Jela miaka 10 kwa kulawiti

MAHAKAMA ya Mkoa Mwera, imemhukumu Ali Ngwali Juma kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 10 baada ya kupatikana na kosa la kutorosha mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitano na kumlawiti.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Nayla Abdul-basit baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Alisema kwa kosa la kwanza mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu na kosa la pili la kulawiti atakwenda jela miaka saba.

Ilidaiwa Julai 25 mwaka jana saa 7.00 mchana Miwani wilaya ya Kati, mshitakiwa alimtorosha mtoto mwenye umri wa miaka mitano na kumlawiti.

Mshitakiwa alimchukua mtoto huyo na kumpeleka kwenye mashine ya kusagia mpunga iliyopo Miwani na kisha kumfanyia unyama huo.

Katika kesi hiyo jumla ya mashahidi sita walisikilizwa.

Aidha hakimu huyo alisema, amepokea barua kutoka hospitali ya Kidongochekundu ikieleza kuwa ni mgonjwa wa akili, lakini kwa kuwa alikuwa akiuliza masuali yanayohusiana na tukio alilofanya, mahakama haikuona haja ya kuzingatia barua hiyo.

“Kwa kuwa mshitakiwa alikuwa anauliza maswali yanayoendana na siku ya tukio sisi hatuwezi kuamini barua hiyo kwa sababu tunaona ana akili zake timamu na alifanya kwa kujua,”alisema.

Mbali na hukumu hiyo, mahakama ilimtaka mshitakiwa kulipa fidia ya shilingi 200,000.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s