Sekta ya utalii iimarishwe

ikulu.jpg

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, ameitaka Kamisheni ya Utalii kuongeza kasi katika kuimarisha dhana ya utalii kwa wote kwani imeanza vizuri katika kufikia lengo lililokusudiwa.

 

Aliyasema hayo, alipokutana na uongozi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo, Bodi ya Wakurugenzi ya Kamisheni hiyo na Menejimenti katika vikao vinavyoendelea Ikulu mjini Unguja.

 

Alieleza kufurahishwa na kasi iliyoanzishwa na Kamisheni hiyo katika kuuimarisha utalii kwa wote pamoja na kuimarisha mapato na kusisitiza kuwa utalii ndio unaotegemewa kwa kiasi kikubwa katika kuongeza pato la taifa.

 

Alisisitiza haja ya kuandaa mpango thabiti wa kuimrisha utalii wa ndani na kueleza kuwa wananchi wengi wamekua wakisia sifa za maeneo ya kitalii yakiwemo ya kihistoria lakini hawayajui.

 

Mapema, Dk. Shein alikutana na uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Barabara na kueleza haja kwa uongozi wa mfuko huo kutoa mafunzo kwa watendaji kwa lengo la kuwa na wataalamu watakaosaidia masuala ya ujenzi wa barabara.

 

Alisema ipo haja ya kuiwezesha Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara (UUB) ikiwa ni pamoja na kuwatafutia vifaa na kueleza azma ya serikali ya kununua mtambo wa lami na kusisitiza kuwa mfuko huo umefanya kazi vizuri zaidi ya sheria iliyounda mfuko huo.

 

Akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Magazeti ya Serikali  pamoja na uongozi wake, alieleza kuridika kwake na gazeti la Zanzibar Leo hasa pale lilipoanza kuchapishwa Zanzibar kwani fedha nyingi zilikuwa zikitumika kulichapisha Tanzania bara.

 

Alisema hatua hiyo ni uamuzi wa serikali kwani ilijianda kulichapisha gazeti hilo Zanzibar huku akieleza haja kwa uongozi wa gazeti hilo kutoa zawadi kwa waandishi wao huku akisisitiza haja ya ushirikiano kwa bodi, uongozi na wafanyakazi wa gazeti hilo.

 

Aidha, alisema ni vyema gazeti hilo likatoa taarifa zake vizuri ili wananchi wapate habari za kwao kwani wananchi wamekuwa wakipenda kusoma na kufahamu habari za nyumbani.

 

Aliahidi kulitafutia ufumbuzi suala la usafiri kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa shirika hilo haraka iwezekanavyo.

Nae Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi,  aliupongeza muko wa barabara kutokana na uangalizi mzuri wa barabara.

 

Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo, Rashid Ali Juma, alitumia fursa hiyo kueleza mafanikio yaliopatikana katika Shirika la Magazeti huku akimpongeza Dk. Shein kwa kulipatia shirika hilo ofisi za kudumu.

 

Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, alisisitiza haja ya kujitangaza zaidi kiutalii kwa kutambua kuwa Zanzibar ina vivutio vingi vya kitalii ambavyo vyengine hata havijajulikanwa.

 

Nao uongozi wa mfuko wa barabara ulieleza mafanikio yaliopatikana katika mfuko huo ikiwa ni pamoja na kurahisisha upekekaji maendeleo kwenye maeneo yalioongezeka.

 

Nao uongozi wa Kamisheni ya Utalii ulieleza kuwa idadi ya watalii walioingia nchini imeongezeka kutoka 294,243 mwaka 2015 hadi 376,242 mwaka 2016 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 27.9.

 

Ulisema idadi ya watalii kutoka katika masoko mapya yakiwemo Urusi, Ukraine, Jamhuri ya Czech, China, India na Israel imeongezeka kutoka 25,677 mwaka 2015 hadi 53,852 mwaka 2016 ambayo ni sawa na aslimia 110.

 

Aidha, ulieleza kuwa idadi ya watalii wanaorudi matembezi yao hapa Zanzibar imeongezeka hadi kufikia asilimia 17 huku ukieleza kuwa makusanyo ya Kamisheni ya Utalii yameongezeka kutoka shilingi bilioni 1.4 mwaka 2014 hadi shilingi bilioni 2.2 mwaka 2016/2017.

 

Nao uongozi wa Shirika la Magazeti ya Serikali kwa upande wake ulieleza mafanikio iliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuhamia katika jengo la kudumu na gazeti  kuchapishwa Zanzibar.

 

Mhariri Mtendaji wa shirika hilo, Yussuf Khamis alisema gazeti hilo limesambaa Tanzania nzima na kueleza kuwa limekuwa na mvuto.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s