Tanzania ya kwanza kwa kuamini uchawi

hqdefault

IMEELEZWA kuwa Watanzania wanaongoza barani Afrika kwa kuamini uchawi na ushirikina na kusababisha kuwa miongoni mwa mambo yanayokwamisha shughuli za maendeleo nchini.

Taarifa hiyo imetolewa katika ukumbi wa mikutano Welezo wilaya ya magharibi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Baraza la Maaskofu Mtwara, Padri Titus Amigu, wakati wa semina ya viongozi wa ngazi zote za Kanisa Katoliki kanda ya Zanzibar.

Alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika moja nchini Marekani liitwalo P.E.W Research, katika bara la Afrika bado Tanzania ni nchi ya kwanza kuendelea  kuamini kuwa uchawi au ushirikina upo  kwani kati ya kila Watanzania 100, watu saba  tu ndio hawaamini mambo ya uchawi.

Tanzania inafuatiwa na Ethiopia ambao ni watu 13 tu kati ya kila watu 100 ndio hawaamini uchawi, Kenya ni 27 tu kati ya kila 100, Uganda ni ya nne ambapo kila Waganda 100 watu 29 hawaamini uchawi.

Padri Amigu alisema kwa takwimu hizo bado Tanzania itashindwa kupata mafanikio hadi pale wananchi wake watakapoachana na imani hiyo.

Aidha aliitaka jamii kuendelea kuishi pamoja kwa kuaminiana na kusaidiana bila kujali tofauti zao za dini.

“Nchi nyingi duniani zilifarakana na zingine mpaka leo  zinaendelea kupigana baadhi  yao ikiwa chanzo chake ni  jamii kuendeleza dhambi ya ubaguzi, hivyo tujiepushe na dhambi hii,” alisema.

Aidha awaliomba viongozi hao kuwahimiza wafuasi wao kuwa na tabia ya kutunza mazingira yanayowazunguka hasa ukataji miti ovyo ili kuepusha uwezekano wa kutokea majanga.

Semina hiyo ya siku mbili iliyowashirikisha viongozi wa ngazi zote wa kanisa hilo Zanzibar  wakiwemo  Mapadri, Masista na Watawa  ilifungwa na Askofu Augustino Shao wa Kanisa Katoliki Zanzibar.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s