Pemba watakiwa kutumia nishati mbadala

20121213_083827

WANANCHI Pemba, wametakiwa wajitokeza kutumia nishati mbadala ili kukidhi mahitaji ya nishati ya umeme na kuinua kipato chao.

 

Akizungumza katika mkutano wa uhamasishaji wa nishati mbadala mjini Chake Chake, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, alisema wananchi wengi hasa wa vijijini wanahitaji huduma ya umeme, lakini wanaIkosa kutokana na hali ngumu ya maisha.

 

Alisema wakati umefika kwa wananchi hasa wenye kipato cha chini, kuitumia fursa hio ambayo itawaletea faida KUBWA.

 

Alisema  umeme huo ni mwanzo mwema katika kisiwa cha Pemba ambao utasaidia tatizo la ukataji ovyo wa miti linaloendelea.

 

Alisema nishati mbadala ni muhimu kwa matumizi bora ya wananchi, hasa wenye kipato cha chini hivyo ni vyema wakahamasika kuitumia nishati hiyo.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira, Ali Khalil Mirza, alisema kutokana na tatizo la kutokuwepo kwa uzalishaji umeme kwa kutumia vyanzo vyengine, kumeifanya Zanzibar kutegemea chanzo kimoja cha nishati,kutoka Tanzania Bara hali ambayo ni hatari kwa maendeleo.

 

Alisema mwaka 2008 na 2009 Zanzibar kulitokezea hitilafu ya umeme kwa zaidi ya miezi mitatu na kurejesha nyuma ya uchumi jambo ambalo halipaswi kupewa nafasi tena.

 

Nae Mkurugenzi wa Nishati na Madini, Mohamed Abdalla Mohamed, alisema lengo la kuanzishwa mradi wa nishati  mbadala ni kuifanya Zanzibar kuwa na vianzio vyengine vya uzalishaji wa umeme ili kuweza kukidhi mahitaji.

 

Alisema kwa sasa kazi zinazoendelea ni pamoja na ukusanyaji wa taarifa, matayarisho ya sheria na kanuni za nishati mbadala, pamoja na uhamasishaji wa wananchi juu ya masuala ya nishati mbadala na matumizi bora ya nishati.

 

Mradiwa umeme mbadala unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa 2018.

 

Chanzo: Zanzibar Leo

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s