Waliomshambulia mapanga ‘konda’ mbaroni

JESHI la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, linawashikilia watu wawili wanaodaiwa kumpiga mapanga utingo wa gari ya abiria inayoenda Darajabovu.

Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Hassan Nassir Ali, alisema hayo alipokuwa akizungumza na gazeti hili.

Alimtaja utingo alieshambuliwa kuwa ni Khamis Mgaya Juma (30) mkaazi wa Sarajevo.

Alisema bado ni mapema kutaja majina ya watuhumiwa waliokamatwa kwani kuna wengine wanatafutwa.

Alisema tukio hilo limetokea Juni 11 ambapo utingo huyo akiwa katika harakati za kazi alipofika eneo la Amani alianza kudai nauli kwa abiria wake.

Hata hivyo, alisema mmoja ya abiria wake alikuwa mbishi kutoa nauli na baada ya majibizano ya muda mrefu, abiria huyo alimwambia utingo huyo kwamba atamfanyishia.

“Utingo aliendelea na kazi yake ya kuchukua abiria kwenda mjini na kurudi Darajabovu lakini, alipofika kituo cha mwisho alivamiwa na kundi la watu na kuanza kupigwa mapanga na huku wakimwambia kuwa ‘huyu hadaiwi nauli’,” alisema.

Alisema majeruhi ameumiwa sehemu mbali mbali za mwili wake na amelazwa hospitali ya Mnazimmoja kwa matibabu na kwamba taarifa kuwa amefariki sio za kweli.

Mkuu wa wilaya ya magharibi ‘A’, Mwinyiusi Abdalla Hassan, alisema watuhumiwa wawili wamekamatwa ambao ni Abubakar Mkali Ame (20) na Mauli Abdalla Yussuf (16) ambapo wote ni wakaazi wa Munduli.

Alisema kuwa serikali ya wilaya inalaani kitendo hicho na kuvitaka vyombo vya sheria kuchukua hatua kali.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s