Mwinyi aona mwanga Tanzania ya viwanda

RAIS mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, amesema Tanzania ya viwanda imeanza kuonekana baada ya kuwepo mageuzi makubwa ya maendeleo ya teknolojia katika maonyesho 41 ya kimataifa ya biashara ya mwaka huu.

Kauli hiyo aliitoa jana baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho yakiwemo ya Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC), Shirika la Bima, mabanda ya bidhaa za viungo na Wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar.

Mabanda mengine aliyotembelea ni VETA, TBC, Magereza, PBZ, Azam, Kilimo, Zantel na mabanda ya kigeni Saudi Arabia na Misri.

Alisema Tanzania itapiga hatua kubwa ya maendeleo katika uchumi wa viwanda kutokana na kuwepo mambo mengi ya maendeleo aliyojionea kwa macho katika maonyesho hayo.

Nae Waziri Biashara, Charles Mwijage, alisema Tanzania ina viwanda vinne vya kutengeneza soli za viatu, hivyo itapofika Disemba mwaka huu watakuwa hawaagizi tena soli za viatu kutoka nje ya nchi.

Alisema magereza wamepiga hatua kubwa ya utengezaji bidhaa mbali mbali za majumbani na viatu kwa ajili ya jeshi hilo na uhamiaji ambavyo vipo katika viwango bora.

Wakati huo huo, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, alisema mahakama zimeimarishwa zaidi kwa kutumia teknolojia katika usikiliza wa kesi ili kuendana na uchumi wa viwanda.

Alisema changamoto kubwa inayoikabili mahakama ni pamoja na upungufu wa majaji 30 ambao wangeweza kuendesha kesi kwa haraka zaidi, ambapo kwa sasa wamejipanga ndani ya miezi tisa mahakama kuu iwe imeshamaliza kesi zozote za jinai, za ufisadi na rushwa.

Aidha alisema changamoto nyengine ni kuwepo kwa kesi nyingi walizozirithi katika miaka miwili iliyopita, ambapo wanaendelea kuzitolea maamuzi.

Alitoa wito kwa wananchi kuwa na imani na mahakama, ambapo alisisitiza mtu akidaiwa rushwa katika kesi yake asisite kutoa taarifa TAKUKURU.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s