‘Eco School’ Elimu ya Mazingira ianzie Skuli

88d7c89a6067273c1f0f4d5fde423242_400x400

WALIMU Kisiwani Pemba wametakiwa kuwafunza watoto juu ya umuhimu wa suala zima la kuhifadhi mazingira katika maeneo yao.

 

Akizungumza katika ufunguzi wa Semina kwa Walimu wa Skuli zilizojiunga katika mradi wa ‘Eco School’ iliyofanyika katika ukumbi wa mkutano Gombani Chake Chake, Mratibu wa Zayadesa Said Shaaban, alisema.

 

lengo la mradi huo ni kuzisaidia taasisi za kielimu ili waweze kuwafundisha wanafunzi juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

 

Mratibu huyo alieleza Walimu ndio wenye jukumu la kuwafunza wanafunzi walioko mashuleni katika kuyatunza mazingira yaliyowazunguka hivyo ni wajibu wao kutoa taaluma hiyo kwa wanafunzi hao.

 

Sambamba na hayo Mratibu huyo aliwafahamisha walimu kuwa bado mabadiliko ya tabia nchi ni athari kubwa kwa viumbe hai hivyo ni lazima kufuata elimu inayotolewa na wataalamu ili kuepuka hali hiyo.

 

Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo, Mkufunzi kutoka taasisi ya Zayadesa Pemba, Kassim Matitu, alieleza kuwa ‘Eco School’ haiwahusu wanafunzi au walimu peke yao bali ni jukumu la watu wote katika jamii kama Wazazi,Wafanyabiashara, Mashirika yanayoshughulikia masuala ya mazingira pamoja na viongozi wa Serikali za mitaa.

 

Matitu, alifahamisha   ili Skuli iweze kuingia katika mpango huo wa Ikolojia Skulini ni lazima ijidhatiti katika miongozo saba ambayo itaifanya Skuli hiyo iwe ni miongoni mwa Skuli zinazotambuliwa.

 

“Mambo saba ambayo itaifanya Skuli kutambuliwa au kujiunga na mpango huu wa Ikolojia Skulini ni pamoja na kuiarifu na kuishirikisha jamii, kuendesha uhakiki wa mazingira,kuandika muongozo wa Ikolojia,kuunganisha mada na mitaala kuendeleza mpango kazi, kuanzisha kamati za shule pamoja na kufuatilia na kutathmini maendeleo”alifahamisha Matitu.

 

Nae  Meneja wa mradi huo, Talib Kassim, wakati akiwasilisha mada alisema   mradi huu sio kwa Tanzania pekee, bali umeenea ulimwenguni kote ambapo kiasi cha nchi 59 ikiwemo Tanzania tayari zimeshajiunga na mradi huo.

 

“ Huu sio mpango wa Tanzania pekee bali hata huko nchi za wenzetu mpango huu upo na kwa sasa kiasi cha nchi 59 zimejiunga na mradi huu na wanafunzi wapatao milioni 18 tayari washajiunga”,alieleza Meneja huyo.

 

Meneja huo alisema kwa upande wa Zanzibar baadhi ya Skuli za msingi na Sekondari tayari zimeshajiunga ambapo hadi sasa Skuli zipatazo 30 zimejiunga ikiwa katika Kisiwa cha Unguja ni Skuli 21 na Pemba ni Skuli 9.

 

Nae Mwalimu Nassor Mohamed Omar wa Skuli ya Conecting, alisema kuanzishwa kwa mradi huo Skulini kwao kumeleta faraja kubwa kutokana na kupata mafanikio makubwa hasa katika suala zima la kilimo.

 

Alieleza kwa sasa wanafunzi wao wamekuwa ni mabalozi wakubwa katika jamii yao inayowazunguka kutokana na kupata taaluma ya kuhifadhi mazingira

 

Kwa upande wake, Mwalimu kutoka Skuli ya Sekondari Wete, Rukia Salim Haji, alisema   faida waliyoipata katika kuanzishwa kwa Ikolojia Skulini, wameweza kulima mboga mboga katika maeneo yao ya Skuli ambayo imewasaidia katika matumizi yao ya hapo Skuli.

 

Mbali na hayo lakini pia wameweza kuweka mazingira safi na yenye kuvutia katika jamii na hivyo kuifanya Skuli yao ipendeze kwa watu.

 

Mafunzo hayo ya siku moja ambapo lengo lake ni kuwapiga msasa walimu wa Skuli waliojiunga na na mradi huo wa ‘Eco School’ jumla ya mada 5 ziliwasilishwa katika mafunzo hayo.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s