Lazima watoto walindwe – TAMWA

mzuri-issa-tamwa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

06/Agosti/2017

TAMWA inasikitishwa na vitendo vinavyoendelea vya watoto kufungiwa kwenye gari, kukosa hewa na wengine kufariki. Hivyo inatoa wito kwa vyombo husika hasa Jeshi la Polisi kuchunguza matukio hayo kwa kina kwani yanatia wasiwasi.  Inakuwaje ajali kama hiyo itokee mara mbili katika eneo moja na tena ndani ya mwezi mmoja?

Katika mwezi Julai pekee yamepatikana matukio mawili ya aina hiyo ambayo yote yametokea Jang’ombe ambapo watoto wamekutwa katika magari yaliyoegeshwa pembezoni mwa barabara, wanne walikutwa tayari wameshaaga dunia na katika tukio la mwisho wa mwezi Julai wawili walikutwa wahoi ndani ya gari lililofungwa.

Julai 16 mwaka huu watoto wanne walifariki dunia baada ya kujifungia/kufungiwa kwa muda mrefu katika gari iliyokuwa imeegeshwa pembezoni mwa barabara katika maeneo ya Kidongo Chekundu mjini Zanzibar. Watoto hao walitambuliwa kuwa ni Haitham Mustafa Abuubakar (2)  mkaazi wa Kidongo Chekundu, Muslihi Hamza Bakari  (2) mkaazi wa Jang’ombe, Dodo Muhammed miaka miwili na miezi saba mkaazi wa Jang’ombe na Munawar Ahmed Khamis (3) mkaazi wa Jang’ombe.

Jumamosi Julai 29, 2017 watoto wengine 2 walikutwa katika gari lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara katika eneo la Meya Jang’ombe ambalo lilikuwa limefungwa.  Waliokuwamo ndani ya gari hilo wote ni watoto wa familia moja.

 

Sheha wa Shehia ya Jang’ombe Khamis Ahmad Salum alisema matukio hayo yanatia shaka, hivyo alilishauri jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina.  TAMWA inaunga mkono wazo hilo na inasisitiza kuwa vyombo vinavyohusika kulinda hali na mali za raia vifuatilie kwa karibu suala hili ili kuwaondoa hofu wananchi kuwa watoto wao wako salama.

 

Tunalishauri Jeshi la Polisi kufanya upepelezi kuhusu matukio haya kwani si ya kawaida na yanaonekana kuendelea na lisingojee kupewa taarifa ndipo lifanye kazi yake.

 

Kadhalika tukio kama hilo liliwahi kutokea Dunga, wilaya ya Kati, mkoa wa Kusini Machi 28, 2016 ambapo watoto watatu walikutwa wamefariki kwenye gari, watoto hao Sumaiya Yussuf (5), Firdaus Hassan Rajab (5) na Latifa Hassan Rajab (3) walikutwa katika gari saa moja za usiku wakiwa tayari wameshaaga dunia baada ya kufungiwa mchana kutwa.

 

Haki na ulinzi wa watoto uko mikononi mwa jamii nzima.  Tunatoa wito kwa wazazi, walezi na Serikali kuweka mipango mikakati madhubuti kuwalinda watoto kwa kila tukio la uvunjaji wa haki zao kama vile kuwaua, kuwatesa na kuwadhalilisha. Tunawashauri wazazi kuwaangalia watoto wao kwa karibu zaidi ili kufahamu mienendo yao ili kuweza kuzuia uharibifu mapema iwezekanavyo.

 

MZURI ISSA ALI

MKURUGENZI TAMWA

ZANZIBAR.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s