TCRA yazipiga pini kampuni za simu

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imezitaka kampuni za simu za mkononi kusitisha matangazo wakati wateja wanapopiga simu vyenginevyo zitaadhbibiwa.

Akizungumza jijini hapa jana, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandishi James Kubala, alisema kuwekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wateja wanapopiga simu huanza kusikiliza matangazo ya kampuni hizo badala ya watu wanaowapigia.

Alisema sheria na kanuni za kumlinda mtumiaji wa huduma za mwaka 2011 zinataka watoa huduma kutoa matangazo wakati wa kumjibu mteja anapoulizia salio la muda wa maongezi.

Alisema watoa huduma wanaweza kutangaza wakati mteja anapopokea taarifa baada ya kuongeza salio na anapoingia katika orodha ya huduma za kampuni husika.

“Kanuni zipo za kuzuia matangazo kiholela lakini kampuni za simu zinakiuka sana kuanzia leo (jana) sititisheni au mtapambana na adhabu,” alisema.

Alisema wateja wamonesha hisia ya kukerwa na utitiri wa matangazo yasiyozingatia kanuni za mamlaka hiyo.

Kuhusu adhabu, alisema kuna aina nyingi za adhabu zinazoweza kutolewa ikiwemo kuzifungia kabisa zisifanye kazi nchini.

 

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s