TTCL nayo kutuma fedha

TTCL

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amezindua mfumo wa huduma ya kutuma pesa kwa njia ya simu za mkononi wa kampuni ya mawasiliano ya TTCL ujulikanao kama ‘TTCL PESA’ katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Akizindua mfumo huo jijini Dar es Salaam, Samia alisema TTCL imetekeleza agizo la serikali ya awamu ya tano lililoyataka mashirika yote ya umma yajiendeshe yenyewe kwa faida, pia kuwahudumia wananchi na kuondoa urasimu ambao umekuwa ukifanywa na kampuni za kigeni.

“Kuzinduliwa kwa huduma hii ni uthibitisho mwingine kwamba TTCL kama kampuni inayomilikiwa na serikali imejidhatiti kutekeleza kwa vitendo azma ya Rais Magufuli inayotaka mashirika yote ya umma kujiendesha kwa faida na kutoa gawio kwa serikali,” alisema.

Alisema kampuni ya TTCL inaimarika kiutendaji ili kuendana na mabadiliko ya kidijitali kwa na kudhihirisha hilo iliibuka mshindi wa kwanza katika maonesho ya 41 ya kimataifa ya kibiashara ya sabasaba katika utoaji huduma ya mawasiliano Tanzania.

Alisema kuanzishwaa kwa huduma hiyo kutafungua fursa za kibiashara na utoaji huduma kwa watu mbalimbali yakiwemo maeneo ya vijijini, kama kutuma na kupokea pesa, kulipia huduma mbalimbali kama vile bili za umeme na maji.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya TTCL, Omary Nundu, alisema kampuni hiyo ina mpango wa kutengeneza simu nchini.

Alitoa wito kwa wananchi kuanza kutumia huduma ya TTCL kwani ni kampuni ya serikali hivyo watadhihirisha uzalendo kwa nchi yao pamoja na kuikuza kampuni hiyo kimapato.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk.Maria Sasabo, alisema serikali inazidi kuimarisha kampuni hiyo ili iweze kuingia katika soko la ushindani wa mawasiliamno na kapmuni nyengine zinazotoa huduma hizo, kama vile, Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel, Smart  na Zantel.

Samia kuzindua ripoti APRM

Wakati huo huo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua ripoti ya kwanza ya utawala bora iliyoandaliwa chini ya mpango wa APRM kwa Tanzania.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa  APRM Tanzania, Rehema Twalibu, alisema uzinduzi huo utafanyika  leo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini  Dar es Salaam.

Alisema lengo la APRM ni kuzisaidia nchi za Afrika, Tanzania ikiwemo kuhakikisha zinaimarisha utawala bora.

Ripoti ya mwaka 2012 iliisfi Tanzania kwa kudumisha amani na umoja pia kudumisha muungano kwa zaidi ya miaka 50, pamoja na uimarishwaji  wa utoaji huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, maji, usawa wa kijinsia na teknolojia na habari na mawasiliano.

Alisema sifa zingine kwa Tanzania ni kulinda haki binadamu, matumizi ya lugha moja ya Kiswahili na hatua za maendeleo ya kiuchumi nchini.

Alisema uzinduzi wa ripoti ni utekelezaji wa mojawapo ya matakwa ya kiutaratibu katika mchakato wa APRM, ikiwa ni kiashiria kimojawapo cha utekelezaji wa yale yaliyoandikwa kwenye ripoti, pia kielelezo cha utayari wa serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Alisema changamoto zinazoikabili Tanzania kutokana na ripoti ya mwaka 2012, kuwa ni masuala ya demokrasia na siasa, kwani hakuna Tume Huru ya Uchaguzi kwa kuwa viongozi wake ni wateule wa Rais, taasisi za kuzuia na kupambana na rushwa bado hazina meno ya kutosha katika kudhibiti rushwa nchini.

Aidha alisema kumekuwepo na migogogro ya ardhi kati ya wazawa na wawekezaji ambapo baadhi ya wawekezaji wanahodhi ardhi za wazawa bila kutoa fidia kwa wakati wala kuwapatia maeneo mbadala.

Naye, Mkuu wa kitengo cha tathimini za nchi katika sekretarieti ya APRM na Mratibu wa mchakato wa Tananzia, Dk. Rachel Mukamunana, alisema wanatarajia kuona serikali ikizipatia ufumbuzi changamoto zilizoainishwa katika ripori ya mwaka 2012.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s