Nyumba za Fumba sio za matajiri pekee

maxresdefault

FUMBA Town Development, inatarajia kufanya maonesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa katika mradi huo ikiwemo ujenzi wa nyumba za kisasa ili kuhakikisha wazanzibari wanafaidika na mradi huo.

 

Maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika Agosti 5 hadi 6 ambayo yatakayofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud.

images

 

Akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake Migombani, Mtendaji Mkuu wa Fumba Town, Tobias Dietzold, alisema katika maonesho hayo kutakuwa na vitu mbalimbali ikiwemo kuingia katika nyumba hizo, kutembelea bustani na kuangalia jinsi gani ya maji taka yanavyosafishwa na kuwa maji safi.

 

Alisema, pia wazanzibari wataweza kujionea taka zinazosarifiwa kwa kutengeneza mbolea asili za mimea, namna gani ya kuweza kujiajiri kwa kutumia kazi za mikono sambamba na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa Zanzibar.

Strassenperspektive-Post-01_nachtrag

“Waje waangalie, wafahamishwe, waelezwe namna gani kila mzanzibari anaweza kufaidika na kushirikiana katika mradi huu na kupata maelezo kuhusu ujenzi wa nyumba zetu, kazi tunazofanya, kusafisha maji machafu na kuangalia namna gani tunavyotumia takataka kutengeneza mbolea,” alisema.

 

Mtendaji huyo, alisema sababu za kuanza maonesho hayo ni kutangaza kwa wananchi juu ya kuona kila mzanzibari anaweza kufaidia na mradi wa Fumba Town.

Boulevard_render

“Lengo letu ni kufungua milango kwa wazanzibari kujua malengo ya nyumba hizi kununua kwa bei nafuu au kujisajili kwa kukodi kwa kwa shilingi 200,000”. alibainisha.

 

Aidha, alisema asilimia kubwa ya wazanzibari wana mawazo potofu ya kuona nyumba hizo zipo kwa ajili ya matajiri pekee jambo ambalo sio sahihi.

DSC_0023

Alibainisha kuwa, ifahamike kuwa kila mzanzibari anaweza kufaidika na mradi huo na kuingia katika maisha ya kisasa, mapya kwa kuishi na maji safi, kuacha kuchoma moto taka barabarani na kuishi kwa uhuru katika majengo madhubuti.

 

Nae Meneja Mauzo, Said Ali Said, alisema tayari baadhi ya wazanzibari wamejitokeza kununua nyumba hizo wakiwemo wafanyabiashara wa Zanzibar na Tanzania watu wa kawaida wakiwemo wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Diaspora ambao watakabidhiwa rasmi nyumba zao katika maonesho hayo.

DSC_0029

Alisema, lengo la mradi huo si kujenga nyumba za biashara bali ni kujenga mji ambao utakuwa unajitegemea na kujiendesha wenyewe.

 

Hivyo, aliwaomba wazanzibari kutumia fursa zinazotolewa na Fumba Town Development ili kuhakikisha kila mzanzibari anafaidika na mradi huo.

DSC_0100-Edit

Mradi huo, ulifunguliwa Agosti 8 mwaka 2015 na mwishoni mwa mwaka 2016 ulianza rasmi ujenzi ambapo hadi sasa jumla ya nyumba 75-80 zimeshafika katika hatua ya kuezekwa huku awamu ya kwanza itakuwa na nyumba za makaazi ya watu 1020.

chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s