Watakiwa kusimamia mapato ya serikali

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imewataka Mawakala wa bima nchini, kutekeleza vyema majukumu ya kazi zao ili kuhakikisha mapato ya serikali yanaimarika.

 

Kamishama wa mamlaka hiyo, Dk. Baghayo Abdallah Saqware, aliyasema hayo katika uzinduzi wa mkutano wa tatu wa umoja wa mawakala wa bima Tanzania uliofanyika hoteli ya Sea Cliff Mangapwani wilaya ya kaskazini ‘B’ mkoa wa kaskazini Unguja.

 

Alisema kazi kubwa iliopo kwa mawakala hao ni kuongeza wigo katika utendaji wa kazi zao hasa kwa kutafuta njia muafaka za kuongeza matumizi sahihi ya bima kwa Watanzania ambao awali walikuwa hawatumii au walitumia kinyume na utaratibu wa sheria ziliopo.

 

“Nadhani umefika wakati sasa kwa mawakala kuhakikisha mnatoa elimu zaidi kwa Watanzania juu ya umuhimu wa bima ili wananchi wapate elimu sahihi ya kujiunga na huduma zenu, naamini mkifanya hivyo itasaidia kuongeza idadi ya watumiaji, lakini pia mtaisaidia serikali kuongeza mapato,” alisema.

 

Alisema mbali ya njia hiyo lakini pia ni vyema kwa mawakala hao kuhakikisha wanaongeza idadi ya wadau wa bima ambao wanaweza kutoa michango yao juu ya ukuaji na uendeshaji mzuri wa shughuli za bima nchini.

 

Hata hivyo, alisema mbali ya utekelezaji wa majukumu hayo lakini pia umoja wa mawakala hao kuliangalia kwa umakini suala la uajiri kwa watendaji wa chini katika shughuli ya kazi ya bima kwa kutoa kipaumbele kwa Watanzania ili kuisaidia serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa watu wake.

 

Aidha alisema serikali ipo tayari kutoa kila aina ya ushirikiano ili kuona kazi za bima zinafanyika katika utaratibu mzuri.

 

Rais wa umoja wa mawakala wa bima Tanzania, Mohamed Jaffer, alisema lengo la mkutano huo ni kuwakutanisha mawakala wote, kubadilishana mawazo, kutoa michango ya kimaendeleo, kujadili changamoto zinazowakabili pamoja na kutafuta njia muafaka za utekeleza majukumu ya kazi zao kila siku.

 

Alisema mbali ya mambo hayo lakini pia wameandaa utaratibu mpya wa kushirikiana zaidi na serikali katika kuhakikisha wanafikia malengo walijiwekea.

 

Naibu Kamishana bima Tanzania ofisi ya Zanzibar, Juma Makame, alisema suala la bima bado linahitaji ushirikiano wa wote.

 

Mkurugenzi wa fedha kampuni ya Tanzania, Reinsurance Limited, Glogar Ngonyan, alisema mwenendo wa ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya bima unaonekana kwenda vizuri hasa hivi karibuni serikali ilipoweka utaratibu mzuri wa malipo ya bima.

 

Chanzo: Zanzibar leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s