Masheha waonywa kutojihusisha na rushwa

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheir, amesema Sheha yeyote atakaejihusisha na migogoro ya ardhi na vitendo vya rushwa, atakuwa amejifukuzisha kazi.

Alisema utu, uadilifu na uaminifu wa mtu unapotea kwa fedha ndogo hali ambayo inasababisha rushwa na uhujumu wa uchumi.

Aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa masheha walioteuliwa hivi karibuni yaliyofanyika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kiwakujuni.

Aidha, alisema lengo la Masheha kujaza fomu za maadili ni kuhakikisha wanajenga uadilifu katika kazi zao za kuwatumikia wananchi.

Alisema kuna baadhi ya masheha ambao wanaingia tamaa kwa fedha chache na kuacha maadili ya kazi zao kitendo ambacho kinashusha hadhi yao.

Hivyo, aliwataka kuitunza heshima waliyopata kwa kutekeleza wajibu wao kwani wameteuliwa na kula kiapo mbele ya Mwenyezi Mungu.

Alisema ni imani yake kwamba masheha hao watajitahidi kuwa washiriki wazuri na kuwa mfano katika utendaji wao wa kuwatumikia wananchi.

Mbali na hayo, aliwasisitiza kuyachukua mafunzo watakayopatiwa kama kigezo kizuri cha kufanyia kazi katika maeneo yao.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud, aliahidi kuyafanyia kazi na kuyasimamia yale

cha Diplomasia jijini Dar es Salam, Salim Othman Hamad yote yaliolekezwa.

Akiwasilisha mada ya maslahi ya umma, Mwalimu kutoka Chuo, aliwataka masheha hao kuangalia maslahi ya umma na kuacha kuangalia maslahi ya mtu mmoja mmoja ili kujenga uzalendo.

Wakichangia katika mafunzo hayo masheha hao waliiomba serikali kuwajengea ofisi za kudumu ambazo zitawarahisishia katika utendaji wa kazi zao.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s