Wakulima wa karafuu wahimizwa kuyatunza mashamba

IMG-20170810-WA0004

WAKULIMA wa karafuu kisiwani Pemba, wametakiwa kuyatunza mashamba wanayokodishwa na serikali pamoja na kuchuma karafuu kwa umakini.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Khalid Salum Mohammed, baada ya kushuhudia zoezi la ukodishaji wa shamba la mikarafuu katika bonde la Katumeni Makombeni wilaya ya Mkoani.

Alisema wakulima wanaokodishwa mashamba wanapaswa kuyatunza na kuyathamini ili msimu ujao karafuu ziweze kuzaliwa kwa wingi zaidi.

Alisema zao la karafuu limekuwa likisaidia uchumi wa Zanzibar kwa kupatikana fedha za kigeni hivyo wachumaji wanapaswa kuzianika vizuri ili ziuzwe kwa daraja la kwanza.

Alisema fedha zinazopatika kutokana na mauzo ya karafuu nje ya nchi, hutumika kwa shughuli mbali mbali za maendeleo ikiwemo kujenga hospitali, skuli, maji safi na salama miundombinu ya barabara.

Aidha alisema ameridhishwa na hali ya ukodishaji wa mashamba hayo inavyoendelea kwa kupitia mnada, na kuwahimiza wakodishaji kuongeza uadilifu zaidi.

Mapema Ofisa Mashamba kutoka idara ya misitu na mali asili zisizorejesheka, Haji Mussa Haji, alisema malengo yao ni kukodisha mashamba 1903 ambapo hadi sasa wameshakodisha mashamba 1,272 katika wilaya za Wete na Mkoani.

Alisema katika mashamba hayo tayari wameshakusanya jumala ya shilingi milioni 791.2 ambao wilaya ya Mkoani malengo yao ni kukodisha mashamba 683 na tayari wameshakodisha mashamba 408 yenye thamani ya shilingi milioni 70.5 na kwa wilaya ya Wete malengo ni kukodisha mashamba mashamba 1,220 na tayari wameshakodisha mashamba 864 yenye thamani ya shilingi milioni 720.7.

Alisema ukodishaji wa mwaka huu katika mashamba ya serikali umetoa nafasi kubwa kwa wananchi waliokuwa wakiyahudumia mashamba hayo.

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s