Ushirikiano Zanzibar na Ujerumani

771

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amesema ipo haja kwa  miji ya Zanzibar na Potsdam  wa Ujerumani,  kubuni miradi ya pamoja inayofanana  kiuchumi  ili isaidie kunufaisha wananchi.

 

Hatua hiyo alisema itaendeleza ushirikiano wa uhusiano wa muda mrefu uliopo baina ya pande mbili hizo, wakati akizungumza na ujumbe wa viongozi wa manispaa ya Potsdam iliyopo mkoa wa Brandenburg Ujerumani ukiongozwa na Meya wa mji huo, Jann Jackobs, ofisini kwake Vuga.

 

Alisema faida ya ushirikiano baina ya miji ya Zanzibar na Potsdam kwa kipindi kirefu imeanza kuleta matumaini hasa ikizingatiwa ile miradi iliyoanzishwa kwa pamoja baina ya pande hizo mbili ya nyumba za maendeleo za Kikwajuni (majumba ya Mjerumani) na uimarishaji wa miundombinu ya ujenzi wa mitaro ya maji machafu katika manispaa ya Zanzibar.

 

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wake itazingatia namna gani inaweza kusaidia katika uratibu wa uendelezaji wa ushirikiano wa kila siku wa miradi ya pamoja itakayoanzishwa.

 

Alihimiza umuhimu wa kuendeleza ziara za mara kwa mara kati ya viongozi, watendaji na hata wananchi wa kawaida wa miji hiyo ikilenga kudumisha  ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya Ujerumani na Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.

 

Aliuomba uongozi huo wa manispaa ya Potsdam kuwa baalozi wa kuitangaza Zanzibar kiuwekezaji nchini Ujerumani.

 

Alisema Zanzibar iko mbioni kuendelea kuimarisha miundombinu katika sekta ya utalii inayotegemewa kuwa muhimili mkuu wa uchumi fursa ambayo wawekezaji wa Ujerumani wanaweza kuitumia kuweka vitega uchumi vyao katika sekta hiyo.

 

Mapema Meya wa Manispaa ya Potsdam, Jann Jackobs, alisema mambo ya msingi ya ushirikiano kati ya mji wa Potsdam na Zanzibar yameshakubawa na tayari yanawekwa saini kipindi hiki kwa ajili ya utekelezaji wa pamoja.

 

Alielezea faraja yake kutokana na sekta ya utamaduni na utalii kuanza kuonesha matumaini ya mafanikio hasa katika baadhi ya matamasha yanayofanyika moja kati ya pande hizo kushirikisha wadau wa sehemu zote mbili.

 

Alisema masuala ya mazingira na fursa za ajira hasa kwa vijana yanakusudiwa kufanyiwa utaratibu wa utekelezaji wake katika kipindi kifupi kijacho.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s