Madawa yampeleka jela

MAHAKAMA ya Wilaya ya Chake Chake, imemuhukumu Kifungo cha miaka mitano Jela, Mshitakiwa Ramadhan Said Mohammed (24) Mkaazi wa Chachani Chake Pemba, baada ya kubainika na kosa la kukamatwa na madawa ya kulevya.

 

Hukumu iyo ilitolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo,  Nyange Makame Ali, baada ya kubainika kupatikana Madawa ya kulevya kinyume wa kifungu 16 (1)(a) cha sheria namba 9 Mwaka 2009, kama ilivorekebishwa na Sheria Namba 12  ya mwaka 2011sheria ya kuzuia uingizaji na utumiaji wa madawa ya kulevya sheria za Zanzibar.

 

Kwa upande wake muendesha mashitaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, DPP  Moh’d Ali Juma, aliomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ,ili iwe fundisho kwa wenye tabia ya kuuza, uingizaji au usambazaji wa madawa ya kulevya.

 

“Vijana wengi wamekuwa wakipoteza mwelekeo wa maisha yao kwa utumiaji wa madawa huku Taifa likikosa nguvu kazi  “alidai DPP huyo.

 

Kabla ya Mshitakiwa huyo kupewa hukumu hiyo katika utetezi wake alidai kuwa yeye hahusiki na shutuma  hizo na dawa hizo za kulevya hazikuwa zake .

Alidai siku ya tukio alikuwa amekaa maeneo ya Swahili Diver  Chachani  ,ndipo walipotokea askari  na kumkamata baada ya muda mfupi ndipo alipooneshwa madawa hayo na kuambiwa ni yake.

 

Mshitakiwa huyo hata hivyo, aliomba Mahakama imuangalie kwa jicho la huruma kwani hahusiki na kesi ya madawa hayo.

 

Hapo awali, ilidaiwa mahakamani hapo Mshitakiwa huyo mwezi  June 27 mwaka 2016, majira ya saa 3:45 Usiku,  huko Chachani Swahili Diver Chake chake Pemba, bila ya halali alipatikana na kete 40 za unga unaosadikiwa kuwa ni madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa 0.332 kilogaram.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s