Watumia risiti feki kuiba mchanga wa mamilioni.

GARI 49 zinazosafirisha mchanga zimekamatwa kwa tuhuma kuiibia serikali shilingi milioni 27 baada ya kugushi stakabadhi za kununulia biashara hiyo.

Hali hiyo imebainika baada ya Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, kufanya uchunguzi katika mauzo ya mchanga yaliyofanywa Juni 1 hadi 29 mwaka huu, ambapo baadhi ya wafanyabishara hao walivuna rasilimali hiyo kwa kutumia risiti feki.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa wizara hiyo, Hamad Rashid Mohammed, alisema kati ya wafanyabishara hao mmoja aliiba mchanga wenye thamani ya shilingi milioni 5 ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Alisema kati ya gari zilizoshiriki wizi huo, 30 zimewekwa chini ya ulinzi na wameanza kufanya taratibu za kuzichukulia hatua za kisheria.

Alisema wizi huo umeonekana kufanyika zaidi mwezi Juni mwaka huu, baada ya taarifa za benki kueleza kufanyika kwa malipo ili wachimbaji hao waweze kuruhusiwa lakini zilitofautiana na zile zilipokelewa na wasimamizi katika mashamba ya machimbo ya rasilimali hiyo.

“Ufuatiliaji wa kawaida wa takwimu za malipo ya benki na zile za machimboni uligundua tofauti, takwimu za machimboni zilionesha kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wa mchanga wanawasilisha karatasi za malipo za benki zisizo sahihi,” alisema.

Alisema katika kulifanyia kazi suala hilo, tayari wizara hiyo imeanzisha uchunguzi kati ya wizara hiyo pamoja na waliohusika katika Benki ya Watu wa Zanzibar, baada ya kubainika baadhi ya risiti zilizodaiwa kutolewa na benki hiyo kukosa vigezo stahiki vya risiti halali.

Alisema serikali haipo tayari kuwepo mchezo mchafu wa kuhujumu rasilimali za nchi na wizara hiyo itaendelea kujiridhisha, ili kuhakikisha mauzo yaliofanyika katika miezi ya Machi, Aprili na Mei kama ipo sahihi.

Aidha aliiagiza Idara ya Misitu na Maliasili Zisizorejesheka Pemba kwa kufanya operesheni maalum kwa maliasili ya mchanga ili kuhakikisha fukwe, madini na maji zinakuwa katika usalama.

Sambamba na hayo alitoa wito kwa viongozi na wanasiasa kuacha tabia ya kuwaombea misamaha wahalifu wanapokamatwa na badala yake waachie vyombo husika vitekeleze wajibu wake.

Nae, Mwenyekiti Jumuiya ya madereva na matajiri wa gari za mchanga, Msabah Hassan Silima, alikanusha uvumi kwamba kuna watu wamechukua mchanga kwa kupitiliza tani wanazozitaka, bali kosa liliopo ni risiti feki, hivyo waliiomba serikali kuwachukulia hatua kwa wahusika.

Nao madereva wa gari hizo walisema hawajui chochote kinachoendelea kuhusiana na kutumia risiti feki, kwani wao kazi yao wanalipa na kupewa risiti bila ya kujua kwamba halali au feki kwa sababu zote zina mihuri ya taasisi wanayofanyia malipo.

 

  Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s