Hekta 560 zimechimbwa mchanga

mchanga

 

JUMLA ya hekta 560 zimechimbwa mchanga kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya kaskazini ‘B’ Unguja na kusababisha upungufu   mkubwa wa rasilimali hiyo.

 

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Hamadi  Rashid Mohammed, aliyasema hayo Kinduni wilaya ya kaskazini ‘B’ alipokuwa akizungumza na Madiwani na baadhi ya maofisa  wa Idara ya Misitu na Maliasili Zisizorejesheka katika semina ya siku moja  kuhusu changamoto ya uhaba wa mchanga  unaoikabili Zanzibar  na jinsi  ya  kukabiliana na tatizo hilo kwa siku za baadae.

 

Maeneo yanayochimbwa mchanga katika wilaya ya kaskazini ‘B’ ni Pangatupu, Mangapwani, Donge Chechele na Zingwezingwe.

 

Alisema wilaya hiyo ilikuwa  ikitegemewa kwa kuzalisha mazao mbali mbali ya kilimo lakini kutokana na wananchi  waliokuwa wakilima katika maeneo hayo  kubadilisha matumizi ya ardhi  kwa  kuchimba mchanga badala ya kilimo kulikosababishwa na kukua  kwa sekta ya ujenzi, kulipunguza  shughuli za kilimo na hivyo  kuifanya wilaya hiyo kuwa masikini.

 

“Kuyabadilisha mtumizi katika maeneo ya kilimo na kuchimba mchanga ndio sababu pekee kulikoifanya wilaya ya kaskazini B kuwa masikini,” alisema.

 

Hata hivyo, aliwataka Madiwani  kuwaelimisha wananchi wao katika maeneo  wanayoishi   ikiwa ni pamoja na wanafunzi  kuhusu hali  halisi ya upungufu wa mchanga  unaoikabili Zanzibar kwa sasa.

 

Alisema wizara inakusudia kuandaa mwongozo wa kuagiza mchanga, kokoto, mawe na kifusi kutoka nje ya  nchi  ili kukabili tatizo liliopo.

 

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya  wilaya ya kaskazini ‘B’, Fatma  Juma Mohammed,  alisema wameandaa programu ya kuwashajihisha wanafunzi wa skuli za wilaya hiyo  kupanda  miti kwa lengo la kuwaandaa kuanza kujitegemea mapema  katika maisha yao ya baadae.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s