JPM avipa wiki mbili vituo vya mafuta

1-10-2-1

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vyote vya mafuta nchini, kuhakikisha wanaweka na kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs) na atakayekiuka agizo hilo atafutiwa leseni ya biashara yake.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa kilomiya 154 huku akiwataka mawaziri wenye dhamana kuhakikisha wanafuatilia maagizo hayo kuanzia sasa.

“Wanaolalamika kukosa mafuta waendelee kufanya hivyo, ni mara mia tukose mafuta kuliko kuwa na wafanyabiashara wanaokwepa kodi,”alisema Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amepiga marufuku wananchi kutozwa kodi kwa mzigo wenye uzito wa tani moja anapousafirisha kutoka wilaya moja kwenda nyingine.

Alisema Biharamulo imeshika nafasi ya pili kwa umaskini na wananchi wanafanya ulinganisho na hali ilivyo tofauti katika wilaya jirani ya Chato.

Mapema Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, amesema barabara ya Kagoma-Lusahunga imegharimu shilingi 190 bilioni.

Nae Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa, alisema wanaunga mkono msimamo wa Rais kupiga marufuku wanafunzi wanaobeba mimba kuende;ea na masomo na wameanzisha skuli ya wasichana ya bweni kuunga mkono kauli yake.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s