‘Wanaotumia ‘headfone’ hatarini kupata uziwi’

Panasonic_Headphones_33397148_06

Madaktari wa masikio na pua Pemba wameitaka jamii kutojisafisha masikio kwa kutumia vijiti, kusikiliza sauti kwa kutumia ‘headfone’ na kutumia vitu vyenye ncha kali, kwani kufanya hivyo wanajitengenezea uziwi.

Mtaalamu wa masikio na pua, Dk. Issa Ahmada Mselem, wakati akitoa elimu kwa wanafunzi wa madrasa mbali mbali, alisema kuna badhi ya watu hutumia vijiti na pamba kusafisha masikio na kuna wengine hutumia vitu vyenye ncha kali hali ambayo inasababisha  athari kwa masikio bila kujua.

Aidha alisema sio vyema kujisafisha masikio kila mara kwani husababisha kutoboa ngoma ya sikio na hatimae kupata matatizo ya masikio na wengine kusababisha uziwi.

“Vijana wengi mnotumia ‘headfone’ kwa kusikilizia mziki mko kwenye hatari ya kupata uziwi, kwani mnaharibu mpango mzima wa ubongo,” alisema.

Aliitaka jamii kuacha kuondoa kile wanachoamini uchafu wa masikio akisema huo sio uchafu bali ni ukuta maalum iliowekwa kudhibiti masikio yasishambuliwe.

“Ndio maana hata anapoingia mdudu kwenye sikio taka hizi ndio zinazotumika kumdhibiti, wakati mwengie unasikia sikio linavuma na kwa mazoea tunasema mdudu wa sikio, huyo sio mdudu ni zile taka zinakuwa zinapamba na maaduni wa sikio lako,” alisema.

Pia alitahadharisha tabia ya watu kutia vitu kwenye sikio pale anapoingia kitu na kusema ni vyema akakimbilia hosopitali.

Nae Dk. Suleiman Ali Mohamed, alisema matatizo ya masikio pia husababishwa na mafua yanayochelewa kutolewa na kusababisha kuingia ndani na kutnga usaha.

Hivyo, alisema kama mtu ataona dalili za mafua ni vyeme akakimbilia hospitali na kuacha tabia ya kuyavutia kwa ndani kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha ngoma za masikio kubomoka.

“Kuna baadhi ya watu wakitoka taka za masikio hujitia pamba na wengine vitambaa bila ya kuwa na utalamu wowote, kufanya hivyo pia mnasababisha madhara, njooni hospitali mtibiwe,” alisema.

Aliwaomba wazazi kuwa makini na watoto wao kwani mara nyingi hupokea kesi za watoto kujitia vitu kwenye masikio na pua na wengine kutochukua hatua.

Mafunzo hayo yametolewa na Jumuiya ya Zanzibar Outreach Program (ZOP).

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s