Ujenzi barabara Kizimbani-Kiboje waanza

IMG_1792

WIZARA ya Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, imeanza matengenezo ya kuweka kifusi barabara ya kutoka Kizimbani hadi Kiboje, kufuatia kuharibika kulikosababishwa na mvua za masika zilizopita.

 

Akizungumza na waandishi habari, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mustafa Aboud Jumbe, alisema kazi za uwekaji wa kifusi zitachukuwa siku 10 na itaiwezesha barabara hiyo yenye urefu wa kilomita saba kutumika bila ya usumbufu.

 

“Kwa sasa wizara imeamua kuihami hii barabara kwa kuweka kifusi na kuwaondolea kero ya usafiri wananchi”, alisema.

 

Hata hivyo, alisema, azma ya serikali ni kuijenga kwa kiwango cha lami ambacho kitaiwezesha kutumika kwa muda wote wa miongo.

 

Katibu huyo, alisema, awali barabara hiyo ilikuwemo katika programu iliyohusisha barabara ya Jendele-Unguja na Koani-Jumbi, lakini, kufuatia kuondolewa kwa mkadarasi aliyekuwa akitarajiwa kuzijenga barabara hiyo kulifanya kuchelewa kwake.

 

Hivyo, alisema, ni matarajio ya wizara kwamba baada ya kazi hiyo ya uwekaji wa kifusi kwa hatua za awali, utoaji wa huduma za usafiri ikiwemo gari za abiria zitarejea baada ya madereva kugoma kuzipeleka gari zao huko kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dk. Idrissa Muslih Hija, alielezea kufarijika kwake kutokana na matengenezo hayo baada ya kilio cha siku nyingi cha wananchi wa Miwani na vijiji jirani vinavyotumia barabara hiyo.

 

“Sisi serikali ya Mkoa sasa kidogo tunaweza kuwa na amani, tulikuwa tukipita kwenye kipindi kigumu kutokana shida za usafiri wanazozipata wananchi wetu”, alisema.

 

“Lakini kwa hatua hii ya uwekaji wa kifusi, angalau utaleta faraja kabla ya serikali kuijenga kwa kiwango cha lami@, aliongeza.

 

Baadhi ya wananchi walisema, hatua hiyo ya serikali imefufua matumaini yao ya kuzidi kujiletea maendeleo baada ya kukata tamaa kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

 

Diwani wa Wadi ya Kiboje, Victor Fabian, alisema, ni faraja kubwa kwa wananchi ambapo sasa watakuwa wakifanya majukumu yao kama wazalishaji wa sekta ya kilimo kwa uhakika kutokana na kuimarishwa kwa barabara hiyo.

 

Naye dereva wa njia ya Kijichi-Miwani, Juma Mussa Ame, alisema, kutengenezwa kwa barabara hiyo kutawawezesha kurudisha huduma ya usafiri ambayo waliisitisha kutokana na ubovu wa barabara uliyopelekea kuharibika kwa magari.

 

Mapema, Mbunge wa Jimbo la Uzini, Salum Mwinyi Rehani, alisema, ubovu wa barabara hiyo ulikuwa ukiipotezea serikali mapato kutokana na watalii kushindwa kufika eneo la kitalii liliopo Kizimbani hasa wakati wa mvua.

 

“Ni barabara yenye vipaumbele karibu saba ambavyo vilihitajika kwa ajili ya huduma za kijamii”, alisema.

 

Hivyo, alisema, kukamilika kwa uwekaji wa kifusi utarahisha huduma za kijamii kwa wananchi ikiwemo usafirishaji wa mazao, huduma za afya, elimu kilimo kwa ujumla.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s