Dkt.Shein aenda Uingereza

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na ​Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd alipokuwa akiondoka nchini jana kwenda nchini Uingereza kwa ziara ​maalum ya wiki​ mbili

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ameondoka nchini jana kuelekea nchini Uingereza kwa safari maalum ya wiki mbili.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume viongozi mbali mbali wa vyama na serikali walimuaga Dk. Shein wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.

Dk. Shein katika safari hiyo amefuatana na mkewe mama Mwanamwema Shein pamoja na watendaji wengine wa serikali.

Wakati huo huo, Dk. Shein alimtumia salamu za pongezi Rais wa Comoro, Azali Assoumani kwa kutimiza miaka 42 ya uhuru wa taifa hilo.

Alisema kwa niaba yake binafsi, kwa wananchi wa  Zanzibar na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, anatoa pongezi hizo kwa kiongozi huyo na wananchi wake wote katika taifa hilo kwa kutimiza umri huo pamoja na kupongeza mafanikio ya kiuchumi na kijamii yanayondelea kupatikana.

Aidha, alimuhakikishia kiongozi huyo kuwa serikali itaendeleza ushirikiano wake sambamba na kuimarisha uhusiano wa kihistoria ulipo baina ya pande mbili hizo na watu wake.

Alimtakia mafanikio kiongozi huyo pamoja na wananchi wake na kuwatakia maendeleo katika kuimarisha amani na utulivu uliopo.

Chanzo: Ikulu

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s