Hatari yawanyemelea wagojwa wa macho

 

WASTANI wa wagonjwa wa macho 3,000 kutoka mikoa mbali mbali ya Zanzibar na baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa macho na kupatiwa huduma, katika kambi ya siku tano iliopo Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU), Tunguu mkoa wa kusini Unguja.

 

Kati yao, wagonjwa 500 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya jeshi Bububu.

 

Hayo yalielezwa na Mtatibu wa huduma za macho Zanzibar, Dk. Fatma Juma, katika hafla ya ufunguzi wa kambi hiyo, ilioandaliwa na Chuo Kikuu cha Zanzibar kwa kushirikiana na kitengo cha uratibu wa macho Zanzibar, chini ya madaktari bingwa kutoka nchini Pakistani na Saudi Arabia.

 

Dk. Fatma alisema kiasi cha watu 6,500 wapo katika hatari ya kutoona kabisa kutokana na kukabiliwa na aina tofauti za maradhi ya macho.

 

Alisema kati ya wagonjwa hao, 3,500 ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa mtoto wa jicho, wanaweza kuondokana na hali hiyo iwapo watapatiwa huduma za operesheni.

 

Akigusi uwepo wa kambi hiyo, Dk. Fatma alisema ina lengo la kuwaondolea tatizo la tiba wananchi wanaokabiliwa na ugonjwa huo.

 

Nae Waziri wa Afya, Mahamoud Thabit Kombo, aliwataka wananchi wenye matatizo ya macho kujitokeza ili kupata matibabu.

 

Alisema wataalamu hao wamejipanga vilivyo kutoa msaada kwa ndugu zao wa Zanzibar, hivyo akatoa wito kwa wananchi kutumia ipasavyo fursa hiyo.

Alisema ili uchumi wa Zanzibar uweze kuimarika hakuna budi kuwa na watu wenye afya bora.

 

Aidha aliema serikali inaendelea na juhudi za kuimarisha miundombinu ya afya pamoja na kupunguza ghara za upatikanaji wa huduma na dawa kwa lengo la kuwapunguzia ukali wananchi katika upatikanaji wa huduma za afya.

 

Katika hatua nyengine, aliwataka wataalamu hao kuangalia uwezekano wa kutoa fursa kwa madaktari wa macho wazalendo kujifunza kutoka kwao, kupitia programu zao za mafunzo wanazotoa.

 

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s