UN hawatasimamia uchaguzi-SMZ

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Nchi za Ulaya (EU)hazitahusika katika kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Zanzibar . Waziri Kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha amebainisha hilo jana kwenye mkutano wa kampeni wa kumdani mgombea wa CCM jimbo la Magogoni,Asha Mohamed Hilal uliofanyika katika viwanja vya Diwani. …

Advertisements

CCM- mafuta sio ya muungano

Chama Cha Mapinduzi –CCM- Zanzibar kimesisitiza kuwa mafuta na gesi asilia si suala la Muungano bali liliomo kwenye orodha ya mambo ya muungano ni suala la uagizaji na uingizaji wa mafuta ya taa, dizeli na petroli. Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mjini Magharibi Yusuf Mohamed Yusuf amewaeleza wananchi jana …

CCM yawakemea wapinzani

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa (UVCCM) Hamad Yussuf Masauni amewakemea wapinzani wanaowatisha na kuwazomea viongozi wa Chama Cha Mapinduzi katika kampeni zinazoendelea katika uchaguzi wa mdogo Busanda. akihutubia wanachama wa CCM katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Magogoni Visiwani Zanzibar, Masauni alisema chama cha CHADEMA kinaendesha kampeni chafu huko Busanda …