Tanzania yakana kuingilia uchaguzi Kenya

dr-augustine-mahiga

Yasema hakuna mtambo wa kuchakachua matokeo

 

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Augustine Mahiga amesema Tanzania haijawahi wala haitathubutu kwa namba yoyote kuingilia siasa za nchi nyengine nchi rafiki na marafiki kama Kenya.

 

Waziri huyo alitoa ufafanuzi huo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana Tanzania na Kenya kuondolea vikwanzo vya bidhaa na huduma vilivyokuwa wamewekeana.

 

Alisema siasa za Tanzania ni kutoingilia siasa za nchi nyengine, ambapo imelenga zaidi ni kukuza urafiki kwa wote, ukiwemo wa kiserikali na  kutambua vyama mbali mbali vya siasa.

 

“Tunasema uhakika kabisa ni serikali ambayo daima imekuwa karibu na serikali ya Kenya suala la uchaguzi na kuhesabu kura ni suala la wakenya wenyewe, haijawahi Tanzania kuingilia Kenya na Kenya haijawahi kuingia Tanzania katika masuala ya uchaguzi”, alisema.

 

Alisema hatua inatokana na tuhuma zinazoelezwa na vyombo vya habari vya Kenya na baadhi ya wabunge wa upinzani, kuituhumu Tanzania kingilia uchaguzi wa Kenya.

 

Dk. Mahiga alisema hivi karibuni alikuwa nchini Kenya ambapo gazeti la The Standard linalochapishwa nchini humo limeandika habari za kuituhumu Tanzania kuingilia uchaguzi wa Kenya, jambo ambalo sio kweli.

 

Mbele ya waandishi wa habari, waziri huyo alishangaa Tanzania kuingilia uchaguzi huo kukoje, wakati suala hilo hapo awali limeshawahi kutolewa ufafanuzi wa kutosha.

 

Alisema wakati wa kuhesabu kura duniani kote kunakuwa na taarifa mbalimbali, ambapo sayansi hivi sasa imekuwa kwa vile kura zinahesabiwa kwa mfumo wa kielektroniki ambapo hakuna nafasi ya uchakachuaji.

 

Alidokeza taarifa za kila kituo cha kupigia kura huwa zinapelekwa makao makuu ya kuhesabu kwa njia ya kielektroniki na sateliti inanasa kutoka kila kituo hadi makao makuu ya Tume ya Uchaguzi.

 

“Utaalamu huu inawezekana yale masafa yakanaswa kuwa hesabu hiyo imetoka pointi ‘A’ kwenda ‘B’, hivyo kunakuwa na uwiano wa taarifa zinazotangazwa kutoka katika kituo kimoja na kwenda chengine”, alisema.

 

Alisema kwa sayansi ya sasa unaweza kunasa taarifa hadi nje ya nchi, kama unaweza kunasa Ujerumani kutoka Kenya, ambapo kuna taarifa wanasema mitambo ya kunasa taarifa hizo ipo Kigamboni, jambo ambalo alikanusha hakuna kitu kama hicho.

 

Waziri Mahiga alichukuwa nafasi hiyo kwa niaba ya serikali na wananchi kuwahakikishia wakenya na serikali yao kwamba hakuna mtambo wa kunasa taarifa za uchaguzi Tanzania na wala hawaingilii siasa zao za ndani.

 

Alisema wakati wa uchaguzi kunakuwa na maneno mengi ya uchafuzi, uzushi na majungu, ambapo alisisitiza Kenya imebakisha wiki mbili kufanya uchaguzi hivyo aliwatakia kila la kheri na kuwaombea uchaguzi ufanyike kwa uhuru na amani na matokeo yatangazwe kwa uwazi.

 

Hata hivyo alieleza  iwapo kama kutajitokeza kwa watu watundu Tanzania ambao watachezea mitambo, watu hao watadhibitiwa ili uchaguzi uwe wa uhuru na haki wa Kenya kwa vile hakuna mtu aliyeagizwa na serikali ya Tanzania kufanya hivyo.

 

Wakati huo huo Serikali ya Tanzania na Kenya imeondolea na vikwazo vya bidhaa na huduma kwa nchi mbili hizo baada ya viongozi wakuu wa nchi kukutana na mawaziri wa mambo ya nje na kumaliza tofauti za kibiashara.

 

Alisema siku za karibuni waliwekeana vikwazo vya unga wa ngano wa Tanzania na gesi aina ya LPG, ambayo ni ya kimataifa isiingizwe Kenya kutokana haijakidhi ubora wa viwango kwa watumiaji.

 

Alifahamisha kuwa, Tanzania nao waliwawekea vikwazo vya ‘Blue Band’ ya

Kenya isiingie nchini ili kuweza kulipizana, hali ambayo ilivuruga utaratibu wa forodha kwa nchi za Afrika Mashariki.

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s