Wanawake wabanwa na mfumo dume

IMG_3155

WANAWAKE wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wamelalamikia tatizo la baadhi ya wanaume kuendeleza vitendo vya ukandamizani kwa wanawake ikiwemo kuwazuia na kuwakataza wasijiunge na vikundi vya ujasiriamali.

 

Wakizungumza katika kikao maalumu cha kutoa elimu ya ujasiriamali huko Donge mkoa wa Kaskazini Unguja, wanawake hao wamesema wengi wao wamepata mwamko wa kujiunga na vikundi vya ujasiriamali vinavyoanzishwa kwa ajili ya kujikwamua na umasikini.

 

Kwa upande wake, Fatma Juma Masoud alisema baadhi ya wanaume wamekuwa wakiwazuia kushiriki harakati za kimaendeleo kwa madai kwamba pahala sahihi kwa mwanamke ni jikoni na ulezi wa watoto nyumbani.

 

Alieleza kwamba kwamba wanawake wa mkoa huo wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo umasikini, kupigwa na waume zao, udhalilishaji wa kijinsia na kunyimwa haki zao za msingi.

 

Hata hivyo, wakati wanawake hao wakizungumza kwenye mkutano huo  walionyesha wasiwasi kuendelea na ndoa zao, kwani pale watakapobainika kutoka kwa waume zao watapewa talaka.

 

Naye Halima Haji Ali alilalamika kuwa uwepo wa mfumo dume ulioota mizizi ambao walisema unachangia kuwakatisha tamaa wanawake walioamua kujiajiri kupitia nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa mtandao wa wajasiriamali wanawake vijijini, Siti Abbas Ali, alisema taasisi yake kwa kushirikiana na kituo cha huduma za sheria Zanzibar, wameweka mikakati ili kuwawezesha akinamama kujiajiri.

 

Aliitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake ili waweze kubadilika na kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwa ni pamoja na kujiajiri wenyewe.

 

Aliwataka wanawake wanaowekewa vikwazo na waume zao kupeleka malalamiko yao katika taasisi zinazohusiana na masuala yao ili yapatiwe ufumbuzi.

 

Alifahamisha kuwa, wanawake wana haki sawa na wanaume hivyo ni vyema akinababa wawahamasishe wake zao kushiriki hatika harakati za kimaendeleo na kufuta mitazamo hasi kwamba wanawake ni chombo cha starehe.

 

Mwenyekiti huyo alisema mtandao wao unaelewa kuwa katika mkoa huo kuna baadhi ya wanaume wanaendekeza mfumo dume kwa kuwazuia wake zao hata kufanya biashara ndogondogo, jambo alilosema limepitwa na wakati.

 

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s