Mchezo wa ngombe utambuliwe

3

WACHEZAJI wa Ngombe Kisiwani Pemba, wameiyomba Serikali kuwathamini na kuwatambua kama wanavyo watambua na kuwapatia misaada wachezaji wa mpira wa miguu.

 

Walisema wachezaji wa mpira wa muguu wamekuwa na hadhi kubwa Zanzibar, lakini wachezaji wa mchzo wa ngombe ambao ndio asili ya utamaduni wa wazaznibari wamesahaulika pamoja na mchezo wenyewe.

 

Mussa Mbarouk alisema mchezo wa ngombe ni utambulisho tosha wa utamaduni wa mzanzibari, lakini umesahaulika  kutokana na serikali kutokuujali mchezo huo.

 

Alisema kutokana na hali hiyo sasa mchezo huo umekosa hata wachezaji mahiri waliokuwa wakitambulika, pamoja na kutokuwepo kwa ng’ombe wenye hadhi ya kuchezeka.

 

“wachezaji wengi wameacha kucheza mcheoz huo, kutokana na kuona wanachokipata hakiendani na hali halisi ya masiha ilivyo”alisema.

 

Salim Talib Kombo alisema sasa wakati umefika kwa serikali kuufufua mchezo huo, kwa mwaka japo mara mbili kuchezwa ili vijana waweze kujuwa histia yao.

 

Alisema mchezo huo umepoteza haiba na utaalamu wake ulioku aukitumika kuchezwa, hivyo ni vizuri serikali andaa matamasha ya kila mara kwa mchezo huo.

 

Mwajuma Omar Ali alisema zamani walikuwa wkaipiga makofi kila unapochezwa mchezo huo, lakini sasa vijana wamesahau utamaduni wao.

 

Alisema kwa sasa mchezo huo umepoteza wachezaji kutokana na vijana wengi kutokuwa tayari kucheza kutokana na matatizo mbali mbali.

 

Mwajuma alisema wachezaji wanapoumia wanashindwa kuhudumiwa, hali inayowafanya vijana kuukimbia na kukimbilia mpira wa miguu.

 

Chanzo: Zanzibar Leo

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s