Watoto wanne wafa kwa pamoja

download

WATOTO wanne wakiwemo wawili wa familia moja, wamekutwa wamekufa katika mazingira ya kutatanisha katika mtaa wa Jang’ombe mkoa wa mjini magharibi Unguja.

Maiti za watoto hao wenye umri wa miaka miwili, zilikutwa ndani ya gari iliyokuwa imeegeshwa kando ya nyumba ya mmiliki.

Kamanda wa Polisi mkoa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Hassan Nasri Ali, alisema tukio hilo lilitokea Julai 16 saa 2.30 usiku.

Aliwataja watoto hao kuwa ni Haytham Mustafa Abubakar,  Muslim Hamza Bakar,Dodo Mohamed Malali na Munawar Ahmed Khamis wote wakiwa na miaka miwili wakaazi wa  Jang’ombe.

Alisema tarifa za kupotea watoto hao zilitolewa na Maryam Thomas Charles (25) katika kituo cha polisi Ng’ambo na polisi kufungua jalada la upelelezi.

Alisema polisi kwa kushirikiana na familia na mjajirani walifanya juhudi za kuwatafuta watoto hao na ilipofika saa 2.30 usiku maiti zao zilionekana kwenye gari aina ya Toyota Vitz yenye namba za usajili Z 986 DW, mali ya kijana mmoja alietambuliwa kwa jina moja la Omar.

Alisema kilichoonekana mmiliki wa gari hiyo alishindwa kufunga moja milango ya gari hiyo hali iliyosababisha watoto hao kuingia ndani na kujifungia na kushindwa kutoka hali iliyosababisha vifo vyao.

Alisema uchunguzi wa awali unaonesha baada ya mwenye gari kuegesha gari hiyo ufunguo alimkabidhi mama yake na yeye kuondoa kwenye Dar es Salaam kumuuguza mmoja ya wanafamilia alielazwa hospitali ya Muhimbili.

Alisema maiti za watoto hao zimekabidhiwa kwa jamaa zao kwa shughuli za maziko baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu.

Uchunguzi wa hospitali umebaini kuwa vifo vya watoto hao vimesababishwa na kukosa hewa.

Wakizungumza na Zanzibar Leo baadhi ya majirani, walisema tukio hilo linashangaza sana kwani gari ambayo walikuwemo watoto hao milango yake ilikuwa imefungwa.

“Tukio hili linatatanisha sana kwani eneo hili kutwa halikosi watu watoto waliingia vipi hili linatushangaza,” alisema.

Mama mzazi wa mtoto Haytham Abubakar alietambulika kwa jina la Mwatima Muhammed, akizungumza kwa uchungu juu ya kifo cha mtoto wake, aliiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo kwani wao ni wageni ambapo walikuja Zanzibar kwa ajili ya kutafuta maisha.

Wakati huo huo, Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Moudline Castico, aliwaomba wazazi na walezi kuwa makini katika kuwaangalia watoto wao huku akivitaka vyombo vya ulinzi kulifatilia suala hilo.

“Haiwezekani watoto wadogo wafungue mlango wenyewe na kuingia ndani halafu atoke mtu aseme wapo humu isijekuwa wahalifu wanatumia njia nyengine baada ya kukomesha vitendo vya udhalilishaji na kama kuna jini kwanini asijitokeze katika kuwatia abadu wahalifu wanaowadhalilisha kwa kuwabaka watoto wetu,” alisema.

Nae Mkuu wa Wilaya ya mjini, Marina Joel Thomas, alilitaka jeshi la polisi kutomvumilia mtu yeyote atakaebainika kufanya tukio hilo.

Maziko ya watoto hao yalifanyika jana saa 7.00 mchana katika makaburi ya Mwanakwerekwe huku mmoja akichukuliwa na familia yake kwa ajili ya mazishi katika maeneo ya Kiembesamaki.

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s