Qaboos alivyoinawirisha Oman

1460531718_QNASultanQabosOman

MTU hawezi kutaja nchi zilizopiga hatua kubwa ya maendeleo bila kuiweka Oman kwenye orodha hiyo.

Maendeleo ya taifa hilo yaliyopatikana katika kipindi kifupi tangu kiongozi wake Sultan Qaboos bin Said ashike hatamu hayahitaji kurunzi kuyaona.

Kutoka katika hali duni ya maisha, umasikini wa kutupwa wa nchi na watu wake kabla hajaingia madarakani, hadi kulifanya kuwa taifa la kupigiwa mfano kwa kuinua ustawi wa watu, ni kazi kubwa iliyofanywa na kiongozi huyo anayependwa mno na wananchi wake.

220px-Nizwa-Vestiges_de_la_vieille_ville_(3)

Kama mtu aliiona Oman ilivyokuwa kabla mwaka 1970, atapigwa na mshangao iwapo leo atatua uwanja wa ndege wa nchi hiyo, na huenda asiamini macho yake kwa jinsi ilivyobadilika, kunawiri kimazingira, na ukwasi wa serikali na raia wake.

camel-desert-oman-large

Oman ya leo sio ile iliyokuwa kabla Sultan Qaboos hajakalia kiti cha uongozi. Hii ya sasa ni Oman mpya isiyochosha macho kuiangalia kila wakati.

Hapana shaka, kuingia madarakani kwa Sultan Qaboos Bin Said tarehe 23 Julai, 1970, kulikuwa mwanzo wa mapambazuko yaliyowatoa kizani wananchi na kuwapeleka kwenye nuru ambayo kila uchao inazidi kuliangaza taifa hilo lililoko katika peninsula ya Ghuba.

KUIMARIKA KWA UCHUMI

Wakati Sultan Qaboos akiingia madarakani,  kulikuwa na vitu vichache vinavyoweza kuitwa vya maendeleo.

Kwa ujumla taifa hilo lilikuwa nyuma sana kwani hakukuwa na miundombinu yoyote, wala huduma bora za kijamii kama vile afya na elimu.

DSC_0257

Kumbukumbu zinaonesha kwamba wakati huo kulikuwa na kilomita sita tu za barabara ya lami mjini Muscat, na idadi kubwa ya wananchi walitegemea zaidi kilimo na uvuvi kwa kuendesha maisha yao.

Kwa kiasi kikubwa, mabadiliko yote haya yametokana na matumizi sahihi ya rasilimali ya mafuta ambayo Oman imejaaliwa kuwa nayo, lengo likiwa kumaliza enzi za taifa hilo kutengwa kimahusiano na ulimwengu.

Mwanzoni mwa utawala wake, haraka Qaboos aliamua kubadilisha jina la nchi kutoka “The Sultanate of Muscat and Oman” na kuiita “The Sultanate of Oman” akilenga kuleta umoja wa kitaifa.

muscat-oman-jan-15-2014-omans-sultan-qaboos-r-talks-with-european-dpnntj

Wakati huo, Oman ilikuwa na skuli tatu tu, hospitali mbili na kilomita chache za barabara yenye lami.

Sasa Oman ina barabara nyingi kubwa na za kisasa, vituo vya afya katika miji yote mikubwa, na zaidi ya skuli 1,000.

Skuli na mahospitali yalijengwa, na miundombinu ya kisasa ikatandikwa kila kona ya nchi, huku barabara za kisasa kwa mamia ya kilomita zikinyooshwa hadi upeo wa macho.

ministerial-albusaidi_gallery

Aidha mtandao wa mawasiliano ya simu ukaanzishwa, miradi ya bandari na uwanja wa ndege ambayo ujenzi wake ulianza mara tu baada ya Qaboos kuingia, ikakamilishwa kwa kasi ya ajabu.

Mbali na hayo, bandari ya pili ikajengwa huku miundombinu ya umeme ikiimarishwa maradufu.

422836

Serikali ya Qaboos haikuwa na muda wa kulala na kuota, bali mkakati ulikuwa kuleta maendeleo ya haraka, na hivyo ikaanza kusaka njia mpya ya kuimarisha miundombinu ya maji.

Mitambo ya kisasa ya kuhifadhi na kusambaza maji ikajengwa, huku serikali ikishajiisha ushiriki wa sekta binafsi hususan katika miradi ya maendeleo.

WATER

Baadae, bandari zaidi zilijengwa na pia vyuo vikuu mbalimbali vilifunguliwa.

PORTI

Mabenki, mahoteli, makampuni ya bima na magazeti yalianza kuchomoza kadiri nchi ilivyozidi kupaa kiuchumi.

Haya na mengine, yakaifanya Oman kupata mabadiliko makubwa ikitoka kwenye maisha ya kubahatisha na kuwa nchi ya kisasa iliyosheheni miundombinu ya kila aina.

Oman-50Rials-b

Serikali ya Sultan Qaboos ilipanua nyanja za mapato kwa kuanzisha mashirika na mabenki ya biashara, masoko ya hisa na vyanzo vyengine mbalimbali ambavyo vimeipa thamani pesa yake, ‘Rial ya Oman’.

oman3

Hali hiyo imelifanya taifa hilo kuwa na uchumi thabiti usioyumba kwa kipindi chote hata katika wakati ambao nchi nyengine duniani zimepata msukosuko wa kiuchumi.

UHUSIANO NA NCHI ZA NJE

Oman imekuwa na uhusiano mzuri na nchi mbalimbali na haipendi kabisa kujiingiza kwenye migogoro inayohusisha nchi nyengine kwa kupendelea upande wowote.

Sifa hiyo pia imeipandisha Oman katika daraja ya kupatanisha mataifa jirani yanayozozana kwa vipindi na sababu mbalimbali.

201411149812370734_20

Kwa hivyo, kutokana na sifa hiyo, nchi na jumuiya mbalimbali za kimataifa zimeonesha kuvutiwa na siasa za taifa la Oman za kutojiegemeza upande wowote.

 

DINI

Oman inafahamika kuwa ni taifa la Kiislamu lakini haibagui watu wa imani nyengine na madhehebu mbaimbali.

churc

Kila mtu akiwa nchini Oman ana uhuru na haki ya kuabudu kwa mujibu wa imani yake bila ya bughudha.

home1---al-khuwair-mosque

Katika jitihada zake za kupeleka mbele Uislamu, Sultan Qaboos amefadhili ujenzi na matunzo ya misikiti mingi, ukiwemo msikiti wake mkuu, ‘The Sultan Qaboos Grand Mosque’, sambamba na majengo na maeneo mengine matakatifu ya kidini ndani na nje ya nchi yake.

Muscat-Oman-SL-a

 

UHIFADHI WA MAZINGIRA

 

Miongoni mwa sifa zinazomjenga sana kiongozi huyu, ni utashi wake wa kutaka kuifanyia nchi yake mambo makubwa badala ya kuangalia namna nchi itakavyomfanyia yeye binafsi.

Katika hili, suala la uhifadhi wa mazingira chini ya uongozi wake ni jambo linalopewa kipaumbele cha pekee.

oman-22

Mwanzoni mwa miaka ya 1990, kupitia ufadhili wa UNESCO, alitoa fedha kwa ajili ya zawadi ya mpango wake wa kuhifadhi mazingira iliyoitwa ‘The Sultan Qaboos Prize For Environmental Preservation’ (Tuzo ya Sultan Qaboos kwa Uhifadhi wa Mazingira).

Lengo la zawadi hiyo ni kutambua juhudi na mchango wa watu na taasisi nyengine katika usimamizi na utunzaji wa mazingira.

Sultan-Qaboos-Prize-for-Environmental-Preservation-Laureates-Books-Cds-DVDs-For-sale-at-All-Nigeria

Zawadi hiyo imekuwa ikitolewa kila baada ya miaka miwili tangu mwaka 1991 ikiakisi dhamira ya kiongozi huyo kuanzisha Wizara maalumu ya Mazingira.

AAEAAQAAAAAAAAlfAAAAJDcyMzgyMTQxLTg1MDUtNGMyMi1iZTQ1LTRhYWY3MzUxYTk1MA

Wananchi wa Oman wanauchukulia uongozi wa Sultan Qaboos kwa umuhimu wa pekee ikizingatiwa kwamba amekuja na mpango wa kuibadilisha nchi na kuwa ya kisasa katika nyanja zote za maendeleo ambao athari yake inaonekana wazi na kila mwenye macho ambaye anapenda kuyatumia kutazamia vitu vizuri.

tunzo

Haya yote na mengine mengi, ni kiashirio tosha cha dhamira ya dhati aliyonayo Sultan Qaboos ya kuiletea maendeleo nchi yake kwa manufaa ya Waomani wote.

Omani girls wearing traditional jewellery at the National Day ce

Mabadiliko makubwa yanayoshuhudiwa sasa, ni miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyowafanya watalii wengine wapende kuitembelea nchi hiyo.

633094

Mtu anapofika Oman atabaini kwamba, pamoja na Qaboos kuchukua hatua za kujenga Oman mpya, kamwe hakuruhusu mpango huo ufute utamaduni wa asili.

 

Kwa hivyo amefanikiwa kuhifadhi urithi wa utamaduni huo ambao ndio unaolitambulisha taifa hilo mbele ya macho ya walimwengu.

640x392_71986_180805

Mchanganyiko huu wa ukale na usasa bila shaka ndio unaowapa watalii wanaotembelea nchi hiyo vitu vizuri vya kukumbukwa kwa miaka mingi ijayo.

Oman-targets

Kwa hivyo, ujio wa Sultan kwa Waomani na nchi jirani za Kiarabu una umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya nchi hiyo na ustawi wa maisha yao, na hapa ndipo kiongozi huyo alipofanikiwa kujenga imani ya raia wake na mahaba makubwa kwake.

MICE-Group-at-Birkat-Al-Mawz

Wakati Oman ikiadhimisha miaka 47 tangu Sultan aingie madarakani mwaka Julai 23,1970, mbali na maendeleo makubwa yaliyoshuhudiwa katika uongozi wake, jambo jengine linalowafanya Waomani watembee vifua mbele, ni amani na utulivu, usiotoa nafasi kwa mifarakano ya ndani, au uhasama na mataifa mengine.

Oman-to-lead-ME-in-tourism-growth-Report_StoryPicture

Kila leo, Oman imezidi kuwa bora na tulivu kuliko ilivyokuwa jana na juzi, na kwa msingi huu, wengi wamekuwa wakiiombea iendelee kubaki katika hali hiyo kwa manufaa ya Waomani wenyewe na watu wa mataifa mengine wanaoependa maendeleo wakiwemo wawekezaji wazalendo na wale watokao nchi za nje.

Salum Vuai

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s