Sudan Kusini yaiomba Tanzana kuisaidia

SERIKALI ya Sudan Kusini imeoimba Tanzania kuisaidia katika utoaji wa mafunzo kwa wataalamu wake hasa wa sekta ya afya, kilimo na kupatiwa walimu wa lugha la Kiswahili kwa sababu taifa hilo linataka kuanza kufundisha lugha hiyo kwenye skuli zake.

Makamu wa Kwanza Rais wa Sudan Kusini, Jenerali Taban Deng Gai, alitoa maombi hao baada ya kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais,  Samia Suluhu Hassan kando ya mkutano 29 wa wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Aliishukuru Tanzania kwa kuendelea kuiunga mkono Sudan Kusini kupitia jumuiya mbalimbali hususan Jumuiya ya Afrika Mashariki katika juhudi zake za kutafuta amani ya kudumu na kuwavumilia kadri inavyowezekana hasa wanapopitia changamoto mbalimbali.

Alimweleza Makamu wa Rais kuwa Tanzania ni mdau muhimu wa maendeleo kwa taifa hilo changa Afrika hivyo kuna umuhimu kwa Tanzania kuendelea kulisaidia taifa hiyo ili liweze kuimarisha hali ya ulinzi na usalama pamoja na uimarishaji wa utoaji huduma za msingi kwa wananchi wake.

Kwa upande wake, Samia aliihakikishia Serikali ya Sudani kuwa Tanzania itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii ikiwemo juhudi za uimarishaji wa hali ya ulinzi na usalama katika taifa hilo.

Alisema ili Tanzania iweze kushirikiana vizuri na Sudan Kusini ni muhimu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiriano wa Kimataifa  za nchi hizo kuandaa mfumo maalumu wa ushirikiano na utekelezaji wake ambao utaanisha maeneo  ya kushirikiana katika sekta mbalimbali kutokana na taifa hilo changa kuwa na changamoto nyingi hasa kwenye sekta za afya, elimu, kilimo, siasa, ulinzi na usalama.

Katika mazungumzo hayo, Samia aliziomba Wizara za Mambo ya Nje za nchi zote mbili kuandaa mpango huo haraka kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande hizo mbili.

Samia alionesha kuguswa na tatizo na vifo vinavyatokana na uzazi na aliishauri Serikali ya Sudan Kusini, pamoja na changamoto zao za kiuchumi ijaribu kuimarisha kadri itakavyoweza, miundombinu ya barabara, gari ya kusafirisha wangonjwa kwa haraka, vifaa tiba na kuimarisha vyumba vya dharura vya uzazi ili kukabiliana na tatizo hilo.

Kuhusu tatizo la uhaba wa chakula, aliguswa pia na changamoto hiyo inayoendelea kuikumba Sudan Kusini na aliridhika kusikia kuwa kuna jitihada zilifanywa na serikali yao kuja Tanzania kwa ajili ya kutafuta chakula cha kutosha kwa ajili ya wananchi wake.

Alipongeza jitihada zinazochukuliwa na serikali ya Sudan Kusini chini Rais wao, Salva Kiir ya kutafuta suluhu mgogoro wa kisiasa nchi humo.

Wakati huo huo, Samia amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Mauritius, Anerood Jugnauth na kutumia fursa hiyo kuwakabirisha wawekezaji kutoka taifa hilo kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini.

Alisema Tanzania itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano yaliyopo kati ya mataifa hayo mawili itaendelea kujifunza zaidi kutoka kwa Mauritius hasa namna ya kuimarisha shughuli za utalii na namna bora ya kuongeza uzalishaji wa sukari ili kukabiliana na uhaba wa bidhaa hiyo.

Alisisitiza uharakishaji wa kusainiwa mikataba ya makubaliano kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande hizo mbili.

Naye, Waziri Mkuu wa Mauritius, Anerood Jugnauth alimuhakikishia Makamu wa Rais kuwa taifa hilo litaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s