Maiti ya tano yaokotwa kwenye kipolo

download

MAITI nyengine imeokotwa katika bahari ya Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ikiwa imefungwa kwenye mfuko wa kipolo.

Kupatikana kwa maiti hiyo kunafanya idadi za maiti zilizopatikana Zanzibar zikiwa zimefungwa kwenye kipolo na kutupwa baharini katika kipindi cha mwezi mmoja kufikia tano.

Kamanda wa Polisi mkoa huo, Hassan Nasri Ali, alisema maiti hiyo iliokotwa Julai 16 saa 3.00 asubuhi.

Alisema maiti  hiyo ni ya mwanamme mwenye umri baina ya miaka 40-45 na kwamba uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Katika tukio jengine alisema, maiti ya mtoto mchanga wa kiume imeokotwa ikiwa imetupwa jaani katika maeneo ya Darajabovu wilaya ya magharibi ‘A’, Unguja.

Kamanda Nasri alisema, maiti hiyo ilipatikana Julai 14 mwaka huu saa 3.00 asubuhi.

Kamanda Nassir, alisema wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo ili kubaini mtu aliefanya kitendo hicho.

Akizungumzia tukio la kupigwa utingo wa daladala katika maeneo ya Darajabovu, alisema tayari vijana watatu wanashikiliwa akiwemo mpigaji huku majeruhi akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mnazimmoja.

Aidha alisema polisi wamemkamata  Mohammed Haji Vuai maarufu ‘Muu Kijeshi’ ambae ni kiongozi wa kundi la vijana wanaotekeleza uhalifu.

Kamanda Nassir, alibainisha kuwa Jeshi la Polisi halitaishia kwa watu hao kwani lengo lao ni kusafisha kikundi kizima kinachohatarisha usalama wa raia na mali zao hasa katika wilaya ya Magharibi “A” na wilaya ya Mjini.

“Washitakiwa wote wapo ndani na tukipata matokeo kutoka kwa DPP, tutawafikisha mahakamani,” alisema.

Aliwahakikishia wananchi wa mkoa huo kwamba jeshi la polisi halifurahishwi na vitendo vinavyojitokeza, hivyo watachukua kila hatua kudhibiti vitendo hivyo.

Aliwaomba wananchi kushirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha linawafichua wahalifu ili waweze kuchukuliwa hatua.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s