumiwa sms katika simu zao wakitaarifiwa kwamba matangazo hayo yanayorushwa moja kwa moja kupitia TBC hayapo hewani...Mwenyekiti alimtuma Katibu wake Yahya Khamis kwenda kusikiliza kinachoendelea na hatimae kuja na taarifa kwamba ni khitilafu iliyotokana na hali mbaya ya hewa huko Dar es Salaam ambapo kuna mvua tokea juzi...Hata hivyo baadhi ya wajumbe walipingana na uamuzi huo wakihoji ni kanuni gani inayosema kuwa kwa kuwa matangazo yamekatika ndio bunge liakhirishwe lakini Mwenyekiti alijibu kwamba kanuni inamruhusu Mwenyekiti kuchukua maamuzi ambayo anaona yanafaa na kutumia busara hivyo yeye ametumia busara kutokana na kuwa mjadala wa katiba muhimu kusikika na watanzania wote hivyo kwa umuhimu huo ili watu wengine wasije kuona kwamba matangazo hayo yanakatwa kwa hujuma au kuwanyima haki wengine na kuwapa fursa wengine ameamua kuchukua uamuzi huo ili kila upande uweze kusikika huko nje na umma wa watanzania na khasa kwa kuzingatia tayari kuna mkataba kati ya Serikali, Bunge na Shirika la Utangazaji (TBC) kwamba wataonesha live shughuli za majadiliano katika Bunge Maalumu la Katiba. hivyo basi wananchi walikataa kuendelea na mjadala huo hadi hapo matangazo hayo yatakaporudi na ndio Mwenyekiti akatumia busara kuliakhirisha Bunge hadi Jumatatu. Niliona ni vyema nilete hii taarifa ili watu wajue kilichotokea huko BUngeni maana kulishaanza maneno aaah CCM wamekatisha matangazo, wengine serikali haitaki kusikia mawazo ya Tundulisu ...aaaah hapana tutaendelea tena inshallah jumatatu pamoja uhai ambapo watakaotoa ufafanuzi ni kamati mbili zilizobaki ambazo ni Freeman Mboe na Ismail Jussa, baada ya wenye viti kuwasilisha maoni ya wajumbe wengi na wachache .
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Tundu Lisu akitoa ufafanuzi wa maoni ya wajumbe wachache wa kamati yake leo Bungeni ambapo matangazo yalikatika ghafla wakati akiongea.

Ni kweli hali ya hewa leo katika Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea huko Dodoma ilichafuka ghafla na kusababisha kelele na manunguniko kutoka kwa wajumbe wakilalamikia kukatika kwa matangazo ambapo matangazo yanayorushwa moja kwa moja (Live) na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kutoka Bungeni Dodoma yalikatika kulikotokana na sababu za kiufundi.

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samweli Sitta amelazimika kuakhirisha kikao hadi Jumatatu ambapo kabla ya kusikilizwa taarifa za kamati nyengine mbili zilizobaki itabidi Mjumbe wa Bunge hilo Tundu Lisu ataendelea na kutoa ufafanuzi waka ambao aliouanza leo kabla ya kukatika kwa matangazo hayo. Mwenyekiti wa Bunge hilo alilazimika kusitisha shughuli hizo baada ya Mjumbe Freeman Mboe kutoa taarifa za kupokea kwa kukatika kwa matangazo huku baadhi ya wajumbe wengi wakiwa wametumiwa sms katika simu zao wakitaarifiwa kwamba matangazo hayo yanayorushwa moja kwa moja kupitia TBC hayapo hewani…Mwenyekiti alimtuma Katibu wake Yahya Khamis kwenda kusikiliza kinachoendelea na hatimae kuja na taarifa kwamba ni khitilafu iliyotokana na hali mbaya ya hewa huko Dar es Salaam ambapo kuna mvua tokea juzi…

Hata hivyo baadhi ya wajumbe walipingana na uamuzi huo wakihoji ni kanuni gani inayosema kuwa kwa kuwa matangazo yamekatika ndio bunge liakhirishwe lakini Mwenyekiti alijibu kwamba kanuni inamruhusu Mwenyekiti kuchukua maamuzi ambayo anaona yanafaa na kutumia busara hivyo yeye ametumia busara kutokana na kuwa mjadala wa katiba muhimu kusikika na watanzania wote hivyo kwa umuhimu huo ili watu wengine wasije kuona kwamba matangazo hayo yanakatwa kwa hujuma au kuwanyima haki wengine na kuwapa fursa wengine ameamua kuchukua uamuzi huo ili kila upande uweze kusikika huko nje na umma wa watanzania na khasa kwa kuzingatia tayari kuna mkataba kati ya Serikali, Bunge na Shirika la Utangazaji (TBC) kwamba wataonesha live shughuli za majadiliano katika Bunge Maalumu la Katiba. hivyo basi wananchi walikataa kuendelea na mjadala huo hadi hapo matangazo hayo yatakaporudi na ndio Mwenyekiti akatumia busara kuliakhirisha Bunge hadi Jumatatu.

Juzi wakati akitoa ufafanuzi ya maoni ya wajumbe wachache Professa Ibrahim Lipumba pia matangazo hayo yalikuwa yakikatika katika jambo ambalo limekuwa likiwasumbua wananchi wengi ambao wanaofuatilia mjadala huo wa katiba na hivyo baadhi ya wananchi kujenga dhana kwamba hali hiyo husababishwa kwa makusudi ili kuwakosesha wananchi wasisikie maoni kutoka kwa wapinzani ambao wana haki sawa kama wanachama wengine ambao wanahitaji kusikiliza hoja za pande mbili.

Niliona ni vyema nilete hii taarifa ili watu wajue kilichotokea huko Bungeni maana kulishaanza maneno aaah CCM wamekatisha matangazo, wengine serikali haitaki kusikia mawazo ya Tundulisu …aaaah hapana tutaendelea tena inshallah jumatatu pamoja uhai ambapo watakaotoa ufafanuzi ni kamati mbili zilizobaki ambazo ni Freeman Mboe na Ismail Jussa, baada ya wenye viti kuwasilisha maoni ya wajumbe wengi na wachache.

 

2 Replies to “Matangazo ya TBC yakatika ghafla”

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.