Fundo kupata umeme

DSC_0029

 SHIRIKA la Umeme Zanzibar (ZECO) leo linatarajia kusafirisha waya wa umeme wa baharini ambao unatarajiwa kupeleka umeme katika kisiwa cha Fundo kilichopo Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.

 

Akizungumza na waandishi wa habari katika bandari ya Malindi Unguja, Meneja Mkuu wa shirika hilo, Hassan Ali Mbarouk, alisema hatua hiyo imekuja kutokana na ahadi ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, ya kufikisha umeme katika kisiwa hicho.

 

Alisema waya huo uliotengenezwa China una uzito wa tani 50 ambao utachukua umeme kutoka kisiwa cha Ukunjwi hadi Fundo.

 

Aidha alisema waya huo una uwezo wa kutoa huduma kwa muda wa miaka 30.

 

Alisema kazi ya kutandika waya huo inatarajiwa kuanza Agosti 6 na zoezi hilo linatachukua siku tano hadi kukamilika.

 

“Wananchi wa Fundo wajiandae kuanzia Agosti 11 kupata huduma ya umeme, hivyo watumie fursa hiyo kunufaika na huduma hiyo kwa shughuli mbali mbali za maendeleo,” alisema.

 

Akizungumzia gharama za mradi huo, alisema zaidi ya shilingi bilioni mbili zimetumika fedha ambazo zimetolewa na serikali.

 

Alisema usambazaji wa waya huo utafanywa na wafanyakazi wa ZECO kwa kutumia meli ya Mv. Jitihada.

 

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuitunza miundombinu ya huduma hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

 

Alisema baada ya kisiwa hicho kuunganishwa na huduma ya umeme, visiwa vitakavyosalia ambavyo havina huduma hiyo ni Njau, Kokota na Uvinje lakini serikali inaendelea na mchakato kuhakikisha huduma hiyo inafika katika visiwa hivyo siku za usoni.

Chanzo: Zanzibar Leo

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s