Mtoto aliyetelekezwa

MH.SHADYA M.SULEIMAN

WIZARA ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto imekabidhiwa mtoto aliyeokotwa baada ya kutelekezwa na mama yake huko  katika shehia ya Mzambarauni  wilaya ya Wete.

 

Mtoto huyo ambaye alikuwa chini ya Wizara ya Afya tangu Julai 2 mwaka huu, amekabidhiwa kwa Naibu waziri wa wizara hiyo na Ofisa Mdhamini wizara ya Afya Pemba akiwa na afya njema.

 

Akizungumza baada ya kumpokea mtoto huyo, Naibu waziri Shadya Mohammed Suleiman aliwapongeza madaktari wa hospitali ya Wete kwa kusimamia na kuimarisha maendeleo ya afya ya mtoto huyo.

Alisema kwa mujibu wa taratibu na sheria mtoto huyo atakuwa chini ya serikali kupitia wizara ya Uwezeshaji na atakuwa kwenye mikono salama.

 

“Kuanzia leo (jana) mtoto huyu atakuwa chini ya serikali kupitia wizara ya Uwezeshaji na atakuwa katika nyumba za serikali zilizo Mazizini mjini Unguja”,alifahamisha.

 

Aidha aliwataka akinamama kujiepusha na vitendo vya kuwatupa watoto baada ya kujifungua na badala yake wafuate huduma za uzazi wa mpango ambazo zinatolewa bure.

 

Naibu Waziri pia ametumia fursa hiyo kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua stahiki kwa wanaohusika na vitendo hivyo vya kuwatupa watoto wachanga baada ya kujifungua.

 

“Kumchukua mtoto huyu isiwe ndiyo mwisho na suluhisho na kitendo cha kutupwa mtoto, hivyo naviomba vyombo vya sheria kuendelea kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hili na kisha kuchukua hatua stahiki”, alisisitiza.

 

Mapema Ofisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba, Bakar Ali Bakari amesema mtoto huyo ambaye amepokelewa katika hospitali ya Wete na amekuwa katika mikono salama chini ya uangalizi wa madaktari.

 

Alifahamisha kwamba tangu siku aliyokotwa alikuwa chini ya wizara ya Afya na alikuwa anapata huduma akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.

 

Hata hivyo, ndugu na jamaa wa mtoto huyo ameiomba serikali kutoweka vikwazo wakati watakapo hitaji kumuona mtoto wao, ambapo Naibu Waziri aliwataka kufuata taratibu kisheria wanapoahitaji kumuona mtoto wao.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s