Polisi yanasa wanunuzi karafuu mbichi

IMG_7790

 Wakutwa wakipima kwa kikombe na pishi

 JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, limefanikiwa kuwakamata watu watatu akiwemo mwanamke mmoja, wanao tuhumiwa kujihusisha na ununuzi wa karafuu mbichi kwa njia ya kikombe na pishi huko Tandavili shehia ya Piki Wilaya ya Wete.

 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Wete, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Kamishna Msaidizi wa Polisi, Haji Khamis Haji, amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Raya Issa Khamis anayedaiwa kuwa ndiye mnunuzi.

 

Kamanda Haji aliwataja watuhumiwa wegine kuwa ni Ahmada Maulid Ali na Abdalla Nassor na kusema kuwa   watuhumiwa hao wote kwa pamoja, wamenaswa kwenye mtego uliowekwa na askari wa Jeshi lake Jumatano iliyopita majira ya saa 2:30 usiku.

 

Alisema, kwa sasa watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na Jeshi la Polisi na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili na kuendesha shughuli za uhujumu wa uchumi wa nchi.

 

“Tunawashikilia watu watatu ambao tumewakamata wakituhumiwa na kosa la kununua karafuu mbichi kwa njia ya kikombe na pishi, jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi, kwani mwenye mamlala ya kununua karafuu ni Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC) pekee lililopewa mamlaka na nguvu kisheria”, alifahamisha.

 

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman, amevitaka vyombo vya ulinzi kufanya upelelezi na uchunguzi wa kina ili sheria mpya ya karafuu ianze kutumika kwa watuhumiwa hao.

 

Alisema serikali imetuga sheria hiyo ili kuwadhibiti wananchi wanaohujumu uchumi kwa kuuza karafuu kwa njia zisizokubalika, na kuwataka wakulima wa karafuu kuendelea kutoa taarifa sahihi kwa vyombo vya ulinzi wanapobaini kuwepo na vitendo vya uhujumu wa uchumi.

 

“Serikali imekusudia kupambana na wanaohujumu uchumi wa nchi kwa kuuza karafuu sehemu zisizo kubalika, na sheria ya karafuu itaanzia kwa watuhumiwa hawa hivyo ni vyema vyombo vya sheria kufanya uchunguzi wa kina ili adhabu kali ziweze kuchukuliwa”,alisisitiza.

 

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwashauri wakulima wa karafuu, kushirikiana pamoja na serikali ili kuweka ulinzi katika mashamba yao kwa lengo la kudhibiti vitendo vya wizi wa karafuu.

 

Alifahamisha kuwa vitendo vya kuuzwa karafuu kwa njia ya pishi na kikombe unachagiwa na vijana ambao wanaendesha vitendo vya wizi katika mashamba ya wakulima.

 

Nao wakulima wa karafuu Mkoa huo wamelalamikia vitendo vya wizi unaofaywa na watu wasiojulikana hasa nyakati za usiku na wamekuwa wakifuatilia na kumlinda mkulima anapoondoka ndio vitendo hivyo hufanyika.

 

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s