Dereva Bodaboda waiangukia serikali

BODABODA.Still001

SIKU moja baada ya Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi kuendesha operesheni za pikipiki zinazosafirisha watu maarufu kama ‘bodaboda’, madereva wa pikipiki hizo wameiomba serikali iwaruhusu waendelee kufanya biashara ya kubeba abiria.

 

Wakizungumza na Zanzibar Leo katika maeneo tofauti walisema, serikali imekuwa ikiwahimiza vijana kujiajiri, lakini cha kusikitisha wamekuwa wakibugudhiwa katika kazi zao ambazo zimekuwa sehemu ya ajira.

 

Aidha, walisema wakiamua kuondoshwa katika biashara hiyo ni vyema kutafutiwa njia nyengine ya biashara ili iweze kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku.

 

“Kutuondosha hivi tutakuwa hatuna imani kwani wangetuwekea utaratibu mwengine wa kujiajiri ili tuweze kuendesha familia zetu, wengine fedha za kujikimu tunapata katika biashara hii,”alisema Najim Suleiman mmoja wa madereva hao.

 

Alisema kitendo cha serikali kuwazuia kufanya biashara ya bodaboda kinaweza kuwaingiza vijana wengi kwenye mambo ya kihalifu kwani hawatakuwa na kazi.

 

Naye Hassan Muhidin, alisema ni vyema kwa serikali kuzingatia ombi lao kama Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, kuwawekea mazingira bora vijana ambao wamejiajiri katika biashara ya hiyo.

 

“Kwa kweli serikali ituonee huruma imesema tujiajiri, tunajiajiri na tunapata fedha angalau za kujiendesha sisi na familia zetu, lakini hivi sasa watatusababisha tuibe na kujiingiza katika matendo ya kihalifu ambayo hayana maana,” alisema Muhidin.

 

Nae, Katibu wa Bodi ya Usafiri Barabarani, Mohammed Simba Hassan, alisema hadi sasa serikali kupitia sheria ya usalama barabarani ya mwaka 2003 haijaingiza usafiri wa bodaboda kuwa bishara rasmi katika visiwa vya Zanzibar.

 

Alisema, kabla ya kuruhusu biashara hiyo kuna kazi kubwa ambayo inatakiwa kufanywa ili kuhakikisha kwamba wafanyabiashara hao wafahamu sheria za barabarani, ikizingatiwa wanafanya makosa mengi ikiwemo kuendesha bila ya kuwa na leseni.

 

“Kwanza tusaidiane kwa watu hawa kufahamu sheria za barabarani na tukesharidhika kwamba wanafahamu, basi si vibaya maombi haya kuletwa katika vyombo vyetu na kuyafanyia kazi, lakini kwa sasa bado kabisa kwani ukiangalia uendeshaji wa vyombo hivi tu hauridhishi kwa madereva na wengine hata kufanya vitendo vya kihalifu,” alisema.

 

Sambamba na hayo, aliendelea kuwasisitiza kuwa, wana deni kubwa kwa serikali kujiridhisha ili kuona biashara hiyo itaweza kuruhusiwa hapa Zanzibar.

 

Nae, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkadam Khamis Mkadam, alisema katika operesheni iliyofanyika wilaya ya Magharibi ‘B’ jumla ya bodaboda tisa zilikamatwa huku wilaya ya mjini ni 15 ambapo wamiliki wake watafikishwa katika vyombo vya sheria.

 

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s