Ofisa anaswa kwa tuhuma za rushwa

1

MAMLAKA ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), inamshikilia mtendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZAEMA) Ali Othman Mussa, kwa tuhuma za kupokea rushwa ya shilingi milioni tatu, kutoka kwa mlalamikaji mkaazi wa Chake Chake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mdhamini wa mamlaka hiyo Pemba, Suleiman Ame Juma, alisema mtuhumiwa alikamatwa Julai 31 mwaka huu akiwa ofisini kwake Machomane.

Alisema walimkamata baada ya kuweka mtego kufuatilia mlalamikaji kwenda ZAECA kuripoti kuwa mtendaji huyo anamdai rushwa ili aruhusiwe kujenga kiwanda cha mbao katika eneo la Gombani.

“Mlalamikaji alikuja ofisini kwetu na kutuambia kwamba amedaiwa rushwa na mtendaji wa ZAEMA ndipo aruhusiwe kujenga, hivyo tukaandaa mtego kwa kumpa fedha zetu na baada ya kupokea tulimkamata,” alisema.

Alisema awali mlalamikaji alizuiliwa kujenga kwa kisingizo kwamba alitaka kujenga kituo cha kuuzia mafuta (sheli) wakati lengo lake ni kujenga kiwanda cha kupasulia mbao.

“Kwa vile ZAEMA ndio wenye jukumu la kumruhusu mtu kujenga, mlalamikaji hakuruhusiwa kujenga mpaka apeleke fedha taslimu, jambo ambalo lilimfanya kukimbilia ofisi zetu kuripoti,” alisema.

Alisema mtuhumiwa amefikishwa mahakamani na ameachiwa kwa dhamana.

Aliwaomba wananchi kuendelea kuiunga mkono ZAECA ili kukabiliana na vitendo vya rushwa.

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s