Jela kwa kutorosha

VILIO, simanzi zilitawala jana kwa familia ya mshitakiwa Hija Vuai Makame (25) mkaazi wa Jang’ombe baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka moja kwa kosa la kutorosha msichana wa miaka 16.

 

Baada ya mahakama kumpa nafasi ya mwisho ya kuomba, mshitakiwa aliangua kilio huku akiiomba mahakama impunguzie adhabu kwa sababu anategemewa na familia yake na kwamba kaka yake ni mgonjwa wa kifua kikuu na yeye ndie anaekwenda kumchukulia dawa.

 

Hakimu Chausiku Kafuti Kuya wa mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe, alisema ameridhika na maombi ya mshitakiwa na kumpa adhabu ya kutumikia kifungo cha mwaka mmoja.

 

Awali alisema upande wa mashtaka umethibitisha shitaka dhidi ya mshitakiwa, hivyo mahakama ikaamua kumtia hatiani.

 

Mbali ya mshitakiwa, mama yake pia aliangua kilio mahakamani akiomba mahakama imtizame kwa jicho la huruma mtoto wake kwani anategemewa na familia.

 

Mwendesha mashitaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Said Ali aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa huyo ili kurejesha imani za wananchi kwa vyombo vya sheria.

 

Ilidaiwa mshitakiwa huyo alipatikana na kosa la kutorosha msichana aliyechini ya uangalizi wa wazazi wake kitendo ambacho ni kinyume na kifungu 130 (a) sheria namba 6 ya mwaka 2004 sheria za Zanzibar.

 

Ilidaiwa mshitakiwa bila halali alimchukua mtoto huyo ambae hajaolewa na yupo chini ya uangalizi wa wazazi wake kutoka nyumbani kwao Muembenjugu na kumpeleka Fuoni na baadae kumpeleka Melinne Magirisi bila ridhaa ya wazazi wake kitendo ambacho ni kosa kisheria.

 

Tukio hilo lilidaiwa kutokea Febuari 25 mwaka jana saa 3:00 usiku Mwembenjugu wilaya ya mjini mkoa wa mjini magharibi Unguja.

 

Katika kesi hiyo upande wa mashitaka uliwasilisha jumla ya mashahidi watano akiwemo mtoto alietoroshwa.

 

Zanzibar Leo ikizungumza na mama mzazi wa mtoto huyo, alisema familia imepata pigo kubwa kwani mwanawe ndie anaemtegemea kwa kila kitu ikiwemo usimamizi wa ndugu zake.

 

“Najua mitihani ya mungu tu ila tutavumilia kwa yale yote yaliyotokea najua ipo siku mwanangu atapata haki yake,” alisema.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s