Afariki baada ya kuzama baharini

MTU mmoja aliejulikana kwa jina la Vuai Khamis Ame (19) mkaazi wa Bumbwini Makoba wilaya ya kaskazini B Unguja, amefariki dunia baada ya kuzama baharini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Hasina Ramadhan Taufik, alisema hayo alipokuwa akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.

Alisema mwili wa marehemu umekutwa katika ufukwe wa bahari ya Bumbwini Julai 4 saa 11 jioni na kufanyiwa uchunguzi na halafu kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi.

Alitumia fursa hiyo kuitaka jamii kuwa na tahadhari wanapokwenda baharini kwa shughuli mbalimbali ili kujiepusha na ajali.

Akizungumzia tukio jengine, alisema Julai 3 ya mwaka huu saa 2.00 asubuhi Mahonda kiwanda cha sukari watu wanne walikamatwa wakiwa wanaiba waya wa shaba uliozikwa chini ya ardhi.

Aliwataja watu hao kuwa ni Daudi Mazikabi Daudi (26) mkaazi wa Mahonda, Andrea James Pacha (19) wa Kinduni, Fereji Juma Amour (25) wa Muembemakumbi na  Emanuel Fabian Kiula (26) wa Michungwa miwili ambapo watu hao kwa pamoja walipatikana wakikata waya huo uliokuwa na thamani ya shilingi 500,000.

 Aidha alisema Julai 3 ya mwaka huu saa 7.30 mchana Kiwengwa Mafarasi mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Sadala Omar Haji (45) alipatikana na kete 69 za dawa za kulevya.

Alisema kete 44 zilikuwa kwenye kichupa cha plastiki na 25 zikiwa kwenye kifuko cha plastiki ambapo kete zote hizo alizihifadhi katika mfuko wa suruali yake.

Alisema watuhumiwa wote hao wanashikiliwa na jeshi la polisi ili kupitisha uchunguzi na zoezi hilo litapokamilika watafikishwa mahakamani

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s