Tatizo la kitoweo Z’bar kuondoka

IMG_20150731_084710

WAZIRI wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed, amesema Zanzibar inaweza kukidhi mahitaji ya samaki ikiwa wananchi watafuata mbinu bora za ufugaji wa samaki.

 

Alitoa kauli hiyo ofisini kwake Maruhubi nje kidogo wa mji wa Zanzibar, kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wavuvi na wafugaji wa vifaranga vya samaki wa Unguja na Pemba.

 

Alisema wananchi wa Visiwa vya Zanzibar wapatao 23,000 ni wavuvi, huku watu 30,000 wanajishuhulisha na shuhuli  za baharini, hivyo ikiwa watakuwa makini juu ya mafunzo wanayopatiwa tatizo za upungufu wa samaki litapungua.

 

Alisema ufugaji wa samaki kwa njia ya mabwawa ni njia pekee itakayomuwezesha mvuvi au mfugaji kuweza kupata samaki, hivyo ni vyema kwa wavuvi kutumia njia hizo za kitaalamu.

 

Alifahamisha kuwa wataalam hao wanapotoa mafunzo visiwani watajua mazingira ya wavuvi ya ufugaji wa samaki na njia hiyo itawawezesha kutoa mafunzo kulingana na mazingira yaliyopo.

 

Alifahamisha kuwa katika ufugaji huo kutakuwepo na kampuni ambayo itashuhulikia masuala yote ya uvuvi ambapo wavuvi na wananchi watanufaika na ufugaji huo.

 

Alisema Zanzibar ina eneo kilomita 60 za maji madogo na kilomita kilomita 300,000 za maji makubwa ambayo yanaweza kukuza uchumi maradufu wa nchi.

 

Alifahamisha kuwa katika uzalishaji wa vifaranga pia Zanzibar itashirikiana na Shirika la Chakula Ulimwenguni (FAO) katika kuhakikisha wanaendeleza uvuvi wa samaki kwa njia ya mabwawa.

 

Kwa upande wao wavuvi waliopatiwa mafunzo walisema wanaishukuru wizara hiyo na Shirika la FAO kwa kuwapatia mafunzo yatakayowawezesha kupambana na umaskini.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s