Watoto 32,412 wasajiliwa kielektroniki

WATU 32,412 wamesajiliwa katika mfumo mpya wa utoaji vyeti vya kuzaliwa tokea kuanza mfumo mpya wa usajili, ulioanza Aprili 2016.

 

Alisema tayari watu 20,261 wamepatiwa vyeti baada kukamilisha taratibu za usajili.

 

Mfumo huo umeanza kwa baadhi ya vizazi ambavyo vimeanza mwaka 2012-2016 ambao ndio walioingizwa katika mfumo huo na vyote vinavyoendelea kuzaliwa sasa.

 

Akizungumza na Zanzibar Leo ofisini kwake Mazizini, Mrajisi wa Vizazi na Vifo Zanzibar, Shaaban Ramadhan Abdalla, alisema kwa sasa wanaoendelea kusajiliwa na kuingizwa katika mfumo huo ni  watoto waliozaliwa 2010 hadi 2011.

 

Alisema kuna mafanikio mengi yaliyopatikana kupitia mfumo huo ikiwemo udhibiti wa taarifa za wasajiliwa na uhakika wa cheti kinachotolewa kwani awali vyeti vingi vilivyotolewa vilikuwa na makosa.

 

“Hivi sasa hatumsajili mtu kama hana vitambulisho vyake na mweza wake hii inatupa urahisi kujua taarifa sahihi,” alisema.

 

Aidha alisema ofisi yao imekuwa ikihudumia watu 60-70 kulingana na mwamko wa wananchi wanaofika kupata huduma lakini malengo yao ni kuhudumia watu 100 kwa siku.

 

Akizungumzia changamoto zinazowakabili katika mfumo huo, alisema ni pamoja na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu vielelezo wanavyotakiwa kuwasilisha wakati wa usajili kwa kuona wanahangaishwa pamoja na wahusika kutoenda wenyewe kutoa taarifa.

 

Alisema katika kupunguza usumbufu, siku za usoni taarifa za usajili zitasajiliwa hospitali baada ya watoto kuzaliwa.

 

Akizungumzia malalamiko yanayotolewa na wananchi kutopata huduma kwa urahisi zaidi pamoja na kuwa na vielelezo kamili, alikiri kuwepo kwa malalamiko hayo lakini wanayafanyia kazi.

 

“Kweli wanakuja watu na vielelezo kamili lakini sisi tunatoa huduma mchanganyiko kwa mfano anakuja mtu wa 2015 na rekodi zake hazimo katika mfumo huu hadi tukamtafute chini katika rikodi zetu, kweli tunamrudisha na huo ndio usumbufu unapojitokeza,”alisema.

Alisema hatua nyengine zinazotarajiwa kufanyika baadae ni kutenganisha watu ambao watapatiwa huduma katika wilaya zao ikiwemo wilaya ya mjini, magharibi ‘A’ na magharibi ‘B’ ambapo kwa kiasi kikubwa itapunguza msongamano.

 

Aliwaomba wananchi kutambua kuwa ofisi hiyo ina malengo mazuri ya kuwatumikia wananchi kama dhamira ya serikali iliyonayo ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma zao za msingi.

 

Aliwahimiza wafanyakazi kuwa na moyo wa kujitolea katika kutoa huduma kama inavyotakiwa bila kuchoka.

 

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s