Serikali yatakiwa kuwalipa wakulima Bungi

DSC_0107

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imetakiwa kuwalipa zaidi ya shilingi 105.2 wakulima 42 walioathiriwa vipando vyao, ili kupisha ujenzi wa mnara wa kurushia matangazo wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

 

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Valentine Andrew Katema wa mahakama ya mkoa Vuga, wakati alipokuwa akisoma hukumu ya kesi ya madai iliyofunguliwa na wakulima hao dhidi ya serikali.

 

Kati ya fedha hizo shilingi 55,202,487.5 ni fidia za vipando vyao vilivyoathirika na shilingi 50 milioni ikiwa ni usumbufu walioupata katika kesi hiyo.

 

Wadai hao walilazimika kufungua kesi ya madai mahakamani hapo, kupinga malipo ya awali waliyopewa na serikali, ambayo hayakukidhi na hali halisi ya tathmini ya vipando vyao.

 

Katika malipo hayo, wadai hao 42 kwa pamoja walilipwa kiasi cha shilingi 15,002,881 badala ya shilingi 70,203,368 walizotakiwa kulipwa awali, baada ya kufanyiwa tathmini juu ya hasara itakayopatikana katika vipando vyao.

 

Hivyo kutokana na mapungufu hayo, wakulima hao walilazimika kuifungulia kesi ya madai serikali ili waweze kulipwa kiasi cha fedha kilichobakia.

 

Katika kesi hiyo, wadai hao wameiomba mahakama kuitaka serikali kuwalipa fedha za fidia zilizobakia, kama walivyokubaliana hapo awali kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa.

 

Sambamba na ombi hilo, pia wameiomba mahakama kuitaka serikali iwalipe shilingi milioni 100 ikiwa ni gharama za usumbufu waliokabiliana nao katika kesi hiyo, huku gharama za ufunguaji wa kesi hiyo ikiwa juu ya serikali.

 

Baada ya kusikiliza pande mbili hizo, Hakimu Valentine alikubaliana na wadai hao na kuitaka serikali ilipe fidia iliyobakia, pamoja na gharama za usumbufu kwa kima cha shilingi milioni 50 badala ya shilingi 100 milioni, kama walivyoomba wadai hao.

 

Mdaiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambapo katika uamuzi huo, Hakimu Valentine amemtaka pia kulipa gharama za ufunguaji wa kesi hiyo.

 

Haki ya rufaa kwa upande ambao haukuridhika na uamuzi huo umetolewa na Hakimu Valentine Andrew Katema mara baada ya kumaliza hukumu hiyo.

 

Chanzo: Zanzibar Leo

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s