SMZ yashauriwa kutumia kiswahili

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeshauriwa kutumia lugha ya Kiswahili katika sheria zinazotumika ndani ya nchi kwa kuwa asilimia 90 ya wazanzibari wanatumia Kiswahili. Ushauri huo umetolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) alipokuwa akiuliza swali la ngongeza wakati akitaka kujua kwa nini inatumika lugha ya kingereza katika miswaada inayowasilishw akatika barza la wawakilishi …

Zanzibar haihusudu Rwanda

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma amesema wananchi wa nchi ya Rwanda wanaheshimu sheria za nchi yao zinazotungwa na mabaraza ya sheria na ndio sababu kubwa ya kufika malengo yao katika suala zima la usafi katika nchi yao. “Wenzetu wa Rwanda wamefanikiwa kwa kuwa wanafuata sheria zilizotuungwa katika nchi yao na …

Rais asaini miswaada minne

Spika wa baraza la wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho amewaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba jumla miswada minne ya sheria iliyopitishwa na wajumbe hao katika kikao kilichopita tayari imetiwa saini na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na kuwa sheria kamili. Spika Kificho alisema hayo wakati akitoa taarifa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kuhusu …

Wawekezaji wakwepa kodi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekiri kwamba kuna baadhi ya wawekezaji wenye kuwekeza katika sekta ya utalii visiwani hapa huwa wanakwepa kulipa kodi hasa katika maeneo ya wawekezaji katika ukanda wa pwani. Hayo wameelezwa wajumbe wa baraza la wawakilishi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Mwinyihaji Makame Mwadini alipokuwa akijibu swali …

Hakuna dawa ya ukimwi

Na Salma Said, Zanzbar. HAKUNA DAWA YA UKIMWI Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar imesema bado juhudi za kutafuta kinga na tiba za dawa za kutibu virusi vya ukimwi zinaendelea duniani kote bila ya kufikia mafanikio hadi sasa na wenye kujigamba kuwa wana uwezo wa kutibu ukimwi watachuliwa hatua za kisheria. Akijibu swali …