pencheni yaongezwa maradufu

IMG_2606

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeongeza asilimia 125 pencheni kwa watumishi wake wastaafu, ili waweze kujikimu mahitaji yao ya kimaisha.

 

Waziri asiekuwa na Wizara Maalum Said Soudi Said alieleza hayo wakati alipokua akizungumza na gazeti hili katika maeneo ya Malindi mjini Unguja.

 

Alisema hatua hiyo imedhihirisha  wazi umakini na umahiri mkubwa uliopo katika serikali ya awamu ya saba, inayoongozwa na Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye anazingatia vya kutosha hali ya jamii.

 

Aidha alisema, utekelezaji wa mabadiliko hayo ya pencheni kwa wastaafu, yameanzia mwisho wa mwezi wa Julai, ambapo baadhi ya wastaafu hao wanapokea  zaidi ya shilingi 80,000 na wengi zaidi 100,000 kwa mwezi.

 

Waziri huyo alisema, kutokana na jitihada za serikali za kusimamia vyema mapato, matumizi mabaya ya fedha za umma pamoja na kuthibiti mianya ya fedha imesaidia kuimarisha uchumi wa taifa, sambamba na serikali kusimamia zaidi maslahi ya wananchi wake.

 

Alisema suala jengine lililochangia upatikanaji wa mafanikio hayo ni pamoja na utekelezaji wa ilani ya CCM, ambayo imetoa fursa kwa wananchi kuzitumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya maendeleo.

 

“Dk.Shein ndani ya uongozi wake anatilia mkazo na kulisimamia ipasavyo suala la amani na utulivu, ambapo leo wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba wanaendelea kujivunia hazina hiyo muhimu”, alisema.

 

Alifahamisha miongoni mwa sekta zinazoendelea kuimarishwa nchini hasa ikizingatiwa ni sehemu muhimu kwa maslahi ya wananchi na taifa ni kilimo, utalii, afya, elimu na usafiri.

 

Akizungumzia kuhusu hali ya siasa, alisema hana sababu wala mbinu za kubeza ilani na sera za CCM, hasa akizingatia ndio dira la upatikanaji wa maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

 

Hata hivyo alisema, Serikali ya Zanzibar na Tanzania kwa jumla zimejaa wanasiasa wenye uwezo na upeo wa utekelezaji wa ilani ya CCM.

 

“Ni vyema wanasiasa wakaondokana na siasa za chuki na ubaguzi ni wakati wa kuimarisha maendeleo yetu kwa malengo ya vizazi vyetu”, alisema.

 

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s